Soma hapa kuhusu Yakobo ili ujue kuwa Israel sio taifa teule. Ni taifa lenye laana ya kurithi

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,223
22,299
Nimekubali maombi ya wengi wenu kwamba niongee chochote kuhusu huu mgogoro wa wapalestina na waisrael ili kuweka sawa hali ya hewa iliyochafuka kwa maoni yasiyoeleweka. Nikiwa kama mzalendo kwa nchi yangu nimeamua niwaeleweshe wananchi wenzangu mlio kwenye mkwamo na kutokujua nini hasa kinaendelea. Na kama ilivyo kawaida uzi huu ndo utakuwa msimamo kamili wa JF kwa kinachoendelea mashariki ya kati. Moja ya ahadi za mwanaCCM ni kutosema uongo wala kuwa mfitini. Nitakachokiandika hapa ni ukweli mtupu.

Nitaeleza kwa lugha nyepesi itakayoeleweka hata kwa wafuasi wa Mbowe. Tumeona baadhi ya wakristo wakihusisha mgogoro huu na mambo ya kiimani na kutaja baadhi ya vifungu vya biblia kuthibitisha madai yao. Wameenda mbali zaidi kwa kudai kuwa Israel ni taifa teule la Mungu. Hawa WAPUUZWE. Israel sio taifa teule la Mungu huyu tunayemuabudu labda kama yupo Mungu mwingine. Hawana uhalali wowote wa kuitwa taifa teule. Ni taifa lenye laana ya kurithi kwa baba yao aitwaye Israel. Nitafafanua.

Israel kama taifa chimbuko lake ni mtu aitwaye Yakobo mwana wa Isaka ambaye alipewa jina la Israel kwa kile kinachotajwa kuwa alishindana mieleka na malaika kwa usiku mzima (soma Mwanzo 32: 24-28). Tukiyatazama maisha ya Yakobo ndo tutapata majibu ya kwanini hawa Waisrael wamekuwa watu wa kutangatanga na kuchukiwa karibu kila wanakoenda. Kimsingi Yakobo ni baba wa waisrael wote ambaye maisha yake yalitawaliwa na uongo, tamaa na fitina hali iliyofanya maisha yake kuwa ya kukimbia kimbia.

Yakobo ni pacha wa Esau ambaye alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Isaka. Tukio la kwanza la kihuni kufanywa na Yakobo ni pale alipoichukua haki ya uzaliwa wa kwanza ya Esau. Alitumia chakula kumnasa Esau aliyekuwa na njaa kali hatimaye kumkabidhi hiyo haki ya uzaliwa wa kwanza. Tukio la pili la kihuni zaidi kufanywa na huyu baba wa wayahudi ni kumlaghai baba yao na kumpatia baraka ambazo zilikuwa ziende kwa Esau (soma Mwanzo 25 - 27). Haya matukio mawili yalitosha kabisa kuanzisha maisha ya kutangatanga kwa Yakobo kufuatia kaka yake Esau kughadhabika na kutaka kumuua Yakobo. Ilibidi Yakobo akimbilie kwa mjomba wake aitwaye Labani.

Huko ujombani alipata kazi ya kuchunga mifugo ya mjomba wake. Hapa tunaona laana ya utumwa na kudharaulika ilianza na huyu baba wa waisrael. Akiwa kwa mjomba akampenda binti wa Labani aitwaye Rahel mdogo wake Lea. Mzee Labani akamwambia jomba inabidi uchunge mbuzi miaka 7 iwe kama mahari ya kumpata Rahel. Baada ya miaka 7 ikafanyika harusi lakini jioni yake Yakobo anamfunua uso bibi harusi anakuta ni dada mtu Lea na sio Rahel. Wakati kapaniki ndo kuambiwa kuwa kwa tamaduni na mila za kwa Mzee Laban huwa anaolewa mkubwa kwanza ndo anafuatia mdogo kwahiyo isingewezekana aolewe Rahel ndo afuate Lea. Kwahiyo kumpata Rahel inabidi uchunge tena Mbuzi kwa miaka mingine 7. Biblia inasema Lea hakuwa mzuri kama Rahel na alikuwa na makengeza. Ikawa hakuna jinsi lazima akubaliane na hali. Baada ya miaka mingine 7 ndo akampata asali wa moyo wake. Kiukweli baba wa taifa teule alisoteshwa miaka 14 kupata chaguo la moyo wake (soma Mwanzo 29).

