Za jioni.
Kuna msemo usemao adui wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe.
Kwanza tuchukulie mwanamke akiamua kugombea nafasi yoyote ya uongozi, Mfano Urais, Ubunge ama Udiwani sio siri sisi wanawake tutaanza kupiga vita mpaka anaweza acha, uombee sasa huyo mwanamke hajaolewa utasikia mtu mwenyewe hajaolewa atamuongoza nani? Hajazaa, mtu mwenyewe hajazaa atamuongoza nani, vitu vidogovidogo tunapingana.
Mfano mwingine. Mpo njiani wewe na mpenzi au na mume akapita mdada mrembo, au mzuri zaidi yako. Na mume akapiga chabo. Ooh oooh! Ujue wewe naba utanuniwa njia nzima au siku nzima (ila mimi heloo, nikiwa na mpenzi wangu tukapishana na kifaa huwa natoka credits 'mmh msichana au dada bombs huyu sina kinyongo why nisimpe sifa mwanamke mwenzangu mwenye sifa zake?) Kweli huwa natoa sifa.
OK. Tukija Salon hasa za like, mpo wanawake wengi wanaosuka wanaopaka rangi wanaosafisha miguu, uso na mengi mengi, anaongea mnacheka. Akiondoka mmoja kamaliza alichojia huku nyuma wanaanza kumteta huyu aliyeondoka sasa (kuna siku hiyo salon moja nilishangaa sana kila anayeondoka anasimangwa 'hana lolote naye huyu anajifanya ana nywele nzuri sijui pesa wenye pesa wanakuwa hivi? (Kiutani ilibidi niwaombe jamani mimi nikitoka.
Naomba msinitete) waliishia kucheka but sio tabia njema. Mfano mwingine. Inatokea msichana A kampigia simu msichana B. Pengine amemkumbuka na anapenda sana weekend hii amtembelee ashinde huko na wapike wale pamoja, hapo anaongea kwa simu. Akikata tu huyu B ambaye alikuwa anaitikia na kucheka kwanza anaweza sonya na kusema tutaona kama atanikuta 'eti aje kushinda hapa mjinga nini nitaondoka akome.
Kinyume sana kwa wenzetu wa kiume kwa story hiyo juu angefurahi hata haada ya simu na kuhusu jamaa yake amemkumbuka na atahakikisha anamsubilia.
Umbea nao ni dalili ya kutokupendana. Sawa umbeya sio jambo njema hata kidogo lakini kuna wakati watu au palipo na wengi pana neno.
Sasa unafuatwa unasimuliwa jambo Na mwenzio anakusihi sana usiseme Na unaapa kwamba hutasema. Akiondoka tu unatafuta simu ipo wapi na unaongezea na chunvi. Mwanzo wa chuki miongoni mwa sisi wanawake.
Mwenzio ana familia nzuri bora badala uige unaanza kutoa kasoro zote, umehudhuria sherehe ya best ako unaanza kukosoa ukumbi, chakula Mara Nguo rangi sio nzuri lakini wakati yupo ulisifia sana (unafiki)
Jamani wanawake wenzangu kifanyike kitu gani kupunguza chuki hizi ili jamii yetu iwe bora? Maana haya mambo ndo huzaa chuki na watu kuchukiana.
Akhsante.