Kyela: Dr. Mwakyembe amtolea Uvivu Rostam

Kyela: Dr. Mwakyembe amtolea Uvivu Rostam

Pesa za maendeleo zinapelekwa kupitia halmashauri ya wilaya. Kila halmashauri ina budget yake kama ilivyo wizara. Ni kweli kuna mambo ambayo wizara inaweza kufanya moja kwa moja kwenye wilaya, lakini kwa taarifa yako ni machache mno. Mambo mengi hufanywa kupitia halmashauri ya wilaya.

Priorities zetu kule kwenye halmashauri ndio mbovu. Si umesikia madiwani wanapeana 65,000 kwenye vikao vyao? Hizo pesa zingetumika kwa maendeleo, zinaweza kufanya mambo mangapi?

Tumejikita kuzungumzia ufisadi wa ngazi za kitaifa na kimataifa na kusahau kuwa nchi inaliwa katika ngazi ya halmashauri. Ukiangalia ripoti ya CAG kwa kweli utashangaa jinsi ambavyo tusivyoshitushwa na wizi unaofanywa katika ngazi za halmashauri. na ninaamini kwua wizi huu ni mbaya zaidi kwa sababu kinachoibwa ni kile kilichokuwa budgeted for development activities, wala si ten percent
 
Hii ndiyo risala ya wapigakura wa Kyela kwa Mbunge wao

RISALA YA WAPIGAKURA WA KYELA KWA MBUNGE WA KYELA DK. HARRISON MWAKYEMBE JUMAPILI TAREHE 29 MACHI, 2009

Mheshimiwa Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, awali ya yote sisi wapigakura wa Wilaya ya Kyela tunakupa pole kwa msiba uliokupata hivi karibuni wa mama yetu mpenzi, Tukusuma Kibole Mwakyembe. Ninawaomba wapigakura wenzangu wote tuliopo uwanjani hapa tukae kimya kwa dakika moja kwa heshima na kumbukumbu ya marehemu. Ahsanteni.

Mheshimiwa Mbunge, naomba vilevile nikushukuru kwa kukubali mwaliko wetu (tuliokutumia rasmi jana jioni) wa kuyapokea maandamano haya yaliyoanzia Community Centre mpaka hapa Uwanja wa Mwakangale. Madhumuni ya maandamano haya ni kuelezea hisia zetu na kupata maelezo yako kuhusu maana na lengo la kampeni ya chuki ya magazeti yanayomilikiwa na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz. Mbali na kuonyesha dhahiri nia ya kutaka kukuchafua tu kisiasa, magazeti hayo sasa yanadai Mbunge wetu uondolewe ubunge.

Mheshimiwa Mbunge, katika toleo la Machi 24 hadi 30 mwaka huu la gazeti la TAZAMA, moja ya magazeti lukuki anayomiliki Rostam, imeelezwa bayana kwamba utasimamishwa ubunge. Taarifa hii imetushitua sana wapigakura wa Kyela na kutufanya wengi tujiulize KULIKONI? Rostam Aziz, pamoja na kwamba ni fisadi asiyeguswa nchi hii, kapata wapi nguvu na mamlaka ya kumwondoa Mbunge aliyechaguliwa kwa asilimia 93 ya wapiga kura wa Kyela?

Kiu yetu kubwa ya kutaka kuujua ukweli, imezaa wazo la kuja hapa uwanjani leo hii ili utupe picha sahihi badala ya kutegemea maelezo ya juujuu ya magazeti ambayo tayari yamegubikwa na ushabiki.

Mheshimiwa Mbunge, wapigakura wa Kyela tulikusikiliza kwa makini sana ulipoongea na vyombo vya habari Dar es Salaam tarehe 17, mwezi huu. Tulielewa kuwa kampuni hiyo anayoiimba Rostam usiku kucha (ili kukulaumu mbunge wetu) haikuwa miongoni mwa makampuni yaliyojitokeza na kushiriki kwenye mchakato wa zabuni ya umeme wa dharura, na kwamba pamoja na uchanga wake kampuni hiyo ambayo imeanzishwa kushughulikia nishati ya upepo isingeweza kushiriki kwenye zabuni iliyolenga uzalishaji umeme kwa kutumia gesi asilia tuliyonayo. Sasa katika hali hiyo, mgongano wa kimaslahi ambao Rostam Aziz anauimba kila kukicha utokee wapi kama si porojo na uchochezi tu wa kisiasa?

Ikiwa sisi wapigakura wa Kyela (pamoja na uelewa wetu mdogo) tulikuelewa, ni nini kinamfanya Rostam Aziz asielewe? Ni nini kinamfanya kiongozi mwandamizi wa CCM, kama Rostam (ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM) ahangaike kiasi hicho kujaribu kumbomoa kiongozi mwenzake wa CCM, ambaye pia ni Mjumbe wa NEC? Mheshimiwa Mbunge sisi wapigakura wako tunakuomba leo utueleweshe, tujue: KULIKONI!

Mheshimiwa Mbunge, baadhi yetu tunaosoma sana magazeti tunaelewa kuwa Rostam Aziz hajaanza leo kukuchafua. Ameanza tangu Kamati Teule ya Bunge iwasilishe taarifa yake Bungeni mwezi Februari mwaka juzi, 2007 kupitia magazeti yake lukuki ya Mtanzania, Rai, Tazama, Tanzania Leo, Nyundo, Sauti ya Umma, Taifa Tanzania, the African n.k. Tangu muda huo, siku haipiti bila habari au maoni au makala moja au zaidi inayomshambulia Mbunge wa Kyela: mara kaiba maji ya DAWASCO, mara yeye na wenzake waliandika taarifa yao baada ya muda kupita; mara si mwanamtandao; mara anatumiwa na maadui wa Lowassa na Rostam na mambo mbalimbali ya kipuuzi ambayo yamekuja onekana baadaye kuwa uongo mtupu.

Lengo kuu la Rostam Aziz linajulikana kwa Watanzania wote, hata sisi wananchi wa kawaida tu: kuwasafisha wale wote waliohusishwa na kashfa ya Richmond na kuwabeza na kuwazomea wale wote waliokuwa wajumbe wa Kamati Teule ya Bunge.
Tunazo taarifa za uhakika za mafisadi kukutana mara kwa mara kupanga njia za kuwamaliza kisiasa na hata kuwaua wanasiasa jasiri wanaotetea maslahi ya Taifa, ukiwemo Mbunge wetu. Vyombo husika vya dola visilifanyie mzaha suala hili. Ni hatari kwa mstakabali wa Taifa letu!

