Ninahofu hiyo tetesi ni ya kweli na hili la Mwakyembe linafanana kidogo na la Muhunzi wa CUF kule Pemba alieamuwa kutafuta sapoti ya CCM kwa kuenda kinyume na msimamo wa chama chake. Naye Mwakyembe anapuuza wito wa chama chake juu ya kukashifiana. Huyu Mwakyembe amekuwemo ndani ya CCM na kuibeba na sera zake za Ufisadi kwa kipindi chote huku akielewa kuwa chama chake kina mafisadi na hata huko kuingia kwao madarakani kulikuwa kwa ufisadi.
Zengwe la Richmond lilikuwa kafara yake na alikubali kutumiliwa na kundi moja la CCM huku akitegemea kuwa atakuwa salama. Matokeo yake ni uhasama na kila mmoja ameruka kivyake na kumuacha yeye mgeni na kwa kuelewa hili ameshajitambuwa kuwa yeye kwa CCM hana chake 2010 na hivyo hasira zake ni kuenda mrama na wengine na bado tutasikia mengi ya kuichafua CCM kutoka kwa Dr kabla hajafukuzwa au kuacha CCM na kujiunga na CHADEMA. Wasiwasi wangu kuwa kutokana na makundi tayari kwao sijui kama hata akigombea kwa kupitia upinzani kama atafanikiwa.
- Good analysis, unless Mwakyembe ana ni aya kujiunga na upinzani, then anayoyafanya sasa makes sense, lakini kama ni kubali CCM na kwenda kinyume cha maagizo ya chama chake sijui ni strategy gani anayoifikiria,
- Kama lengo lilikuwa kupingana na ufisadi, then unasema exactly how Rostam stole our money, lakini anamiliki baada ya kuiba viwanda viwili vilivyoanzishwa na Mwalimu, that is all?
- I mean kama sio njia za kifisadi kutumika Mwakyembe angekua bado yuko kule chuoni anachora chaki ubaoni, angekua bado bubu kule EAC, hapendi ufisadi aseme yote, sasa akishaanza kuwakaidi hata waliomfikisha alipo inakuwa vigumu sana wengine kumuelewa analenga nini? Na wapi?
- Ndio maana ninasema ninamuona akihamia upinzani, kwa sababu akienda mbele ya CCM, ni nani atakayemuunga mkono kiongozi aliyekaidi maagizo ya CCM? Hata Chadema walipomuambia Wangwe asubiri vikao, alipogoma walimsimamisha uongozi, sasa why is Mwakyembe doing this tunashindwa kupata jawabu,
- Labda anatafuta sympathy na wananchi, lakini bila kusema legally what is his or our case against Rostam, hatusaidii wananchi na taifa ingawa sio siri anapata cheap popularity kama ya Mrema mwanzoni alipotoka CCM, unless anatayarisha political gorund work ya kuingilia upinzani then it makes sense anyoyafnya sasa hivi.
- Ukweli ni kwamba after this Mwakyembe amewaweka pabaya sana wale wote viongozi muhimu wanaom-support kwa chini chini, na hata publicly kwa sababu sioni anacholenga zaidi tu ya kuingia upinzani, watamsaidiaje kwa kumshambulia kiongozi mwenziwe ambaye hajawahi kumshambulia hadharani zaidi tu ya kujibu tu mashambulizi yake last time tena kwa one sentence?
- Hapa ninaacha wazi scenario moja tu ambayo imewahi kutumika in the past, kwamba is Muungwana behind him? Kwamba do it ili niwatose kina Rostam kwenye uchaguzi ujao? Hii scenario ni very attempting, lakini can Muungwana pull urais bila Rostam and the gang? Ili atafute urais na nani? Majuzi kwenye matatizo ya UV-CCM Muungwana took Nchimbi's side against his son over Isaack aliyekuwa katibu wa muda wa umoja huo,
- Na ni jana amemteua Isaack Nchimbi's man kuwa DC, kwenye uchaguzi wa uwt wote yaani Muungwana na Rostam's gang walikuwa one side ya Auntie Sophia, eti sasa Muungwana anataka kuwageuka wenzake kwa kumtumia Mwakyembe? Wengine mnisaidie kufikiri, lakini until nitakapopata the inside bado ninaziamini hizi scenario mbili, na ni mawazo yangu tu!
1. Mwakyembe anataka kujiunga na upinzani, hii ninaipa 90%.
2. Muungwana anamtumia ku pull a monkey over Rostam and the gang 10%.
Wazee wa sauti ya umeme FMES!