Kyela: Dr. Mwakyembe amtolea Uvivu Rostam

Kyela: Dr. Mwakyembe amtolea Uvivu Rostam

Sikonge,

Mkuu wangu swala la mzizi wa ufisadi kuwa Kikwete sikubaliani nao hata kidogo..Ufisadi nchini sii mti ila ni magugu ktk mimea yetu ambayo tumeipanda..Hatukupanda mbegu za Ufisadi, hakuna mti hapa mkuu wangu na kama upo basi hauna madhara isipokuwa ni faida kwetu kupata kivuli..

Rostam ni magugu yaliyoota ndani na mazao yetu, kila maji tunayomwagilia mimea yetu magugu haya hunyonya maji kwa sababu yana mizizi mirefu inayoingia na kupishana na ile ya mimea yetu hivyo... kazi moja tu kuzing'oa mmoja mmoja kama ilivyo desturi yetu...

Zambia, Malawi na hata Zimbabwe wao waliupanda mti huo wenyewe, Hakuna businessman hata mmoja ambaye alikuwa na sauti nchini mwao Ni mtawala mmoja anaamua kuwa fisadi kwa kutumia kiti cha Ikulu kama vile Moi na Mkapa hawa unapokata mizizi yao mti mzima huondoka..Lakini mkuu wangu mzingira ya Ufisadi nchini kwetu sii ya mtu mmoja au kiongozi mmoja ni MAFIA gang... na siku zote Mafia zina faida na hasara zake hivyo unaanza na mtu mmoja mmoja pindi unapokusanya ushahidi..Rostam is the Hitman, The fixer na majina yote unayoweza kumpa na ndiye anayeunganisha misheni zote ndani na nje ya chama..Ndiyo sababu kubwa ya kupewa Mweka fedha wa Chama CCM mtu ambaye hana CPA wala sidhani kama ana NAD..nitarudia kusema kumbuka ile sinema ya Untouchables, pale stesheni walipomkamata yule mhasibu..Mchezo mkali sana.

Kwa hiyo mazingira ya nchi hizo ktk kile tunachopigana nacho ni tofauti kabisa.. Kama ingelikuwa Mkapa ndio mzizi ningekubaliana na mawazo yenu na kama tulifanya makosa basi ni wakati wa Mkapa.. sasa hivi tunacheza na Mafia nzima sii Lowassa pekee wala Rostam pekee wapo wengi wamejipanga na wengine tunao humu humu JF.. Hapa wanapita na pengine wengine wanaulizana huyu Mkandara ndio nani? anajiamini vipi!.. ebu tupeni habari zake na kuna wajinga wanakwenda puta..

Hivyo nachotaka uelewe ni kwamba Ufisadi nchini sio mti kama kina Chiluba bali ni magugu ambayo yameota pamoja na mazao yetu.. Ni lazima tuyang'oe kwa mpangilio pekee!
 
Mwakiembe did nothing new, kama ni ufeki wa richmond ulishajurikana even before ya kamati yake (ya bunge) haijaanza kazi, kamati ilende kuthibitisha tu yaliyokuwa yanavuma....after all akina mwakiembe walikuwa wakifanya kazi kama kamati, sasa nashindwa kuelewa ushuja wake ni upi wakati alikuwa na wenzake kwenye hiyo kamati aidha walitumwa na bunge kufanya hilo it was not his initiative..sasa mbona wengine hamwasifii au wao walikuwa wasindikizaji tu? Tz imejaa maovu kibao lakini sijamsikia kuongelea hayo mengine, ukali wake upo kwenye Richmond and Dowans tu......acheni ushabiki wa kisiasa za ligi kuu, mtaendelea watesa wananchi for no reason...mchunguzeni mtu kwa mapana before kuanza wapigia debe kwa nguvu huvyo...siyo kila abiria anayepanda basi la ubungo basi anaenda ubungo....of course kama wewe ni mpambe wake utanufaika na ku win kwake so u have reason kuchombeza
 
care4all,
Mkuu kuna sehemu Mwakyembe kasema yeye ni shujaa au kuna mtu humu kamwita shujaa kwa sababu ya ile report ya Richmond!..mbona mnababaika Hovyo..
Na kibaya zaidi kama mlijua report ile ni ya kamati vipi mnamsakama Mwakyembe pekee wakati mkijua ukweli, hata maamuzi ya Dowans wametolewa na kamati ya Bomani (nishati na madini).. sijasikia mtu akimtaja Bomani humu..
 
Sikonge,
Mkuu wangu swala la mzizi wa ufisadi kuwa Kikwete sikubaliani nao hata kidogo..Ufisadi nchini sii mti ila ni magugu ktk mimea yetu ambayo tumeipanda..Hatukupanda mbegu za Ufisadi, hakuna mti hapa mkuu wangu na kama upo basi hauna madhara isipokuwa ni faida kwetu kupata kivuli..
!
Lakini Mkandara Raisi Kikwete ndiye mtu ambaye ana uwezo wa kuondoa magugu yoote kutoka kwenye mzizi na asiache kitu, najua magugu mengine yanafanana na mimea yenyewe na wengi tuu hawawezi kutofautisha, lakini nina uhakika Raisi anajua mimea na magugu, Sasa swali ni kwamba kwa nini hayaondoi magugu? na najua Nguvu na uwezo anao.!
 
