Kyela: Dr. Mwakyembe amtolea Uvivu Rostam

Kyela: Dr. Mwakyembe amtolea Uvivu Rostam

Kama huyo Rostam ni mchafu kama inavyodaiwa, na ushahidi upo. Sasa kwa nini hapelekwi mahakamani?

I'm afraid there is no smoking gun type of paper trail directly linking Rostam to any of the purpoted ufisadi.
 
Heee! Ng'waniyami, hukusikia viongozi wa ngazi za juu akiwemo PM akisema kuwa Kagoda wakifikishwa mahakamani nchi itatikisika? Halafu kumbuka JK yuko mikononi mwa huyu fisadi, yeye na EL ndo walioratibu shughuli yote ya kumweka madarakani na huenda wanajua siri zake nzito ndo maana hachukuliwi hatua yoyote. Fahamu hilo ndugu yangu.
 
Big up mwakyembe washambuliye mafisadi hadi wasalimu amri,pambana nao ndani ya CCM hadi ibakie CCM ya 1977.
 
I refuse to believe that this Rostam guy has everyone wrapped around his finger. Something is telling me that he's not what he's cracked up to be and that some folks may throw blame to him just to cover their own behinds and divert attention away from them. Really, it just doesn't make any sense to me at all. How can one person be mentioned or have his name surface in just about every recent major scandal? How can that be?
 
To give you a vague example: When a ring leader of a notorious armed group is caught, the group shakes! Rostam may be an icon for corrupt businessmen and leaders in our country...so if he goes down, others may follow.
 
Huu ndiyo unafiki wetu Watanzania anaposimama mtu kutaka kupambana na mafisadi tunamgeuzia kibao na kumuona yeye mbaya badala ya yule mbaya wetu wa kweli. Rostam kahusika na wizi wa mapesa ya EPA kupitia Kagoda wa shilingi bilioni 40, lakini hadi hii leo hajaguswa kwa kisingizio cha hakuna ushahidi wa kutosha. Rostam kahusika na kashfa ya Richmond kwa kutudanganya Watanzania kwamba kampuni yake ilikuwa na HQ Houston, Texas na wana utaalamu katika kuzalisha umeme kumbe ilikuwa ni kanyabwoya tu. Amelipwa bilioni 200 bila kuzalisha hata tone la umeme na juzi karibu aiuze mitambo yake michakavu kwa shilingi bilioni 60 kinyume na taratibu za manunuzi serikali. Kama siyo Watanzania kuja juu basi mitambo hiyo ya kanyabwoya ingenunuliwa kwa hiyo 60 Billioni na Rostam kuendelea kuwafanya Watanzania kama kichwa cha mwendawazimu. Sasa yeye hapa ndiyo anaonekana shujaa na kuanza kutetewa!!

Ama kweli Waafrika ndivyo tulivyo!!!! wizi wa bilioni 240 uliofanywa na fisadi Rostam (Richmond 200 bilioni na Kagoda 40 billioni) Anatokea mtu anapambana na na Rostam bila woga, yeye ndiye anaonekana mbaya kwamba eti kajiharibia!!!!! Siku yoyote nitamthamini mtu ambaye anaweka mbele maslahi ya Watanzania mbele bila kujali maslahi yake mwenyewe hata kama kufanya hivyo kunaweza kabisa kukaharibu hadhi yake ndani ya chama cha mafisadi. Chenge fisafi bado anapeta ndani ya chama, Mramba fisadi bado anapeta ndani ya chama, Lowassa fisadi bado anapeta ndani ya chama, Karamagi fisadi bado anapeta ndani ya chama lakini leo hii Mwakyembe ndiyo anaonekana mbaya ndani ya chama na machoni mwa baadhi ya wanachama hapa jamvini!!!! Ama kweli tenda wema uende zako!!!! lakini history haidanganyi inawezekana kabisa ndani ya chama Mwakyembe akaonekana ni mkorofi lakini miongoni mwa Watanzania wengi tuliochoshwa na unafiki na ufisadi uliokithiri ndani ya CCM na Serikali siku zote tutauheshimu mchango wake katika vita dhidi ya mafisadi.