Tumeona kwa masikitiko makubwa kuwa Rostam akiguswa kidogo tu, kama ambavyo Mbunge wetu ulivyomgusa tarehe 17 mwezi huu, viongozi waandamizi wa CCM wanajitokeza mara moja kuingilia kati. Bahati nzuri Mbunge wetu hukufungua tena mdomo, lakini Rostam Aziz kwa kutumia magazeti yake hayo ya udaku, ameendelea na kampeni yake hiyo chafu bila wasiwasi na bila kukemewa.

Sisi wapigakura wa Kyela tunajiuliza na tunataka kujua: Je hii ni sera ya CCM? Je, Rostam anaendesha mchezo huu mchafu tena kwa muda mrefu dhidi ya viongozi wenzake kwa Baraka za Chama? Kama si hivyo, mbona Chama cha Mapinduzi hakikemei mchezo huo mchafu wa Rostam?

Mheshimiwa Mbunge, leo wapigakura wa Kyela tunamtumia Rostam Aziz ujumbe ufuatao: Pamoja na mbinu zake za kifisadi, hawezi kumwondoa mbunge wetu madarakani! Vilevile Bwana Rostam atambue kuwa Dk. Mwakyembe alichaguliwa na asilimia 93 ya wapigakura wa Kyela na atake asitake katika uchaguzi mkuu mwakani wana-Kyela tunasema: RAIS NI JAKAYA MRISHO KIKWETE na MBUNGE NI HARRISON GEORGE MWAKYEMBE!

Tunamtahadharisha Rostam Aziz kuwa kama huko nyuma alizoea kuwaangusha watu kwa kutumia vijigazeti vyake hivyo vya kigaidi, safari hii amekwaa kisiki cha mpingo!
Tunaomba vilevile tutume ujumbe wa pili kwa CCM. Wana-Kyela tunaipenda sana CCM, chama cha Baba wa Taifa ambaye daima tutampenda na kumuenzi! Ili CCM ipate ushindi wa uhakika na wa kishindo mwakani, lazima iandae mazingira mazuri kwa ushindi huo: iwaondoe katika safu ya uongozi watu wote wenye tuhuma za ufisadi. Kwa mfano, tunaelezwa na vyombo vya habari vinavyoaminika kuwa Rostam Aziz ana tuhuma ya kuchota fedha za EPA zaidi ya shilingi bilioni 40 kupitia kampuni yake ya KAGODA, lakini bado ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM!

Hivi, CCM bila Rostam Aziz na mafisadi wenzake, haiwezekani? Mheshimiwa Mbunge, kwa hayo machache tunaomba tusikie sauti yako na sisi tutakuwa mabalozi kwa wenzetu wengine ambao hawakuelezwa na hawajafika hapa.

Kyela Oyee!!! Mwakyembe Oyee!!! Rostam Aziz na Mafisadi Wenzake ziiiii!!!

Imesomwa na Gabriel Mwakalinga, Katibu wa Kamati ya Maadalizi ya Maandamano ya Amani ya Wapigakura wa Kyela, tarehe 29 Machi, 2009.
 
ILI CCM IPATE USHINDI MKUBWA MWAKANI:

KYELA WATAKA MAFISADI WAACHIE NGAZI

Na Mwandishi Wetu, Kyela

Wapigakura Wilayani Kyela wamewataka wanaCCM wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi kung'atuka mapema ili Chama hicho kipate ushindi wa kishindo kwenye Uchaguzi Mkuu mwakani.

Katika Risala waliyomsomea Mbunge wao Dk. Harrison Mwakyembe katika Uwanja wa Mwakangale mjini hapa juzi Jumapili, wamesema kung'atuka kwao mapema kutakuwa kielelezo cha ukomavu wao kisiasa.

"Ili CCM ipate ushindi wa uhakika na wa kishindo mwakani, lazima iandae mazingira mazuri kwa ushindi huo: iwaondoe katika safu ya uongozi watu wote wenye tuhuma za ufisadi", walisema.

Risala hiyo iliyosomwa kwa niaba ya wenzake na mtaalamu wa teknolojia ya habari Gabriel Mwakalinga, ilitoa mfano wa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ambaye "ana tuhuma za kuchota fedha za EPA zaidi ya shilingi bilioni 40 kupitia kampuni yake ya KAGODA, lakini bado ni Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM".

"Hivi CCM bila Rostam Aziz na mafisadi wenzake haiwezekani?" Risala hiyo iliuliza na kumtaka Mbunge wa Kyela asivunjwe moyo na kampeni ya majitaka ya mafisadi.

Risala hiyo iliongeza kuwa lengo kuu la kampeni hiyo ya majitaka inaeleweka kuwa ni "kuwasafisha wale wote waliohusishwa na kashfa ya Richmond na kuwabeza na kuwazomea wale wote waliokuwa wajumbe wa Kamati Teule ya Bunge, hasa Mbunge wetu uliyekuwa Mwenyekiti."

"Pamoja na mbinu zao za kifisadi, hawawezi kumwondoa Mbunge wetu madarakani. ... watake wasitake katika uchaguzi mkuu ujao Rais ni Jakaya Kikwete na Mbunge ni Harrison Mwakyembe", risala ilidai.

"Tunamtahadharisha Rostam Aziz kuwa kama huko nyuma alizoea kuwaangusha watu kwa kutumia vijigazeti vyake hivyo vya kigaidi, safari hii amekwaa kkisiki cha mpinmgo na amekamata pasipo kamatika", ilimalizia.

Akijibu risala hiyo katika mkutano uliotanguliwa na maandamano ya amani yaliyovunjwa na Polisi kwa madai kuwa yangevuruga ziara ya Naibu waziri wa Fedha ambaye jina lake halikutajwa, Dk. Mwakyembe aliwashukuru wapigakura wake kwa imani kubwa waliyonayo kwake.

Alitumia zaidi ya dakika 15 kupangua hoja alizoziita za "Rostam Aziz na magazeti yake" kuwahakikishia wapigakura wake kuwa hakuvunja sheria wala kanuni za Bunge na hajawa na mgongano wowote wa kimaslahi.

"Kinachojitokeza hapa ni hasira za mafisadi kunyang'anywa kitumbua mdomoni kutokana na maamuzi ya Bunge kuinyang'anya Richmond na Dowans mradi wa kufua umeme kwa kutumia gesi asilia. Baada ya mipango yao ya kuiuzia Serikali mitambo chakavu kushindikana hasira zote zimeelekezwa kwangu", amedai.

