Kwenye msitu wangu kuna black mamba/ koboko natafuta njia za kumwangamiza bila kuleta madhara kwenye jamii

Wengi msilolijua kuhusu nyoka na porini ni kwamba tunakutana na nyoka wengi sana porini na barabarani hasa vijijini ila nyoka wanatuepuka bila sisi kuwaona.
Nyoka anahisi hatari ya binadamu kwa kishndo chake tuu akiwa mbali na anakuepuka. Na ndio maana ni rahisi kumuona nyoka akiwa kwenye windo, au sehemu ya wazi au kumbabatiza " encounter" yani papo kwa papo mmekutana, hakutarajia wala hukutarajia.
 
Hapo achana na kufuga nyuki. Fuga hao Koboko. Wanalipa sana. Unaweza ukawa unawakamua sumu yao unaweka kwenye vikopo unauza. Au unachinja unakuja uza kwa wachina. Wachina wanapenda sana nyama ya koboko. Na hiyo sumu ya koboko ni very expensive.

Hata ngozi yake inatumika kutengenezea viatu, pochi, mikanda na ni very expensive. Achana na nyuki endeleza kufuga koboko. Yaani umenifanya mpaka mwili usisimke. Nikasema kweli upele unamwotea asiye na kucha.

Hapa ilitakiwa uje kuuliza soko la sumu ya koboko, nyama na ngozi yake. Chakula si issue sana. Fuga panya walishe koboko wako wanenepe wazaane. Utatajirika sana.

Usione kama ni tatizo hiyo ni fursa ndugu. Ni fursa ya utajiri.
 
Kama uliwaona koboko maana yake wapo wengi mitaa hiyo, ni nyoka flani hapendi bugudha wala kelele. Hapo kwenye mti alikuwa kwenye mawindo ya ndege na ingekuwa yupo chini msingemuona angewaepuka kwa kusikia vishindo na kelele mkiwa mbali. Mimi nafuga nyuki.
Fuga nyuki na uwe na tahadhari wakati wote kwa kuvaa mavazi ya kukinga nyuki na nyoka. Kwa kuwa kuna koboko vaa kofia ngumu kichwani, huyo nyoka ni msumbufu na anambinu sana, anaweza kukuwinda akiwa kwenye mti akagonga kichwa.

Ni nyoka bingwa wa kujificha usimuone na ni bingwa wa "camouflage" hasa akiwa wa Kijani. Anaweza tulia kwenye nyasi au kwenye mti usimuone ukapita akaendelea na shughuli zake.

Mimi nafuga nyuki, najua habari za nyoka na nyuki wenyewe. Usiogope nyoka wala nyuki ila kuwa na tahadhari. Ni kawaida kufungua mzinga kukutana na nyoka. Penye nyoka pana nyuki na penye nyuki pana nyoka. Ni wanyawa wenye "coexistence" moja na wanapendana.

Jaribu kufanya shughuli zako kama ni kufuga nyuki mitaa hiyi kwa tahadhari ila msijifanye eti mnataka kupambana na nyoka hao kuwamaliza, mtajipa kibarua kigumu na mtasanda. Mtatumia nguvu nyingi kupambana na nyoka kuliko kuzielekeza nguvu hizo kufanya shughuli za kiuchumi porini.

Nyongeza: Koboko hapigwi na fimbo wala mawe, anapotaka kukugonga akisala anakufuata huku anajinyonga nyonga kwa kasi ni ngumu kumchapa au kumpiga jiwe. Kufumba na kufumbua ushapigwa sindano kadhaa. Koboko anatupiwa shuka/blanketi ndipo zinafuata fimbo akiwa ndani ya shuka.

Mbinu za kupambana na Koboko: Beba fimbo ndefu ya kisukuma ile, beba shuka au blanketi zito wastani, ukikosa beba kikoi cha kimasai kila unapoingia pori, vaa kofia ngumu. Shuka/blanketi litakuokoa mbele ya koboko. Akisala kukufuata mtupie shuka kwa lengo la kumfukia na kumpunguzia kasi kisha mshambulie na fimbo. Ni mrefu ana mwili mkubwa, shuka huwa linamchanganya na kumfunika sehemu ya mwili au pote. Atataka kupambana na shuka akifikiri ni wewe ndipo unamshambulia kwa urahisi na fimbo au kukimbia yani toka nduki kama umeme mzee.
 
Jf salaam🙏

Ni muda sasa tangu aanze kuonekana huyu nyoka hatari koboko na inasemekana wapo wawili.

Taarifa zilianza kunifikia kutoka Kwa wazee wangu maana huo msitu ukweli sio wangu ni wa mzee ila kaniruhusu kufanya shughuli zozote za kujiingizia kipato.

