Kwanini wanawake wengi wetu hatupendani?

Kwanini wanawake wengi wetu hatupendani?

Nishakuja

Ila bana sisi wanaume wa ajabu sana yaani hawa wanawake sikuwa na mazoea nao kabisa. Ila sasa kuna siku wakawa wanatukanana na kwa kuwa ni majirani zangu mimi nikaingilia kati. Sasa dah ndo yakatokea yaliyotokea.

Wanisamehe sana na tamaa zangu
Viboko vinakufaa!!
 
Sema mmezidi kusemana asee huwa najaribu kuwaza hivi nkioa huyo mwanamke atakuwa wa namna gani,msemaji au mpole,
Je atapenda familia yangu,je atakuwa na kifua juu ya mambo ya ndani ?? Maana kadir siku znavoenda mnatishaa mnasema kwa mashoga zenu adi ya ndani halafu siku mkivurugana wanaishia kukusema mpaka mume wako.mnakosea wap nyie viumbe?
Haaa haaaaaa
 
Hello again na wanawake! Nina kesi kubwa na wewe ntakufata PM tuyajenge on why tulipigwa ban watu wengi kwenye uzi wetu ule.
Btw, watu wengi wanabidi wafanyie kazi sana utu wao wa ndani ndipo watafufuka upya. Wivu, husda, roho mbaya ni dalili za wazi kuwa umekufa "inside you". Ukiwa vizuri inside you vitu vingi havitakupa shida.
Njoo Pm.Au ulishaenda shost??Mi ndo Naenda.
 
Kwa hiyo unaonaje tukiwa tunajilipua kama ndugu zetu wa kike
ukizingua unapewa za uso muda huo huo

Mkuu na hiyo ndio njia sahihi ya kuepuka maradhi ya kujitakia! Yaani inatakiwa iwe ni titi 4 tati haina kusubiri, kama sio mabanzi basi ni onyo kali sana, hata kama amekuchafulia shati kwa bahati mbaya mkunjie sura muda huo huo.
 
Hata Mimi nimeshangaa sana.Walau Umeona kidogo.Wanawake hatupendani.Na huwa najiuliza kwa nini inakuwa hivyo.
Muda mwingine ni mihemko isiyokiwa na hata chembe ya busara kidogo!

Kwa hiyo comment yake anaonekana tu huyo Englishlady ni mtu anaeongozwa na mihemko
 
Aisee mkuuu wanawake ni watu wa ajabu sana..majuzi hapa mama yeyooo alinitumia picha za maza angu mana wanaishi wote uko mjini anapofanyia kazi wife na mm niko wilaya za vijijini sasa maza amekuwa pale kwa ajili ya matibabu takribani miezi5..sasa.Sasa si nilichukua zile picha nikamtumia sister angu ili aone maza alivyonawiri nn...heeee..jibu lake sasa sifa eti zinaenda kwa house girl...na mm sikumchelewesha nikamwambia huyo house girl ndo ameolewa??huyu house girl anajua huyu mama nguo anazovaa zinanunuliwa sh ngapi??...alinyamaza kimya mkapa leo hatujawasiliana...nikajua ni wivu tuuu wa kike..yani bada ya ku appreciate wifi yake anakaa vzri na mama ake..ye akaona amsifie beki3...wanawake hawapendani kwa kweli...


Aseeh!, kazi ipo..
 
Huyo mama aliyetaka kupeleka nguo kwa ndugu ni mwanaume? Na hizo nguo alitaka kupelekea wanaume tu? Tabia nyingi ulizotaja hapo zinaendana na uwezo na hadhi. Hata wanaume wa uwezo na hadhi ya chini wana tabia hizo hizo. Wanakaa barazani wakinyoana na kula kashata huku wakimjadili kila anayepita. Kuna msemo kuwa "simple minds discuss people". Ukienda saluni za ushuani utaenda saluni moja mwaka na kitakachokuwa kinaongea ni TV tu. Kila mtu yuko busy na mteja wake na mteja na simu yake au kitabu chake.

Kwenye kupeana kura mwanamke aliyeambiwa hawezi na akaamini anaweza asiamini kuwa mwenzie anaweza. Hata hivyo tuna wanawake wengi tu ni viongozi wa kuchaguliwa na hawajaolewa wala hawana watoto na wamechaguliwa na wanawake wenzao kwani ndo wapiga kura wengi. Kwa hiyo msemo wa wanawake hatupendani ni propaganda zaidi kuliko uhalisia. Mwanamke anayejitambua hawezi kumpa kura mwanamke na kumnyima mwanaume kwa sababu ya jinsi zao.


Hello again na wanawake! Nina kesi kubwa na wewe ntakufata PM tuyajenge on why tulipigwa ban watu wengi kwenye uzi wetu ule.
Btw, watu wengi wanabidi wafanyie kazi sana utu wao wa ndani ndipo watafufuka upya. Wivu, husda, roho mbaya ni dalili za wazi kuwa umekufa "inside you". Ukiwa vizuri inside you vitu vingi havitakupa shida.


Wamoja wa wadada wa nguvu, me love you.

Mmesema kweli, ukiwa vizuri ndani yako kwa kujitambua, kujielewa wewe kama wewe na confidence juu, mtu mwingine hata kusumbua kiasi kwamba mpaka umuonee vibaya.
 
Lakini pia wakati mwingine tunakuwa vizuri tu hata wenyewe.
Kuna mahali nilifanya Internship, na karibu 70% ya wafanyakazi ilikuwa wanawake. Niliingia kwa woga nikijua kutakuwa na issues za hapa na pale, lakini ikawa tofauti.
Nilipata wasiwasi coz kuna journal niliona iliongelea issue ya wanawake kuwekeana vikwazo especially makazini.

Ingawa kulikuwa na wadada wawili watatu wenye issues hapo mahala, lakini mostly things were calm na kazi zilifanyika vizuri tu.
We did just fine.
 
Mpaka namalizia chuo nakumbuka palijengeka matabaka zaidi ya sita Miongoni Mwa wanawake niliosoma nao, yaani ni mwendo wa kuhama room.kuna tabaka la masista du,wenye nyodo,wacha Mungu,wababe,wapiga msuli,mama huruma yani kila Mtu anaponea yani ni mwendo wa kuangalia tu.
 
Halafu wote tajwa wanaelewana kinafiki au hawaelewan kabisa.
 
Mkuu na hiyo ndio njia sahihi ya kuepuka maradhi ya kujitakia! Yaani inatakiwa iwe ni titi 4 tati haina kusubiri, kama sio mabanzi basi ni onyo kali sana, hata kama amekuchafulia shati kwa bahati mbaya mkunjie sura muda huo huo.
Haaa haaaa.Huu Ni Ushauri au nini Jamani.Alielewa aje
 
Back
Top Bottom