Mwakiembe did nothing new, kama ni ufeki wa richmond ulishajurikana even before ya kamati yake (ya bunge) haijaanza kazi, kamati ilende kuthibitisha tu yaliyokuwa yanavuma....after all akina mwakiembe walikuwa wakifanya kazi kama kamati, sasa nashindwa kuelewa ushuja wake ni upi wakati alikuwa na wenzake kwenye hiyo kamati aidha walitumwa na bunge kufanya hilo it was not his initiative..sasa mbona wengine hamwasifii au wao walikuwa wasindikizaji tu? Tz imejaa maovu kibao lakini sijamsikia kuongelea hayo mengine, ukali wake upo kwenye Richmond and Dowans tu......acheni ushabiki wa kisiasa za ligi kuu, mtaendelea watesa wananchi for no reason...mchunguzeni mtu kwa mapana before kuanza wapigia debe kwa nguvu huvyo...siyo kila abiria anayepanda basi la ubungo basi anaenda ubungo....of course kama wewe ni mpambe wake utanufaika na ku win kwake so u have reason kuchombeza

Kwa kweli mbuluga ziliwaharibu akili watanzania, hii ndo hasara ya misaada mpaka vyakula vilivyopewa madawa ya kupunguza kufikili: Hivi kama wewe una akili sawasawa, ni kamati ngapi zimeshafanya kazi kama ya mwakyembe kwa hapa Tanzania toka uzaliwe kama si ubabaishaji. Rostam/Lowasa/Kikwete wote ni wezi. Hizi shule za siku hizi, mtu kujua kutype tu kwenye computer mnaanza kutoa pumba zenu. fikiria kwanza kabla ya kutoa argument moron.
 
Kwa kweli mbuluga ziliwaharibu akili watanzania, hii ndo hasara ya misaada mpaka vyakula vilivyopewa madawa ya kupunguza kufikili: Hivi kama wewe una akili sawasawa, mtu kujua kutype tu kwenye computer mnaanza kutoa pumba zenu. fikiria kwanza kabla ya kutoa argument moron.

- Mkuu acha hizi lugha, tunajua kua una hasira sana na yaliyotokea kwa sababu yanakugusa wka karibu sana kama mwananchi, pole sana lakini heshimu wengine kwenye mijadala tunataka kueilmishana sio kushushana hadhi bila ya kuonyesha tofauti za hoja.

Respect!

FMES!
 
- Mkuu acha hizi lugha, tunajua kua una hasira sana na yaliyotokea, pole sana lakini heshimu wengine kwenye mijadala tunataka kueilmishana sio kushushana hadhi bila ya kuonyesha tofauti za hoja.

Respect!

FMES!

hahahaha mkuu huo ndo uzalendo wa kutetea masrahi ya nchi.
 
Lusajo,
Mkuu wangu lini mwenye shamba akajua kutofautisha mimea na magugu wakati yeye husubiri mafao ya mtaji wake..
Kikwete ni rais wetu ambaye kazi yake kubwa ni kuhakikisha sisi tunakwenda shambani na zana zote zinazohitajika ktk kulima zao tulokusudia..Tumlaumu Kikwete kwa yote yanayotokana na ukosefu wa mbegu, zana na hata usimamizi lakini jamani hata kung'oa magugu shambani tunataka hadi mwenye shamba aje kutuambia yapi magugu na ipi mimea wakati sisi ndio tuko shambani na tumepanda mbegu za mazao..

Hivi nikuulize wewe, kweli UWT wakitaka kumsimamisha Rostam mahakamani Kikwete atafanya nini?..Kuna kijana kamzaba kofi la kerbu Mwinyi, Ulimsikia Kikwete?..sheria ilichukua mkondo wake. Tukitaka kuzungumzia Richmond Bungeni au Kortini Kikwete hana nguvu ya kuzuia ndio utaratibu wenyewe.. Sasa kama hatujafanya hivyo hata kujaribu tu tuone kama Kikwete ataingilia tumeshindwa na tunaanza kumwita yeye aje..
Mkuu wangu Kikwete hana ushahidi wowote wa Rostam zaidi ya kuwa bwana shemeji na starehe anazozipata toka kwa...Unajua mimi nadhani anatucheka sana! kwa sababu kisha mvua Rostam wadhifa ktk chama (Mweka hazina) na serikalini (wizara ya Miundombinu) hivi sasa Rostam, Lowassa, karamagi, Msabah woote hawa ni raia tu.. wadhifa walioshika ni Ubunge kama mbunge Dr. Slaa au Mwakyembe nafasi ambazo wamechaguliwa na sisi wananchi na wenye uwezo pekee wa kutengua nafasi hizo..
Kikwete kisha fanya kazi yake jamani katuachia sisi mamlaka ambayo kisheria yeye hawezi kuingilia unless kuna nguvu inayotaka kuishinda mahakama zetu...
Tusiwe wepesi sana kumlaumu Kikwete ktk swala la Ufisadi kwani katusafishia kila njia ya kuweza kuwafikisha watu hawa mahakamani..Kwa ujinga wetu tunataka afanye kinyume cha sheria wakati yeye ni kingozi wa nchi nzima ati afungue mashtaka..Hawa sii Wahaini ni criminals...
 
Hii bado sana kwa nchi zetu za kiafrika, Raisi wetu ana madaraka makubwa sana na katiba pia inamlinda, na Raisi ndiye anayeteua (Hawa watu hawachaguliwi) watu woote ambao ndio wanaweza kupambana na mafisadi. sasa ni nani aliyeteuliwa atajitoa muhanga? Bila ya maelekezo kutoka kwa huyo mtu aliyemteua na ambaye ndiye bosi wake? Hii ni kazi kubwa sana kwetu na labda mpaka katiba ibadilishwe. lakini Raisi wetu ana madaraka makubwa sana.
 
