A
Anonymous
Guest
Sisi baadhi ya Walimu Wilayani Kilwa tunazuiwa kujiunga katika Chama cha CHAKUHAWATA licha ya kuwa kuna wenzetu kati ya Walimu zaidi ya 300 wameshaamua kuhama kutoka CWT na kuhamia upande huo wa pili kutokana na makato makubwa ya CWT.
Kinachofanyika CWT wanaenda kwa Afisa Utumishi kuzuia Walimu wasitoke hali ambayo inachangia kuwavunja moyo Walimu katika ufanisi wa kazi kwa kuwa kwa nini watulazimishe tuendelee kubaki CWT?
Tunaomba Rais Samia Hassan Suluhu atamke neno la kuturuhusu Walimu tuende kwenye chama tunachokitaka, kwani kuna dalili za upigaji na rushwa kwa viongozi wa CWT kwa jinsi wanavyotuganda tusiondoke, wana jambo na maslahi yetu hawa, wanachama tunajua ndio maana baadhi yetu tunaamua kuhama.
Aidha, kuna mpango wa Walimu 23 waliohamia CHAKUHAWATA wanataka warudishwe tena CWT.
Jamiiforums tunaomba mtupazie sauti Kwa kuwa nyie mmekuwa sauti ya wanyonge.
Ni mimi Mwalimu kutoka Wilaya ya Kilwa Masoko Mkoa wa Lindi.