Huku akishangiliwa kwa nguvu na umati mkubwa uliokusanyika uwanjani hapo, Dk. Mwakyembe aliwahakikishia wapigakura wake kuwa hawezi kuvunjwa moyo kwa kampeni ya majitaka ya magazeti yanayomilikiwa na mtu "asiye na staha na taadhima stahili" katika jamii ya Watanzania.

Alimtuhumu Rostam Aziz kutumia mbinu za wezi wa Kariakoo kwa kupiga kelele za "mwizi, mwizi" wao wenyewe wanapofukuzwa kwa kupora mali ya wengine.

"Rostam anakabiliwa na tuhuma nyingi za kifisadi. Amevigeuza kuwa bohari za vipuri na vifaa vya kuchimbia madini viwanda vyetu vya ngozi alivyovinunua kwa lengo la kuviendeleza; ni mmoja wa watu wanaotuhumiwa kuchota mabilioni ya fedha kutoka kwenye mfuko wa Import Support; ana tuhuma za kumiliki Dowans na Kagoda.

"Ili wananchi wasiendelee kumhoji kwa ufisadi huo, anatumia magazeti yake kuwazulia tuhuma wana-CCM wenzake kwa zamu: atazua jambo kuhusu Mwakyembe, atamrukia Spika Sitta, mara Selelii, mara Mama Anne Kilango, mara Ole Sendeka na kadhalika", alisema.

Dk. Mwakyembe aliwaambia wapigakura wake waliotulia kumsikiza kuwa alifarijika sana kusoma bango lenye maneno KIKWETE NJIA NYEUPE MWAKANI, PAMBANA NA MAFISADI na kusisitiza kuwa Rais Kikwete kafanya mengi mazuri kwa Kyela na nchi, hivyo anastahili kuungwa mkono.

Aliungana na wapigakura wake kuwataka wana CCM wote wanaoandamwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi kuachia ngazi kwenye Chama kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanakiokoa Chama chao.

"Kung'atuka ni hatua ya ukomavu wa kisiasa na ishara ya mapenzi kwa Chama chako. Nawaomba wasisubiri mpaka wang'olewe, wajiondoe wenyewe ili Chama kifanikiwe katika Uchaguzi Mkuu mwakani", alisema.

Mkutano huo ulitanguliwa na maandamano ya amani kulaani magazeti yanayojaribu kumchafua Mbunge wao na kumpa moyo aendelee na mapambano dhidi ya ufisadi. Maandamano hayo yalivunjwa na Jeshi la Polisi kwa amri ya Kamanda Mkuu wa Polisi wa Mkoa licha ya kwamba vyombo vya usalama wilaya viliisharishia yafanyike.

Wakazi wa Kyela wanamlaumu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile na Mkuu wa Wilaya mstaafu wa Kyela, Mashimba Hussein Mashimba, kwa kuvuruga maandamo hayo ya amani. Viongozi hao walionekana wakikutana kwa faragha kabla ya maadamano hayo na kuwapigia simu baadhi wa watu maarufu wa Kyela kusitisha maadamano hayo.

Wananchi wengine walishangazwa na kitendo cha Mashimba kujiingiza kwenye masuala yasiyomhusu kwani alishastaafishwa.

Dk. Mwakyembe aliwapa pole wananchi kwa usumbufu na kuahidi kumlalamikia rasmi Rais Kikwete kuhusu ubabe wa kitoto unaofanywa na uongozi wa Mkoa bila kujali madhara ya ubabe wao kisiasa.

"Kwa akili yao finyu wanadhani wanamkomoa Mwakyembe, kumbe wanamharibia aliyewateua kwa wananchi", alisema.

mwisho
 
Hi hakuna lolote hapa wote ni mafisadi..mwakyembe ni fisadi pia....kilichmtoa university kujiunga na ccm kugombea ni ulaini wa kuukata ukiingia ccm ni kupata chako mapema.. Waliona yale wakati wa mkapa ukiingia ccm umeukata kuna mteremko wa kukomba mali...hilo ndio alofata mwakyembe ..hilo ndilo alofata rostam...wote malengo yao ni hayo.....lakini rafiki ytangu mwakyembe ameingia ccm tayari amechelewa...mambo magumu..hamna tena chagua chako mapema...watu wa mkapa wamemaliza kila kitu....sasa anaanzisha siasa za mtikila za ugozi...za walalahoi...kwani ccm wako watu weupe wangapi jamani.....huyu ni mkabila mbaguzi na mdini....kwake yeye rostam ndio matatizo ya watanzania..wakati tatizo ni ccm...sera mbovu...na uongozi mbovu......hivi...nani anahoji...songas mkataba uko vipi...wanazalisha gesi...ujazo gani kwa mwaka....kwanini songas wasiuze gas kwa tanesco kwa bei ya chini ili tupate umeme wa uhakika ? Lakini kwa sababu wale ni wazungu basi kwa asili ya mnyachusa hawezi kuhoji mzungu.....kwao ni kama waungu..lakini mhindi ama mwarabu basi kwake tatizo..amesahau kama yeye amesomeshwa na prof. Issa shivji ni mhindi na sio mweusi....lakini mwakywembe anasema ngozi nyeusi hawatakiwi kuendelea....ni muongo .....na mbaguzi anastahili kuogopewa kama ukoma chambilicho nyerere..
Hizi hoja za epa na richmond zote zimeibuliwa na wapinzani sio ccm ....sasa huyu aache kutupotezea lengo.....kama kweli alikua anauchungu na uoza ulipo basi mwakyembe angegombea ubunge kupitia upinzani..lakini wapi alifata utamu ulipo ccm waku chuma mapema kama alivoingia rostam....
Wanaiba kweli hathubutu kuwasema....watu wanakomba dhahabu kama tanzania haina wenyewe.....lakini.....dhahabu za wazungu kimyaaaaaaaaaaa .
Mwakyembe ndugu yangu........umechelewa ...ccm ina wenyewe na weyewe wameshakomba kila kiti....hata kingunge tayari ana parking system sasa wewe......umechelewa unabaki kuimba rostam.....weeeee
 
Kuna mambo mawili yanahitaji kusahihishwa hapa.