Unafiki uliokithiri miongoni mwa Watendaji wa juu wa ndani ya chama na Serikali ndiyo unaifanya Tanzania kuwa katika hali mbaya kama tuli nayo. Sijamsikia Chiligati wala huyo Malecela wakikemea ufisadi uliokithiri ndani ya chama na serikali ukiwemo ule uliofanywa na Mkapa wa kujiuzia mgodi wa Kiwira wenye thamani ya shilingi bilioni 7, kwa shilingi milioni 700 tu ambayo ni 10% ya thamani ya mgoni na hadi hii leo alicholipa Mkapa ni shilingi 70 milioni tu ambayo ni 1% ya thamani ya mgodi huo!!!! Mgodi unakufa hauzalishi chochote wafanyakazi wanahaha hawana mishahara miezi minane sasa lakini wanafiki na watetezi wa mafisadi ndani ya CCM hawajatoa kauli yoyote kuhusu mgodi huo!!!! Rais wa nchi naye yuko kimya kuhusu mgodi huo ambao unakufa taratibu huku wanafiki wakiogopa kumgusa Mkapa ambaye alijipatia mgodi huo kwa njia za kifisadi, lakini leo hii wako tayari kutumia makucha yao dhidi ya Mwakyembe!!!!!!! Mungu inusuru Tanzania!!!

Bubu naona unazikataa hoja na kuleta ushabiki kwenye majadiliano. Lengo letu ni kupashana ukweli na hatutokua tayari kuona kuwa imani yetu kwa mtu anatumia kwa manufaa yake.
Mwakyembe ni msomi mzuri ambae angekuwa na njia nzuri za kuonyesha ubaya wa Rostam na angefanya hivyo kabla hajaguswa nae. Unataka kutwambia nini kama baada ya kufichuliwa siri ya kumiliki utajiri wa kutia mashaka ndipo anapokurupuka na kuanza kusema maBAYA AMBAYO ANAYAJUA. kWANGU NISE NA ELIMU NINAFAHAMU KUWA SASA HAPIGANII MASLAHA YA TAIFA BALI ANAPIGANIA MASLAHI YAKE.

BUBU unasema utamtetea anaepigania vita vya ufisadi na kusema kuwa RA katuibia 40 billion lakini tunajuwa pesa hizo kazipeleka wapi. Kazipeleka katika kumsimika Mwakyembe na wenziwe katika Bunge letu na serikali yetu. Sasa huyu Mwakyembe yeye anakuwa tofauti na wengine kwa namna gani? Haramu haizai halali na kwa maana hiyo Mwakyembe kwa kubebwa na RA kufikia Ubunge akubali kuwa si msafi kwani kafika pale kwa majitaka.
Halafu BUBU mwizi ni mwizi tu na wala sio kweli kuwa tunaowaita wazalendo hawaweki pesa nje jee Chenge ana nwele za singa? Mwizi ni mwizi hata akiwa nani na kwa hivyo tutamzungumza RA kwa ubaya wake na tutamzungumza Mwakyembe kwa kupotoka kwake na wala hatupendellei kwani majambazi hayatoki uarabuni.
 
Let us think out of box Wakuu! G. T has a point

1: GT hajasema kwamba RA si Fisadi
2: GT anasikitishwa na namna Mwakyembe anavyolipeleka hili suala, siyo standard ya Mwakyembe.
3: Ili Mwakyembe aeleweke ni Lazima aache kuzungumzia Watu, azungumze Ishu, Atueleze ni nini alikificha kwenye Kamati ya Richmond ambacho kingeiumbua Serikali.
4: Mwakyembe anaogopa Kivuli chake Mwenyewe, kama ni GHOST alilitengeneza mwenyewe kwa kutolizungumzia kwenye kamati yake, sasa linamsumbua.

Nadhani Mwakyembe alikuwa anajaribu ili aone CCM itamfanya nini RA, baada ya kukugundua kumbe hata CCM haimuwezi ( Ndiyo maana akina Malecela wamemung’unya Maneno) sasa hana pa kuegemea ameamua kutumia kivuli cha Uzalendo na Ka Umaarufu alikokapata kwenye Ishu ya Richmond kujikinga.

Ushauri wangu:

Too Much speaking expose your Ignorance na Mgema ukimsifia Tembo atalitia Maji, Kaa Kimya Dr.
 
Tushaongea sana kuhusu mapungufu ya Mwakyembe kwenye thread ya press conference yake, sasa kuwa fair Rostam naye inabidi amulikwe ipaswavyo.

