Kwanini wagonjwa wanaogopa Mloganzila?

Kwanini wagonjwa wanaogopa Mloganzila?

Ulisoma Research Methods, kuna:-

1. Research Question
2. Conclusion

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Wanaosema Mloganzila ndiyo hospitali kubwa (na bora) JMT kwanini:-
1. Big Ben Mkapa alifia hospitali ndogo (basi) ya Muhimbili?

2. JPM alilazwa JKCI na kufia Mzena?

3. John Kijazi alifia MNH?

4. Matajiri wakubwa walifia Aga Khan?

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Screenshot 2023-10-30 135554.png
 
Baba yangu mdogo alipoambiwa tu anaenda mloganzila hakumaliza wiki akafariki ,

Binafsi jumatano ya wiki iloisha tulikuwa na mjadala mrefu sana kuhusu mloganzila ,, (PIA JINA LAKE BAYA LINAOGOPESHA)
Kuna kitu kikubwa tu cha kuweka sawa kwenye akili za wengi ila mimi binafsi nikiambiwa nikatibiwe huko ,niacheni tu kwani safari yetu ni moja sema muda ndio tofautii
 
Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila.
Shida ya kwanza inaanzia hapa! Inapoitwa hospitali ya mafunzo, unategemea jamii iwe na mtazamo upi?

Kwamba unaenda hospitali kufanyiwa mafunzo?


Hospitali karibia kubwa zote zina vyuo vya afya. Lakini kukosekana kwa neno hospitali ya mafunzo kwenye majina ya hospital hizo kunawapa faraja wagonjwa kabla ya mambo mengine yoyote. Achilia mbali kuwa mda mwingine wagonjwa watahudumiwa na wanachuo wa mafunzo.


Ila hapo mloganzila, mtu anenda anajua kabisa mimi naenda kufanyiwa mafunzo na wanafunzi
 
Shida ya kwanza inaanzia hapa! Inapoitwa hospitali ya mafunzo, unategemea jamii iwe na mtazamo upi?

Kwamba unaenda hospitali kufanyiwa mafunzo?


Hospitali karibia kubwa zote zina vyuo vya afya. Lakini kukosekana kwa neno hospitali ya mafunzo kwenye majina ya hospital hizo kunawapa faraja wagonjwa kabla ya mambo mengine yoyote. Achilia mbali kuwa mda mwingine wagonjwa watahudumiwa na wanachuo wa mafunzo.


Ila hapo mloganzila, mtu anenda anajua kabisa mimi naenda kufanyiwa mafunzo na wanafunzi
Mloganzila sio hospital ya mafunzo toka kipindi cha Magufuli
 
Tujadili kupata uelewa mpana.

Kumezuka mtazamo hasi unaoshika kasi ya kusambaa kwenye jamii pana kama moto wa nyika ambapo ndugu za wagonjwa na wagonjwa wenyewe wamejenga dhana hasi juu ya huduma za tiba, uuguzi na uchunguzi zinazotolewa na Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila.

Unaweza kusikia haya kwenye jamii yakihojiwa:-

Amepewa rufaa!!??

Ndiyo.

Kwenda wapi!!?

Eti Mloganzila!!

Uuuwiii... Mungu wetu tusaidie...

Huyo harudi... tujihesabie huyo si wetu tena... jamani lakini kwanini hivi?

Wamewapa sababu gani ya kumpeleka Mloganzila!!?? Kwani mmeshindwa bei MNH?

Hapana, eti wanasema wagonjwa wamejaa MNH hakuna nafasi.

Maskiniii... kwani hatuwezi kuungana tukachangishana tumtoe huko tumpeleke hospitali binafsi bora mara 100?

Sijui mwenzenu mie nimechanganyikiwa mazima sijui cha kufanya, nawaza mengi bila majibu.

NB.
Hiyo hapo juu ni taswira halisi inayojengeka kwenye jamii kuhusu Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila.

Maswali:-
1. Rufaa inatokaje hospitali kuu ya taifa kwenda hospitali ndogo ya mafunzo? Rufaa za kimatibabu zinapanda juu hazishuki chini kwa mujibu wa itifaki ya tiba.

2. Hospitali ya Mafunzo inakosaje (inasajiliwaje) bila kuwa na madaktari bingwa wanaopaswa kuwepo hospitalini full time?

3. Ni uwiano gani wa wagonjwa mahututi wanapona na wasiopona?

4. No. 3 hapo juu ni asilimia ngapi?

5. Wakati MUCHS inafundisha wanafunzi wa udaktari na uuguzi MNH (kabla ya Mloganzila) No. 3 na 4 takwimu zilikuwaje?

6. Wakati MUCHS iko MNH je, dhana hasi ya wagonjwa na ndugu zao kuogopa kufa kwa kigezo cha matibabu-mafunzo ilishamiri?

7. Unadhani nini kifanyike kuondoa dhana hasi hii na kurejesha matumaini yaliyotoweka ya wagonjwa na ndugu zao kwa Mloganzila kama siyo jamii nzima?

8. Kwanini viongozi na matajiri hawapewi rufaa kwenda Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila ilhali madaktari bingwa na wauguzi bingwa wanapangiwa kufanya tiba-mafunzo pale?

9. Ina maana Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila ni ya makabwela ambao ndiyo roho zao zinatumika kufundishia?

10. Inakuwaje mfano wagonjwa wa saratani wanalazwa Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila wakati vifaatiba vya teknolojia ya hali ya juu viko Hospitali-bobezi ya Saratani Ocean Road ambayo ni Hospitali bingwa pekee ya Saratani EAC, Shoroba za Kusini mwa Afrika na Afrika ya Kati.

NB.
Jamii itapomaliza mjadala na kujipatia plan B yafuatayo yatajiri:-

1. Hospitali binafsi zitatajirika.

2. Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila itakosa wagonjwa wa kufundishia na itakuwa inawatafuta hospitali binafsi kwa gharama kubwa.

3. Viwango vya mafunzo Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila vitashuka ubora.

Tujadili.
Serukali inayojali afya na ustawi wa raia wake, wangeifanya Mloganzila kuwa hadhi kubwa zaidi ya MNH.

Lakini ukweli ni kuwa kuna vifaa tiba vizuri kule ingawa hakuna mabingwa wa kutosha
 
Back
Top Bottom