nikamwona mmama mtu mzima kasimama kachukua maik na kusema 'namzawadia mpenzi wangu gari' ,kijana yupo hightable anachekacheka tu utadhani binti anayefanyiwa kitchen party!
hata aibu hana Loh!
Akakabidhiwa funguo ya gari na hilo limama na mahela juu kama miss Tanzania! Kijana meno 32 yote nje!
......daaah! Kwa staili hii ukimwi utaisha kweli? Kwasababu siamini kama huyo mama ana huyo kijana pekee lazima atakuwa na mume au mibwana mingine ! Na kijana naye atakuwa tu na agemate wake.
Aisee sijui kwanini nimesikitika hivyo!
so,vijanaa!tafuteni kazi Fanyeni kazi msipende vya bure jamani acheni kutembea na mama zenu mnajidharirisha ohoo mtakufa siku si zenu shauri yenuu ! ...ntarudi!
Aaaaaaaaaaaahaaaaa kumbe nimeshajuwaaaaaaaaaaaaaaa!
Umemzimikia kia umempenda pia kijana HB sio kiviile, ila kwa ule mtiti unajuwa huwezi kumchomoa!
pale kwa jimama! Kumbe huwezi kulumangia ugali wa kachumbari kachumbari!
haahaahaa! Sa ye ka kazoea kuhongwa miye atanipa nini? Teh!
Eiyer huyo!!!Nadhani hapa mwenye tatizo ni wewe
Hivi ni wapi umesoma kuwa kuna maelekezo ya umri wa wanandoa/wapenzi?
Vipi kuhusu wewe ulieondoka kwenu kama mwandishi wa magazeti ya udaku kwenda kufuatilia maisha ya watu na kuyaleta JF?
Huoni aibu?
Inaonekana hiki ndio kilichokutoa roho!
Yaani watu wengine bana
Kwanza ulikua unasikia tu kuwa kijana anatoka na huyo mama,hii inamaana kuwa hukua na uhakika
Hapa uasema huamini kama huyo mama ana huyo kijana tu
Una matatizo makubwa wewe
Sekunde kadhaa ulikua hujui sasa unadai huamini kama huyo mama ana huyo kijana tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Ni kitu gani kilikufanya usiamini uwezekano wa huyo mama kuwa na huyo kijana kimahusiano?
Halafu baada ya muda mfupi ni nini kilikufanya uamini kuwa huyo mama nana watu wengine?
He!!!!!!!!
Hujui ni kwanini umesikitika hivyo?????????
Unakumbuka ulichokisema mwanzoni??
Kumbe tuhuma zote zile ulikua hujui ni kwanini unazitoa!!!!!!!!!
JF kuna maajabu sana siku hizi!!!!!!
Hta hapa hujui ni kwanini unasema haya?
Halafu mwanzo ulisema kuwa huyo kijana amemaliza chuo siku sio nyingi
Hukusema hatafuti kazi,so umejuaje haya?
Hapa huenda kuna mambo yafuatayo:
Moja:kuna ka jamaa ulikagharamia sasa kamekumwaga hivyo unatumia hili tukio kujitafutia nafuu
Pili hii story ni ya kutunga!
Hata miye ni babu, tena naitwa bebi. Ubabu wangu niliuacha mikumi kabisa
Rafiki wala usisumbuke kujua wanawake wanavyo waza maana .......... mnh!Heheheh....lakini angelikuwa ni binti mduchu anazawadiwa fweza za kutosha na zee jitu zima...aaah wadada mngepiga makofi na si ajabu nanyi mngetamani muwe na mtu kama huyo!!
Bado naendelea kutaka kujua namna wanawake wanavyowaza aisee, mabesti zangu namomba mnisaidie
uzee mwisho chalinze mjini kila mtu BABY!!!!!!!!!
Rafiki wala usisumbuke kujua wanawake wanavyo waza maana .......... mnh!
As usual !!!!!
Mrembo hujambo?
Yeah I can see!!!!!
mimi sijambo munkari anatakiwa atulie wakati anajibu maswali yako!!!!!
Sugar mummy wapo tena wengi tu, na ukweli ni kwamba huwa nakereka sana kusikia kijana mwenye nguvu zake na akili zake timamu anawekwa ndani na sugar mummy na kuanza kuhudimiwa, kweli huwa nasikitika sana maana mchezo huwa ni sawa kabisa na kijana kushindwa kujitambua kuwa yeye ni nani ana wajibu gani katika jamii iliyomzunguka.
Mwanaume ni kichwa na kiongozi wa nyumba kwa mujibu wa vitabu vya dini, na kitendo cha kuikataa hadhi na heshima uliyopewa ya kuongoza nyumba, inaweza kumuingiza mpaka kwenye hatari ya kwenda kuwekwa kimada na mwanaume mwenzake endapo hilo jimama litampiga chini na akakosa shughuli ya kumpa kipato. tabia hizi huwa wafanya vijana wa namna hii wabetweke na kugeuka watu wa kupenda starehe na kutunzwa bila kujishughulisha. Huu ni uanaume wa aina gani huu?
Nakushukuru kwa kulizungumzia hili suala. Ni aibu vijana, hebu tuache upuuzi huu, na tufanye kazi na kula kwa jasho la mikono yetu wenyewe.
watu8, rafiki yangu na ndg yangu wa karibu, ukweli ni kwamba si kila jambo tunaweza kulinganisha kwa wanawake na wanaume. Suala la mwanaume kuoa binti mdogo si sawa na kijana kwenda kuoa mama mtu mzima. Kiutamaduni na kiimani tangu enzi na enzi hali ilikuwa hivyo. Lakini huo mchezo ulioingia sasa wa vijana kuoa mijimama, si kwa sababu ya mapenzi waliyonayo kwao, bali kuwageuza hao miradi. Na hii imewafanya baadhi yao kuwa wazembe, wavivu na watu wasiojituma kwenye kazi. Wamepoteza hadhi na sifa za kuwa wanaume jambo ambalo ni hatari sana.
watu8 sijui wanawake watawaza nini, lakini ktk hali hii, wanawake ni haki yao kutunzwa na wanaume. Mwanaume ni lazima awe mkuu wa nyumba na mtunzanji na mlinzi wa hiyo familia. Mwanamke anaweza kumtunza mwanaume tena hasa wa ndoa lakini si kwa staili hii ya vijana kutunzwa na mimama.
haahaahaa! Daah! Nnawangu kifaa cha maana so hapa cna jibu!