Wote wana mapungufu, lakini in the grand scheme of things Rostam ni tishio kubwa kama Tsunami wakati Mwakyembe ni upepo wa kupetea pepeta.
 
Wana JF,

Kutokana na habari za uhakika ni kuwa:-
Mwakyembe alibebwa na watu wengi sana kuwa pale alipo. Siku hizo alikuwa mtu mwenye akili sana na mawazo mazuri sana. Alisikiliza watu na kuchukua ushauri wao. Hii ilimsaidia sana kuwa mbunge na mtu mashuhuri. Mara baada ya kuwa MBUNGE ndipo Mwakyembe mtu akawa amezikwa na Mwana siasa akazaliwa. Akafanya mambo ya Bush kuwa ama uko na mie ama hauko na mie. Ukijifanya wee ni mtu neutral basi wewe pia unakuwa adui yake. Washauri wake wote akawazika hai katika kaburi la SAHAU. Wengine walikuwa ni wafanyabiashara wasiojali nani ni mbunge wao yaani wanakula huku na huku kama Mengi. Yeye hawa wote wakawa maadui zake wakubwa.

Biada ya miaka 4, muda umefika wa kurudisha makaratasi ili WAHASIBU wakuchambue umeifanyia nini taranta yako ya miaka 5 uliyopewa. Akiangalia mbele, nyuma, kushoto9 na kulia anakuta ile timu iliyomuweka pale yote kashaitibua, kaisaliti. Walimsihi asifanye hivyo, yeye akaona wanachemka na yeye ni MSOMI. Msomi kama yeye hawezi kuhangaika na wazee walioishiwa (Kama Malecela vile). Wazee wakaja kuwa vibosile tena na jamaa akawa analialia.

Nafikiri Dr Mwakyembe angelifaa ajifunze kutoka kwa RA. Rostam yule yeye anacheka na kila mtu. Wee mtukane tu ila baadaye anacheka na wewe na kama vile hakijafanyika kitu ila ukikaa vizuri kwenye anga zake, timu yake INAKULIMA.

Anavyofanya sasa, hata CHADEMA itabidi wamteme. Itakuwa kama wanamleta Wangwe mpya ndani ya CHADEMA. Itakuwa ni kuhesabu tu siku kabla jamaa hajaanza kurusha maugomvi yake ya magambo. Wahaya wanasema "USIJIGAMBE MBELE YA WAGAMBIRWA".

Mwakyembe, tafuta wapi ulipoangukia na nenda ukatubu......... Usipopaona au ukifikiri bado umesimama basi kweli umeishiwa. Wapambe wake mwambieni Dr, umeanguka chini sana. Hii FMes kaielezea vizuri sana. Fuateni wosia wake na msaidieni Dr. Vinginevyo ni kuwa MWAMPAKA MAFUTA NA MGONGO WA CHUPA. Atajiona Babu K. kumbe "wamhogo" yaani WAPIII!!!!!

Nakuachia huu wimbo wa Gambler, unaoasa watu wajue muda wa kukimbia meza ya kamali. Vinginevyo ujuwe wee si mcheza kamali wa kwelikweli.

YouTube - Kenny Rogers - The Gambler

.......eti nini?.........ajifunze kutoka kwa RA.....halafu aende "KUTUBU"!!! (wow.......thats incredible!!).........inaelekea wamfahamu vyema sana huyu RA.........."RA anacheka na kila mtu........"

duuh aisee.....mafisadi kiboko
 
Tushaongea sana kuhusu mapungufu ya Mwakyembe kwenye thread ya press conference yake, sasa kuwa fair Rostam naye inabidi amulikwe ipaswavyo.

Wote wana mapungufu, lakini in the grand scheme of things Rostam ni tishio kubwa kama Tsunami wakati Mwakyembe ni upepo wa kupetea pepeta.

Umenena vyema Kiranga, Rostam ni Tishio kubwa kama Tsunami, sasa Jambo la Msingi ni Kuangalia ni kwa Namna gani tunapambana na huyu mtu, but kwa Approah hii ya Mwakyembe na Ukimya wa Rostam obvious unampa credits adui yako.