Mzee Laban pia alikuwa mzee wa dhuluma kwenye malipo ya Yakobo. Zamani malipo yalikuwa ni kulipana mifugo jinsi inavyozaliwa lakini Labani alikuwa akikiuka makubaliano mara kwa mara ikafikia hatua Yakobo akaamua kutoroka pamoja na wake zake. Alichukua kila kilicho chake na kusepa. (Soma Mwanzo 31). Kimsingi maisha ya Israel hadi uzeeni yalikuwa ya misukosuko sana. Hata watoto wake aliowazaa walikuwa watu wa ajabu kama vile wenye laana. Fikiria watoto wa Yakobo walifikia hatua ya kumuuza mdogo wao aitwaye Yusufu kwa wamisri (soma Mwanzo 37). Fikiria hawa watoto 12 wa Yakobo wenye laana ya kumuuza mwenzao ndo wanatajwa kuunda kabila 12 za waisrael. Kimsingi hata kabila litarithi laana.

Katika kosa la kiufundi alilofanya Yakobo ni kukubali kuacha nchi yake ya Kanaani na kuhamia Misri yeye na familia yake yote kwa kukubali pendekezo la farao wa wakati huo. Ikumbukwe baada ya kuuzwa utumwani, mambo yalibadilika na Yusufu kufikia cheo cha kama Waziri Mkuu kwa hapa Tanzania. Farao wa wakati huo alimkubali sana Yusufu na kushauri ailete familia yake yote iishi Misri. Kukubali wazo la kuhama Kanaani na kwenda Misri ilikuwa ni upuuzi mtupu unaowagharimu hadi leo. Lakini wangefanyaje wakati Yakobo tayari alishazoea hali ya kuhamahama. Hakuwa na utulivu wowote. Soma Mwanzo 45: 17 - 28.

Mara baada ya kifo cha Yusufu na watu wote wa kizazi chake kufa ndo pakaibuka Farao mpya aliyeshtushwa na wingi wa waisrael Misri na jinsi walivyo na nguvu. Huyu Farao ndo alianzisha balaa kwa wayahudi. Kwa kumalizia nisema Waisrael toka enzi za Farao wamekuwa watu wa kunyanyasika na kuishi kwa mashaka matupu. Aliyoyafanya Hitler kwa wayahudi yalikuwa ni mwendelezo tu kwasababu biblia inamtaja mtu aitwae Haman kuamuru waisrael wote wauwawe. Warumi nao kwa miaka mingi wamewatawala wayahudi. Tukichanganya matukio yote ya kihistoria itoshe kusema Israel ni taifa lililorithi laana ya baba yao Yakobo. Misukosuko yote inayowapata ni laana. Ninaweza sema ni taifa teule kwenye upande wa laana. Ni funzo kwa sisi tulio hai tusidhulumu haki za watu. Laana yake huenda hadi kwa watoto. Chanzo cha Israel kuwa taifa la laana ni tamaa tu ya baba yao.
 
Wewe mbona unakuwa muongo kama kikundi cha kiharamia cha Hamas kinachosingizia Israel kulipua hospitali kumbe ni chenyewe kimeua Wapalestina wenzao!
 
Home boy wekeza tu kueleza ilani za chama huku kugumu yani kwa akili za mboga mboga utaishia kusema mambo hivi.

Kuweka tu mambo sawa hii inayoitwa Israel ya sasa ni tofauti na kile kinachosemwa kwenye biblia.Hii modern Israel ni taifa la juzi tu linapishana kidogo tu na Tanganyika yako kuundwa.The true Israel mentioned in the bible has been changing.In OT(Israel has been conceptualized as Jacob and his sons) while in NT(Isreal has been conceptualized as a church(refer to letters of Paul the apostle)).
 
Nilidhani una point ila hapo mwishoni ndo ukaharibu kila kitu. Nitazidi kuwaelimisha. Ahadi ya mwanaCCM ni pamoja na kutumia elimu yake kwa manufaa ya umma.
 
Ndgu mbona mweupe hvyo kwnye biblia.unaleta tasfiri za uongo.eti yakobo alikuwa anachunga mbuzi kwa mjomba wake'unajua malaika akambariki na akamwita israel na cyo yakobo? unajua hata milango ya kuingilia imetajwa kwa majina ya wana wa yakobo 12 ufunuo 7 na 14.unajua jina la taifa la israel imetokana na yakobo.
 
Alikuwa anakuchunga wewe?
 
Nimekubali maombi ya wengi wenu kwamba niongee chochote kuhusu huu mgogoro wa wapalestina na waisrael ili kuweka sawa hali ya hewa iliyochafuka kwa maoni yasiyoeleweka. Nikiwa kama mzalendo kwa nchi yangu nimeamua niwaeleweshe wananchi wenzangu mlio kwenye mkwamo na kutokujua nini hasa kinaendelea. Na kama ilivyo kawaida uzi huu ndo utakuwa msimamo kamili wa JF kwa kinachoendelea mashariki ya kati. Moja ya ahadi za mwanaCCM ni kutosema uongo wala kuwa mfitini. Nitakachokiandika hapa ni ukweli mtupu.

