Kwanini Waisrael walikataa kuja Uganda?

Kwanini Waisrael walikataa kuja Uganda?

Mwarabu huyu huyu aliyeendesha biashara ya utumwa Pwani na bagamoyo na anaetesa wafanyakaz wa ndani huko saudia au mwingine/?kweli unamahaba na waarabu kijanaa, ungekuwa demu ungewapa tigo

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
Kwanza biashara ya utumwa ilikuwepo mataifa yote na hao wazungu ndiyo walikuwa mstari wa mbele kusafirisha hiyo 'bidhaa' kutoka afrika magharibi kwenda Marekani. Soma historia kijana.

Pili hao waafrika mababu zenu ndiyo walishiriki kikamilifu kwenye hiyo biashara kwa kuwauza waafrika wenzao kwa hao waarabu na wazungu waliokuwa wakifanya biashara hii.

Tatu wanaotesa wafanyakazi hata nyinyi watanzania mupo wengi tu, tena mateso mabaya sana yasiyo na mfano.

Ukimnyooshea mwenzako kidole kimoja, vinne vinakunyooshea wewe.
 
Nasikia ilipangwa na wakubwa kuwa waisrael watafutiwe eneo Uganda na kuhamishiwa hapo. Hilo ndo lingekuwa Taifa lao cha ajabu nasikia ni Waisrael wenyewe walioanza kuukataa katakata mpango huo. Wajuzi naomba mnijuze;

1. Kwanini hawa jamaa walikataa kuhamia Uganda kwenye mito na ardhi yenye rutuba tele na kukubali kule Middle East kwenye joto kali na migogoro isiyokwisha? au kuna kitu wanafahamu kuhusu Afrika ndio maana wakajikimbilia zao?

2. Mnafikiri kama wangepewa kipande flani cha Ulaya, amerika au Asia wangekataa pia? wajuzi naomba mnieleweshe kidogo maana sielewi elewi (nahisi kama Afrika kuna jambo flani la giza hv (litatokea) na hawa jamaa weupe wanalijua vizuri).
Ilipangwa pia waje Mpwapwa Dodoma wakakataa it is not the promised land so is Uganda
 
Kwani hao jamaa kwao hasa ni wapi mkuu,na ilikuaje wakapatelekeza wote mpaka vibabu na kwenda kutangatanga huko kwa Hitler
Sidhani kama ni kweli eti Wayahudi wote wale tunao waona basi wamaetokea UHAMISHONI, wengi tu walikua bado wana ishi hapo hapo mashariki ya kati.
 
Mkuu uko sahihi! Baada ya mateso mazito yaliyosababishwa na Hitler,Umoja wa Mataifa wa wakati huo ulipendekeza kuwahamishia Uganda au Ajentina lakini walikataa kwa sababu walitaka kurudi katika nchi ya Ahadi ambayo Mungu aliwapa mababu zao Ibrahimu,Isaka na Yakobo.Na bila shaka walilikumbuka Agano la Mungu alilofanya na mababu zao,(Kumbukumbu30:1-10)
 
Wewe sasa ndio hujui kitu, kama huna habari na hilo, hata Museveni ashaliongelea hilo suala mbele ya Netanyahu, akasema wangepigana vita hadi mwisho wa dunia
Basi sawa mkuu ngoja nitafuatilia. Maana anapenda kujifunza vingi hasa nisivyovijua kabisa.
 
“You will never be able to live here in peace, because you left here black and came back white” Gamal Abdel(1952) 2nd President of Egypt Gamal Nasser (Quote about fake jews currently in Israel) Gamal Nasser was the leader of Egypt from 1954 until his death in 1970.
 
Mtu wa kwanza kaingiaje kwenye hoja kama hii?
Hata waisrael walipotawanyika huko duniani bado kulibakia waisrael wachache pale Israel.
Na pia historia yao hawakuwai kuisahau, daima walijiapisha kurudi kwao siku moja.
Mtu wao WA Kwanza ( Ibrahim) Kama sijakosea , yaani huyo jamaa katokea iraQ
 
Uganda pia ilikuwemo katika moja ya maeneo waliyoambiwa wapewe.
Siyo Kweli, ingawa plan iliitwa British Uganda Scheme, eneo lilolokuwa limetengwa lilikuwa Kenya siyo Uganda. Wakati huo waingereza walikuwa wanaitawala Kenya kutokea Uganda, kwani Uganda ilikuwa ni Colony, wakati Kenya ni Protectorate, lakini zote kwa pamoja zikiwa zinaitwa British East Africa. Angalia hata Wikipedia wameiweka pia, ingawa wikipedia siyo reference nzuri lakini hapa hawakukosea. Kuna kitabu nitakutafutia ambacho kina history ndefy ya Taifa la Israle kuazia enzi za King David hadi Modern Day Israel.

