“Laana” ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

“Laana” ni nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Quemu, Jun 30, 2008.

 1. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2008
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hivi, tumekuwa tukisikia vitisho vya “kimaneno” mbalimbali katika jamii yetu...

  Mojawapo ya vitisho hivyo ni upewaji “laana”.

  Inasemekana kuwa “laana” utolewa na mzazi kwa mtoto aliye mtukutu au aliye kaidi mwongozo wa wazazi.

  Tetesi ni kwamba “laana” inayorushwa na mtu mwingine, zaidi ya mzazi wako, huwa haikudhuru.

  Jamani, hiki kitisho huwa kinafanya kazi kweli? Au ni moja ya mikwara “bogus” ambayo imetapaa kila kona ya utamaduni wetu?

  Je “laana” ni nini?
   
 2. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  "Inaitwa LAANA JAMII", jamii inaweza kukulaani yakakupata kweli.
   
 3. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Laana ni kumuapiza mtu au jamii .. ili kama anakwenda/kaenda kinyume na jambo fulani au miiko .. ambapo kabainika au hajabainika .. adhurike na abainike ..

  Mtu /jamii hutoa kiyapo ili iwe kama hukumu kwa yeyote atakae/anaenda kinyume na taratibu ambazo mwenzake/jamii a/itaona ni kitendo cha kinyama au kupitiliza kosa au ubaya.

  Laana inampata mtu kweli ... inaweza hata ikaangamiza familia nzima
  Mtu yeyote anaweza kumlaani na kulaaniwa kutegemea na kosa alilolifanya
  Hata mke/mume anaweza kumlaani mwenziwe akadhurika ... kadhalika mama huweza kumlaani hata mtoto pia
   
 4. H

  Haika JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  mfano hiviii:
  sisi watanzania tumelaaniwa ndio maana unaona tuna kichwa cha mwendawazimu.
   
 5. w

  wajinga Senior Member

  #5
  Jul 1, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Laana inakupata ukimtendea mtu yeyote mabaya. Kwa hiyo chunga. Ishi kwa maadili na usiwe tapeli au fisadi kwani utapata laana.
   
 6. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2008
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Bubu,
  A)Kwa hiyo jamii mzima inaweza kutoa laana kwa mwanajamii?

  B)Au mwanajamii anaweza kutoa laana kwa jamii mzima?


  Naima,
  Umesema laana = kuapiza. Kuapiza as in "Haki ya Mungu", "naahidi sitafanya kinyume na matakwa yako", or what?

  Haika,
  Sasa ni nani ametulaani sisi? Je ni sisi wenyewe tumejilaani?

  Speaking of kujilaani, je inawezekana kwa mtu kujilaani mwenyewe?

  Wajinga,
  Kwa hiyo sio lazima mtu au jamii ikulaani...yaani hata mazingira uishiyo au matendo ufanyayo yanaweza kukulaani?
  ******************************************************

  Asanteni kwa ufafanuzi wenu.

  Kutokana na ufafanuzi wenu hapo juu, ninalazimika kufikiri kuwa "laana" ni "imani." Kama vile tunaposema fulani "amelogwa", tuna express imani yetu kuwa kuna tendo la "kichawi" limetokea kwa mtu huyo.

  Sasa kama "laana" ni imani, basi ni wale tu wanafuata imani hiyo ndio wana hatari ya kudhurika. Au?

  I mean, kuna tofauti gani kati ya "imani" ya laana na "imani" ya dini...iwe ya kiislam, kikristo, au kipagani? Zote si ni imani tu....na zinafanya kazi kwa wanao amini. Au?
   
 7. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ...inakupata kutoka wapi, kwa nguvu ya nani, gani, inaitwaje, electromagnetic force or something?
   
 8. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Si kweli kwamba laana inatoka kwa mzazi tu. Na pia mtoa laana hupatwa na laana vilevile. Maandiko yanasema USILAANI.


  .
   
 9. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2008
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo laana inaweza kudunda na kukurudia mwenyewe? lol

  Kuhani ameuliza swali kwamba hii "laana" inatoka kwenye nguvu gani? Na nini hasa?

  Tunajuwa kuwa kuna wata wanaamini "uchawi" ni sehemu ya sayansi. Lakini kuna wengine waamini "uchawi" unatokana na nguvu ya giza (whatever that means).

  Je laana urushwa kwa kutumia nguvu gani?
   
 10. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Sikubali kwamba kuna laana kama ya mzazi wako kukufanyia kitendo fulani unapata kichaa, ila naamini katika the karmic and natural laws of cause and effect.