La kwanza ni maelezo kwamba waandishi wa habari waliopo Kyela walipigwa marufuku kwa sababu wanamwandika vibaya, hilo sio kweli hata kidogo, na ni uzushi mkubwa. Kyela wapo waandishi wa habari wa kujitegemea wawili tu na wasio na chombo maalumu cha kukiandikia, na siku hiyo walikuwepo na ushahidi ni Richard Kilumbo ambaye siku hiyo alipeleka habari hiyo Tanzania Daima baada ya kuombwa na mwakilishi wa gazeti hilo mkoani Mbeya ambaye siku hiyo alikuwa Dar, hivyo alishirikiana na mwenzie kutoka Mbeya. Wawakilishi wa makampuni ya habari wote wako Mbeya mjini hivyo husambaa kule kwenye tukio kubwa kwa mkoa kwa wakati ule, ni magazeti machache sana yenye waandishi wake wilayani. Waandishi waliokuwepo Kyela siku hiyo walifika kila mtu mmoja kwa utaratibu wake, baadhi ni baada ya kupata maelekezo toka kwa wahariri wao Dar na wengine waliandamana na Naibu Waziri wa Fedha ambaye siku hiyo alienda Kyela na wengine walienda rasmi kwa ajili ya mkutano huio baada ya kupata taarifa kutoka mjini kyela kuhusu kuwepo maandamano na mkutano.

Pili ni suala la hisa, alichokiri ni kushiriki kwake kwenye kuisimamisha hiyo Kampuni na kwamba suala la hisa watu wakaangalie records za kampuni hiyo kuanzia 2007 hawatalikuta jina lake humo hivyo kuwashauri wanaoshikia bango hilo kufanya utafiti na sio kuendesha propaganda zinazodhalilisha hata elimu waliyonayo.

Nimeona niweke sawa mambo hayo mawili kwani yanapotosha hata uchangiaji wa hoja husika.

Nsesi,

Hao waandishi wa Kyela wawili unaowasema umeongea nao kuthibitisha ulichokiandika hapo juu? Hao waandishi mimi nilikaa nao kule nyuma kabisa na walipigwa marufuku ndio maana hawakusogelea lile jukwaa kama inavyokuwa kawaida yao kwenye mikutano mingine.

Kwa taarifa yako hao vijana wanafahamiana na hao waandishi kutoka Mbeya na walikuwa wote hata kwenye internet cafe kabla ya mkutano huo. Hao waandishi kutoka Mbeya ndio waliwataka hao vijana waende wote lakini wakasema wao wamepigwa marufuku.

Kama unataka uhakika kwanini hao vijana hawakuwa pale mbele sawa na waandishi wengine, basi wapigie simu wao wenyewe kuwauliza. Au mpatie mwana JF mwingine yeyote namba yao awaulize, mmoja wao anaitwa Mwaisaka na mwulize ilikuwaje hakuwa kule mbele?

Hata diwani wa Kyela mjini ambaye kikawaida ndiye alitakiwa awe mwenyeji wa mkutano huo naye hakutakiwa kule mbele, alikuja kimya kimya na kukaa kule nyuma akisikiliza.

Ule mkutano ulikuwa na mizengwe mingi sana. Pia ukweli ni kwamba uliandaliwa na mbunge mwenyewe na wapambe wake kinyume na hao waandishi walivyoonyesha. Ule mkutano wa kumpongeza Mwakyembe baada ya Richmond ni kweli uliandaliwa na wananchi na kweli wana Kyela wa kila aina walishiriki. Huu wa sasa ilikuwa siasa tu na kudanganya watu.

Hiyo risala wanasema walimtumia mwaliko mbunge siku ya Jumamosi? Ujinga mtupu, vijana wa Mwakyembe walikuwa wanatangaza huo mkutano toka Jumatano. Mimi niliambiwa kule boarder na vijana kwamba mbunge amewaita eti wakamsafishe, sasa hivi anasema yeye ndiye alialikwa? Kweli siasa ni utapeli. Hiyo risala mbona kama imeandikwa na Mwakyembe mwenyewe?
 
Last edited:
Tumejikita kuzungumzia ufisadi wa ngazi za kitaifa na kimataifa na kusahau kuwa nchi inaliwa katika ngazi ya halmashauri. Ukiangalia ripoti ya CAG kwa kweli utashangaa jinsi ambavyo tusivyoshitushwa na wizi unaofanywa katika ngazi za halmashauri. na ninaamini kwua wizi huu ni mbaya zaidi kwa sababu kinachoibwa ni kile kilichokuwa budgeted for development activities, wala si ten percent

MN, sikubaliani na dhana yako ya kutaka kuonyesha wizi ngazi ya Kitaifa athari yake ni ndogo ukilinganisha na ngazi za halmashauri. Kama unaufahamu wizi wowote ule hata kama ni ngazi ya halmashauri haujakatazwa kuuweka hapa jamvini tuujadili. Je, wizi wa EPA wa shilingi 133 billioni ulikuwa ni 10% ya kiru gani? Je, wizi wa Meremeta wa shilingi 155 billioni ulikuwa ni 10% ya kitu gani? Je, wizi wa shilingi 200 billioni uliofanywa na fisadi Rostam na makampuni yake ya kifisadi Richmond/Dowans ulikuwa ni 10% ya kitu gani!!!? Ni kosa kubwa kutaka kuonyesha wizi ngazi ya kitaifa athari yake si kubwa kama ule wa halamshauri.
 
Hii ndiyo risala ya wapigakura wa Kyela kwa Mbunge wao

RISALA YA WAPIGAKURA WA KYELA KWA MBUNGE WA KYELA DK. HARRISON MWAKYEMBE JUMAPILI TAREHE 29 MACHI, 2009

Mheshimiwa Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, awali ya yote sisi wapigakura wa Wilaya ya Kyela tunakupa pole kwa msiba uliokupata hivi karibuni wa mama yetu mpenzi, Tukusuma Kibole Mwakyembe. Ninawaomba wapigakura wenzangu wote tuliopo uwanjani hapa tukae kimya kwa dakika moja kwa heshima na kumbukumbu ya marehemu. Ahsanteni.

Mheshimiwa Mbunge, naomba vilevile nikushukuru kwa kukubali mwaliko wetu (tuliokutumia rasmi jana jioni) wa kuyapokea maandamano haya yaliyoanzia Community Centre mpaka hapa Uwanja wa Mwakangale. Madhumuni ya maandamano haya ni kuelezea hisia zetu na kupata maelezo yako kuhusu maana na lengo la kampeni ya chuki ya magazeti yanayomilikiwa na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz. Mbali na kuonyesha dhahiri nia ya kutaka kukuchafua tu kisiasa, magazeti hayo sasa yanadai Mbunge wetu uondolewe ubunge.

