Kwanini wanaume wengi hufeli swali hili wakitongoza?

Kwanini wanaume wengi hufeli swali hili wakitongoza?

enzi hizo ni newbie katika haya mambo nilikuwa namtaja mtu ambaye wote hatumjui, mfano
dame: namba yangu kakupa nani
mimi: sergei lavrov na mchezo unaisha..
 
Swali rahis sana hili! Kulijibu inategemea amekuuliza kwa "kiimbo gani ". Jibu nzuri. Namwambia usihangaike kuulizia na kumjua alienipa namba ila naomba usikilize kilichonifanya nikahangaika mitaa yote kutwa jua mvua kali kutafuta namba yako ndicho kikubwa.

Yes wew genius mkuu! Baada ya hapo hawezi kkuuliza tena mpaka a day mna meet face to face huwa ndio inakuwa hivyo! Na siku mkikutana akirudia swali hilo wala usimjibu muangalia machoni kwa sekunde 5 mpaka 10 bila kuongea chochote wala kupepesa macho then mjibu hivi ! Call her name like .....Jane/Tinam? Msogelee karibu Hata ukiweza zaidi mshike mkono note: usimkumbatie maana unaweza kuharibu kabisa then vuta pumzi na mwambie "muda wa kumfikiria alie nipa number yako wala sina nahisi muda nilio nao tu wa kuzungumzia pendo langu kwako hautoshi! Please nakupenda that is what matter most , sawa mpenzi? (Hato likumbuka tena hilo swali labda siku mkitoka leba)
 
jamani hawa viumbe ni wetu tumeumbiwa ss wanaume na tumeagizwa tushi nao kwa akili sawa, pindi unachukua namba kwa huyo mtu anaemfahamu huyo binti muulize taarifa zote za msingi kuhusu huyo demu sawa kama anaishi wapi,anaitwa nani,kasoma shule wapi na anapendelea nini sawa. mwenzenu kila siku nawagegeda kwa kuchukua namba kawa watu swali kama hilo ni raisi sana ukiwa unajiamni akikuuliza mjibu hivi
1.mwambie namba ulinipa ww mwenyew siku hiyo mlikuwa na mwenzako maeneo karibu na stendi japo mlikuwa na haraka sijui kama unanikumbuka coz ni mwezi umepita sasa tokea unipe namba yako,atakuuliza kimekusibu nn mpka unitafute,mjibu nilikuwa napitia contact za simu hapa nimekuona na nilivutiwa sana nawe siku hiyo thus why nimekutafuta.
2.jaribu kuwa mbunifu na kutawala mazungumzo akikuuliza kitu au swali mjibu kwa ufupi na badilisha mada faster but mada ihusiane na alichokuuliza, mfano unataka nn kwang sasa, mwambie jaman sory kama nakukwaza au kukusumbua (cykologically yy atajihisi amekosea na atakuwa kimya kwa mda) sasa hapo ndio point ya ushind kwako mwambie hiv hapo unatokea mitaa gani mbna kama vile ww ni mgeni hapo coz hiyo mitaa naifahamu vizur sana
 
Mleta mada Wee Veepe!?? Kwanza umeshahitimisha kwamba ni swali ambalo wanaume wengi linawapa shida!!!! Sijui utafiti huu uliufanyia wapi?, cha ajabu, unaomba watu wakuambie majibu sahihi ya swahili hilo yaweje!!!!!??? Hii nini? Si useme tu kama unahitaji msaada!!
 
Unamwambia tu ulipo ipata namba yake. ...unamweleza na hitaji la moyo wako kwake. .....akileta pozi achana nae kwani hakuna kitu kipya kwake na maisha yataendelea kama kawa! !!!![emoji12]
 
''Endelea kuuliza namba yangu alikupa nani uzeekee kwenu" hahaha nilikutana na huu msemo dogo anaulizwa na demu namba yangu alikupa nani,dogo anapotezea kwa kujibu hivo
 
Namba nimepata LOANS BOARD sisi ndo tunachambua wadaiwa sugu na kuwapunguzia 50% ya madeni yao.
 
Wanaume wamekuwa wakijifanya ni mabingwa kama siyo majabali wa kutongoza lakini mara baada tu ya ujio wa simu za mkononi hakika zimekuwa ni kama ni mateso makubwa kwao.

Nalisema hili kutokana na kwamba unaweza kumkuta mwanaume anapambana au anahangaika kuipata namba ya mwanamke fulani ambaye hajuani nae au labda namba yake kaipata tu kwa mtu ili aanze kumtongoza kwa simu ama kwa kumpigia au kumtumia meseji lakini imekuja kujulikana kuwa hakuna mtihani mgumu au swali gumu ambalo wanaume wengi hukumbana nalo na ambalo wengi wao hushindwa kulijibu na hatimaye kujikuta wanajichanganya na wanamkosa huyo mwanamke.

Utakuta mwanaume anaanza kujitutumua kwa kuwasiliana na huyo mwanamke lakini akiulizwa tu swali hili " je namba yangu umeitoa wapi au kakupa nani? " wengi wao hukata tamaa kabisa na hata kuishiwa tena nguvu za kuendelea kuwasiliana na yule binti au mwanamke kwani hakuna swali ambalo wanaume wengi hawalipendi na hawaliwezi kulijibu kama hilo.

Labda leo tupate uzoefu kutoka kwa wanaume ambao naamini humu mpo wengi ni kwanini wengi wenu pamoja na jeuri zenu zote mkiulizwa tu hilo swali tajwa hapo juu huwa mnajiumauma na hatimaye kusepa na kuishia kulalamika tu?

Na je unadhani majibu sahihi ya kumjibu mwanamke ambaye hujuani nae halafu umepata tu namba yake kwa mtu na unataka kumtongoza endapo atakuuliza hilo swali kuwa " namba yangu umeitoa wapi au namba yangu kakupa nani? " ni yapi au ni lipi?


Hiyo ni kwa wanaume wajinga tu....utamtafutaje mwanamke wakati wewe mwanamme? Wacha waje kujigonga kwako na kupigana juu yako kisha unajiokotea kiulainiiiii tena bila hata kulipa.
 
Back
Top Bottom