Kwa maana hiyo hata wewe ukipata nafasi ya kuihujumu hii nchi utaikamua mpaka damu ya mwisho kama anavyofanya huyu fisadi Rostam?
1)wapi nimesema Rostam anahujumu nchi?
2)kama ni fisadi au la hiyo ni kazi ya vyombo vya sheria na hakuna chombo hata kimoja kilichomshitaki au kumhukumu
Ama kweli nchi hii watu wengi wameoza na akili zao ni kutafuta mali kwa namna yoyote ile. Rostam ni mmoja wa watu wanaochangaia kuharibu uchumi wa nchi hii na kuendelea kuweka mzigo mzito juu ya wananchi wa kawaida wanaoishi kwa kubangaiza.
1) kuna ubaya gani watu kutafuta mali kihalali?
2) kachangia kuharibu uchumi wa Tanzania kivipi?
Tuna huduma mbovu mahospitalini na miundo mbinu mibovu ya umeme na barabara kisa kuna watu wana matrilioni ya pesa kwenye akaunti zao huku wakiwa na uraia wa nchi tatu kama Rostam.
1)kuna ubaya gani mtu kuwa na na matrilioni kwenye akaunti?
2)Hospitali kukosa dawa, mtaro wa haideri plaza kutozibwa,posta mpya kunuka maji machafu na wananchi kukosa maji safi ni majukumu ya Rostam pia?
3)Lete ushahidi kuwa Rostam ana uraia wa nchi tatu
4)Zitaje na namba zake za uraia wa nchi hizo
Jua ya kuwa mtu anapokuwa na uraia wa nchi zaidi ya moja na huku ana mapesa lukuki kama Rostam mtu huyo ni jangili wa kutupwa na anapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote.
1) Rejea majibu yangu hapo juu
2)Lete ushahidi kuwa Rostam ni Jangili
3)Je Mengi naye ni Jangili kwa sababu ana pesa luluki?
Tangu lini mwarabu na mhindi akawa na uchungu wa kuona maendeleo kwenye nchi za Kiafrika?
1)Prof Issa Shivji ni mhidi je hana uchungu na Tanzania?
2)Kuwa na uchungu na nchi lazima uwe na ngozi nyeusi kama Grey Mgonja?
Wengi wapo kwa maslahi yao binafsi na kwa ndugu zao walioko India, Canada na Uarabuni.
1)kuna ubaya gani kuwa na ndugu India,Canada na Uarabuni?
2)kuna ubaya gani kuwa na maslahi binafsi?
Waangalie watu kama akina Manji na Dewji wanatoa pesa zao kwenye klabu za mpira kama na kulipia watu waingie bure kwenye mpira mamlioni ya pesa,
1)ushasahau kuwa hapo juu lisema hivi:
Tangu lini mwarabu na mhindi akawa na uchungu wa kuona maendeleo kwenye nchi za Kiafrika?
2)Kwa hiyo kuwaingiza watu mpirani bure ndio kigezo chako kikubwa cha kuwa mtu anafaa?
Akina Somaia wanachangia uchanguzi wa UVCCM milioni 400 lakini na wanajua namana ya kuzirudisha pesa zao iwe ni kwa kukwepa kulipa kodi au "deals" chafu za kibiashara lakini hawachangii miradi yoyote ya maendeleo.
Kalaghabaho
Lete ushahidi kuwa Somaia kakwepa kulipa kodi