Mara kadhaa amekuwa akionekana na muda wa usiku kupiga kelele flani Hivi.

Nakumbuka baada ya kupata mapumziko mafupi nilienda kijijni kwa wazee wetu. Nikafika na nikaenda mlimani(msituni) lengo nikufanya research kwa kina Ili niwekeze ufugaji wa nyuki (asali).

Nilimchukua dogo mmoja ambae Huwa anachunga mbuzi wangu tukaenda naye huku akinifotoa picha za kila aina na Kila Rangi.

Mwisho tukafika kwenye mti mzuri wenye kijani kibichi wenye matawi mazuri akanipigia picha za kutosha pale.

Baada ya hapo tukakaa chini ya mti huo kwenye jiwe huku nikipitia picha nilizopigwa na kufuta zile sikuzipenda

Tukiwa hapo tunapiga story ghafla tukasikia kelele za ndenge flani juu ya mti Mimi kelele zile nazijua huwa ni Alert ya hatari fulani wameiona wale ndege.

Kuinua macho juu sikuamini nilichokiona ni yeye koboko mtesa ametulia tulii Wala hatikisikii kama amekufa.

Dogo(muha) kumuona akapanic akaanza mbio nikamwambia simama hapohapo akasimama huku nami nikitoka eneo la tukio hadi kwa dogo.

Nyoka ni mkubwa na anaogopesha na kwa mazingira yale huwezi mshambulia kwa kutumia njia zetu hizi za asili(fimbo)

Maana ni mstuni vinginevyo anakuua ndani ya muda mfupi tu hakuna sehemu ya ku escape asikudhuru.

KUMBUKUMBU ZANGU

Miaka ya nyuma tukiwa wadogo nilishuhudia maiti za Watoto wenzetu watu na ng'ombe 7 zikiwa zimelala Chali (kufa).

Ni baada ya Hawa Watoto kuona huyo nyoka aina ya koboko na kumshambulia ndipo alipowageuka na kuwauma wote wawili na ng'ombe zao zote Saba na zilikufa hapohapo!

Nakumbuka kipindi hicho hicho nikiwa primary mtoto mwingine darasa letu Moja akiwa anaenda kuokota maembe kwenye mti wa mwembe akamuona koboko Kasimama wima naye pasina kujua alianza kumshambulia.

Hapo hapo alimgonga na kufa mama yake alisikia kelele za mwanae akilia Kwa uchungu Kwa sababu ilikuwa mbali na mwembe na mara zote walikuwa wanaenda Watoto kadhaa kuokota maembe pale. ile anatoka akamsaidie alimkuta tiyari kashafariki na nyoka amepanda juu ya mtu flani mfupi.

Ndipo alipo piga yowe kuomba msaada na walifanikiwa kumuua.

Inavyosemekana na Mimi naweza kuwa shahidi wa hili ni kwamba....

Nyoka aina ya black mamba ni wapole kupita kiasi pale anapokuwa katika Hali yake ya kawaida.

Pia anasikia kuliko kawaida anaupeo mkubwa wa kuhisi hatari na hata harufu na hivyo kujiweka tiyari Kwa ajiri ya mapambano.

Akiona mazingira aliyopo sio salama kwakwe kufanya shambulio hujiondokea kabla hujamfikia Wala kumuona.

Lakini pale ukimuona wewe jua kakusubiri na amejiandaa Kwa muda mrefu sana amegojea tu ulianzishe upate unachostahili.

Kwa matukio hayo mawili ambayo siyo ya kusimuliwa na hili langu Mimi mwenyew Tena mwezi 2 tu mwka huu nakubaliana na hili kuwa Hawa nyoka ni wapole na ni hatari.

Tukio la wale watoto wawili na ng'ombe wao. Sisi ndo tulikuwa wa kwanza kumuona yule nyoka na ilikuwa Hivi.....

Siku Moja tunaenda machungani katikati ya njia kulikuwa na mti flan Hivi kama kichaka (ipo miti Ina randa na kutengeneza kichaka kizito)

Tulipitisha mifugo yetu yote salama na sisi wenyewe tukapita salama mtu wa4 ndo akatumbia oneni yule nyoka tukarudi kumtazama asee alikuwa mrefu sana na ametulia kama hajui kinachoendelea...

Tulichokifanya ni kwenda kuwambia wakubwa wetu karibu na eneo lenyewe. Na walipokuja wakamuona na kumtambua walitumbia ondoeni ng'ombe na mifugo yenu hapa tukafanya hivo.

Nao walipoona tumeondoka waliondoka pia bila kumfanya chochote.

Bahati mbaya sana Kwa wenzetu siku chache mbele wao walipo muona tu ujasiri uliwaingia na kuanza kumshambulia huo ndo ulikuwa mwisho wao na ng'ombe wao pia.