Naam, Rais wetu ana madaraka makubwa sana lakini kaamua kutoyatumia. Ndiyo matatizo ya kuingia madarakani kwa kubebwa na mafisadi. Waliombeba wengi wao wana tuhuma nzito za ufisadi dhidi yao akina Lowassa, Karamagi, Rostam, Yussuf Manji, Jeetu patel, Subhash patel na wengineo. Jamaa hawezi kufurukuta mbele yao maana si ajabu wanaushahidi wa kutosha kuhusu nini kilichofanyika hadi jamaa akaingia Ikulu na wakiuweka hadharani basi itakuwa ni kashfa ya Karne.
 
Lusajo,
Mkuu bado unarudia swali lile lile ambalo jibu lake unalo mfukoni..
Nimesema yule kijana aliyempiga kofi Mwinyi alipata wapi ruksa? na Kikwete alifanya nini! hakuna.. Marehemu Ditto (Mungu amrehemu) tena mshikaji wake wa damu JK alipoharibu ni Kikwete aliyetoa amri ya kukamatwa kwake au hata kuachiwa kwa dhamana?.. Je, si hao hao watu wanaotakiwa kuifanya kazi..
Hivi tujiulize TAKUKURU wameisha kabidhiwa kesi ya Richmond na wameshindwa kufikisha mahakamani au bado ipo bungeni tena imefungwa na hakuna mjadala..Kuna mtu anaweza kusema ilikuwa amri ya Kikwete?..
Kumbuka swala la Mkapa, Kikwete alisema;- Jamani eeeh mwacheni mzee wa watu astaafu.. neno MWACHENI ni ombi likiwa na maana wenye mamlaka yote ni sisi tumwache na sio yeye kamwachia huru...Kikwete angeweza kabisa kusema sitaki kusikia mtu akitaka kumshtaki Mkapa..I said so! na msifanye kitu. Mkapa alikuwa akituita mbumbumbu, maskini na wajinga... that's type ya leadership tunaitaka sio!
Kuhusu uchaguzi wa viongozi bora mkuu wangu hata mimi ningekuwa rais kesho sidhani kama ningeweza kupata wasafi wote au kuchukua hatua kutokana na fununu za magazetini..Labda ningeondoka na mawaziri wawili watatu safi serikali ya JF, lakini siwezi kujua nani mzuri kwangu toka wanachama wa JF..na sina kigezo zaidi cha kuamini mtu hasa mwafrika maskini inapofikia swala la utajiri..
Nitarudia kusema Kikwete ni rais wa nchi, hakusanyi wala kutafuta sababu za kufunga watu isipokuwa kuongoza nchi na sisi ndio kazi yetu na tukishindwa tutawakilisha kwake...Pia mwenye hii site JF hawezi kuwa sauti ya kufungia watu humu wapo Moderators ambao huchukua jukumu la kumfungia mtu bila ya kuwasiliana na mwenye site hii..na wanaifanya kazi yao bila kuuliza kwanza ruksa..Na wakiboronga wao kutomfungia mtu, tunanazidi kupiga kelele hadi wanaelewa hasira zetu bila kumtafuta mwenye site kwani haitasaidia..kumbuka tu kuwa JF ni chombo chako pamoja na kwamba kinamilikiwa na mtu..Ukisha elewa nguvu hiyo basi huna haja kabisa ya mmiliki kujihusisha na malumbano.
Kama tunataka Rostam, Lowassa, na wengine wote wafikishwe mahakamani inawezekana kabisa.. Kumbuka kuwa kisheria hata katiba yetu inaruhusu kumfikisha Mkapa mahakamani na Dr. Slaa kasema inawezekana kabisa kisheria licha ya ombi ya Kikwete iwe hao manyan'gau ati kwa sababu Masha na Nchimbi ndio mawaziri wa wizara ya mambo ya ndani..

Yona na Mramba wote hawa wamefikishwa mahakamani kuna copy yoyote inayoonyesha Kikwete katoa amri wakamatwe..haya Chenge majuzi tu naye yamkuta hatukuona amri ya Kikwete.. nasema hivi mkuu hawa wote ni Criminals kwa ushahidi tuliokuwa nao tunaweza kabisa kufungua mashtaka na kuwalazimisha UWT au TAKUKURU kufanya kazi yao..Tusimame kidete hapa tutafanikiwa na inawezekana lakini mnapokata tamaa na kudandia wagon la Rostam ndio tuna lost kabisa!

Mbona huyo Lau Masha mwenyewe tumefikia kuomba ajiuzuru, tena kisheria na kufikisha hoja bungeni inakuwaje tumeshindwa kabisa kufikisha hoja ya Rostam au Lowassa mahala popote zaidi ya magazetini!..tena tunazunguka kwa majina ya Richmond na Dowans wakati tunawajua majina yao vizuri!...Kisha tunamlaumu rais.
Hapana mkuu wangu, Kikwete anaweza kuwa na mapungufu mengi mengine lakini sio katika hili.. Sisi siku zote ni waoga na wanafiki. Mtu kama Mwakyembe leo hii ndiye tunamtupia hasira zetu zote kwa sababu tu kasema ukweli.. na kama sio yeye tunawaruka maadui kutafuta mchawi mwingine wakati gonjwa ni Rostam..

