barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Juzi kati Waziri wa Katiba na Sheria Dr.Mwakyembe alisikika kupitia kipindi kimoja cha "East Africa Tv/Radio" akilalamika jinsi alivyomshindwa Masogange katika vita vya madawa ya kulevya.Dr Mwakyembe anasema hata baada ya ushahidi wote kuonyesha kuwa "mzigo" ulipitishwa hapa Dsm kuelekea J'burg,lakini bado Masogange alimponyoka.
Anasema,baada ya muda,alihamishwa ktk Wizara hiyo na kupelekwa sehemu nyingine,kitu kilichomfanya ashindwe kuendeleza harakati za vita hiyo.Sisi tutamuamini Dr kwa yale anayoyasema,wengi wanaomfahamu wanasita kumuamini.
Lakini haya yote,hayaondoi ukweli kuwa,Dr Mwakyembe,daktari wa sheria,mwanazuoni,wakili,Waziri na Mbunge wa Jimbo la Kyela,alielemewa na Masogange mpaka akawa anamletea "nyodo".
Mjadala mkubwa aliouibua Dr Mwakyembe,ni huyo "kijana" wake aliyekuwa "anamsaidia" katika vita hivi,bahati nzuri au mbaya,licha ya kusema "kijana" wake anatakiwa alindwe huko gerezani,bado Dr aliamua kumtaja kwa jina moja la JINGU,hivyo aliotoa mwanya wa kudadisi;Huyo "kijana wake Jingu ni nani haswa?"
Dr Mwakyembe hajasema huyo "kijana" wake alifungwa kwa kosa gani hasa,yeye kama mwanasheria na waziri,ametumia njia gani za kisheria kuhakikisha huyo "kijana" wake anatoka huko gerezani?Na je Mwakyembe ana uhakika kuwa huyo "kijana" wake aliomsaidia kwa 99% ni kweli yupo huko gerezani kwa "kubambikiwa" au ni stahili yake.
Na je,kukamatwa kwake huyo "kijana" kuna uhusiano wowote na "msaada" kwa Dr Mwakyembe?Au kukamatwa kwake "kunahusishwa" tu,lakini kuna jambo lingine tofauti na "msaada" huo kwa Dr?
Clemence Jingu Mbaruck (bila shaka ndio huyu "kijana" wa Dr Mwakyembe) alikuwa Meneja wa Usalama (Manager Security) wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania.Alihudumu kwa nafasi andamizi kabla ya cheo hicho katika kitengo cha Usalama katika uwanja wa Julius Nyerere kwa muda mrefu.
Kwa maelezo ya Kamishna Rogers Sianga,moja ya mbinu kubwa ya "drug lords" ni ku-recruit watu ktk kila kitengo wanachopita ili iwe rahisi kwao kupitisha mizigo yao,kitengo cha usalama ktk viwanja vya ndege,ni moja ya "waajiliwa" wa mitandao hii.Hivyo hawa huwa na "details" za lini,saa ngapi,nani,na ndege gani itapitisha mzigo kuingia au kutoka nje ya nchi.
July 2015,mzigo wa kilo 262 wa pembe za ndovu ambao ni sawa na tembo 50 ulikamatwa katika uwanja wa ndege wa Zurich Uswis,ukiwa umetoka Dsm kuelekea China.
Mzigo huo ulikamatwa ukiwa ndani ya begi za raia wa China.Begi hizo zilipita bila kuonekana Tanzania, iwe kwa macho au kwa "Screening machine".
Soma Nyara za Serikali zawafikisha kizimbani Maafisa 4 wa TAA
Watuhumiwa wanne ambao ni wafanyakazi wa Kitengo cha Usalama wakiwemo wanajeshi watatu wa JWTZ (ambao huwa wapo attached ktk kitengo cha usalama wa kiwanja) na Manager Security Jingu walitiwa kizuizini kwa tuhuma za kuhisika kufanikisha mzigo huo kupita bila kukamatwa.