Nitaeleza kwa lugha nyepesi itakayoeleweka hata kwa wafuasi wa Mbowe. Tumeona baadhi ya wakristo wakihusisha mgogoro huu na mambo ya kiimani na kutaja baadhi ya vifungu vya biblia kuthibitisha madai yao. Wameenda mbali zaidi kwa kudai kuwa Israel ni taifa teule la Mungu. Hawa WAPUUZWE. Israel sio taifa teule la Mungu huyu tunayemuabudu labda kama yupo Mungu mwingine. Hawana uhalali wowote wa kuitwa taifa teule. Ni taifa lenye laana ya kurithi kwa baba yao aitwaye Israel. Nitafafanua.

Israel kama taifa chimbuko lake ni mtu aitwaye Yakobo mwana wa Isaka ambaye alipewa jina la Israel kwa kile kinachotajwa kuwa alishindana mieleka na malaika kwa usiku mzima (soma Mwanzo 32: 24-28). Tukiyatazama maisha ya Yakobo ndo tutapata majibu ya kwanini hawa Waisrael wamekuwa watu wa kutangatanga na kuchukiwa karibu kila wanakoenda. Kimsingi Yakobo ni baba wa waisrael wote ambaye maisha yake yalitawaliwa na uongo, tamaa na fitina hali iliyofanya maisha yake kuwa ya kukimbia kimbia.

Yakobo ni pacha wa Esau ambaye alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Isaka. Tukio la kwanza la kihuni kufanywa na Yakobo ni pale alipoichukua haki ya uzaliwa wa kwanza ya Esau. Alitumia chakula kumnasa Esau aliyekuwa na njaa kali hatimaye kumkabidhi hiyo haki ya uzaliwa wa kwanza. Tukio la pili la kihuni zaidi kufanywa na huyu baba wa wayahudi ni kumlaghai baba yao na kumpatia baraka ambazo zilikuwa ziende kwa Esau (soma Mwanzo 25 - 27). Haya matukio mawili yalitosha kabisa kuanzisha maisha ya kutangatanga kwa Yakobo kufuatia kaka yake Esau kughadhabika na kutaka kumuua Yakobo. Ilibidi Yakobo akimbilie kwa mjomba wake aitwaye Labani.

Huko ujombani alipata kazi ya kuchunga mifugo ya mjomba wake. Hapa tunaona laana ya utumwa na kudharaulika ilianza na huyu baba wa waisrael. Akiwa kwa mjomba akampenda binti wa Labani aitwaye Rahel mdogo wake Lea. Mzee Labani akamwambia jomba inabidi uchunge mbuzi miaka 7 iwe kama mahari ya kumpata Rahel. Baada ya miaka 7 ikafanyika harusi lakini jioni yake Yakobo anamfunua uso bibi harusi anakuta ni dada mtu Lea na sio Rahel. Wakati kapaniki ndo kuambiwa kuwa kwa tamaduni na mila za kwa Mzee Laban huwa anaolewa mkubwa kwanza ndo anafuatia mdogo kwahiyo isingewezekana aolewe Rahel ndo afuate Lea. Kwahiyo kumpata Rahel inabidi uchunge tena Mbuzi kwa miaka mingine 7. Biblia inasema Lea hakuwa mzuri kama Rahel na alikuwa na makengeza. Ikawa hakuna jinsi lazima akubaliane na hali. Baada ya miaka mingine 7 ndo akampata asali wa moyo wake. Kiukweli baba wa taifa teule alisoteshwa miaka 14 kupata chaguo la moyo wake (soma Mwanzo 29).

Mzee Laban pia alikuwa mzee wa dhuluma kwenye malipo ya Yakobo. Zamani malipo yalikuwa ni kulipana mifugo jinsi inavyozaliwa lakini Labani alikuwa akikiuka makubaliano mara kwa mara ikafikia hatua Yakobo akaamua kutoroka pamoja na wake zake. Alichukua kila kilicho chake na kusepa. (Soma Mwanzo 31). Kimsingi maisha ya Israel hadi uzeeni yalikuwa ya misukosuko sana. Hata watoto wake aliowazaa walikuwa watu wa ajabu kama vile wenye laana. Fikiria watoto wa Yakobo walifikia hatua ya kumuuza mdogo wao aitwaye Yusufu kwa wamisri (soma Mwanzo 37). Fikiria hawa watoto 12 wa Yakobo wenye laana ya kumuuza mwenzao ndo wanatajwa kuunda kabila 12 za waisrael. Kimsingi hata kabila litarithi laana.