Kila siku hushangaa sana, siwahi kusikia hata siku moja Mtanzania hata mmoja akidai Rostam afikishwe mahakamani kwa kutumia vibayta madaraka..Tena basi ebu niulize kitu hapa, hivi wakati Richmond/Dowans ilipoingia nchini huyu Rostam hakuwa wizara ya Miundombinu au?..
 
Mkuu Mkandara, naheshimu sana mchango wako na jitihada zako za kuonyesha upande wa pili wa shilingi, lakini with all due respect I do not agree with you on Kikwete.
He has failed us terribly na ameonyesha ya kuwa he is a weak leader. When your government falls apart ni lazima uwe hatua moja mbele na uwe na viongozi wengine wa kuchukua madaraka lakini mpaka sasa hivi anaonyesha ya kuwa uongozi wake, viongozi aliowateua kuanzia mawaziri, majaji etc ni kwamba analipa fadhila na kuwawaweka washikaji. Na hapo ndipo tatizo linapoanza wakati unaona kama kuna hatua zinazochukuliwa kama kukomoana.
Umetolea mfano wa Yona na Mramba, naomba niulize kama haikuwa na baraka za JK unafikiri wangefika hapo vigogo hao? Na umeuliza kwa nini basi Karamagi, Lowassa, RA hajafikishwa hapo? Please don't say ni kutokana na kukosekana kwa ushahidi kwa sababu makaratasi yapo kama yale ya akina Mramba imeandikwa Top Secret. Kama ya akina Yona, ishu ya Richmond pia ni cabinet decision. Lakini akina Yona na Mramba are pawns in a power struggle game that is why they are wherer they are and you know it. So tafadhali usitoe mfano huu kama kigezo kuwa eti JK anakemea mafisadi. Naomba nimwone RA Kisutu ndo nitajua yuko serious. Lakini hata tukinyimwa misaada na tukila nyasi, RA hatapandishwa kizimbani. Because JK owes RA a big one - for making him president. Hii si siri na RA mwenyewe anatamba huko Kempinski! He is the kingmaker!
 
Susuviri,
Kwanza shukran kwa heshima ulonipa maanake sii kazi ndogo kutazama upande wa pili...
Mimi hata siku mmoja sijasema Kikwete ni kiongozi mzuri au mbora zaidi isipokuwa ktk issue hii..ka fail sehemu nyingi sana na sielewi sababu zaidi ya kwamba kiti cha Ikulu ni kikubwa kuliko uwezo wake..
Lakini pamoja na yote hayo, Yona na Mramba wamefikishwa mahakanani na vyombo vyetu hakuna ushahidi unaoonyesha kuna baraka za Kikwete..zaidi ya kwamba pengine (dhana) alifuatwa na kuulizwa.
Swala hapa ni Rostam/Lowassa na Mafisadi wengine wote!.. nikirudi nyuma swala la Richmond lilikuwa lizimwe toka mwanzo, Kikwete mwenyewe akalifufua na likafikia watu wake wote kawaondoa katika serikali yake.. Sii rahisi hata kidogo kwa rais JK kumwondoa Lowassa/Rostam, Megji, Karamagi na list nzima ya timu yake kwa sababu ya mtambo mmoja wa Richmond wakati wamevuta mabillioni ya EPA, IPTL na kadhalika...
Kikwete ametuonyesha kila dalili ya kwamba tunaweza kuchukua sheria alipo waondoa ktk madaraka ya chama na serikalini..Mafisadi wote sasa hivi wako loose na ndio maana nikatoa mfano wa Chenge, wee unafikiri kama angekuwa bado Waziri wa sheria angefikishwa hata Polisi?.. kavuliwa madaraka ni raia kama wewe na alikwenda polisi na wapambe tu wa mitaani, hivyo kazi kwetu.. Ajabu, bado sisi tunataka Kikwete afungue mashtaka against raia ambao kesi zake tumezikalia sisi wenyewe..
Sikiliza Mkuu wangu Susuviri, kwa nini kesi hizi zimekwama bungeni?.. ni kwa sababu wabunge wengi walioko bungeni wamepita kwa mkono wa Rostam/Lowassa na Kikwete hana wabunge wa kujaa mkononi..
Hizi habari za kwamba anapigwa vita sii za uongo, anaweza kabisa kumtosa Rostam na Lowassa ikiwa kuna habari za Uhaini, na ikiwa kaweza kuwaputa tonge la madaraka mdomoni ashindwe vipi kuwamaliza ikiwa sheria inamruhusu yeye peke yake kutoa maamuzi..
Tofauti ya Kikwete na marais wengi waliotangulia ni kwamba Kikwete ni Muungwana anafuata sheria zaidi na ndio maana hata sisi walalahoi tunabwabwaja humu JF at peace!..kuna watu wanamwona kashindwa kazi kutokemea waandishi uchwara... wengine wanasema nchi imeshinda kwa ajili ya Uhuru huu tunaopewa sisi.. Huo ni upande wapili wa shilingi hiyo hiyo mkuu wangu..Lakini kila swala hili lilipofikishwa kwake aliwakanya na kuwaambia ni Uhuru anaotaka kuona ukipatikana.. Straight in their face iwe Lowassa au Rostam.
sasa jamani atupe nini zaidi?.. why toka leo sisi tusitafute haki yetu badala yake tunasema sana na kulaumu wakati hata dogo la kujaribu tunashindwa kufanya!..When wewe umesikia Lowassa au Rostam wakitajwa ama kutishiwa kushtakiwa kama sio mtu mmoja tu Mtikila..Na kesho yake sote tukamgeuka!..Mwakyembe kasema kidogo sote tunamwona mchawi sasa kweli Kikwete ndiye pekee anakubalika kusema lolote kuhusiana na hawa jamaa!..
YES, Kikwete ana mapungufu yake na mengi tunayazungumza humu lakini hili mkuu wangu nimetazama pande zote na kuona kwamba sisi wenyewe ndio wa kujilaumu..watu hawa hawana kinga yoyote zaidi ya kuwa wafanyabiashara wenye mahela..Rostam hatushindi hata kidogo ila wengi wanaogopa kusikia ni bwana shemeji. Lowassa ndiye alikuwa mshikaji wa JK kama tulivyoshindwa kuwasimamisha Yona na Mramba wakati wa Mkapa, tuliwapongeza sana tu..Ndivyo Tulivyo!
 
