Kwanini Waisrael walikataa kuja Uganda?

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
1,349
2,000
Nasikia ilipangwa na wakubwa kuwa waisrael watafutiwe eneo Uganda na kuhamishiwa hapo. Hilo ndo lingekuwa Taifa lao cha ajabu nasikia ni Waisrael wenyewe walioanza kuukataa katakata mpango huo. Wajuzi naomba mnijuze;

1. Kwanini hawa jamaa walikataa kuhamia Uganda kwenye mito na ardhi yenye rutuba tele na kukubali kule Middle East kwenye joto kali na migogoro isiyokwisha? au kuna kitu wanafahamu kuhusu Afrika ndio maana wakajikimbilia zao?

2. Mnafikiri kama wangepewa kipande flani cha Ulaya, amerika au Asia wangekataa pia? wajuzi naomba mnieleweshe kidogo maana sielewi elewi (nahisi kama Afrika kuna jambo flani la giza hv (litatokea) na hawa jamaa weupe wanalijua vizuri).
 
Luggy

JF-Expert Member
Aug 6, 2012
3,030
2,000
nasikia ilipangwa na wakubwa kuwa waisrael watafutiwe eneo uganda na kuhamishiwa hapo. hilo ndo lingekuwa taifa lao. ajabu nasikia ni waisrael wenyewe walioanza kuukataa katakata mpango huo. wajuzi naomba mnijuze;

1. kwanini hawa jamaa walikataa kuhamia uganda kwenye mito na ardhi yenye rutuba tele na kukubali kule middle east kwenye joto kali na migogoro isiyokwisha?!!! au kuna kitu wanafahamu kuhusu afrika ndo maana wakajikimbilia zao?

2. mnafikiri kama wangepewa kipande flani cha ulaya, amerika au asia wangekataa pia? wajuzi naomba mnieleweshe kidogo maana sielewi elewi (nahisi kama afrika kuna jambo flani la giza hv (litatokea) na hawa jamaa weupe wanalijua vizuri).

karibuni kwa kutoa elimu!
Kwani Uganda ni kwao?,
Walikataa kwa sababu si kwao
 
Ravalomanana

JF-Expert Member
Sep 8, 2018
761
1,000
Hakuna kitu kama hicho ulikoambiwa umedanganywa kabisaaa
Walipewa eneo na UN acha ubishi na hii ilikua ni kabla ya mwaka 1948 ambao ni mwaka nchi ya israel ilianzishwa kama sikosei, kabla ya hapo walikua wanaishi Germany na nchi nyingine za ulaya ila kutokana na mateso ya adolph hitler wakaomba UN iwatafutie eneo na walipewa Uganda lakini walikataa, baada ya kutokubali kwenda Uganda wakaamua kwenda eneo ambalo wapo leo hii kwa kufuata hadithi za kwenye Bible na wakawakuta wapalestine
 
KISIWAGA

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
4,091

Kwani hao jamaa kwao hasa ni wapi mkuu,na ilikuaje wakapatelekeza wote mpaka vibabu na kwenda kutangatanga huko kwa Hitler
 
NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
1,349
2,000
Walipewa eneo na UN acha ubishi na hii ilikua ni kabla ya mwaka 1948 ambao ni mwaka nchi ya israel ilianzishwa kama sikosei, kabla ya hapo walikua wanaishi Germany na nchi nyingine za ulaya ila kutokana na mateso ya adolph hitler wakaomba UN iwatafutie eneo na walipewa Uganda lakini walikataa, baada ya kutokubali kwenda Uganda wakaamua kwenda eneo ambalo wapo leo hii kwa kufuata hadithi za kwenye Bible na wakawakuta wapalestine
ahsante sana kiongozi kwa elimu hii....akiendelea kubisha tena basi atakuwa mshindi wa ubishi na tutamtafutia mji kama zawadi; binafsi nampatia chato!
 
NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
1,349
2,000
Kama wewe ni muislam au ni mkristo unajua kabisa kwamba israelites kwao ni pale Jerusalem na huo ugomvi wao na hao ndugu zao wa kambo ni 5000 iliyopita unless una mashaka na imani yako
hata sina mashaka na imani yangu, nina mashaka na hatua yao ya kukataa ardhi nzuri na eneo lenye amani.
 
Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
11,910
2,000
Sasa kama wapalestina ni ndugu zao,na wa Wapalestina ni Waarabu kabisa inakuwaje waka transform kutokana kwenye Uarabu hadi kwenye uzingu?
 
Come27

JF-Expert Member
Dec 1, 2012
6,017
2,000
Walipewa eneo na UN acha ubishi na hii ilikua ni kabla ya mwaka 1948 ambao ni mwaka nchi ya israel ilianzishwa kama sikosei, kabla ya hapo walikua wanaishi Germany na nchi nyingine za ulaya ila kutokana na mateso ya adolph hitler wakaomba UN iwatafutie eneo na walipewa Uganda lakini walikataa, baada ya kutokubali kwenda Uganda wakaamua kwenda eneo ambalo wapo leo hii kwa kufuata hadithi za kwenye Bible na wakawakuta wapalestine
Bora hawakuenda Uganda, maana wangeanzisha migogoro mingi kama South Africa
 
sala na kazi

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
4,890
2,000
Inferior complexity ya waIsrael ndio inawafanya wanakuwa mbogo..

Wanahisi wanaonewa...ogopa sana watu wa dizaini hii
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom