Kwenye msitu wangu kuna black mamba/ koboko natafuta njia za kumwangamiza bila kuleta madhara kwenye jamii

nacho kataa nikuwa cobra wapo humo na ushahidi ni hayo magamba yao pale wanapojivua {sijui kitaalamu} kitendo cha yeye kutoka gamba la juu
Tatizo unatunga habari mpaka unajichanganya mwenyewe katika maelezo.

Wewe umesema kwenye msitu wako kuna koboko haukusema na King Cobra. Sasa imekuaje kuaje tena kumuongeza Cobra katika list ghafla?
 
Simple tip
Chemsha mayai yaive vizuri kaweke eneo wapopatikana akimeza basi utakuwa unamwita marehemu koboko "logic nyoka hawezi tofautisha yai bichi na lilioiva hivyo atalimeza na mfumo wao wa mmeng'enyo wa chakula haumeng'enyi vitu vigumu hvyo atakufa kwa constipation"case closed
 
Tatizo unatunga habari mpaka unajichanganya mwenyewe katika maelezo.

Wewe umesema kuna koboko, mara sasa hivi unaongeza tena na Cobra. Nafikiri umeamua kuja tu kujiandikia tu ili kupima upepo kuhusu huyo koboko wako.
mkuu kama hatuelewani basi tuachane. ulipo sema kuwa cobra ndo huwa ana mla black mamba nikakujibu sio kweli kwa sababu hata hao wamo humo pori na magamba huwa tunayaona wao ni weusi na wanatabia ku mwaga mate pindi mnapokutana nae. hao kwetu si tishio huwa wanauliwa mara nyingi tu
 
Nafikiri baadhi ya story za Koboko hapa JF zimekuchukua kweli kweli kiasi ambacho kimekufanya uamini kila unachoambiwa kuhusu Koboko bila kufanya utafiti ili ujue mtemi wake ni nani.
 
Tafuta wazee wa Kikwere hao ni kiboko ya Koboko.
wakwere si watu wa pwani?
Simple tip
Chemsha mayai yaive vizuri kaweke eneo wapopatikana akimeza basi utakuwa unamwita marehemu koboko "logic nyoka hawezi tofautisha yai bichi na lilioiva hivyo atalimeza na mfumo wao wa mmeng'enyo wa chakula haumeng'enyi vitu vigumu hvyo atakufa kwa constipation"case closed
hii nitaifanya mkuu
 
Inanikumbusha nilinunuaga shamba tabora nikaanza project ya kufuga kuku. Siku moja napigiwa simu na madogo kuwa kuku wote wanaolalia mayai wamegongwa na nyoka wamekufa. Nikaenda nikakuta hadi wamebadilika rangi, walikua kuku kama 15 hivi wanaolalia, wengine walikua wanalala juu kwenye mbao wakasalimika. Nilikuaga sijui hatari yoyote ya huyo nyoka japo madogo walinambia ni koboko maana alikunywa na baadhi ya mayai tukakuta maganda tu.
 
Unaposema huo msitu ni mlimani basi inawezekana ni pori,sasa una uhakika gani mkuu kwamba hao nyoka wapo wawili tu? Kwani hawazaliani? Mbona ni kama maeneo ambayo siyo salama kwa mishemishe za binadaamu,utawahamishaje na msitu ukabaki,maana ingekuwa kuwamaliza ni kuchoma tu msitu
 
pole sana mkuu
 
Kipindi cha sensa tulipima tukapata heka nane mstu pekee
 
siyokweli na huenda umesimuliwa tu. Hadi sasa hao ndo wengi huwa tunaona magamba yao yakutosha tu. mimi najua kiboko chake ni bundi na hawa nguchiro. pamoja na hao kuwepo lakini nyoka bado anaokana mara kwa mara
IMG-20240326-WA0009.jpg
 
Koboko hana tatizo ila tatizo lipo kwetu sie wanadamu, angekuwa yupo kwenye makazi ya watu hapo sawa lakini huyo yupo porini hana shida.....ukiona nyoka amemgonga mtu ujue mtu ndio amemfuata vinginevyo hawezi kukufanya chochote sana sana atatafuta sehemu nyingine ya kujificha.

Kama huna uwezo wa kumdhibiti yaani ni heri umwache uwe unaingia msituni Kwa uangalifu kuliko kujifanya kumpiga alafu ukamkosa au ukamjeruhi, kitakachotokea Kila akikutana na binadamu atakuwa anamdunga tena Kwa kulazimisha Kwa Kila anaetokea mbele alidhani adui yake
 
Back
Top Bottom