Mkuu MKandara, nimekusikia na from this point of view you are right: the general population of Tanzania shares the blame kwa hali tuliyo nayo hivi sasa kuanzia wabunge wanaolindana, upinzani, wapiga kura etc. Lakini political structure ya Tanzania inampa Rais madaraka makubwa. Na kusema kuwa eti JK ni muungwana na ametoa uhuru mkubwa zaidi wa habari haitoshi. Mi naamini hata Mkapa angeendelea kwa awamu nyingine (God forbid) angelazimika kukubali uwazi uliopo. But we can debate that angle another day.
Kikwete is infamously doing nothing about everything. Siyo kwamba ana any lofty vision about freedom of expression ni kwamba hataki kuudhi mtu. That is not leadership!

Ile cabinet reshuffling iliyotokea ni kwamba ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kwa waziri mkuu kujiuzulu katika kashfa nzito kama hii ya Richmond. Mi sidhani kama JK ndo hakuruhusu Richmond izimwe ili ipelekwe hadharani. Ukweli ni kwamba Lowassa aliona kuwa wabunge wananungunika and he tried to play chicken. Aliamini kuwa wabunge wanamwogopa wasingeweza kufanya lolote. Kuna uhasama wa Lowassa na Sitta involved. There are a number of factors, it has nothing to do with JK, believe me! He is a bystander. They did not count with Mwakyembe na ndo maana Lowassa and company wanamchukia hivyo Mwakyembe. Wao walitegemea Harrison na wenzake 'watamezea'. Kumbuka Mwakyembe alizungumzia vitisho na pesa walizokuwa wanapata wakiwa katika kamati. Once the damage was done, ilibidi JK ashauriwe kwamba wale ambao wanapigiwa sana kelele watolewe kutoka cabinet. Chenge alikuwa mchafu sana, ditto for Meghji etc. Na wali-panic. Kuhusu Chenge unasema ni raia tu si kweli ni mbunge na ni very powerful man kama unavyoona kesi yake inavyoendeshwa kwa polisi kumnyenyekea. Na kama kweli JK angetaka basi angeanza kumpeleleza Chenge kwa ajili ya vijisenti alivyodai waingereza wamekuta katika account.
Na hapo bado sijamgusia Dr Idris Rashid. ....
Our president is just taking credit for doing nothing and for being present in class. Afadhali basi awe pro-active hata kama atafanya makosa lakini he tried siyo kujifurahisha kwa trip za nje na kujirusha... he should focus entirely on his job. Umekiri kwamba you are ready to conisder the fact that kiti cha urais umezidi uwezo wake, well, weak leadership is not leadership. I am not ready to give him any credit because tokea ameingia madarakani sijaona hata policy paper moja serious ikitoka, sijasikia any plans zaidi ya kutekeleza yale yaliyopangw enzi za Mkapa na yale ya wafadhili, sijaona utekelezaji wa ahadi yoyote kati ya ahadi zake 100 alizotoa siku alipohotubia bunge kwa mara ya kwanza.
 
Susuviri,

Ni Waluguru au Wapogoro ambao husema hamsindile hamnoga?

Miye hata kumbeza nimeacha, maana laiti angekuwa na ubabe kama Che Nkapa wa kujibishana, ,ningeendelea kumpiga makonzi.

Walipokwenda Butiama wakampiga roba kuhusu Muafaka na Ufisadi, nikajua kumbe hata ndani ya Chama yeye ni Selule babkubwa!
 
Mkuu Mkandara, hoja zako zinashawishi sana hasa kama msomaji wa hoja hizo hataamua kufikiria kwa uangalifu.

Hivi tujiulize TAKUKURU wameisha kabidhiwa kesi ya Richmond na wameshindwa kufikisha mahakamani au bado ipo bungeni tena imefungwa na hakuna mjadala..Kuna mtu anaweza kusema ilikuwa amri ya Kikwete?..
Inasemekana kuwa TAKUKURU wameshakabidhi reports zao nyingi kwa DPP kuhusiana na kesi mbalimbali zinazowahusu baadhi ya viongozi wa serikali. Kuliwahi kutokea malalamiko kutoka TAKUKURU kuhusiana na hatua ambazo DPP alitakiwa kuchukua, lakini hakufanya hivyo. Inasemekana pia kuwa DPP hajaridhishwa na utoshelezi wa uthibitisho wa hatia za watuhumia. Hakuna report za TAKUKURU zinazopelekwa Bungeni kwasababu zozote. Kumbuka Kamati ya Bunge iliyochunguza shutma za Richmond ilikuwa na jukumu la kubainisha ukweli wa shutuma hizo na kuthibitisha kwa Bunge kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za tenda ya umeme wa Richmond. Sina uhakika kuwa report kama ile inamtosha DPP kufungua mashitaka au lah. Ila jukumu la kufanya hivyo analo DPP.