Mheshimiwa Mbunge, katika toleo la Machi 24 hadi 30 mwaka huu la gazeti la TAZAMA, moja ya magazeti lukuki anayomiliki Rostam, imeelezwa bayana kwamba utasimamishwa ubunge. Taarifa hii imetushitua sana wapigakura wa Kyela na kutufanya wengi tujiulize KULIKONI? Rostam Aziz, pamoja na kwamba ni fisadi asiyeguswa nchi hii, kapata wapi nguvu na mamlaka ya kumwondoa Mbunge aliyechaguliwa kwa asilimia 93 ya wapiga kura wa Kyela?

Kiu yetu kubwa ya kutaka kuujua ukweli, imezaa wazo la kuja hapa uwanjani leo hii ili utupe picha sahihi badala ya kutegemea maelezo ya juujuu ya magazeti ambayo tayari yamegubikwa na ushabiki.

Mheshimiwa Mbunge, wapigakura wa Kyela tulikusikiliza kwa makini sana ulipoongea na vyombo vya habari Dar es Salaam tarehe 17, mwezi huu. Tulielewa kuwa kampuni hiyo anayoiimba Rostam usiku kucha (ili kukulaumu mbunge wetu) haikuwa miongoni mwa makampuni yaliyojitokeza na kushiriki kwenye mchakato wa zabuni ya umeme wa dharura, na kwamba pamoja na uchanga wake kampuni hiyo ambayo imeanzishwa kushughulikia nishati ya upepo isingeweza kushiriki kwenye zabuni iliyolenga uzalishaji umeme kwa kutumia gesi asilia tuliyonayo. Sasa katika hali hiyo, mgongano wa kimaslahi ambao Rostam Aziz anauimba kila kukicha utokee wapi kama si porojo na uchochezi tu wa kisiasa?

Ikiwa sisi wapigakura wa Kyela (pamoja na uelewa wetu mdogo) tulikuelewa, ni nini kinamfanya Rostam Aziz asielewe? Ni nini kinamfanya kiongozi mwandamizi wa CCM, kama Rostam (ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM) ahangaike kiasi hicho kujaribu kumbomoa kiongozi mwenzake wa CCM, ambaye pia ni Mjumbe wa NEC? Mheshimiwa Mbunge sisi wapigakura wako tunakuomba leo utueleweshe, tujue: KULIKONI!

Mheshimiwa Mbunge, baadhi yetu tunaosoma sana magazeti tunaelewa kuwa Rostam Aziz hajaanza leo kukuchafua. Ameanza tangu Kamati Teule ya Bunge iwasilishe taarifa yake Bungeni mwezi Februari mwaka juzi, 2007 kupitia magazeti yake lukuki ya Mtanzania, Rai, Tazama, Tanzania Leo, Nyundo, Sauti ya Umma, Taifa Tanzania, the African n.k. Tangu muda huo, siku haipiti bila habari au maoni au makala moja au zaidi inayomshambulia Mbunge wa Kyela: mara kaiba maji ya DAWASCO, mara yeye na wenzake waliandika taarifa yao baada ya muda kupita; mara si mwanamtandao; mara anatumiwa na maadui wa Lowassa na Rostam na mambo mbalimbali ya kipuuzi ambayo yamekuja onekana baadaye kuwa uongo mtupu.

Lengo kuu la Rostam Aziz linajulikana kwa Watanzania wote, hata sisi wananchi wa kawaida tu: kuwasafisha wale wote waliohusishwa na kashfa ya Richmond na kuwabeza na kuwazomea wale wote waliokuwa wajumbe wa Kamati Teule ya Bunge.
Tunazo taarifa za uhakika za mafisadi kukutana mara kwa mara kupanga njia za kuwamaliza kisiasa na hata kuwaua wanasiasa jasiri wanaotetea maslahi ya Taifa, ukiwemo Mbunge wetu. Vyombo husika vya dola visilifanyie mzaha suala hili. Ni hatari kwa mstakabali wa Taifa letu!

Tumeona kwa masikitiko makubwa kuwa Rostam akiguswa kidogo tu, kama ambavyo Mbunge wetu ulivyomgusa tarehe 17 mwezi huu, viongozi waandamizi wa CCM wanajitokeza mara moja kuingilia kati. Bahati nzuri Mbunge wetu hukufungua tena mdomo, lakini Rostam Aziz kwa kutumia magazeti yake hayo ya udaku, ameendelea na kampeni yake hiyo chafu bila wasiwasi na bila kukemewa.

Sisi wapigakura wa Kyela tunajiuliza na tunataka kujua: Je hii ni sera ya CCM? Je, Rostam anaendesha mchezo huu mchafu tena kwa muda mrefu dhidi ya viongozi wenzake kwa Baraka za Chama? Kama si hivyo, mbona Chama cha Mapinduzi hakikemei mchezo huo mchafu wa Rostam?

Mheshimiwa Mbunge, leo wapigakura wa Kyela tunamtumia Rostam Aziz ujumbe ufuatao: Pamoja na mbinu zake za kifisadi, hawezi kumwondoa mbunge wetu madarakani! Vilevile Bwana Rostam atambue kuwa Dk. Mwakyembe alichaguliwa na asilimia 93 ya wapigakura wa Kyela na atake asitake katika uchaguzi mkuu mwakani wana-Kyela tunasema: RAIS NI JAKAYA MRISHO KIKWETE na MBUNGE NI HARRISON GEORGE MWAKYEMBE!

Tunamtahadharisha Rostam Aziz kuwa kama huko nyuma alizoea kuwaangusha watu kwa kutumia vijigazeti vyake hivyo vya kigaidi, safari hii amekwaa kisiki cha mpingo!
Tunaomba vilevile tutume ujumbe wa pili kwa CCM. Wana-Kyela tunaipenda sana CCM, chama cha Baba wa Taifa ambaye daima tutampenda na kumuenzi! Ili CCM ipate ushindi wa uhakika na wa kishindo mwakani, lazima iandae mazingira mazuri kwa ushindi huo: iwaondoe katika safu ya uongozi watu wote wenye tuhuma za ufisadi. Kwa mfano, tunaelezwa na vyombo vya habari vinavyoaminika kuwa Rostam Aziz ana tuhuma ya kuchota fedha za EPA zaidi ya shilingi bilioni 40 kupitia kampuni yake ya KAGODA, lakini bado ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM!

