Kwanini wagonjwa wanaogopa Mloganzila?

Kwanini wagonjwa wanaogopa Mloganzila?

Tujadili kupata uelewa mpana.

Kumezuka mtazamo hasi unaoshika kasi ya kusambaa kwenye jamii pana kama moto wa nyika ambapo ndugu za wagonjwa na wagonjwa wenyewe wamejenga dhana hasi juu ya huduma za tiba, uuguzi na uchunguzi zinazotolewa na Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila.

Unaweza kusikia haya kwenye jamii yakihojiwa:-

Amepewa rufaa!!??

Ndiyo.

Kwenda wapi!!?

Eti Mloganzila!!

Uuuwiii... Mungu wetu tusaidie...

Huyo harudi... tujihesabie huyo si wetu tena... jamani lakini kwanini hivi?

Wamewapa sababu gani ya kumpeleka Mloganzila!!?? Kwani mmeshindwa bei MNH?

Hapana, eti wanasema wagonjwa wamejaa MNH hakuna nafasi.

Maskiniii... kwani hatuwezi kuungana tukachangishana tumtoe huko tumpeleke hospitali binafsi bora mara 100?

Sijui mwenzenu mie nimechanganyikiwa mazima sijui cha kufanya, nawaza mengi bila majibu.

NB.
Hiyo hapo juu ni taswira halisi inayojengeka kwenye jamii kuhusu Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila.

Maswali:-
1. Rufaa inatokaje hospitali kuu ya taifa kwenda hospitali ndogo ya mafunzo? Rufaa za kimatibabu zinapanda juu hazishuki chini kwa mujibu wa itifaki ya tiba.

2. Hospitali ya Mafunzo inakosaje (inasajiliwaje) bila kuwa na madaktari bingwa wanaopaswa kuwepo hospitalini full time?

3. Ni uwiano gani wa wagonjwa mahututi wanapona na wasiopona?

4. No. 3 hapo juu ni asilimia ngapi?

5. Wakati MUCHS inafundisha wanafunzi wa udaktari na uuguzi MNH (kabla ya Mloganzila) No. 3 na 4 takwimu zilikuwaje?

6. Wakati MUCHS iko MNH je, dhana hasi ya wagonjwa na ndugu zao kuogopa kufa kwa kigezo cha matibabu-mafunzo ilishamiri?

7. Unadhani nini kifanyike kuondoa dhana hasi hii na kurejesha matumaini yaliyotoweka ya wagonjwa na ndugu zao kwa Mloganzila kama siyo jamii nzima?

8. Kwanini viongozi na matajiri hawapewi rufaa kwenda Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila ilhali madaktari bingwa na wauguzi bingwa wanapangiwa kufanya tiba-mafunzo pale?

9. Ina maana Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila ni ya makabwela ambao ndiyo roho zao zinatumika kufundishia?

10. Inakuwaje mfano wagonjwa wa saratani wanalazwa Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila wakati vifaatiba vya teknolojia ya hali ya juu viko Hospitali-bobezi ya Saratani Ocean Road ambayo ni Hospitali bingwa pekee ya Saratani EAC, Shoroba za Kusini mwa Afrika na Afrika ya Kati.

NB.
Jamii itapomaliza mjadala na kujipatia plan B yafuatayo yatajiri:-

1. Hospitali binafsi zitatajirika.

2. Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila itakosa wagonjwa wa kufundishia na itakuwa inawatafuta hospitali binafsi kwa gharama kubwa.

3. Viwango vya mafunzo Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila vitashuka ubora.

Tujadili.
Unapewa mwanafunzi ndio akutibu unategemea nini? Hospital za hivyo Huwa sitaki kabisa kwenda kufanywa specimen wa mazoezi.
 
Mnalinganisha death rate ya Mloganzila na hospitali za kutibu ukurutu na kikohozi mnakuja kulalamika hapa.

Mnajua status za wagonjwa wanaoenda kutibiwa Mloganzila. Ile ni heavy duty, hao wagonjwa wangefia hizo kliniki zilizochangamka ila wakawahishwa Mloganzila angalau kujaribu kuokoa maisha yao kwa vifaa vya kisasa zaidi.

Ukitaka kulinganisha vifo vya hospitali pia linganisha na chanzo cha kifo. Sasa mtu figo zimefeli completely unataka asife hiyo miujiza anatoa daktari wa hospitali gani nchi hii. Mloganzila inapokea wagonjwa walioshindikana lazima vifo vyao viwe vingi, ukiwatoa ukawapeleka hospitali nyingine watakufa mapema na kwa wingi zaidi kuliko pale.
Pia mloganzila kuna sehemu za kuhifadhi maiti za kutosha, hivyo MNH huwapa rufaa wanaokufa kule mortuary! Hivyo hupeleka marehemu wakihemea mashine ili muone mgonjwa hakufia MNH.
 