Clemence Jingu (kijana wa Mwakyembe) na wenzake waliwekwa mahabusu kwa tuhuma ya Uhujumu uchumi,na kesi yao kusomwa mahakama ya Kisutu na baadae kurudishwa rumande sbb kesi hii haina dhamana.
Mpaka leo,Jingu yupo ndani akiendelea kusota kutokana na kesi hii.Ni kesi inayotambulika kama ya "Uhujumu Uchumi" ambayo haina dhamana.Kukamatwa kwa Jingu kulitokana na nafasi yake kama "Manager Security" ambaye inaonekana (sababu mahakama haijathibitisha) alishiriki kufanikisha mzigo huo kupita bila kizuizi.
Huwezi kupita na mzigo wa kilo 262 wa meno ya tembo bila kuonekana kwa macho wala kwa mashine.Ni lazima uwe na mtandao wa maana utakaorambishwa "asali".Mtandao huu wa kuramba "asali" hauishii kwa "security officers" wanaokagua mizigo magetini tu,ni lazima ufike mpaka kwa "boss".Na pengine swali lilikuwa,"mzigo mkubwa kama huu unaweza kupita bila Manager Security kujua?"
Leo Dr Mwakyembe,wakili,Waziri na Mbunge,bila kujali usiri wa taarifa za mtoa taarifa kaamua kututajia hadharani mtu aliyekuwa anamsaidia kwa 99%.Tena kwa kumtaja ktk chombo cha habari.Lakini sidhani kama amejiridhisha kuwa kuwekwa ndani kwa "mtoa taarifa" wake ni kweli kwa sbb ya vita ya madawa ya kulevya?
Na hata kama ni hivyo,Je Dr hana namna ya kisheria iwe kwa kumuwekea mawakili au msaada wowote wa kisheria kuhakikisha "kijana" wake anatoka!?Na ana uhakika kuwekwa ndani kwa Jingu ni sbb ya "uadui wa kutoa ushirikiano wa 99%?".
Zaidi ya hapo,Dr ametuonyesha kuwa hana "kifua",inawezakana huyo "kijana" wake alikuwa anampa habari hizo sbb ni Waziri na bosi wake,sasa inakuwaje leo aamue kutaja chanzo chake cha habari kwa jina na mahali alipo?Alipoamua kumtaja Jingu hadharani,alitupa nafasi ya kudadisi;huyo Jingu "kijana" wa Mwakyembe ni nani?
Leo Masogange na washirika wake na wote waliokamatwa enzi za Mwakyembe kupitia uwanja wa JNIA,wanajua Jingu ndio aliowachoma.Hali hii ya kukosa "kifua" cha kutunza siri unazopewa ktk uwajibikaji,haiwezi kuwakatisha tamaa maafisa wengine wa JNIA katika vita hivi vya sasa?
Maana kwa kauli hii ya Dr,ni wazi kuwa hata maafisa wengine wa usalama JNIA wanaweza kuogopa kutoa taarifa kwa kuhofia siku moja huko mbele ya safari mtu atakuja kutaja chanzo chake cha habari.
Wakati tukimkumbusha Dr Mwakyembe,wakili,mbunge na waziri kufuatilia kwa kina kukaa mahabusu kwa "kijana" wake Jingu kulisababishwa na nini haswaa,pia tumkumbushe kuwa awe na tabia ya kuwa na "kifua".Kifua cha kiume hutunza siri,kifua cha kiume hakiropoki,kifua cha kiume huundwa na mifupa imara ya kustahimili kuhifadhi hata maneno ya kimbea.
Ndio maana,ni nadra sana kukuta wanaume wanasutana kwa maneno ya uwongo na umbea,sababu jadi ya wanaume wa kiafrika ni kukaaa na kufunika siri za jamii na za familia katika kifua.Dr Mwakyembe,zaidi ya udaktari wake,uanazuoni,ubunge na uwaziri;Yeye ni MWANAUME wa kiafrika.