Kama ana ushahidi wa kutosha isitoshe yeye alikuwepo kwenye Kamati ya Richmond atuambie basi nini hakikusemwa. Kama akiendelea kukaa kimya sisi tumweke katika kundi gani sasa. Apunguze Munkari
 
- Rostam sio tishio tumeruhusu njaa yetu kwua tishio letu, sasa kama kawaida yetu tunajaribu kutafuta mchawi kila mahali badala ya kujiangalia sisi wenyewe, ni njaa yetu ndio tishio letu!

- Mama Clinton, majuzi amesema nini Mexico, ni tatizo lao US la kubwia unga sana ndio maana mpakani kuna matatizo, simple and clear tujiangalie wenyewe kwanza!

FMES!
 
Huu ndiyo unafiki wetu Watanzania anaposimama mtu kutaka kupambana na mafisadi tunamgeuzia kibao na kumuona yeye mbaya badala ya yule mbaya wetu wa kweli. Rostam kahusika na wizi wa mapesa ya EPA kupitia Kagoda wa shilingi bilioni 40, lakini hadi hii leo hajaguswa kwa kisingizio cha hakuna ushahidi wa kutosha. Rostam kahusika na kashfa ya Richmond kwa kutudanganya Watanzania kwamba kampuni yake ilikuwa na HQ Houston, Texas na wana utaalamu katika kuzalisha umeme kumbe ilikuwa ni kanyabwoya tu. Amelipwa bilioni 200 bila kuzalisha hata tone la umeme na juzi karibu aiuze mitambo yake michakavu kwa shilingi bilioni 60 kinyume na taratibu za manunuzi serikali. Kama siyo Watanzania kuja juu basi mitambo hiyo ya kanyabwoya ingenunuliwa kwa hiyo 60 Billioni na Rostam kuendelea kuwafanya Watanzania kama kichwa cha mwendawazimu. Sasa yeye hapa ndiyo anaonekana shujaa na kuanza kutetewa!!

Ama kweli Waafrika ndivyo tulivyo!!!! wizi wa bilioni 240 uliofanywa na fisadi Rostam (Richmond 200 bilioni na Kagoda 40 billioni) Anatokea mtu anapambana na na Rostam bila woga, yeye ndiye anaonekana mbaya kwamba eti kajiharibia!!!!! Siku yoyote nitamthamini mtu ambaye anaweka mbele maslahi ya Watanzania mbele bila kujali maslahi yake mwenyewe hata kama kufanya hivyo kunaweza kabisa kukaharibu hadhi yake ndani ya chama cha mafisadi. Chenge fisafi bado anapeta ndani ya chama, Mramba fisadi bado anapeta ndani ya chama, Lowassa fisadi bado anapeta ndani ya chama, Karamagi fisadi bado anapeta ndani ya chama lakini leo hii Mwakyembe ndiyo anaonekana mbaya ndani ya chama na machoni mwa baadhi ya wanachama hapa jamvini!!!! Ama kweli tenda wema uende zako!!!! lakini history haidanganyi inawezekana kabisa ndani ya chama Mwakyembe akaonekana ni mkorofi lakini miongoni mwa Watanzania wengi tuliochoshwa na unafiki na ufisadi uliokithiri ndani ya CCM na Serikali siku zote tutauheshimu mchango wake katika vita dhidi ya mafisadi.

Unafiki uliokithiri miongoni mwa Watendaji wa juu wa ndani ya chama na Serikali ndiyo unaifanya Tanzania kuwa katika hali mbaya kama tuli nayo. Sijamsikia Chiligati wala huyo Malecela wakikemea ufisadi uliokithiri ndani ya chama na serikali ukiwemo ule uliofanywa na Mkapa wa kujiuzia mgodi wa Kiwira wenye thamani ya shilingi bilioni 7, kwa shilingi milioni 700 tu ambayo ni 10% ya thamani ya mgoni na hadi hii leo alicholipa Mkapa ni shilingi 70 milioni tu ambayo ni 1% ya thamani ya mgodi huo!!!! Mgodi unakufa hauzalishi chochote wafanyakazi wanahaha hawana mishahara miezi minane sasa lakini wanafiki na watetezi wa mafisadi ndani ya CCM hawajatoa kauli yoyote kuhusu mgodi huo!!!! Rais wa nchi naye yuko kimya kuhusu mgodi huo ambao unakufa taratibu huku wanafiki wakiogopa kumgusa Mkapa ambaye alijipatia mgodi huo kwa njia za kifisadi, lakini leo hii wako tayari kutumia makucha yao dhidi ya Mwakyembe!!!!!!! Mungu inusuru Tanzania!!!