Ni kawaida mgonjwa kukata moto wakiwa kitengo cha ICU watu wa kitengo huko huona jambo la kawaida tu

Ova
 
Unapewa mwanafunzi ndio akutibu unategemea nini? Hospital za hivyo Huwa sitaki kabisa kwenda kufanywa specimen wa mazoezi.
Muhimbili kuna chuo pia na wanaotibu siyo wanafunzi, daktari hawezi mpa rufaa mgonjwa akatibiwe na mwanafunzi. Mloganzila kuna vyumba vya kuhifadhia maiti vingi. Wagonjwa mahututi hupelekwa mortuary
 
Mmmh...

Mloganzila ndiyo hospitali kubwa nchini?

Mloganzila ndiyo inapokea wagonjwa walioshindikana kwingineko?

Mloganzila siyo hospitali ya mafunzo?

MNH nayo siyo ya mafunzo?

MUCHS wanafundishia wapi?
Umesoma kweli alichoandika jamaa? Hahaha
 
Tujadili kupata uelewa mpana.

Kumezuka mtazamo hasi unaoshika kasi ya kusambaa kwenye jamii pana kama moto wa nyika ambapo ndugu za wagonjwa na wagonjwa wenyewe wamejenga dhana hasi juu ya huduma za tiba, uuguzi na uchunguzi zinazotolewa na Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila.

Unaweza kusikia haya kwenye jamii yakihojiwa:-

Amepewa rufaa?

Ndiyo.

Kwenda wapi?

Eti Mloganzila!!

Uuuwiii... Mungu wetu tusaidie.

Huyo harudi... tujihesabie huyo si wetu tena... jamani lakini kwanini hivi?

Wamewapa sababu gani ya kumpeleka Mloganzila? Kwani mmeshindwa bei MNH?

Hapana, eti wanasema wagonjwa wamejaa MNH hakuna nafasi.

Maskiniii. Kwani hatuwezi kuungana tukachangishana tumtoe huko tumpeleke hospitali binafsi bora mara 100?

Sijui mwenzenu mie nimechanganyikiwa mazima sijui cha kufanya, nawaza mengi bila majibu.

NB.
Hiyo hapo juu ni taswira halisi inayojengeka kwenye jamii kuhusu Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila.

Maswali:-
1. Rufaa inatokaje hospitali kuu ya taifa kwenda hospitali ndogo ya mafunzo? Rufaa za kimatibabu zinapanda juu hazishuki chini kwa mujibu wa itifaki ya tiba.

2. Hospitali ya Mafunzo inakosaje (inasajiliwaje) bila kuwa na madaktari bingwa wanaopaswa kuwepo hospitalini full time?

3. Ni uwiano gani wa wagonjwa mahututi wanapona na wasiopona?

4. No. 3 hapo juu ni asilimia ngapi?

5. Wakati MUCHS inafundisha wanafunzi wa udaktari na uuguzi MNH (kabla ya Mloganzila) No. 3 na 4 takwimu zilikuwaje?

6. Wakati MUCHS iko MNH je, dhana hasi ya wagonjwa na ndugu zao kuogopa kufa kwa kigezo cha matibabu-mafunzo ilishamiri?

7. Unadhani nini kifanyike kuondoa dhana hasi hii na kurejesha matumaini yaliyotoweka ya wagonjwa na ndugu zao kwa Mloganzila kama siyo jamii nzima?

8. Kwanini viongozi na matajiri hawapewi rufaa kwenda Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila ilhali madaktari bingwa na wauguzi bingwa wanapangiwa kufanya tiba-mafunzo pale?

9. Ina maana Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila ni ya makabwela ambao ndiyo roho zao zinatumika kufundishia?

10. Inakuwaje mfano wagonjwa wa saratani wanalazwa Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila wakati vifaatiba vya teknolojia ya hali ya juu viko Hospitali-bobezi ya Saratani Ocean Road ambayo ni Hospitali bingwa pekee ya Saratani EAC, Shoroba za Kusini mwa Afrika na Afrika ya Kati.

NB.
Jamii itapomaliza mjadala na kujipatia plan B yafuatayo yatajiri:-

1. Hospitali binafsi zitatajirika.

2. Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila itakosa wagonjwa wa kufundishia na itakuwa inawatafuta hospitali binafsi kwa gharama kubwa.

3. Viwango vya mafunzo Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila vitashuka ubora.

Tujadili.
Mimi hapa nimefurahishwa na uzi wako umeuwasilisha kwa lugha fasaha lugha tamu na adhimu ya kiswahili hayo mengine watajibu wajuvi wa huko!
 
Hata mimi kma naumwa ni heri nikaponee nyumbani kuliko mloganzira yani niliyoshuhudia yanatosha pale kuna mlango wa shetani pale nasema hapafai narudia tena hapafai pale usithubutu nasema hv nasikia uchungu sana mloganzia kuna shetani wa kifo .
 
Back
Top Bottom