Huyo mama aliyetaka kupeleka nguo kwa ndugu ni mwanaume? Na hizo nguo alitaka kupelekea wanaume tu? Tabia nyingi ulizotaja hapo zinaendana na uwezo na hadhi. Hata wanaume wa uwezo na hadhi ya chini wana tabia hizo hizo. Wanakaa barazani wakinyoana na kula kashata huku wakimjadili kila anayepita. Kuna msemo kuwa "simple minds discuss people". Ukienda saluni za ushuani utaenda saluni moja mwaka na kitakachokuwa kinaongea ni TV tu. Kila mtu yuko busy na mteja wake na mteja na simu yake au kitabu chake.
Kwenye kupeana kura mwanamke aliyeambiwa hawezi na akaamini anaweza asiamini kuwa mwenzie anaweza. Hata hivyo tuna wanawake wengi tu ni viongozi wa kuchaguliwa na hawajaolewa wala hawana watoto na wamechaguliwa na wanawake wenzao kwani ndo wapiga kura wengi. Kwa hiyo msemo wa wanawake hatupendani ni propaganda zaidi kuliko uhalisia. Mwanamke anayejitambua hawezi kumpa kura mwanamke na kumnyima mwanaume kwa sababu ya jinsi zao.