Master BUBU nahisi unafiki upo upande wako kwa hili. Inaonyesha wazi kuwa kilichoonyshwa kwenye posting ni cha kweli na umekielewa lakini kwa utashi wako unakimbia hoja na kuleta suala la uzalendo vs unaowaita si wazalendo.
Cha msingi katika majadiliano yetu ni kuangalia matendo ya watu kwa mustakabali wa manufaa ya wote na kwa matiki hiyo iwe Mwarabu au msukuma hana haki ya kujinufaisha kw jasho letu.
Tukija kwenye ishu yenyewe ni kuwa mpaka sasa tumeshindwa kuestablish ushahidi kamili wa kumuhusisha RA na Richmond, Dowans, EPA na Kagoda lakini tumeweza kusikia kutoka mdomoni mwake Mwakyembe kuwa ana mradi. Sawa mradi unaweza kuwa wa manufaa kwa Taifa lakini pengine utaratibu wake uliotumiwa si sahihi na pengine hii ndio sababu kubwa ya kumfanya Mwakyembe afiche kuhusika kwake. Kwanini afiche na kuanza kutowa kauli za kubadilika badilika, mara mradi wenyewe hauna fedha mara nimeshauza hisa mara anamiliki yeye na wazalendo wengine na mengine chungu nzima. Kwangu mie kumsikia mbunge sio mfanyabiashara akimiliki hisa za billioni 1.5 ni mshituko. Nashindwa kuelewa kuwa Mwakyembe huyu na ushujaa wake kumbe ni bepari na najiuliza chumo hilo alilipatia ndani ya Bunge au nje ya Bunge.Kama ilikuwa nje ya Bunge na akaamuwa kuingia Bungeni kwa kutumia Chama kilichotumia fedha za umma kuingia madarakani basi hana tofauti na fisadi mwenziwe RAna iwapo kipato hicho amekipata akiwa Bungeni sioni kama yuko kule kwa maslaha ya wengine bali kwa maslaha yake binafsi.
Kumkingia kifua Mwakyembe eti ni mzalendo dhidi ya tunaemwita si mzalendo nina hofu kuwa sitosimama hapo na badala yake nitampendelea mtu wa jimbo langu dhidi ya wa jimbo jengine ndani ya Tanzania na hivyohivyo kumpendelea mtuwa dini yangu ,baadae kabila langu. Nafikiri hatuwajadili watu kwa wasifu wao bali kwa vitendo vyao. Hapa hatuchagui Miss Bantu.
 
Mkuu kitu gani ambacho hujaelewa mbona hakuna utata wowote. Kama umefuatilia mjadala huu kwa makini majibu yote yapo wazi hakuna shida inayoonekana kwa Dr. Mwakyembe kama unavyodai. Hakuna anacho kificha kashakiri anamiliki hiyo kampuni hatahivyo kauza share zake na uthibitisho wa doc sasa shida ipo wapi. Niukweli kampuni haijaanza kazi hakuna maslahi binafsi hapo tusimtafutie sababu
 
Kama Rostam ni Fisadi ,Mwizi,mbadhirifu,mtoa rushwa,mzuia maendeleo na kadhalika mbona mpka leo hakuna ushahidi uliopelekwa mahakamani kumhukumu?

Mbona wametinga akina Yona na Mgonja lakini Rostam hajatinga?

Kwa sababu Tanzana tunacho kitu kinaitwa RULE OF LAW na hakuna anayesema iko perfect lakini tuhuma hizi mnazozitoa humu kwenye internet na zikawa zinakuwa picked na print media ni nothng but innuendos....msitake kuniambia kuwa hatuna Polisi, PCCB,Special branch,DPP,MAHAKAMA zetu na kadhalika ambazo baada ya kutazama ushahidi (kama upo) kuwa Rostam ni mwizi wa pesa za umma au fisadi then atahukumiwa lakini si kuambiana kuwa fulani mwizi bila kuwa na ushahidi wowote uliopelekwa mbele ya vyombo vya sheria

Tatizo lililopo JF ni nothing but POLITICS OF ENVY ambazo at most zinachanganywa na lots of ignorance about basic facts about presumption of innocence until proved otherwise...nimeuliza swali hapa nionyesheni kesi hata moja ambayo Mahakama zetu za sheria zimemhukumu Rostam kuwa ni Fisadi na mmeshindwa kuniletea
 
- Rostam sio tishio tumeruhusu njaa yetu kwua tishio letu, sasa kama kawaida yetu tunajaribu kutafuta mchawi kila mahali badala ya kujiangalia sisi wenyewe, ni njaa yetu ndio tishio letu!