Yowe lilipigwa nyoka huyo akauliwa.

Nimekuja kuomba ama kufundishwa njia/mtego Ili nimuue bila kuathiri watu wa maeneo hayo.

Msitu huu nimepanga kufugia nyuki Kwa wingi lakni kinacho niogopesha ni uwepo wa black mamba kwenye eneo hili.

Eneo ni zuri sana Kwa nyuki kwani maji yapo si zaidi ya mita250 na nyuki ni wengi sana hasa kwenye mapango ya miti,mawe na wengine hujitengenezea asali juu ya mti tu.

Najua humu Kuna watu wa maliasili na wataalamu wa maswala haya naombeni namna ya kumuondoa huyu mdudu na nimeambiwa wapo wawili.

Wapo walio waona Kwa nyakati tofauti na maeneo tofauti na usiku hupiga kelele zao Kwa kupokezana wasi wasi wangu zaidi watazaliana na kuongezeka zaidi.

Ahsanteen sana.

View attachment 2945391
Tafuta Nyegere(Honey badger) dume na jike.. Ni vigumu kuwapata ila ukiwasiliana na wenyeji na ukatangaza pesa utaletwa .. Hao Koboko wako wataliwa ndani ya wiki moja.. Na wasipoliwa basi watahama eneo hilo na kutokomea mbali kabisa.. Koboko ni chakula cha Nyegere.. Nimesema ulete dume na jike ili wakae kwenye hilo pori.. Ukileta mmoja tu lazima atahama kutafuta mwenza.. Ila wawili wataweka makazi yao hapo..
 
Hapo achana na kufuga nyuki. Fuga hao Koboko. Wanalipa sana. Unaweza ukawa unawakamua sumu yao unaweka kwenye vikopo unauza. Au unachinja unakuja uza kwa wachina. Wachina wanapenda sana nyama ya koboko. Na hiyo sumu ya koboko ni very expensive.

Hata ngozi yake inatumika kutengenezea viatu, pochi, mikanda na ni very expensive. Achana na nyuki endeleza kufuga koboko. Yaani umenifanya mpaka mwili usisimke. Nikasema kweli upele unamwotea asiye na kucha.

Hapa ilitakiwa uje kuuliza soko la sumu ya koboko, nyama na ngozi yake. Chakula si issue sana. Fuga panya walishe koboko wako wanenepe wazaane. Utatajirika sana.

Usione kama ni tatizo hiyo ni fursa ndugu. Ni fursa ya utajiri.
Daaah...hawa motivation sprakers watakuja kuua watu
 
Nilifikiri kuna Inland Taipan 🤷🏾‍♂️🤷🏾‍♂️🤷🏾‍♂️
 
paka anaua nyoka yeyote yule isipokuwa chatu .......paka anauwezo mkubwa wakuona kasi ya nyoka yoyote yule (kasi ya kurusha mate au ya kung'ata) anaiona in slow motion ndo maana anaweza epuka mate au mdungo wa nyoka na kumchapa makofi meng tu mpaka akaded ..........hakuna cha koboko au king kobra wote n wachumba tu kwa paka.
 
Jf salaam🙏

Ni muda sasa tangu aanze kuonekana huyu nyoka hatari koboko na inasemekana wapo wawili.

Taarifa zilianza kunifikia kutoka Kwa wazee wangu maana huo msitu ukweli sio wangu ni wa mzee ila kaniruhusu kufanya shughuli zozote za kujiingizia kipato.

Mara kadhaa amekuwa akionekana na muda wa usiku kupiga kelele flani Hivi.

Nakumbuka baada ya kupata mapumziko mafupi nilienda kijijni kwa wazee wetu. Nikafika na nikaenda mlimani(msituni) lengo nikufanya research kwa kina Ili niwekeze ufugaji wa nyuki (asali).

Nilimchukua dogo mmoja ambae Huwa anachunga mbuzi wangu tukaenda naye huku akinifotoa picha za kila aina na Kila Rangi.

Mwisho tukafika kwenye mti mzuri wenye kijani kibichi wenye matawi mazuri akanipigia picha za kutosha pale.

Baada ya hapo tukakaa chini ya mti huo kwenye jiwe huku nikipitia picha nilizopigwa na kufuta zile sikuzipenda

Tukiwa hapo tunapiga story ghafla tukasikia kelele za ndenge flani juu ya mti Mimi kelele zile nazijua huwa ni Alert ya hatari fulani wameiona wale ndege.

Kuinua macho juu sikuamini nilichokiona ni yeye koboko mtesa ametulia tulii Wala hatikisikii kama amekufa.

Dogo(muha) kumuona akapanic akaanza mbio nikamwambia simama hapohapo akasimama huku nami nikitoka eneo la tukio hadi kwa dogo.