1621442198696.png


1621442429565.png
 
Waisraeli sio makaburi, wanajua nchi yao ilipo na wanao ushahidi wa kutosha kuwa mahali walipo ndio kwao. Kama Jerusalem ingeweza kuhamishiwa Uganda, wangekubali kwenda Uganda.

Vv

Mkuu, mfano sisi huku tujikusanye watu milioni 5 alafu tuchukuliwe mpaka Asia huko kwa akina kim, tukajikatie kijisehemu cha kuishi bila idhini yao, je! Tutakua na uhalali kwa hilo?


🇦🇷🇦🇷🇦🇷🔥🔥
 
Hizi story za imani fake za ajabu sana. Ni sawa wangoni watake kurudi south Afrika eti kudai ardhi mababu zao walipokuwa wanaishi. Au aje mtu hapo kwenu adai ni kwake eti Mungu wake kasema hilo eneo ni nchi yake ya ahadi

Hata mimi naona ni upumbavu tu 😂😂


🇦🇷🇦🇷🇦🇷🔥🔥
 
Kiuhakika hasa na wala siyo kwa kuwasema vibaya lakini Jews walikuwa hawapendwi katika mataifa mengi sana ya Ulaya. Kila walipokuwepo basi biashara zote walikuwa wanazihodhi wao, yaani mfano, mabenki ambayo yaliyokuwa yanakopesha kwa riba kubwa sana na biashara nyingi za kilaghai laghai hivi.

Jaribu kusoma historia nyingi za Europe utakumbana na jamaa hawa na biashara zao zisizoeleweka. Hata hapo Ujerumani, Poland na Urusi mfano, chuki zilianza dhidi ya Jews kwa mtazamo kwamba wao ndiyo wanaoleta umasikini kwa wananchi (sawa na kwetu hivi sasa tunavyosema wahindi ndiyo wanaotusababishia umasikini).
Mkuu Jew gani ambao walikuwa hawapendwi Mkuu,kitu ambacho hakipo kinawezaje kutopendwa??.Hao wanaoitwa species za Israel zilishafutika miaka na miaka.Soma vitabu sikiliza hotuba na mahojiano ya kwa nini Mgogoro wao.

Ulimwengu umejaa hadaa,UK na USA walifanikisha mambo haya kwa malengo yao wanayoyajua wao wenyewe.
 
Kumbuka hata walipokuwa Misri walikaa utumwani miaka 430 ndiyo wakarudi kwao

Kwao ni wapi? Yani wameishi egypt miaka 430 halafu warudi kwao kule walipo palestina!!! Hizi akili za wapi? Makafiri wa kiyahudi wamewaingiza chaka aise
 
Hizi story za imani fake za ajabu sana. Ni sawa wangoni watake kurudi south Afrika eti kudai ardhi mababu zao walipokuwa wanaishi. Au aje mtu hapo kwenu adai ni kwake eti Mungu wake kasema hilo eneo ni nchi yake ya ahadi

Makafiri wa kiyahudi wamewapotosha hawa viumbe
 
Nasikia ilipangwa na wakubwa kuwa waisrael watafutiwe eneo Uganda na kuhamishiwa hapo. Hilo ndo lingekuwa Taifa lao cha ajabu nasikia ni Waisrael wenyewe walioanza kuukataa katakata mpango huo. Wajuzi naomba mnijuze;

1. Kwanini hawa jamaa walikataa kuhamia Uganda kwenye mito na ardhi yenye rutuba tele na kukubali kule Middle East kwenye joto kali na migogoro isiyokwisha? au kuna kitu wanafahamu kuhusu Afrika ndio maana wakajikimbilia zao?

2. Mnafikiri kama wangepewa kipande flani cha Ulaya, amerika au Asia wangekataa pia? wajuzi naomba mnieleweshe kidogo maana sielewi elewi (nahisi kama Afrika kuna jambo flani la giza hv (litatokea) na hawa jamaa weupe wanalijua vizuri).
Hii habari umeitoa wapi?
 
Back
Top Bottom