Ningekuwa mimi ningejibu hivi.
1. Kwanza, nimekusoma kama mtu ambaye anakubalika kwenye jamii, kama nilivyo mimi. Unajiheshimu kwa mavazi na kauli. U mcheshi na mkarimu kwa wote. Nimechukua muda kukuchunguza, sijakurupuka "from nowhere". Mimi si wale wanaojitosa kichwa-kichwa bila kwanza kumchunguza na kumfahamu kidogo mtu ninayetaka kujenga urafiki naye.
2. Pili, mti wenye matunda ndio upigwao mawe. Wewe ni mzabibu, tena mzabibu wenye zile zabibu zenye harufu na matunda yaliyo bora zaidi. Kwa nini nisivutiwe nawe mpaka nikaitafuta namba yako?
3. Kuna rafikiyo ambaye ni msiri wangu ndiye aliyenipa namba yako kwa masharti kwamba nisilitaje jina lake kwako iwapo ungeniuliza. Kwa kuwa nimekula kiapo, siwezi kumsaliti.
Tuendelee na mahusiano yetu. Kwangu sioni kikwazo, lakini iwapo hujaridhia, Binti Mwema, nieleza, nitaacha kukufuata.
Asante.
Wako Mtiifu.
--------------------
Hivi ndivyo ningemjibu hilo swali.
Sijui wengine wangemjibu kwa namna gani.