- Mama Clinton, majuzi amesema nini Mexico, ni tatizo lao US la kubwia unga sana ndio maana mpakani kuna matatizo, simple and clear tujiangalie wenyewe kwanza!

FMES!

...ni tatizo la serikali yenu ya CCM,tunaomba muachie ngazi kazi imewashinda maana umaskini na rushwa vinaongezeka kila siku,tafadhari mjiuzuru maana kwenye uchaguzi hatuwawezi maana hatuna tume wala polisi na kura za kununua!
 
Mkuu kwanza karibu jamvini.
Pili inawezekana wewe ni mmojawapo wa hao waandishi kutoka Kyela? Kwasababu umesikiliza hotuba yake hiyo na kuja hapa kuweka conclusions zako,ingekuwa jambo la maana kama ungetuwekea hapa hotuba hiyo na sisi tu ijudge accordingly.

Mwakyembe siyo mjinga kiasi mnachodhani,CCM wamebweteka na wananchi wanatakiwa walijuwe hilo,halafu eti mkuu wa nchi anatoa pongezi juzi hapa kuwa eti kwa Mama Kilango kwasababu ya vita dhidi ya ufisadi,yani ccm wapumbavu wana acknowledge kwamba kuna ufisadi na mafisadi,na kuna vita dhidi ya mafisadi ambao wako ndani ya chama,lakini ikifikia wakati wa kuzungumzia kuhusu ufisadi huo na kuwazungumzia mafisadi hao,wao ni wa kwanza kudai ushahidi. na kuitana kwenye vikao vya chama. Hivi ndugu zangu mnatoa wapi balls za kuzungumza upupu kama huo? Mnadai ushahidi na wakati huo huo mlisha acknowledge kuwa kuna ufisadi?Mwakyembe si mjinga na ccm mtafikia mahali mchague kati ya mafisadi na wazalendo,katika political situation ya sasa kama kuna watu wanafananisha situation ya Mwakyembe na Mrema basi ni ccm waliopofushwa macho na ufisadi kiasi cha kushindwa kuona kama ufisadi wenyewe upo....Ufisadi Umekuwa halali na ndio maana ni mazungumzo tu...Kama kuna watu wanamtetea RA kwasababu hajapelekwa mahakamani na huku wakijua mizizi ya ufisadi ilivyo ndani ya ccm basi hao hawana nia njema na Taifa na ndio maana hata bado tunaendelea kutawaliwa na no wonder tulifanywa watumwa kiurahisi na bado sisi ni kama watumwa tu, especially kifikra! Yani RA ni malaika kwasababu kuna wanaodai kuwa kaonewa na mswahili ambaye yeye ndiyo anataka kuwa na pesa kama RA,ROHO KOROSHO YA KITUMWA NA FIKRA FINYU,Kwasababu ni mswahili,kuna watakaotamani hata kumtoa roho mswahili mwenzao kwasababu si utamaduni wetu sisi miafrika kufurahia maendeleo ya wenzetu,kama ni mzungu ama mwarabu wala hakuna atakeyejiuliza. Mwakyembe anatolea mfano wa viwanda ambavyo viliuwawa na mafisadi halafu kuna wanaodai eti ni cheap popularity kwa kumtaja mwalimu....Wananchi wamedharauliwa mpaka mwisho na tuna vibaraka watumwa wa akili wanaozidi kutufukarisha...La ajabu ni kwamba kuna wanaoheshimika kuwa ndio wasomi wengi sana hapa JF lakini ndio hao hao current days Mangungo,haingii akilini kabisa kusahau ufisadi wote wa kina RA kwasababu tu eti kuna wanaodai hayo mambo yamalizwe ndani ya chama ambacho ndicho mwanzilishi na mlezi wa mafisadi na ufisadi...Mtavutana sana nyie ccm lakini siku ya kufa nyani miti yote huteleza....Na kama nyie mnaojidai kuwa ni wastaarabu sana kwa kuendelea kuzikumbatia sheria za kifisadi kwa kuzitumia loopholes ni wazi hamtaki mabadiliko na chama chenu cha mafisadi ni kigumu kwa wazlendo wa kweli wanaotaka mabadiliko ya kweli...Tatizo ni kwamba wengi wamebakia kwenye upuuzi ule ule wakidhani mambo ni yale yale...Kama mama Kilango alisema mambo hayo yalishamalizwa bungeni,halafu mme wake naye anakuaja na kudai yakamalizwe ndani ya chama..Then wapi utofauti kati ya maslahi ya Taifa na ya chama?
Ufisadi umeanzia ndani ya chama,na licha ya ccm kukubali kuwa ufisadi huo upo,hakuna aliyechukuliwa hatua zozote za kichama ili kuweza kusema kweli wanapiga vita ufisadi.

