Habari za kutoka hapa Kyela ni kwamba dr. Mwakyembe leo kamvaa Rostam kweli kweli. Kamwita fisadi namba moja, kaiba mali ya Tanzania na ni mbumbumbu, hajui kitu, hata bungeni haongei. Anasema Rostam katumia ufisadi kuiba viwanda viwili alivyoanzisha Nyerere na sasa kafanya godowns zake.
Katika mkutano wake alikuwa ameongozana na waandishi habari kutoka Mbeya baada ya wale wa Kyela kupigwa marufuku kuhudhuria mkutano huo kwa madai kwamba huwa wanamwandika vibaya.
Alitumia muda mwingi kumtukana Rostam.
Pia kasema yeye ni kweli anamiliki shares kwenye hiyo kampuni pamoja na vijana wengine kama 50 wazalendo wa nchi hii na kwamba hiyo kampuni bado haijaanza.
Anasema alipoenda Singida alishangiliwa sana na wananchi wakamwambia kama Kyela hawamtaki basi wao Singida wapo tayari kumpa ubunge.
Kuna mengi mheshimiwa kaongea ambayo mpaka mtu unajikuna kichwa, hivi kweli ni muhimu? Labda ndio siasa zetu zilipofikia sasa. Inaelekea maneno ya Malecela hawajayasikia kabisa.
Wenye taarifa zaidi mnaweza kuongea.
Mkuu kwanza karibu jamvini.
Pili inawezekana wewe ni mmojawapo wa hao waandishi kutoka Kyela? Kwasababu umesikiliza hotuba yake hiyo na kuja hapa kuweka conclusions zako,ingekuwa jambo la maana kama ungetuwekea hapa hotuba hiyo na sisi tu ijudge accordingly.
Mwakyembe siyo mjinga kiasi mnachodhani,CCM wamebweteka na wananchi wanatakiwa walijuwe hilo,halafu eti mkuu wa nchi anatoa pongezi juzi hapa kuwa eti kwa Mama Kilango kwasababu ya vita dhidi ya ufisadi,yani ccm wapumbavu wana acknowledge kwamba kuna ufisadi na mafisadi,na kuna vita dhidi ya mafisadi ambao wako ndani ya chama,lakini ikifikia wakati wa kuzungumzia kuhusu ufisadi huo na kuwazungumzia mafisadi hao,wao ni wa kwanza kudai ushahidi. na kuitana kwenye vikao vya chama. Hivi ndugu zangu mnatoa wapi balls za kuzungumza upupu kama huo? Mnadai ushahidi na wakati huo huo mlisha acknowledge kuwa kuna ufisadi?Mwakyembe si mjinga na ccm mtafikia mahali mchague kati ya mafisadi na wazalendo,katika political situation ya sasa kama kuna watu wanafananisha situation ya Mwakyembe na Mrema basi ni ccm waliopofushwa macho na ufisadi kiasi cha kushindwa kuona kama ufisadi wenyewe upo....Ufisadi Umekuwa halali na ndio maana ni mazungumzo tu...Kama kuna watu wanamtetea RA kwasababu hajapelekwa mahakamani na huku wakijua mizizi ya ufisadi ilivyo ndani ya ccm basi hao hawana nia njema na Taifa na ndio maana hata bado tunaendelea kutawaliwa na no wonder tulifanywa watumwa kiurahisi na bado sisi ni kama watumwa tu, especially kifikra! Yani RA ni malaika kwasababu kuna wanaodai kuwa kaonewa na mswahili ambaye yeye ndiyo anataka kuwa na pesa kama RA,ROHO KOROSHO YA KITUMWA NA FIKRA FINYU,Kwasababu ni mswahili,kuna watakaotamani hata kumtoa roho mswahili mwenzao kwasababu si utamaduni wetu sisi miafrika kufurahia maendeleo ya wenzetu,kama ni mzungu ama mwarabu wala hakuna atakeyejiuliza. Mwakyembe anatolea mfano wa viwanda ambavyo viliuwawa na mafisadi halafu kuna wanaodai eti ni cheap popularity kwa kumtaja mwalimu....Wananchi wamedharauliwa mpaka mwisho na tuna vibaraka watumwa wa akili wanaozidi kutufukarisha...La ajabu ni kwamba kuna wanaoheshimika kuwa ndio wasomi wengi sana hapa JF lakini ndio hao hao current days Mangungo,haingii akilini kabisa kusahau ufisadi wote wa kina RA kwasababu tu eti kuna wanaodai hayo mambo yamalizwe ndani ya chama ambacho ndicho mwanzilishi na mlezi wa mafisadi na ufisadi...Mtavutana sana nyie ccm lakini siku ya kufa nyani miti yote huteleza....Na kama nyie mnaojidai kuwa ni wastaarabu sana kwa kuendelea kuzikumbatia sheria za kifisadi kwa kuzitumia loopholes ni wazi hamtaki mabadiliko na chama chenu cha mafisadi ni kigumu kwa wazlendo wa kweli wanaotaka mabadiliko ya kweli...Tatizo ni kwamba wengi wamebakia kwenye upuuzi ule ule wakidhani mambo ni yale yale...Kama mama Kilango alisema mambo hayo yalishamalizwa bungeni,halafu mme wake naye anakuaja na kudai yakamalizwe ndani ya chama..Then wapi utofauti kati ya maslahi ya Taifa na ya chama?
Ufisadi umeanzia ndani ya chama,na licha ya ccm kukubali kuwa ufisadi huo upo,hakuna aliyechukuliwa hatua zozote za kichama ili kuweza kusema kweli wanapiga vita ufisadi.
Kuna kauli nyingine za kipuuzi kuwa eti MK anatumia issue ya ufisadi,hili neno "Ufisadi" mmeshalifanya lionekane kama ni sifa nzuri na ndio maana mna brush off,wananchi wanatakiwa wasisahahu kuwa ufisadi ndio rushwa na machafu yote yanayotufanya masikini hadi leo,sasa hilo lisipokuwa the maini issue then si ni sawa na kujaza maji kwene gunia?
This is a defining moment,hilo sasa liko wazi...Tusubiri tuone wananchi watakavyoamua coming 2010, maana kelele zetu hapa JF hazisaidii kama wananchi hawatafanya mabadiliko kwasababu kama kuna watetezi wa wazi wazi wa ufisadi,then ni wananchi wamewapa nguvu hizo watu hao...Wananchi wakiwapa ccm fundisho kwa kutowachagua next time,then watajiuliza mara mbili mbili kabla ya kuzungumza ama kufanya maamuzi yenye kutetea ufisadi.....Sijui sana kuhusu huko mitaani kwamba maoni hasa ya wananchi wa kawaida ni yapi hayo,najua wananchi wa kawaida hapo bongo hawana access ya internet na sidhani kama mawazo yao ni swa na ya wanaotetea mafisadi humu ndani,hata hivyo kipimo kikuu ni hapo 2010.