Kuhusu uchaguzi wa viongozi bora mkuu wangu hata mimi ningekuwa rais kesho sidhani kama ningeweza kupata wasafi wote au kuchukua hatua kutokana na fununu za magazetini..Labda ningeondoka na mawaziri wawili watatu safi serikali ya JF, lakini siwezi kujua nani mzuri kwangu toka wanachama wa JF..na sina kigezo zaidi cha kuamini mtu hasa mwafrika maskini inapofikia swala la utajiri..

Mkuu katika kuteua viongozi, mimi napata shida sana kuamini kuwa hiyo ni kazi ngumu kiasi hicho. Inaweza kuwa ngumu kama jukumu hilo utalifanya mwenyewe, bila maandalizi na kwa siri. Ninachoamini ni kwamba, mtu yeyote anapoona kuna uwezekano akapata nafasi anayoiwania (mfano Urais), anatakiwa aanze kujiuliza maswali kadhaa:
1. Ni serikali ya namna gani atakayoiunda na kwanini (mseto, ukubwa wake n.k.)
2. Ni malengo gani anayotaka kuyafikia kwa muda mfupi, wa kati na mrefu
3. Ni akina nani wanaofaa kushiriki katika uongozi ili kufanikisha mipango hiyo na ni katika nafasi zipi (uwaziri, n/Waziri, Katibu wakuu n.k)
4. Nini anachotarajia kukipa kipaumbele cha kwanza (first priority) na nini anachotakiwa kukipa kipaumbele kidogo (least priority). List of priorities (inaweza kutokana na manifesto, ila inakuwa na mikakati zaidi)
5. Baada ya muda wake wa uongozi (miaka 5) atakuwa amefikia malengo gani?

Maswali hayo machache, si ya kutosha, bali atleast kiongozi anatakiwa kujua majibu yake kabla hajaanza kazi rasmi. Majibu ya maswali hayo ndio sababu ya nia yake kuongoza nchi. Vinginevyo, nia yoyote iwayo itakuwa ni ya kupotezea wananchi muda tu.

Kama tunataka Rostam, Lowassa, na wengine wote wafikishwe mahakamani inawezekana kabisa....

Yona na Mramba wote hawa wamefikishwa mahakamani kuna copy yoyote inayoonyesha Kikwete katoa amri wakamatwe..haya Chenge majuzi tu naye yamkuta hatukuona amri ya Kikwete.. nasema hivi mkuu hawa wote ni Criminals kwa ushahidi tuliokuwa nao tunaweza kabisa kufungua mashtaka na kuwalazimisha UWT au TAKUKURU kufanya kazi yao..Tusimame kidete hapa tutafanikiwa na inawezekana lakini mnapokata tamaa na kudandia wagon la Rostam ndio tuna lost kabisa!

Mkuu, unalosema kuhusu uwezo, haki na ruhusa ya kufungua mashitaka ni sahihi kabisa. Ila ujue tu kwamba, kila kimtokeacho kiongozi wa juu wa serikali, kinahitaji baraka za kisiasa kabla hakijafanyika. Niweza kuapa kuwa, kama JK angetaka akina Mramba, Yona, Mgonja na wengine wasingefika Kisutu. Na kama angetaka pia, akina EL, RA, NK, na wengine wanaotajwa humu wangefikishwa Kisutu kujibu mashitaka yao. Mkuu, hakuna hatua inayochukuliwa nchi hii bila ridhaa ya utashi wa kisiasa. Hata kuondoa wamachinga barabarani inatokana na utashi wa kisiasa. Ninaweza kuhisi tu kwamba, kuanzia sasa hakutakuwa na kiongozi mpya atakaefikishwa mahakani kwa tuhuma za ubadhirifu wowote (EPA, Richmond/Downs, Kagoda n.k.). Sisi wananchi tukitaka kushitaki tunaweza. Ila mashitaka hayo hayatafika mbali kwani utashi wa kisiasa utayapinga kwa kushinikiza mahakimmu kuchukua hatua za kuyadhoofisha. Mahakama zetu zinaingiliwa sana na serikali katika maamuzi yake (jaji Mkuu alilalamikia hili pia).

Mbona huyo Lau Masha mwenyewe tumefikia kuomba ajiuzuru, tena kisheria na kufikisha hoja bungeni inakuwaje tumeshindwa kabisa kufikisha hoja ya Rostam au Lowassa mahala popote zaidi ya magazetini!..tena tunazunguka kwa majina ya Richmond na Dowans wakati tunawajua majina yao vizuri!...Kisha tunamlaumu rais.
Hata hoja ya LM kujiuzuru imefika wapi? Ilijadiliwa? Jibu ni hapana. Haitajadiliwa na hajajiuzuru/hatajiuzuru.

EL na wenzake walijadiliwa Bungeni kwa ukamilifu kabisa. Bunge kama kawaida yake ikaridhia hatua za kuchukuliwa na viongozi hao pamoja na wengine. Hatua zilizokwisha kuchukuliwa zinajulikana kwa uchache wake. Angalau ungesema hawa wamechukuliwa hatua, ningekuelewa zaidi. Ila LM hajafanywa lolote, alikingiwa kifua sana tu.