Nyoka ni mkubwa na anaogopesha na kwa mazingira yale huwezi mshambulia kwa kutumia njia zetu hizi za asili(fimbo)

Maana ni mstuni vinginevyo anakuua ndani ya muda mfupi tu hakuna sehemu ya ku escape asikudhuru.

KUMBUKUMBU ZANGU

Miaka ya nyuma tukiwa wadogo nilishuhudia maiti za Watoto wenzetu watu na ng'ombe 7 zikiwa zimelala Chali (kufa).

Ni baada ya Hawa Watoto kuona huyo nyoka aina ya koboko na kumshambulia ndipo alipowageuka na kuwauma wote wawili na ng'ombe zao zote Saba na zilikufa hapohapo!

Nakumbuka kipindi hicho hicho nikiwa primary mtoto mwingine darasa letu Moja akiwa anaenda kuokota maembe kwenye mti wa mwembe akamuona koboko Kasimama wima naye pasina kujua alianza kumshambulia.

Hapo hapo alimgonga na kufa mama yake alisikia kelele za mwanae akilia Kwa uchungu Kwa sababu ilikuwa mbali na mwembe na mara zote walikuwa wanaenda Watoto kadhaa kuokota maembe pale. ile anatoka akamsaidie alimkuta tiyari kashafariki na nyoka amepanda juu ya mtu flani mfupi.

Ndipo alipo piga yowe kuomba msaada na walifanikiwa kumuua.

Inavyosemekana na Mimi naweza kuwa shahidi wa hili ni kwamba....

Nyoka aina ya black mamba ni wapole kupita kiasi pale anapokuwa katika Hali yake ya kawaida.

Pia anasikia kuliko kawaida anaupeo mkubwa wa kuhisi hatari na hata harufu na hivyo kujiweka tiyari Kwa ajiri ya mapambano.

Akiona mazingira aliyopo sio salama kwakwe kufanya shambulio hujiondokea kabla hujamfikia Wala kumuona.

Lakini pale ukimuona wewe jua kakusubiri na amejiandaa Kwa muda mrefu sana amegojea tu ulianzishe upate unachostahili.

Kwa matukio hayo mawili ambayo siyo ya kusimuliwa na hili langu Mimi mwenyew Tena mwezi 2 tu mwka huu nakubaliana na hili kuwa Hawa nyoka ni wapole na ni hatari.

Tukio la wale watoto wawili na ng'ombe wao. Sisi ndo tulikuwa wa kwanza kumuona yule nyoka na ilikuwa Hivi.....

Siku Moja tunaenda machungani katikati ya njia kulikuwa na mti flan Hivi kama kichaka (ipo miti Ina randa na kutengeneza kichaka kizito)

Tulipitisha mifugo yetu yote salama na sisi wenyewe tukapita salama mtu wa4 ndo akatumbia oneni yule nyoka tukarudi kumtazama asee alikuwa mrefu sana na ametulia kama hajui kinachoendelea...

Tulichokifanya ni kwenda kuwambia wakubwa wetu karibu na eneo lenyewe. Na walipokuja wakamuona na kumtambua walitumbia ondoeni ng'ombe na mifugo yenu hapa tukafanya hivo.

Nao walipoona tumeondoka waliondoka pia bila kumfanya chochote.

Bahati mbaya sana Kwa wenzetu siku chache mbele wao walipo muona tu ujasiri uliwaingia na kuanza kumshambulia huo ndo ulikuwa mwisho wao na ng'ombe wao pia.

Yowe lilipigwa nyoka huyo akauliwa.

Nimekuja kuomba ama kufundishwa njia/mtego Ili nimuue bila kuathiri watu wa maeneo hayo.

Msitu huu nimepanga kufugia nyuki Kwa wingi lakni kinacho niogopesha ni uwepo wa black mamba kwenye eneo hili.

Eneo ni zuri sana Kwa nyuki kwani maji yapo si zaidi ya mita250 na nyuki ni wengi sana hasa kwenye mapango ya miti,mawe na wengine hujitengenezea asali juu ya mti tu.

Najua humu Kuna watu wa maliasili na wataalamu wa maswala haya naombeni namna ya kumuondoa huyu mdudu na nimeambiwa wapo wawili.

Wapo walio waona Kwa nyakati tofauti na maeneo tofauti na usiku hupiga kelele zao Kwa kupokezana wasi wasi wangu zaidi watazaliana na kuongezeka zaidi.

Ahsanteen sana.

View attachment 2945391

ni mkoa ngani mkuu?? Hawa viumbe wanapatikana zaidi mikoa ya Tabora, Shinyanga, kigoma , Geita. Tafta wale wataalam wa nyoka ( waganga wa kienyeji ) atawatoa wote
 
Back
Top Bottom