BUBU, angalia jinsi cheap politics inavyotumiwa na Mwakyembe. Nini lengo la kumtaja Nyerere? kupata sapoti ya wananchi wasioelewa mambo. Nafikiri kwa wewe mwelew unajuwa kuwa viwanda karibu vyote vilivyoanzishwa wakati wa nyerere tuliviua na baadae majengo tukauza. Huoni desperation ya Mwakyembe na badala yake eti unaita kuwa anasema kwa maslaha ya Taifa. Kama ni mfuasi wa Nyerere basi asingekuwa na hisa huku akiwa Mbunge. Najua kuwa hakuna tatizo kuwa na hisa baada ya sisi wenyewe kuamuwa hivyo nakwa njia hiyo hiyo najuwa kuwa hakuna tatizo la kuweka godowns kwenye majengo ya kiwanda tulichokiuwa.
Mkuu shujaa wetu kaamuwa kututelekeza na kutetea maslahi yake kwa kutumia migongo yetu.
Habari za kutoka hapa Kyela ni kwamba dr. Mwakyembe leo kamvaa Rostam kweli kweli. Kamwita fisadi namba moja, kaiba mali ya Tanzania na ni mbumbumbu, hajui kitu, hata bungeni haongei. Anasema Rostam katumia ufisadi kuiba viwanda viwili alivyoanzisha Nyerere na sasa kafanya godowns zake.
Katika mkutano wake alikuwa ameongozana na waandishi habari kutoka Mbeya baada ya wale wa Kyela kupigwa marufuku kuhudhuria mkutano huo kwa madai kwamba huwa wanamwandika vibaya.
Alitumia muda mwingi kumtukana Rostam.
Pia kasema yeye ni kweli anamiliki shares kwenye hiyo kampuni pamoja na vijana wengine kama 50 wazalendo wa nchi hii na kwamba hiyo kampuni bado haijaanza.
Anasema alipoenda Singida alishangiliwa sana na wananchi wakamwambia kama Kyela hawamtaki basi wao Singida wapo tayari kumpa ubunge.
Kuna mengi mheshimiwa kaongea ambayo mpaka mtu unajikuna kichwa, hivi kweli ni muhimu? Labda ndio siasa zetu zilipofikia sasa. Inaelekea maneno ya Malecela hawajayasikia kabisa.
Wenye taarifa zaidi mnaweza kuongea.
Kama kweli hayo yanayodaiwa kuwa Mwakyembe kasema, basi huyu jamaa atakuwa ni bonge la reckless kwa sababu kama hawezi kuyathibitisha hayo madai yake, Rostam anaweza ku counter na slander lawsuit! Mwakyembe should know better (if what is said to be said is true).
..Katika suala la kununuliwa mitambo ya Dowans Mwakyembe ametajwa na nani?
Mwakyembe ameingia kwenye mgogoro kwa kutajwa kuwa alikuwa na conflict of intererst juu ya umeme. Alijitetea na kuanzia hapo alikuwa na sapoti nzuri tu. Hata waliomakini wamejaribu kumtahadharisha lakini sikio la kufa.
Kuna tetesi ambazo nimezisikia hapa, nasema tetesi kwasababu siwaamini wanaozisema. Wanasema Dr. Mwakyembe anatafuta njia ya kuhamia CHADEMA.
Wanasema kwenye mkutano wa leo yule kijana wa CHADEMA aliyewahi kuwekwa ndani wakati ule wa ziara ya JK ndiye alikuwa mbele katika waandaaji. Pia wanataja uhusiano wa Dr. Mwakyembe na Mbowe pamoja na Mengi kama sababu za kuamini hivyo.
Pia inaelekea kuna mpambano mkali unaandaliwa Kyela 2010 kati ya Dr. Mwakyembe na jamaa mmoja nasikia yuko nje ya nchi.
Mimi nilikuwa hapa kwa muda na niliyoyaona leo sina hamu, hii wilaya imegawanyika kweli kweli. Sikuona viongozi wowote wa CCM pale mbele badala yake kulikuwa na wapambe wa mheshimiwa waliokuwa wanamwaga sifa kibao.
Angalieni hili jimbo 2010 inaelekea kutakuwa na vituko.
Halafu sijakuelewa, kumfagilia Rostam. Soma Mtanzania ya Jumapili tarehe 29-03-2009 utaona kuna uzushi pale unasema Mwakyembe aendelea kuumbuliwa pia Selelii afilisika Kisiasa hapo utajua kuna jambo
Mwakyembe inaelekea kuwa yuko so bitter...yaani vagi lake na Rostam juzi jumamosi alilihamishia kwenye fainali ya kombe la NSSF kwenye mechi ya timu ya UHURU v/s HABARI CORP.
So sad huyu jamaa nilikuwa namheshimu miaka ileee alipokuwa na kile kiofisi chao cha LEGAL AID na Dr MVUNGI pale kwenye jengo la SUKITA enzi hizo Mwakyembe alikuwa ni mtu kweli kweli sasa tangu aingie kwenye siasa amekuwa kama mwehu vile
Mpka leo sielewi what was the point ya kupandishana pesa jumamosi...lakini ndio hao wanasiasa wetu
AMA KWELI PESA MWANA HARAMU
Lakini hata kama akitambika uchi huyu mwakyembe, ukweli utabaki pale pale kuwa yeye ni miongoni mwa wale wabunge waliokula milioni 5 za Rostam wakati wa Kampeni sasa leo hii asitake kujidai yeye ni msafi kuliko wote.
In short Rostam ni kama Nyerere tena naweza kusema zaidi kwenye hii game ya Politics za TZ, Maana mwalimu yeye alikuwa ni mcheza Game kwenye politics tuu lakini Rostam ni mpaka Biashara in other words HE OWNS THE CURRENT RULING ELITES na hawana cha kumfanya baada ya kula pesa zake
So Mwakyembe should spare himself further embarrassment kuendelea kutukanana na mtu ambaye hamjibu except ana rewind ule mkanda wa makabidhiano now and then
Mwisho zaidi nasema I CANT KNOCK ROSTAM'S HUSTLE....jamaa ni mtafutaji na anaitumia opportunity anavyoona itamnufaisha
Ugonjwa wetu mnajua tatizo lake lilianzia wapi na dawa yake wote mnaijua
This is a defining moment,hilo sasa liko wazi....
kwenye chess inaitwa "check mate"!