Kwanini wanaharakati wengi waliovuma kipindi cha Magufuli wamepoteza umaarufu wao awamu hii?

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,834
18,835
Kipindi cha Magufuli tulishuhudia kuibuka kwa wanaharakati wengi mtandaoni
Kuna ambao walikuwepo tangu zamani lakini umaarufu wao ukaongezeka mara dufu kipindi cha Magufuli na wengine hawakuwahi kuwepo kabisa katika harakati za siasa kabla ya urais wa Magufuli
Baadhi ya Wanaharakati hao ni

Fatma Karume: Fatma Karume ni wachache walikuwa wanamjua kabla ya awamu ya tano, ambapo alipaa kiumaarufu alipokuwa wakili wa Tundu Lissu na baadae ofisi yake kupigwa bomu na kisha kuvuliwa uwakili. Kipindi cha Samia hasikiki tena kama ilivyokuwa awamu ya 5,


Tundu Lissu: Tundu Lissu ni mwanaharakati wa siku nyingi, lakini umaarufu wake uliongezeka mara dufu kipindi cha Magufuli kutolana na ukosoaji wake na kupigwa risasi zilizokaribia kidogo kuchukua uhai wake, kipindi hiki cha Samia hasikiki tena kama kipindi cha Magufuli

Kigogo: Huyu ni mtu anayedaiwa jina lake halisi ni Didier Mlawa, Kigogo alivuma sana kipindi cha Magufuli kutokana na kumkosoa kwa lugha kali na kuvujisha habari nyingi za Ikulu, awamu hii ya Samia hasikiki tena

Mdude Nyagali: Mdude Nyagali ni mwanaharakati kutoka kipindi cha Kikwete, lakini umaarufu wake ulikuwa mara dufu kipindi cha Magufuli, kutokana na ukosoaji wake wa kutumia lugha kali, Mdude pia alitekwa na watu wasiojulikana na kunusurika kuuawa, na baadae kufungwa kwa kesi ya madawa ya kulevya na kukaa ndani muda mrefu, huyu naye hasikiki awamu hii kama awamu iliyopita

Maria Sarungi: Maria Sarungi ni mwanaharakati wa kitambo, lakini harakati zake na umaarufu vilifikia kilele chake kipindi cha Magufuli ambapo yeye na mwenzake Fatma walifahamika kama "shangazi"

Askofu Emmaus Mwamakula: Askofu huyu naye aliibuka kipindi cha Magufuli, alipata umaarufu kwa kukosa na alikuwa akiandamana sana na viongozi wa Chadema, sasa hivi amepoa

Cyprian Musiba: Musiba ambaye alikuwa ni mwanahabari, aligeuka kuwa mwanahakati aliyezua gumzo kipindi cha Magufuli, tofauti yake na wanaharakati wengine ni kuwa yeye alikuwa akiitetea utawala wa Magufuli na sio kukosoa


Wengine ni kama Rugemeleza Nshala, aliyekuwa Rais wa TLS, Askofu Bagonza, Abdul Nondo na wengine
 
Back
Top Bottom