Kuna kauli nyingine za kipuuzi kuwa eti MK anatumia issue ya ufisadi,hili neno "Ufisadi" mmeshalifanya lionekane kama ni sifa nzuri na ndio maana mna brush off,wananchi wanatakiwa wasisahahu kuwa ufisadi ndio rushwa na machafu yote yanayotufanya masikini hadi leo,sasa hilo lisipokuwa the maini issue then si ni sawa na kujaza maji kwene gunia?

This is a defining moment,hilo sasa liko wazi...Tusubiri tuone wananchi watakavyoamua coming 2010, maana kelele zetu hapa JF hazisaidii kama wananchi hawatafanya mabadiliko kwasababu kama kuna watetezi wa wazi wazi wa ufisadi,then ni wananchi wamewapa nguvu hizo watu hao...Wananchi wakiwapa ccm fundisho kwa kutowachagua next time,then watajiuliza mara mbili mbili kabla ya kuzungumza ama kufanya maamuzi yenye kutetea ufisadi.....Sijui sana kuhusu huko mitaani kwamba maoni hasa ya wananchi wa kawaida ni yapi hayo,najua wananchi wa kawaida hapo bongo hawana access ya internet na sidhani kama mawazo yao ni swa na ya wanaotetea mafisadi humu ndani,hata hivyo kipimo kikuu ni hapo 2010.

Naona kama inferior complex inakusumbuwa. What does it mean by SISI MIAFRIKA. Ni miafrika kama nyie mliolemazwa na ukabila kiasi ya kwamba watu wanafaidika kwa jasho lenu lakini mnahalalisha eti anaekunyonya ni Muafrika mwenzio. Mbinafsi haa kabila wala dini na mbinafsi yeyote ataweka maslahi yake mbele. Alichofanya RA kama upo ushahidi wa hilo na anachofanya Mwakyembe vyote ni kwa manufaa yao binafsi.

Mimi kama mimi simpi shavu mtu anaetumia madaraka kujipatia chumo nje ya utaratibu eti ni muarika mwenzangu. Mwakyembe alikuwa ni mouthpiece tu Kamati ya watu wengi na kuna waliofanya ujasiri zaidi kuliko aliofanya mwakyembe. Kumbuka Mama Anna Kilango alivyosimaa kidete wakati Mwakyembe akiwa anakigugumizi kumkabili Lowassa. Kumbuka Zitto na jitihada zake na uangalie mifano miwili hiyo. Anne bado anaendelea kuwa shujaa kwasababu hana uchafu aliohusishwa hadi sasa na Zitto kwa msimamo wake anpoteza umaarufu.
Vitendo ndivyo vitakayomuweka mtu sehemu yake inayostahiki na Mwakyembe vitendo vyake vimemfikisha katika majadiliano haya. Tuna haki kumsema yule tunaehisi anajinufaisha na Mwakyembe kutumia Bunge kujinufaisha na kutumia kazi ya Bunge kujikweza si vitu vya kubarikiwa. Tutawalani wabinafsi iwapo ni weupe au weusi au wawe na dini gani.
 
Gonjwa letu tunalijua lakini tunajidai hatulijui..sasa kumlaumu Rostam ni kama escape route...kwa taarifa yenu hata kama kesho Rostam akienda kuishi sayari nyingine matatizo yetu na ujinga wetu utabaki pale pale
 
Back
Top Bottom