Hivi, CCM bila Rostam Aziz na mafisadi wenzake, haiwezekani? Mheshimiwa Mbunge, kwa hayo machache tunaomba tusikie sauti yako na sisi tutakuwa mabalozi kwa wenzetu wengine ambao hawakuelezwa na hawajafika hapa.

Kyela Oyee!!! Mwakyembe Oyee!!! Rostam Aziz na Mafisadi Wenzake ziiiii!!!

Imesomwa na Gabriel Mwakalinga, Katibu wa Kamati ya Maadalizi ya Maandamano ya Amani ya Wapigakura wa Kyela, tarehe 29 Machi, 2009.

Mkuu Nsesi,

Hii risala iliandikwa na Wana Kyela?

Sijafika Kyela mwaka mmoja sasa, inaelekea ndugu zangu wamepiga hatua mbele sana mpaka wanasoma magazeti kama The African.

Pia nimefurahi kusoma kwamba waliweza kumsikiliza mbunge wao kwa makini alipoongea
Dar. Hii ilikuwa kwenye radio au kwenye TV? Huko nyuma ilikuwa haiwezekani hata wana Kyela 100 wamsikilize mbunge wao akiongea kwenye TV maana sehemu za kufanya hivyo ni za kuhesabika. Mwaka mmoja ni mrefu labda sasa Kyela imepiga hatu kubwa mbele. Tumpongeze sana mbunge wetu kwa kuwasukumia mawasiliano ya karibu wananchi wa Kyela mpaka wanaweza kumsikiliza kwa wingi na kwa makini akilonga tokea Dar.

Kwi kwi kwi!!!! I love JF!
 
Nsesi,

Hao waandishi wa Kyela wawili unaowasema umeongea nao kuthibitisha ulichokiandika hapo juu? Hao waandishi mimi nilikaa nao kule nyuma kabisa na walipigwa marufuku ndio maana hawakusogelea lile jukwaa kama inavyokuwa kawaida yao kwenye mikutano mingine.

Kwa taarifa yako hao vijana wanafahamiana na hao waandishi kutoka Mbeya na walikuwa wote hata kwenye internet cafe kabla ya mkutano huo. Hao waandishi kutoka Mbeya ndio waliwataka hao vijana waende wote lakini wakasema wao wamepigwa marufuku.

Kama unataka uhakika kwanini hao vijana hawakuwa pale mbele sawa na waandishi wengine, basi wapigie simu wao wenyewe kuwauliza. Au mpatie mwana JF mwingine yeyote namba yao awaulize, mmoja wao anaitwa Mwaisaka na mwulize ilikuwaje hakuwa kule mbele?

Hata diwani wa Kyela mjini ambaye kikawaida ndiye alitakiwa awe mwenyeji wa mkutano huo naye hakutakiwa kule mbele, alikuja kimya kimya na kukaa kule nyuma akisikiliza.

Ule mkutano ulikuwa na mizengwe mingi sana. Pia ukweli ni kwamba uliandaliwa na mbunge mwenyewe na wapambe wake kinyume na hao waandishi walivyoonyesha. Ule mkutano wa kumpongeza Mwakyembe baada ya Richmond ni kweli uliandaliwa na wananchi na kweli wana Kyela wa kila aina walishiriki. Huu wa sasa ilikuwa siasa tu na kudanganya watu.

Hiyo risala wanasema walimtumia mwaliko mbunge siku ya Jumamosi? Ujinga mtupu, vijana wa Mwakyembe walikuwa wanatangaza huo mkutano toka Jumatano. Mimi niliambiwa kule boarder na vijana kwamba mbunge amewaita eti wakamsafishe, sasa hivi anasema yeye ndiye alialikwa? Kweli siasa ni utapeli. Hiyo risala mbona kama imeandikwa na Mwakyembe mwenyewe?

Wizi mtupu!!! Fisadi Rostam kaamua kutumia mabilioni yake aliyoyapata kwa njia za haramu kuwapa baadhi ya Watanzania kitu kidogo ili wampiganie vita vyake ambavyo sasa inaelekea vinamuelemea!!! Kweli baadhi ya Watanzania ni wanafiki wakubwa siku zote watajali maslahi yao badala ya yale Taifa!! Sasa wameamua kumsafisha fisadi Rostam kwa kila hali ikiwemo kumpaka matope Mwakyembe na yeyote yule ambaye hayuko upande wa mafisadi. Hili halitakubalika hata siku moja, siku zote tutasimamia upande wa haki. Mwakyembe hana tuhuma zozote dhidi yake ya kutufisadi Watanzania hata kwa senti tano, lakini huyo fisadi Rostam mnayemtetea kishatufisadi shilingi 240 billioni. Imagine kiasi hiki cha fedha kingefanya mambo makubwa mangapi ili kuinua viwango vya maisha ya Watanzania ambao wengi wao wanaishi katika ufukara wa kutisha. Wizi mtupu!!!
 
MN, sikubaliani na dhana yako ya kutaka kuonyesha wizi ngazi ya Kitaifa athari yake ni ndogo ukilinganisha na ngazi za halmashauri. Kama unaufahamu wizi wowote ule hata kama ni ngazi ya halmashauri haujakatazwa kuuweka hapa jamvini tuujadili. Je, wizi wa EPA wa shilingi 133 billioni ulikuwa ni 10% ya kiru gani? Je, wizi wa Meremeta wa shilingi 155 billioni ulikuwa ni 10% ya kitu gani? Je, wizi wa shilingi 200 billioni uliofanywa na fisadi Rostam na makampuni yake ya kifisadi Richmond/Dowans ulikuwa ni 10% ya kitu gani!!!? Ni kosa kubwa kutaka kuonyesha wizi ngazi ya kitaifa athari yake si kubwa kama ule wa halamshauri.

Bubu Ataka Kusema,

Wizi wowote ni mbaya, juhudi lazima zifanywe kukabiliana na madhambi yote Tanzania. Kuanzia kwa wanasiasa mpaka sisi wenyewe maofisini ambao tunanyanyasa Watanzania kila siku kwasababu mbalimbali.