....Kikwete anaweza kuwa na mapungufu mengi mengine lakini sio katika hili.. Sisi siku zote ni waoga na wanafiki. Mtu kama Mwakyembe leo hii ndiye tunamtupia hasira zetu zote kwa sababu tu kasema ukweli.. na kama sio yeye tunawaruka maadui kutafuta mchawi mwingine wakati gonjwa ni Rostam..

Mkuu, JK ni Rais wa nchi, Mkuu wa majeshi ya ulinzi na Usalama, Mwenyekiti wa CCM. Ameshika DOLA.

Huwezi kumtoa kwenye majukumu ya kuhakikisha nchi inaendeshwa kwa kufuata sheria, kwa amani na utulivu na kulinda rasilimali za nchi na usalama wa raia na mali zao. Haiwezekani Rais akawa nje ya jukumu la kuhakikisha mtu, au kikundi cha watu wanaohujumu rasilimali za nchi/umma wanafikishwa kwenye mamlaka za sheria, ili kuwa fundisho kwa wengine na kadiri inavyowezekana kuhakikisha mali hizo zinarudi kwa umaa na zinatumika kwa ufanisi kwa maendeleo ya nchi na taasisi za umma.

Kila siku hushangaa sana, siwahi kusikia hata siku moja Mtanzania hata mmoja akidai Rostam afikishwe mahakamani kwa kutumia vibaya madaraka..Tena basi ebu niulize kitu hapa, hivi wakati Richmond/Dowans ilipoingia nchini huyu Rostam hakuwa wizara ya Miundombinu au?..

RA hajawahi kuwa kiongozi wa ngazi yoyote serikalini. Na kwahiyo, hajawahi kuwa katika wizara ya Miundombinu. Nakuhakikishia, angekuwa Wizara hiyo, angejenga kila kitu hapa nchini. Hakuwepo ila alihakikisha alijenga Shekilango Road na barabara nyingine kadhaa kwa utaratibu ambao singependa kuuingilia.
 
Mkuu, unalosema kuhusu uwezo, haki na ruhusa ya kufungua mashitaka ni sahihi kabisa. Ila ujue tu kwamba, kila kimtokeacho kiongozi wa juu wa serikali, kinahitaji baraka za kisiasa kabla hakijafanyika. Niweza kuapa kuwa, kama JK angetaka akina Mramba, Yona, Mgonja na wengine wasingefika Kisutu. Na kama angetaka pia, akina EL, RA, NK, na wengine wanaotajwa humu wangefikishwa Kisutu kujibu mashitaka yao. Mkuu, hakuna hatua inayochukuliwa nchi hii bila ridhaa ya utashi wa kisiasa. Hata kuondoa wamachinga barabarani inatokana na utashi wa kisiasa. Ninaweza kuhisi tu kwamba, kuanzia sasa hakutakuwa na kiongozi mpya atakaefikishwa mahakani kwa tuhuma za ubadhirifu wowote (EPA, Richmond/Downs, Kagoda n.k.). Sisi wananchi tukitaka kushitaki tunaweza. Ila mashitaka hayo hayatafika mbali kwani utashi wa kisiasa utayapinga kwa kushinikiza mahakimmu kuchukua hatua za kuyadhoofisha. Mahakama zetu zinaingiliwa sana na serikali katika maamuzi yake (jaji Mkuu alilalamikia hili pia).

Hata hoja ya LM kujiuzuru imefika wapi? Ilijadiliwa? Jibu ni hapana. Haitajadiliwa na hajajiuzuru/hatajiuzuru.

EL na wenzake walijadiliwa Bungeni kwa ukamilifu kabisa. Bunge kama kawaida yake ikaridhia hatua za kuchukuliwa na viongozi hao pamoja na wengine. Hatua zilizokwisha kuchukuliwa zinajulikana kwa uchache wake. Angalau ungesema hawa wamechukuliwa hatua, ningekuelewa zaidi. Ila LM hajafanywa lolote, alikingiwa kifua sana tu.

Mkuu, JK ni Rais wa nchi, Mkuu wa majeshi ya ulinzi na Usalama, Mwenyekiti wa CCM. Ameshika DOLA.

Huwezi kumtoa kwenye majukumu ya kuhakikisha nchi inaendeshwa kwa kufuata sheria, kwa amani na utulivu na kulinda rasilimali za nchi na usalama wa raia na mali zao. Haiwezekani Rais akawa nje ya jukumu la kuhakikisha mtu, au kikundi cha watu wanaohujumu rasilimali za nchi/umma wanafikishwa kwenye mamlaka za sheria, ili kuwa fundisho kwa wengine na kadiri inavyowezekana kuhakikisha mali hizo zinarudi kwa umaa na zinatumika kwa ufanisi kwa maendeleo ya nchi na taasisi za umma.

RA hajawahi kuwa kiongozi wa ngazi yoyote serikalini. Na kwahiyo, hajawahi kuwa katika wizara ya Miundombinu. Nakuhakikishia, angekuwa Wizara hiyo, angejenga kila kitu hapa nchini. Hakuwepo ila alihakikisha alijenga Shekilango Road na barabara nyingine kadhaa kwa utaratibu ambao singependa kuuingilia.

Recta, (Mkandara).

