Kweli nimeamini ma "sugar mamy" wapo! Loh!

Kweli nimeamini ma "sugar mamy" wapo! Loh!

Wabongo bana kwa wivu, kilasiku tunasema tunaenda na wakati hakuna kuchaguliana mpenzi, kulikoni leo unasema hawaendani size: ni kwenye kiatu kwenye K hakuna size
 
ujumbe uwaendee pia wadada wanaotoka na mibaba saizi ya babu zao tena ni waume za watu. jaman mnatesa familia za wenzenu, sio vizuri

Nina jirani yangu hapa msichana boy friend wake kazeeka hadi kawa kibogoyo;alistaafu kazi serikalini kama Katibu Mkuu wizara ya Fedha miaka 21 iliyopita;ana miaka 81 sasa na demu ana 23!

Mapenzi ni hela bana;kama dogo anavuta majani mwacheni!
 
mwache kijana katoa huduma katunukiwa......... na wewe wataka?
 
kiroho safi, waache wapeane kitu roho inapenda mioyoni mwao, kama niaje niaje mnasue basi ktk mtandao huo!
 
Nimewafikiria wanangu na watoto wa ndugu zangu...tusali sana ...hizi ni siku za mwisho. Nina mtoto wa dada yangu alinisimulia mwenzao college amekufa kwa kulishwa sumu na sugar mummy wake...stori ni kuwa mume alijua kuwa akienda kazini mkewe upeleka chakula kwa dogo. siku hiyo kavizia kaweka sumu kwenye hotipoti...kijana ile anakula tu chaliii...ni chuo cha Dar wala si mbali...niliona kama movie vile. Ukizaa mtoto wa kiume mwenye mvuto ni majanga these days...wanawindwa haooo

Nimejickia vibaya!...namfikiria mdogi wangu wa kiume alieanza chuo my God
 
aah me hayo yote yamepita kushoto,hao mamama wakwapi? Nitafutieni na mimi kwasababu i am broke now
 
Dada yangu Munkari hiyo ndiyo haki sawa kwa wote, wakati wakina dada wanatoka na Babu/Baba zao huku nako masela wanabanjuka na Bibi/Mama wanaomilikiwa na hao hao.

Hapo tuliosoma "Chemistry" tunasema, Balanced Equation. 2H[SUB]2(g)[/SUB] + O[SUB]2(g)[/SUB] -> 2H[SUB]2[/SUB]O[SUB](l)[/SUB], na watu wanakunywa maji.

Hahahaaaa..... Nimeipenda hiyo equation..! Umenikumbusha mbali saaana..!!
 
kweli kunyata anyate paka...akinyata kicheche ohh anavizia kuku hata kama alikua anafanya mazoezi...Au kupanda apande mbuzi...akipanda punda tu ohoooo kaua. hii misemo yote nimeiamini....
hivi dada zetu mnavongonoka na wazee umri wa babu zenu... hamuyaoni????????????

huyu naye akaenda huko kwenye bd party akajionee mwenyewe jinsi wenzake wanavyojua kutunza ka-serengeti kake. Ameona, wivu tayari, oh! atakufa kwa ukimwi, Oh! Anaye mwingine, Wewe uliyeleta thread ni bikra? Usinyoshee wengine kidole kimoja tu kumbe wewe vitatu vyakuangalia wewe. Koma tena ukomae. Mama wa watu kajichagulia na aliyepata kura kachaguliwa akasema naam nipo tayari. Wewe umetokapi kuwatabiria kifo? Utangoja saaaaana. Nasema Acha wivu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom