Kwanini wanaume wengi hufeli swali hili wakitongoza?

Kwanini wanaume wengi hufeli swali hili wakitongoza?

Ningekuwa mimi ningejibu hivi.

1. Kwanza, nimekusoma kama mtu ambaye anakubalika kwenye jamii, kama nilivyo mimi. Unajiheshimu kwa mavazi na kauli. U mcheshi na mkarimu kwa wote. Nimechukua muda kukuchunguza, sijakurupuka "from nowhere". Mimi si wale wanaojitosa kichwa-kichwa bila kwanza kumchunguza na kumfahamu kidogo mtu ninayetaka kujenga urafiki naye.

2. Pili, mti wenye matunda ndio upigwao mawe. Wewe ni mzabibu, tena mzabibu wenye zile zabibu zenye harufu na matunda yaliyo bora zaidi. Kwa nini nisivutiwe nawe mpaka nikaitafuta namba yako?

3. Kuna rafikiyo ambaye ni msiri wangu ndiye aliyenipa namba yako kwa masharti kwamba nisilitaje jina lake kwako iwapo ungeniuliza. Kwa kuwa nimekula kiapo, siwezi kumsaliti.

Tuendelee na mahusiano yetu. Kwangu sioni kikwazo, lakini iwapo hujaridhia, Binti Mwema, nieleza, nitaacha kukufuata.

Asante.

Wako Mtiifu.

--------------------

Hivi ndivyo ningemjibu hilo swali.

Sijui wengine wangemjibu kwa namna gani.

Umetisha Mkuu. Hapo demu hachomoi, kwa mistari hiyo???
 
Maswali haya huwa nayapenda sana
Mimi nawaambiaga nimepewa na rafiki yake tena kwa kuinunua lakin sharti nisimtaje huyo rafik
 
Hawa wa siku hizi hilo swali hata hawaulizagi,ukiona umeulizwa ujue umeonekana haueleweki!

Anyway mimi huwa nikipata namba na iwapo nimekusudia kweli kumpata huyo muhusika huwa namtumia 50,000 kwa njia ya simu alafu nakaa kimya hadi apige yeye na wengi huwa wanapiga,akipiga unampongeza kwa kuwa na roho nzuri na ubinadamu alionao na baada ya hapo kazi ni kwako,asipopiga baada ya siku mbili namuandikia text nikimwambia kuwa nilikosea kumtumia hela juzi na sio mbaya kama akinirudishia hata nusu.hapa tayari unakuwa umelianzisha na hakuna kurudi nyuma.
Hii mbinu imesimama..mtaani kuna binti anajichengua...na kazi anayofanya ni ngumu sana kumpata na kuongea naye..ngoja nitafute namba yake!!
 
Ntamwambi namba yako nilivyokuwa nataka kutuma hela likatokea jina lako ambalo sikulitegemea kutokea kwani hujapata hela yeyote ileeee??

Akijibu nyodoo huyoo hata namba yake nafutaaaa
 
Kwahiyo ulikosea namba halafu tena unamtongoza? Hivi inaingia tena akilini hapo? Kwa jibu lako hili tu naanza kuamini kuwa ni kweli Wanaume wengi wa siku hizi hawajui kutongoza.
Nakutongoza sasa,mimi najua
 
Back
Top Bottom