..Mkuu Macos, Kweli Umechukia but did you have to repeat it Three Times??? teh teh
..binafsi nilikuwa mstari wa mbele kumlima Dr.Mwakyembe kule kwenye hoja ya mgongano wa kimaslahi.
..lakini katika huu mpambano wake na Rostam Azizi namuunga mkono Dr.Mwakyembe 100%.
..Rostam ndiye chief financier wa kampeni chafu za ki-mafioso za wanamtandao. wamewachafua watu wengi sana kama Salim Salim, John Malecela etc ili kuingia madarakani.
..nina imani ukifanyika uchunguzi wa kina kuhusu kampeni nzima ya wanamtandao, ikiwemo kutumia fedha toka nje ya nchi[Iran], tunaweza kuishia kuwa na impeachable offences.
..serikali ya mtandao wameanza kuiba tangu awamu yao ya kwanza ya uongozi. hawana hata ule "uungwana" wa Mzee Mwinyi na Mkapa wa kuchapa kazi ktk awamu ya kwanza, na kuanza kuiba na kukwapua ktk awamu ya pili.
MN, sikubaliani na dhana yako ya kutaka kuonyesha wizi ngazi ya Kitaifa athari yake ni ndogo ukilinganisha na ngazi za halmashauri. Kama unaufahamu wizi wowote ule hata kama ni ngazi ya halmashauri haujakatazwa kuuweka hapa jamvini tuujadili. Je, wizi wa EPA wa shilingi 133 billioni ulikuwa ni 10% ya kiru gani? Je, wizi wa Meremeta wa shilingi 155 billioni ulikuwa ni 10% ya kitu gani? Je, wizi wa shilingi 200 billioni uliofanywa na fisadi Rostam na makampuni yake ya kifisadi Richmond/Dowans ulikuwa ni 10% ya kitu gani!!!? Ni kosa kubwa kutaka kuonyesha wizi ngazi ya kitaifa athari yake si kubwa kama ule wa halamshauri.
Si kweli. Baba yake aliweka majaji wawili, na ni mmoja tu aliye msapoti kwenye kesi, Thomas. Mwenzake, Souter, alishageuka liberal kitambo kabla ya kesi. Unaweza kujaribu ku predict jaji atakavyo amua kwa kuangalia historia ya falsafa yake katika siasa za sheria, sio nani kamumeka.
Hakuna aliyejua atashinda kesi kwa vile "majaji wengi wamewekwa pale na baba yake." Sikonge tafadhali.
hawa akina Mwa wana umoja duh!
mwakipesile,mwakyembe,mwakanjala,mwasote,mwakilanga
gotta give it to watu wa Mbeya mtu wenu mnae to the end
Ugomvi uko kwetu sisi wa Pwani...kidogo ukishaboa tuu bas tunakuacha waku hang maana hatuna muda wa kujibizana kama huamini muulizeni yule mzaramo wa kujipaticha...aka BANGUSILO
....Rostam ndiye chief financier wa kampeni chafu za ki-mafioso za wanamtandao. wamewachafua watu wengi sana kama Salim Salim, John Malecela etc ili kuingia madarakani.
Du! Hizi ni nadharia za ufashisti. Hivi wewe una amini juu ya demokrasia? na haki zinazotakana na uadilifu wa kisanduku cha kura. Nakushangaa kwa nini ukatae matakwa ya wengi ambao kwa kutumia kisanduku cha kura huwa wanaiafiki CCM?Huwezi kumuunga mkono aliekuwemo ndani ya CCM,kwani kila mmoja ana yake kumshinda mwenziwe ,wote ni uoza mtupu ni lazima wapigwe na chini wote asibakie hata mazururaji.
Ngw'aninyami said:Okay JokaKuu aka Anaconda aka Reticulated Python....that above is a statement of fact. Now, can you back it up with indisputable proof?
...Rostam ndiye chief financier wa kampeni chafu za ki-mafioso za wanamtandao. wamewachafua watu wengi sana kama Salim Salim, John Malecela etc ili kuingia madarakani.
Ngw'aninyami,
..tunahitaji insiders kama wale wa kwenye kashfa ya Richard Nixon ya Watergate to bring to the light jinai zilizofanywa na wanamtandao.
Kitila Mkumbo said:Lakini tujiulize haya yote anayoyaongea Mwakyembe ni kwa faida ya nani au yanatusaidiaje sisi wananchi anaotuwakilisha. Kwamba Rostam ni 'fisadi' sio geni, walilisema vizuri zaidi akina Slaa. The question is why is becoming bitter on Rostam now, especially after he (Rostam) raised the issue of his project in Singida?
Nami pia ni staunch supporter wa aina ya wabunge kama Mwakyembe, lakini nina issues naye sana, hasa tangu alipojaribu bila mafanikio kuhalalisha mauaji wananchi wasio na hatia kule Zanzibar january 2001. Kila aongeapo Mwakyembe huwa najiuliza ni yeye au anabeba ajenda ya mtu fulani? In short, can Mwakyembe stand on his own and 'be counted'.
Muhimu zaidi: Tuyapime haya aliyoyasema huko Kyela kama yana tija kwa wapiga kura wake na wananchi kwa ujumla. Kwamba anapendwa kiasi kwamba 'sisi watu wa Singida tunataka aje awe mbunge wetu', haya yana tija kweli???
Kwenye post yangu sikusema kwua wizi wa ngazi ya kitaifa ni mdogo. Nilichosema ni kuwa wizi wa ngazi ya halmashauri ni mbaya zaiai (na sidhani kama kauli hii inamaanisha kuwa wizi wa ngazi ya kitaifa si mbaya).Kwa maoni yangu, kutokana na mfumo wa kibajeti wa siku hizi, fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo ya moja kwa moja kwa wananchi zinapitia kwenye halmashauri. Ukiangalia ripoti ya CAG, ni asilimia 22 tu ya fedha hizi ndizo hasa hufanya kazi ya maendeleo. Sijajua katika ufisadi wa ngazi ya kitraifa ni asilimia ngapi ya fedha zinatumika moja kwa moja kwenye mipango iliyopangwa.
Kinachonifanya niuone wizi wa ngazi ya halmashauri kwua ni mbaya zaidi ni kwa sababu fedha zinazochotwa zililenga kuleta maendeleo moja kwa moja na si kama zile za ten percent ambazo sizipoenda kwa mtu binafsi zinaweza zisiingie kwenye mfuko wa moja kwa moja wa bajeti.
Ni kweli kuwa wizi ni mbaya sehemu yoyote, lakini wizi huu wa fedha zilizolenga kwuahudumia wananchi moja kwa moja, kwa maoni yangu, ni mbaya zaidi