Umelielezea hili safi sana. Kikwete ni au alihusika katika ufisadi na au alikuja kujua kuwa kawekwa hapo kwa pesa za ufisadi na jamaa wamemuwekea bomu kifuani na wameshika remot control. Ndiyo maana hadi Masha (deepgreen??) na yeye anaweza kuboronga na asifanywe kitu. RA ndiyo kabisa tuachane naye. Hawa kawatengeneza yeye kama Miungu watu.

Rais wa Tanzania ana madaraka makubwa sana hadi mwenyewe alikiri na kusema wanaangalia jinsi ya kuyapunguza. Ila hadi leo miaka 4 sijasikia kitu. Kwa nini asingeligawa madaraka kwa wenzie hasa PM na serikali???
Ni yeye anateuwa Mkuu wa Polisi, mkuu wa upelelezi, Takururu, majaji, nk na ni amiri jeshi wa jeshi la Tanzania. Nafikiri kama angeliamua kufanya MAPINDUZI kutoka mikononi mwa MAFIA, ingelitosha kumuweka sana MWAMUNYANGE, boss wa POLISI na mkuu wa upelelezi kuwa watu wake na wawe wachapa kazi kweli. Kumuweka mkuu wa upelelezi MSANII ni kujiwekea mwenyewe matatizo.

Kuna haja ya Tanzania kuwa na kitu kama FBI na CIA. Ila hata hivi kama alivyosema RECTA, ni kuwa bado UTASHI WA SIASA huamua. Hata USA, kwenye kesi ya URAIS, ilipofika mahakamani, Bush ilijulikana atashinda kwani majaji wengi wamewekwa pale na baba yake. Hivyo kusema tutamaliza magugu /mizizi ni kuwa hatuwezi ila walau tujiwekee misingi ambayo hayo magugu hayatajiotea na kuwa makubwa kama EL, RA, Karamagi etc.

Kwa hili nafikiri tukubaliane kuwa Mwakyeme kumshambulia gugu mmoja ni kupoteza muda. Bado kuna haja ya kutafuta njia ya maana kushambulia magugu yote kwa mpigo na kuweka njia za kudhibiti ili yakiota basi tuyawahi. Tumesikia USA uzembe wao wa kulea wauza/watumia unga kumewafanya wazee wa unga Mexico wawe na pesa za kutisha hadi kuanza kuwatishia wenyewe sasa USA. Ila wenzetu walau wanajua kukubali kosa na kuanza kulisolve. Sisi ni au hatulioni kosa na au twaamini kuwa kweli kosa lipo na twaweza sisi kulisove wenyewe wakati SI KWELI. Bila MUUNGWANA kulivalia njuga, Bunge, na mwisho wapiga kura ni kwamba Mwakyembe atapiga sana kelele juu RA ila hiyo itakuwa ni kampeni za uchaguzi na si kuuwa magugu.
 
Kuna mambo mawili yanahitaji kusahihishwa hapa.

La kwanza ni maelezo kwamba waandishi wa habari waliopo Kyela walipigwa marufuku kwa sababu wanamwandika vibaya, hilo sio kweli hata kidogo, na ni uzushi mkubwa. Kyela wapo waandishi wa habari wa kujitegemea wawili tu na wasio na chombo maalumu cha kukiandikia, na siku hiyo walikuwepo na ushahidi ni Richard Kilumbo ambaye siku hiyo alipeleka habari hiyo Tanzania Daima baada ya kuombwa na mwakilishi wa gazeti hilo mkoani Mbeya ambaye siku hiyo alikuwa Dar, hivyo alishirikiana na mwenzie kutoka Mbeya. Wawakilishi wa makampuni ya habari wote wako Mbeya mjini hivyo husambaa kule kwenye tukio kubwa kwa mkoa kwa wakati ule, ni magazeti machache sana yenye waandishi wake wilayani. Waandishi waliokuwepo Kyela siku hiyo walifika kila mtu mmoja kwa utaratibu wake, baadhi ni baada ya kupata maelekezo toka kwa wahariri wao Dar na wengine waliandamana na Naibu Waziri wa Fedha ambaye siku hiyo alienda Kyela na wengine walienda rasmi kwa ajili ya mkutano huio baada ya kupata taarifa kutoka mjini kyela kuhusu kuwepo maandamano na mkutano.

Pili ni suala la hisa, alichokiri ni kushiriki kwake kwenye kuisimamisha hiyo Kampuni na kwamba suala la hisa watu wakaangalie records za kampuni hiyo kuanzia 2007 hawatalikuta jina lake humo hivyo kuwashauri wanaoshikia bango hilo kufanya utafiti na sio kuendesha propaganda zinazodhalilisha hata elimu waliyonayo.

Nimeona niweke sawa mambo hayo mawili kwani yanapotosha hata uchangiaji wa hoja husika.
 
... Hata USA, kwenye kesi ya URAIS, ilipofika mahakamani, Bush ilijulikana atashinda kwani majaji wengi wamewekwa pale na baba yake.

Si kweli. Baba yake aliweka majaji wawili, na ni mmoja tu aliye msapoti kwenye kesi, Thomas. Mwenzake, Souter, alishageuka liberal kitambo kabla ya kesi. Unaweza kujaribu ku predict jaji atakavyo amua kwa kuangalia historia ya falsafa yake katika siasa za sheria, sio nani kamumeka.

Hakuna aliyejua atashinda kesi kwa vile "majaji wengi wamewekwa pale na baba yake." Sikonge tafadhali.
 
Back
Top Bottom