Kwanini wanawake wengi wetu hatupendani?

Kwanini wanawake wengi wetu hatupendani?

Naona ushaidi wa wazi huu hapa heloo!

Yaani anakutuhumu wewe ni ME kisa tu umeandika kitu asichokubaliana nacho!!! duuh!
Sikubaliani nawe asilani!!

hayo maneno ya kusema wanawake hatupendani yanatoka kwa mwanaume.

Na wanaume ndio hawawapendi wanawake kila siku masimango kwa wanawake hata humu JF.

Kwa andiko lako hili naanza kukuona kama wewe ni me aisee
 
Huwa nasikia wanawake hampendani ila sjathibitisha kama kweli mpo hivo

Nachojua hata sis wanaume baadhi yetu hatuna upendo kati yetu.
Actually binadamu wote tuna wivu na wivu huo ukizidi mara nyingi uzaa chuki ndani yake, ila sema kwa wanawake uenda mbele zaidi na kuzianika wazi wazi na hapo ndipo tunapata ile kauli ya "wanawake hawapendani"
 
Haaaaa haaaaa.Huyo Dada naye Chiboko.Au walishagombana.Nionavyo Mimi Ni kwamba kabla ya wewe kuoa Kuna vile vimsaada Sasa akina WiFi Hakuna.Unategemea ampende kwa lipi
Wivu tuu wa wanawake...hawajawihi gombana wala nn
 
Sawa mkuu

Ila hii tabia ya wanaume kufichaficha mambo inapunguza life span yetu

Kabisa mkuu inapunguza sana, kuna mtu mnaweza mkaishi nae poa tu nyumba moja kwa kipindi kirefu ila siku mkizinguana tu anakumbushia hadi maudhi yako ya 2013 ambayo wewe ulikuwa huyajui. siku zote hizo alikuwa anaumia tu moyoni.
 
Wanawake pendaneni basi.

Unajua sisi ndio inatakiwa tujifunze upendo kutoka kwenu. Kwanza nyie ndio viumbe wenye uhuruma sana katika jamii ya binadamu.
 
Kabisa mkuu inapunguza sana, kuna mtu mnaweza mkaishi nae poa tu nyumba moja kwa kipindi kirefu ila siku mkizinguana tu anakumbushia hadi maudhi yako ya 2013 ambayo wewe ulikuwa huyajui. siku zote hizo alikuwa anaumia tu moyoni.
Kwa hiyo unaonaje tukiwa tunajilipua kama ndugu zetu wa kike
ukizingua unapewa za uso muda huo huo
 
Kwanza nakubali,pili c wote japo hata wale wachache pia wanazo hizo element za chuki.Kiufupi ni ulimbukeni,kutokujitambua na kutokujiamini na nikijua tu kwamba unatabia hizo bac hutokaa karibu namimi.....
 
Haaaaa haaaaa.Huyo Dada naye Chiboko.Au walishagombana.Nionavyo Mimi Ni kwamba kabla ya wewe kuoa Kuna vile vimsaada Sasa akina WiFi Hakuna.Unategemea ampende kwa lipi
Kwani huyo house girl ni mwanaume??
 
Kweli kabisa.Jambo Dogo linakuzwaaa yaani.Yaani Hata ile appreciation wkt mwingine Hakuna.
Mfano.Kuna mama mmoja alikuwa anarudi kijijini kwao kulima Akaona Si vibaya akusanye vitenge Na Nguo za zamani Kidogo awapelekee wa nyumbani .Aisee walimu weka kikao.Kwa nini awape Nguo za zamani asiwanunulie mpya ?? Wakasema au ndo Dharau za mjini hizi? Lakini nia ya mleta Nguo Walau ziwafae kushindia kwa kuwa Hawana.

Huyo mama aliyetaka kupeleka nguo kwa ndugu ni mwanaume? Na hizo nguo alitaka kupelekea wanaume tu? Tabia nyingi ulizotaja hapo zinaendana na uwezo na hadhi. Hata wanaume wa uwezo na hadhi ya chini wana tabia hizo hizo. Wanakaa barazani wakinyoana na kula kashata huku wakimjadili kila anayepita. Kuna msemo kuwa "simple minds discuss people". Ukienda saluni za ushuani utaenda saluni moja mwaka na kitakachokuwa kinaongea ni TV tu. Kila mtu yuko busy na mteja wake na mteja na simu yake au kitabu chake.

Kwenye kupeana kura mwanamke aliyeambiwa hawezi na akaamini anaweza asiamini kuwa mwenzie anaweza. Hata hivyo tuna wanawake wengi tu ni viongozi wa kuchaguliwa na hawajaolewa wala hawana watoto na wamechaguliwa na wanawake wenzao kwani ndo wapiga kura wengi. Kwa hiyo msemo wa wanawake hatupendani ni propaganda zaidi kuliko uhalisia. Mwanamke anayejitambua hawezi kumpa kura mwanamke na kumnyima mwanaume kwa sababu ya jinsi zao.
 
Kwa hiyo wewe kaka unaona sifaaa??umefanya nini Sasa.Acha kudharau Wanawake.Sijaenda Hata kidogo.Njoo Pm

Nishakuja

Ila bana sisi wanaume wa ajabu sana yaani hawa wanawake sikuwa na mazoea nao kabisa. Ila sasa kuna siku wakawa wanatukanana na kwa kuwa ni majirani zangu mimi nikaingilia kati. Sasa dah ndo yakatokea yaliyotokea.

Wanisamehe sana na tamaa zangu
 
Hawapendani kweli
Sasa Ushmen sasa ameanza kufanya nini.Mbona anasema tuendelee kufarakana aendeleew kuwapanga.Ushmen popote ulipo.Pm inakuhitaji
 
Hii txt mkuu umeandika kwa hisia pole mkuu jaribu kutembelea sehem za ufukwe weekend ili mind ako iwe na furaha walau basi mkuu sawa eehh
Ukiona hivyo ujue yamemkuta.Maana asingeandika hivyo Bila ya kumkutaa.Naninaonyesha jinsi gani Wanawake ambavyo tuna safari ndefu
 
Ukiona hivyo ujue yamemkuta.Maana asingeandika hivyo Bila ya kumkutaa.Naninaonyesha jinsi gani Wanawake ambavyo tuna safari ndefu
Sema mmezidi kusemana asee huwa najaribu kuwaza hivi nkioa huyo mwanamke atakuwa wa namna gani,msemaji au mpole,
Je atapenda familia yangu,je atakuwa na kifua juu ya mambo ya ndani ?? Maana kadir siku znavoenda mnatishaa mnasema kwa mashoga zenu adi ya ndani halafu siku mkivurugana wanaishia kukusema mpaka mume wako.mnakosea wap nyie viumbe?
 
Back
Top Bottom