It's simplistic kuamini matatizo yetu yote ni Rostam. Sawa tuendelee kumwandama Rostam na mafisadi wengine wote na wakati huo huo kuendelea kuboresha capacity kwenye sehemu mbalimbali hasa kwenye halmashauri ambako pesa nyingi sana zinatumiwa vibaya. Wakati mwingine sio ufisadi au wizi, ni uwezo mdogo wa kuamua lipi linafaa na lipi halifai. Wabunge ni wajumbe wa vikao hivi vya halmashauri, mimi ningependa kuwaona ndio wanasaidia kuongeza uwezo kwenye hizo halmashauri. Bahati mbaya wengi wao huwa hawahudhurii hivyo vikao hata kwa muda ule ambao hawawi bungeni.

Tujitahidi kupambana na matatizo ya Tanzania kwa pamoja (holistic approach).
 
One is innocent until proved otherwise by the courts of law beyond reasonable doubt

hiyo ndiyo status aliyonayo Rostam sasa hata mpige makelele kiasi gani hakuna mahakama iliyomhukumu kuwa ni fisadi

money.jpg

labda mngeweza kupunguza emotions zenu na kujadili mambo based on facts

narudia kusema leo hii matatizo yetu tunayajua lakini tunaweka pamba masikioni tuuu

na hatari zaidi ni hizi politics on envy ambazo hazitotufikisha kokote kule
 
Mtanzania, hauko peke yako wenye wazo kama hilo kuhusu usomaji magazeti. Lakini ukweli ni kwamba Kyela ni wasomaji wazuri wa magazeti na wasambazaji wazuri wa kile walichokisoma au kukisikiliza hususani kwa habari zinazowahusu. Kyela ni miongoni mwa wilaya zenye mauzo mazuri ya magazeti ndio maana hata mgawo wake uko juu. Hakuna Kampuni inayopeleka chini ya gazeti (daily serious papers) 50 kwa siku, ni Mtanzania tu ambao wameshuka hadi 20!

Ukiondoa jiji la Mbeya, sehemu zenye wasomaji kwa mujibu wa mauzo ya makampuni mbali mbali ni Kyela, Tukuyu na Vwawa, mji wa Tunduma ni kwa magazeti ya michezo zaidi. Kwa mfano hilo hilo The African lilipotoa umuhimu kwa habari dhidi ya hatua ya DC Mashimba kuzuia harambee ya kina mama wauza mchele pale Kyela mijini kwa misingi ya kisiasa hakukuwa na mabaki, hata asiyeielewa hiyo lugha alinunua kwa ajili ya kumbukumbu!

Hivyo Mkuu usishangae sana katika hilo, hiyo ndiyo Kyela. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya kabla ya 2006, Evarista Kalalu aliwahi nichekesha kuhusu wilaya hiyo aliposema, "anzisha jambo hapa ulipo baada ya nusu saa taarifa zitafika katika kila nyumba wilayani humo!"

Usisahau pia kuwa ni wilaya yenye wastaafu kibao na vijana kama Mwakalinga walioishi Marekani kwa miaka lukuki leo hii wamerudi nyumbani kwao Kyela.
 
RA ameleta umafia TZ na huo umafia wake utammaliza yeye mwenyewe asubiri tu ipo siku TZ itaongozwa na kiongozi makini na mwadilifu.
 
Mtanzania, hauko peke yako wenye wazo kama hilo kuhusu usomaji magazeti. Lakini ukweli ni kwamba Kyela ni wasomaji wazuri wa magazeti na wasambazaji wazuri wa kile walichokisoma au kukisikiliza hususani kwa habari zinazowahusu. Kyela ni miongoni mwa wilaya zenye mauzo mazuri ya magazeti ndio maana hata mgawo wake uko juu. Hakuna Kampuni inayopeleka chini ya gazeti (daily serious papers) 50 kwa siku, ni Mtanzania tu ambao wameshuka hadi 20!

Ukiondoa jiji la Mbeya, sehemu zenye wasomaji kwa mujibu wa mauzo ya makampuni mbali mbali ni Kyela, Tukuyu na Vwawa, mji wa Tunduma ni kwa magazeti ya michezo zaidi. Kwa mfano hilo hilo The African lilipotoa umuhimu kwa habari dhidi ya hatua ya DC Mashimba kuzuia harambee ya kina mama wauza mchele pale Kyela mijini kwa misingi ya kisiasa hakukuwa na mabaki, hata asiyeielewa hiyo lugha alinunua kwa ajili ya kumbukumbu!

Hivyo Mkuu usishangae sana katika hilo, hiyo ndiyo Kyela. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya kabla ya 2006, Evarista Kalalu aliwahi nichekesha kuhusu wilaya hiyo aliposema, "anzisha jambo hapa ulipo baada ya nusu saa taarifa zitafika katika kila nyumba wilayani humo!"

Usisahau pia kuwa ni wilaya yenye wastaafu kibao na vijana kama Mwakalinga walioishi Marekani kwa miaka lukuki leo hii wamerudi nyumbani kwao Kyela.

Mkuu Nsesi,

Hiyo risala haijaandaliwa na watu wanaokaa Kyela, huo ndio ukweli wenyewe.

Kwa anayeijua Kyela vizuri, akisoma tu atagundua imeandaliwa na watu ambao hawaishi na kushinda Kyela.

Mafanikio mema kwenye vita hivi vya propaganda. Laiti tu tungetumia usomi wetu kuelemisha watu na kuwaambia ukweli badala ya kujiingiza kwenye propaganda ambazo hazimwongezei tija mwananchi wa Kyela.

Nimeisoma hiyo risala mara kadhaa, nafikiri ninajua nani wameiandika.

Hilo la habari kufika kila nyumba ni kwasababu ya majungu ya Kyela. Vijana hawana kazi za kufanya na wamefanya mtaji wa majungu na kukosanisha wanasiasa kama biashara yao ya kuwafanya waishi mjini. Ni aibu kweli kwa wilaya kama Kyela na resources zote hizo kutegemea Rungwe hata kwa mchicha, huku vijana wamejaa vijiweni wanasubiri waheshimiwa wakawape pesa ya soda.
 
Ukweli ni kwamba huyu mheshimiwa RA ni fisadi wa kutosha. sasa kapata upenyo wa kuwalaghai wasio na access na informations ili ajaribu kupaka matope wote wanaompinga na kuwatisha wengine wanaotaka kumpinga.

Huyu ni fisadi asiyeweza kujificha lkn ukitaka kujua ni vp alivyokomaa kifisadi, haoni aibu kabisa kuendelea kutaka kunyonya watanzania.