  Hivyo basi, kwa mfano wa "laana" ya wazazi (wengine wanaita kukosa radhi), wazazi hawa ni watu ambao kwa kawaida wanapenda sana watoto zao. Na wazazi kwa kawaida huvumilia mengi sana mabaya ambayo watoto wao wanaweza kuwafanyia, hivyo basi, ikifikia kipindi wazazi wameshindwa kuvumilia na kutoa "laana" basi huyu mtoto anayepewa laana anakuwa kashaharibikiwa tayari na matokeo yake anaweza kupatwa na mabaya.

  Akipatwa na mabaya watu wanasema ni kwa sababu ya laana ya wazazi, bila kujua kuwa hiyo laana / kukosa radhi kumekuja baada ya wazazi kukata tamaa kwamba kuna redemption yoyote kwa mwana wao.

  Kwa hiyo laana ni matokeo, si sababu.
   
 11. Mtimti

  Mtimti JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2008
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 914
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 60
  laana ni maapizo kutoka kwa MWENYEZI MUNGU,ni mambo uyafanyayo ambayo MWENYEZI MUNGU hayupo radhi nayo na UNAYEMFANYIA hayupo radhi nayo,mfano;MWNYEZI MUNGU amewalaani(hawatapata japo bahati ya kuuona mlango wa pepo) wale wote wanaowasodoma/sodomwa(mchezo wa kinyumenyume),
  tumeshazoea kusikia kuwa wazazi ndio wenye kutoa laana,si kweli,mzazi yeye kazi yake ni kumshtakia mwenyezi MUNGU.pia si vizuri kwa mwanadamu kulaani laani au kujiona kama umelaaniwa,kwani kwani NENO LINAUMBA.
   
 12. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2008
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Pundit
  Utawaambiaje wale wanao amini kuwa familia fulani "imelaaniwa" kwa sababu wana mtiririko wa matatizo fulani fulani? Je hali hii usababishwa na sio "laana", bali matokeo ya utukutu?

  Je laana ndio huitwa "spell/curse" kwa kizungu?
   
 13. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2008
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Neno Mungu, limedhihirisha kuwa "laana" ni imani. Na kama imani nyingine yeyote, basi wale tu waaminio ndio hudhurika.
   
 14. Mtimti

  Mtimti JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2008
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 914
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 60
  kumbuka kuwa hapa duniani wapo wanaoabudu miti,ng'ombe,milima,mito nk,na hawa wote wana makatazo yao,na wakienda kinyume nayo hulaaniwa,hivyo laana ipo kwa mwenye kuamini na asiyeamini
   
 15. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Yote ni cause and effect, au inaweza hata kuwa genetics.

  Mfano, inawezekana katika familia fulani kuna genes za kuwafanya watu wawe susceptible kwa magonjwa ya akili, au ulevi, watu wengi wakitokea kuwa na ukichaa au ulevi watu watasema "wamelaaniwa" kumbe ni genetics.

  Mara nyingine inakuwa ni habits zilizojengeka kwa siku nyingi tu.

  Laana ni more of curse kuliko spell, spell inaweza kuwa kitu kam hypnotism zaidi kuliko laana.
   
 16. K

  Kizito Member

  #16
  Jul 1, 2008
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Laana ni kama mbegu mbaya ipandwayo ardhini, mbegu mbaya yoyote ile huota kwa bidii sana tena bila hata kuiwekea mbolea, lakini panda mbegu nzuri hata ukiiwekea mbolea vipi utavuna mavuno kidogo sana.

  Sasa "laana" ni maneno ambayo mtu huambiwa iwe kwa kukatazwa jambo au hata kwa kuonywa au hata kwa kusisitizwa vyovyote neno hilo litakavyotoka basi haling'oki mawazoni mwa huyo mtu sasa basi kwa kuwa maneno hayo hujengeka mawazoni mwake kila kitu atakachokifanya akishindwa kufanikiwa tu atasingizia ni ile "Laana"

  Na usiombe maneno hayo yalipokuwa yanatolewa kama kulikuwa na watu ndio kabisa watayasambaza hadi kila mtu atajua umelaaniwa, na kila mtu kama alitaka kufanya biashara na wewe atasitisha na ndipo nawe utakapoanza kuona kuwa ile laana inakuathili.

  Kuhusu mtoa "laana" ni mtu yeyote anaweza kutoa "laana" sio lazima mzazi.
   
 17. talentboy

  talentboy JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2016
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 1,142
  Trophy Points: 280
  Hiyo familia itakuwa na mkosi/nuksi na sio laana!
   
 18. y

  yofre Senior Member

  #18
  Nov 20, 2016
  Joined: Nov 20, 2016
  Messages: 144
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  kwa mtazamo wangu....laana inatolewa na mtu yeyote yule....ila huyo mtu kama anakupenda kwa ukweli bila unafiki,yaani kama mama ako basi laana inakupata,ILA kama anakupenda kiunafki,basi laana inakuwa barakaa kwako
   
Loading...