..kwa historia ya Tanganyika, ukiona Waziri Mkuu halaumiwi basi ujue hafanyi kazi yake vile inavyotakiwa na hamsaidii Raisi.
..Waziri Mkuu ndiye kiranja mkuu wa mawaziri na msimamizi wa utekelezaji wa majukumu ya serekali.
..Mtendaji mwenye majukumu hayo, lazima awe " front " muda mwingi, na ktk mazingira ya Tanganyika lazima ataangushiwa lawama nyingi.
..Fuatilieni historia ya Mawaziri Wakuu kama Mzee Kawawa, Edward Sokoine, Joseph Warioba, Cygwiyemwisi John Malecela, Frederick Sumaye, Edward Lowassa, Mizengo Pinda.
..Wote walikuwa mstari wa mbele kusimamia serekali. Na mambo yalipoharibika walibeba lawama badala ya Raisi kubeba lawama hizo.
..Suala kama la ununuzi wa korosho, awamu zilizopita Waziri Mkuu ndiyo angekuwa mstari wa mbele na siyo Raisi hata kama final say ilikuwa ni ya kwake[raisi].
Nakubaliana nawe 100% na hatuwajawahi kuwa na Waziri Mkuu aliyejificha ficha kama Maja
Katika orodha yako yupo pia CD Msuya, ambaye kama mawaziri wakuu wengine alibeba lawama kwa niaba ya serikali. Wote walikuwa wasaidizi wazuri wa Rais Bungeni na nje
Kassim Majaliwa amekuwa waziri mkuu tofauti kabisa. Akiwa Bungeni hata pale serikali inapobanwa yeye hubaki kutazama tu na zipo nyakati kauli za mawaziri zinatia kinyaa
Huwezi kumsikia akikemea jambo au akipongeza, yaani ni ''lame duck'' PM
Jana alikuwa katika mazishi ya Mzee Mengi. Kauli za Makonda za kibaguzi na akiwa RC sehemu ya watendaji wa PM ilibidi Waziri mkuu asimame na kukemea
Waziri mkuu alikuwa kimya kana kwamba hakuna kilichotokea, aliridhia ubaguzi tu. Kimyaa
Ni afadhali Bushir Ally alikemea lakini yeye ni wa CCM siyo serikali
Maneno ya Bushir yalipaswa kusemwa na Waziri mkuu, tofauti alikuwa kimyaa akitafuta wema
Kwa mtazamo wangu, huyu Waziri mkuu hamsaidii Rais, hasaidii serikali na nchi
Ukimya wake ni kutaka kuonekana mzuri akilenga siku za baadaye kuwa mbeba bendera CCM
Lakini pia kuna element za woga. Alipo waziri mkuu hakuna attention kama alipo Bashite
Huu ni woga kwamba ukimgusa umekwenda na maji. Na woga huo hadi kwa mawaziri
Ni Waziri mkuu aliyetekeleza majukumu yake tofauti na historia ya mawaziri kuu wa Tanzania