Kashiriki kikamilifu akisaidiana na ndugu zake wa estate kwenye ufisadi wa mashamba ya mpunga kule mbeya Mbarali.
 
mahakama gani imemhukumu?
 
..
Inasemekana kuwa TAKUKURU wameshakabidhi reports zao nyingi kwa DPP kuhusiana na kesi mbalimbali zinazowahusu baadhi ya viongozi wa serikali. Kuliwahi kutokea malalamiko kutoka TAKUKURU kuhusiana na hatua ambazo DPP alitakiwa kuchukua, lakini hakufanya hivyo. Inasemekana pia kuwa DPP hajaridhishwa na utoshelezi wa uthibitisho wa hatia za watuhumia. Hakuna report za TAKUKURU zinazopelekwa Bungeni kwasababu zozote. Kumbuka Kamati ya Bunge iliyochunguza shutma za Richmond ilikuwa na jukumu la kubainisha ukweli wa shutuma hizo na kuthibitisha kwa Bunge kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za tenda ya umeme wa Richmond. Sina uhakika kuwa report kama ile inamtosha DPP kufungua mashitaka au lah. Ila jukumu la kufanya hivyo analo DPP.

Mkuu, unalosema kuhusu uwezo, haki na ruhusa ya kufungua mashitaka ni sahihi kabisa. Ila ujue tu kwamba, kila kimtokeacho kiongozi wa juu wa serikali, kinahitaji baraka za kisiasa kabla hakijafanyika. Niweza kuapa kuwa, kama JK angetaka akina Mramba, Yona, Mgonja na wengine wasingefika Kisutu. Na kama angetaka pia, akina EL, RA, NK, na wengine wanaotajwa humu wangefikishwa Kisutu kujibu mashitaka yao. Mkuu, hakuna hatua inayochukuliwa nchi hii bila ridhaa ya utashi wa kisiasa. Hata kuondoa wamachinga barabarani inatokana na utashi wa kisiasa. Ninaweza kuhisi tu kwamba, kuanzia sasa hakutakuwa na kiongozi mpya atakaefikishwa mahakani kwa tuhuma za ubadhirifu wowote (EPA, Richmond/Downs, Kagoda n.k.). Sisi wananchi tukitaka kushitaki tunaweza. Ila mashitaka hayo hayatafika mbali kwani utashi wa kisiasa utayapinga kwa kushinikiza mahakimmu kuchukua hatua za kuyadhoofisha. Mahakama zetu zinaingiliwa sana na serikali katika maamuzi yake (jaji Mkuu alilalamikia hili pia).

Hata hoja ya LM kujiuzuru imefika wapi? Ilijadiliwa? Jibu ni hapana. Haitajadiliwa na hajajiuzuru/hatajiuzuru.

EL na wenzake walijadiliwa Bungeni kwa ukamilifu kabisa. Bunge kama kawaida yake ikaridhia hatua za kuchukuliwa na viongozi hao pamoja na wengine. Hatua zilizokwisha kuchukuliwa zinajulikana kwa uchache wake. Angalau ungesema hawa wamechukuliwa hatua, ningekuelewa zaidi. Ila LM hajafanywa lolote, alikingiwa kifua sana tu.

Mkuu, JK ni Rais wa nchi, Mkuu wa majeshi ya ulinzi na Usalama, Mwenyekiti wa CCM. Ameshika DOLA.

Huwezi kumtoa kwenye majukumu ya kuhakikisha nchi inaendeshwa kwa kufuata sheria, kwa amani na utulivu na kulinda rasilimali za nchi na usalama wa raia na mali zao. Haiwezekani Rais akawa nje ya jukumu la kuhakikisha mtu, au kikundi cha watu wanaohujumu rasilimali za nchi/umma wanafikishwa kwenye mamlaka za sheria, ili kuwa fundisho kwa wengine na kadiri inavyowezekana kuhakikisha mali hizo zinarudi kwa umaa na zinatumika kwa ufanisi kwa maendeleo ya nchi na taasisi za umma.

RA hajawahi kuwa kiongozi wa ngazi yoyote serikalini. Na kwahiyo, hajawahi kuwa katika wizara ya Miundombinu. Nakuhakikishia, angekuwa Wizara hiyo, angejenga kila kitu hapa nchini. Hakuwepo ila alihakikisha alijenga Shekilango Road na barabara nyingine kadhaa kwa utaratibu ambao singependa kuuingilia.

Mkuu Recta,

Hapo juu......tuko ukurasa mmoja Mkuu......mwenye macho na asome...na kuelewa.......na sio ushabiki tu wa oooohhh mbona hamjampeleka mahakamani........
 
Mkandala
Tanzania Daima - Mwakyembe augua ghafla bungeni
Pole sana Mh. Dk. H. Mwakyembe, Shujaa wa karne ya 21 Tanzania, wengi walipewa kazi wakashindwa kutetea maslahi ya Watanzania, WEWE KWA UWEZA WA MWENYEZI

www.jamiiforums.com/matangazo-madogomadogo/25339-msiba-mwakyembe-afiwa-na-mama-yake-3.html
mheshimiwa na shujaa wetu, hon,Dr. harrison mwakyembe amefiwa na mpendwa Mama yake mzazi, kwa mujibu wa mtangazo ya vifo ya radio free afrika monitored here

Mwakyembe anapoficha mambo kulinda ?heshima ya serikali? | Jamii Blog Network
kwa hakika, kauli ya Mheshimiwa Mwakyembe imezua maswali mengi zaidi kuliko majibu miongoni mwa Watanzania wanaomchukulia kama shujaa wao

issamichuzi.blogspot.com/2008/06/mwakyembe-amwaga-cheche-bungeni-leo.html
Duh!! inamaana mzee wa vijesenti alitaka kumtanguliza shujaa wetu hivi hivi!! Mwakyembe mwambie mzee wa ndumba kwamba mungu bado yupo nawe

NK zipo nyingi tu hizo
 
hawa akina Mwa wana umoja duh!

mwakipesile,mwakyembe,mwakanjala,mwasote,mwakilanga

gotta give it to watu wa Mbeya mtu wenu mnae to the end

Ugomvi uko kwetu sisi wa Pwani...kidogo ukishaboa tuu bas tunakuacha waku hang maana hatuna muda wa kujibizana kama huamini muulizeni yule mzaramo wa kujipaticha...aka BANGUSILO
 
Back
Top Bottom