Katika kosa la kiufundi alilofanya Yakobo ni kukubali kuacha nchi yake ya Kanaani na kuhamia Misri yeye na familia yake yote kwa kukubali pendekezo la farao wa wakati huo. Ikumbukwe baada ya kuuzwa utumwani, mambo yalibadilika na Yusufu kufikia cheo cha kama Waziri Mkuu kwa hapa Tanzania. Farao wa wakati huo alimkubali sana Yusufu na kushauri ailete familia yake yote iishi Misri. Kukubali wazo la kuhama Kanaani na kwenda Misri ilikuwa ni upuuzi mtupu unaowagharimu hadi leo. Lakini wangefanyaje wakati Yakobo tayari alishazoea hali ya kuhamahama. Hakuwa na utulivu wowote. Soma Mwanzo 45: 17 - 28.

Mara baada ya kifo cha Yusufu na watu wote wa kizazi chake kufa ndo pakaibuka Farao mpya aliyeshtushwa na wingi wa waisrael Misri na jinsi walivyo na nguvu. Huyu Farao ndo alianzisha balaa kwa wayahudi. Kwa kumalizia nisema Waisrael toka enzi za Farao wamekuwa watu wa kunyanyasika na kuishi kwa mashaka matupu. Aliyoyafanya Hitler kwa wayahudi yalikuwa ni mwendelezo tu kwasababu biblia inamtaja mtu aitwae Haman kuamuru waisrael wote wauwawe. Warumi nao kwa miaka mingi wamewatawala wayahudi. Tukichanganya matukio yote ya kihistoria itoshe kusema Israel ni taifa lililorithi laana ya baba yao Yakobo. Misukosuko yote inayowapata ni laana. Ninaweza sema ni taifa teule kwenye upande wa laana. Ni funzo kwa sisi tulio hai tusidhulumu haki za watu. Laana yake huenda hadi kwa watoto. Chanzo cha Israel kuwa taifa la laana ni tamaa tu ya baba yao.
Uko sawa mkuu.
Yesu walimkataa Hawa Wana wa yakobo na kuwaambia nyumba yenu imeachwa Hali ya ukiwa (Empty)
Soma hapa

Luka 13:34-35 (KJV) Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga kwa mawe waliotumwa kwako, mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hamkutaka.
Angalieni, mmeachiwa nyumba yenu! Nami nawaambia, Hamtaniona tena kamwe, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Kwa mantiki hiyo hakuna taifa teule la Mungu labda Mungu wao mwingine isipokuwa wa bible. Mimi kama pharaohMtakatifu nakubaliana nawewe.

Swali dogo kwetu sisi waafrica hao ambao daily mnawaita ni taifa la Mungu mara Nchi takatifu kwahiyo Mungu wao alikuwa wapi Hadi makombora ya Hamas yakatinga kwenye ardhi takatifu kama mnavyojidanganya?
Inakuwaje basi Hilo Taifa teule litengemee msaada kutoka USA Ili Hali Lina Mungu wao ambao Hadi udongo wake mwamposa anawauzie buku kijiko Ili utatue matatizo yenu inakuaje usitatue matizo ya Wana Israel kwanza?
 
Ndgu mbona mweupe hvyo kwnye biblia.unaleta tasfiri za uongo.eti yakobo alikuwa anachunga mbuzi kwa mjomba wake'unajua malaika akambariki na akamwita israel na cyo yakobo? unajua hata milango ya kuingilia imetajwa kwa majina ya wana wa yakobo 12 ufunuo 7 na 14.unajua jina la taifa la israel imetokana na yakobo.
Luka13 :34-35 soma hapo kwanza
 
Mimi bado nashindwa kabisa kuelewa ...Sisi wazaramo ,wanyakyusa,wamatumbi tunaingia wapi kwenye hii Biblia kiasi cha kutukanana na kuwatetea hao wayahudi??

Yaani hata mtu akisema maoni yake tu kuwa hawa wayahudi wagomvi Sana basi anaambulia matusi kutoka Kwa ndugu zake wazaramo au wanyakyusa wenzake ..yote kuwatetea hawa wayahudi....

Hivi miaka 100 Tu baadae wakiibuka wazaramo wa claim Dar kwao waanze kutuhamisha tutawaelewa?

Yet eti tunawaelewa hao wayahudi wanaposema ardhi yao Kwa ushahidi WA miaka zaidi ya elfu moja iliyopita??...na Sisi wandengereko ndo tunashadadia eti eeh hao hao Taifa teule... seriously??
 
Back
Top Bottom