Kwanini wagonjwa wanaogopa Mloganzila?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Tujadili kupata uelewa mpana.

Kumezuka mtazamo hasi unaoshika kasi ya kusambaa kwenye jamii pana kama moto wa nyika ambapo ndugu za wagonjwa na wagonjwa wenyewe wamejenga dhana hasi juu ya huduma za tiba, uuguzi na uchunguzi zinazotolewa na Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila.

Unaweza kusikia haya kwenye jamii yakihojiwa:-

Amepewa rufaa?

Ndiyo.

Kwenda wapi?

Eti Mloganzila!!

Uuuwiii... Mungu wetu tusaidie.

Huyo harudi... tujihesabie huyo si wetu tena... jamani lakini kwanini hivi?

Wamewapa sababu gani ya kumpeleka Mloganzila? Kwani mmeshindwa bei MNH?

Hapana, eti wanasema wagonjwa wamejaa MNH hakuna nafasi.

Maskiniii. Kwani hatuwezi kuungana tukachangishana tumtoe huko tumpeleke hospitali binafsi bora mara 100?

Sijui mwenzenu mie nimechanganyikiwa mazima sijui cha kufanya, nawaza mengi bila majibu.

NB.
Hiyo hapo juu ni taswira halisi inayojengeka kwenye jamii kuhusu Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila.

Maswali:-
1. Rufaa inatokaje hospitali kuu ya taifa kwenda hospitali ndogo ya mafunzo? Rufaa za kimatibabu zinapanda juu hazishuki chini kwa mujibu wa itifaki ya tiba.

2. Hospitali ya Mafunzo inakosaje (inasajiliwaje) bila kuwa na madaktari bingwa wanaopaswa kuwepo hospitalini full time?

3. Ni uwiano gani wa wagonjwa mahututi wanapona na wasiopona?

4. No. 3 hapo juu ni asilimia ngapi?

5. Wakati MUCHS inafundisha wanafunzi wa udaktari na uuguzi MNH (kabla ya Mloganzila) No. 3 na 4 takwimu zilikuwaje?

6. Wakati MUCHS iko MNH je, dhana hasi ya wagonjwa na ndugu zao kuogopa kufa kwa kigezo cha matibabu-mafunzo ilishamiri?

7. Unadhani nini kifanyike kuondoa dhana hasi hii na kurejesha matumaini yaliyotoweka ya wagonjwa na ndugu zao kwa Mloganzila kama siyo jamii nzima?

8. Kwanini viongozi na matajiri hawapewi rufaa kwenda Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila ilhali madaktari bingwa na wauguzi bingwa wanapangiwa kufanya tiba-mafunzo pale?

9. Ina maana Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila ni ya makabwela ambao ndiyo roho zao zinatumika kufundishia?

10. Inakuwaje mfano wagonjwa wa saratani wanalazwa Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila wakati vifaatiba vya teknolojia ya hali ya juu viko Hospitali-bobezi ya Saratani Ocean Road ambayo ni Hospitali bingwa pekee ya Saratani EAC, Shoroba za Kusini mwa Afrika na Afrika ya Kati.

NB.
Jamii itapomaliza mjadala na kujipatia plan B yafuatayo yatajiri:-

1. Hospitali binafsi zitatajirika.

2. Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila itakosa wagonjwa wa kufundishia na itakuwa inawatafuta hospitali binafsi kwa gharama kubwa.

3. Viwango vya mafunzo Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila vitashuka ubora.

Tujadili.
 
Akili za kijinga tu za watanzania walio wengi.pale mloganzila wana madaktari wengi tu tena wenye uzoefu na mabingwa kutoka muhimbili . Vifaa vya kutosha vipo .labda niwaulize tu ni hospitali gani wagonjwa hawafi?
Omba MUNGU usijepelekwa pale au nduguyo mkiwa kwenye hatua mbaya. Walioshuhudia (wengine zaidi ya mara 1) wanaweza kuwa na ufahamu wa tofauti na wako.
 
Tujadili kupata uelewa mpana.

Kumezuka mtazamo hasi unaoshika kasi ya kusambaa kwenye jamii pana kama moto wa nyika ambapo ndugu za wagonjwa na wagonjwa wenyewe wamejenga dhana hasi juu ya huduma za tiba, uuguzi na uchunguzi zinazotolewa na Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila.

pitali ya Muhimbili-Mloganzila vitashuka ubora.

Tujadili.
Kuna mjamaa alitaka afanyiwe ukarabati wa maumbile yake juzi, jamaa wakamtonya kuwa akienda harudi jamaa akasepa hakwenda!
 
Sema wabongo tunajua kujazana hofu,
Mleta mada kaja na maswali na conclusion bila kuwa na uelewa hata wa Mloganzila na Muhimbili zilivyo 😂😂😂
Hajui kuwa hata mloganzila na Muhimbili- Upanga ni hospital moja 😂
Hajui kuwa Mloganzila ina death rate ndogo sana kuliko MNH-Upanga,

Hajui kuwa MNH-MLG ilishatolewa chini ya MUHAS toka 2017 huko kipindi cha mwendazake ikawa chini ya MNH hivyo sio hospital ya mafunzo tena,

Kwa kukusaidia, Ile ni hospital ya taifa pale wanaenda watu hoi bin taaban walioshindwa hospital nyingine zooooote nchini hapa,
.halafu nenda japo siku moja MLG kaongee na wagonjwa wa pale na ndugu wakupe maoni yao
 
Akili za kijinga tu za watanzania walio wengi.pale mloganzila wana madaktari wengi tu tena wenye uzoefu na mabingwa kutoka muhimbili . Vifaa vya kutosha vipo .labda niwaulize tu ni hospitali gani wagonjwa hawafi?
me nimemuelewa mtoa mada kuna mpaka hajataka kuuelezea.
rate ya wagonjwa mahututi kati ya wanaofariki na wanaopona wanaopelekwa mloganzila 📌🔨 hii ndo inatia shaka
 
Tujadili kupata uelewa mpana.

Kumezuka mtazamo hasi unaoshika kasi ya kusambaa kwenye jamii pana kama moto wa nyika ambapo ndugu za wagonjwa na wagonjwa wenyewe wamejenga dhana hasi juu ya huduma za tiba, uuguzi na uchunguzi zinazotolewa na Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila.

Unaweza kusikia haya kwenye jamii yakihojiwa:-

Amepewa rufaa!!??

Ndiyo.

Kwenda wapi!!?

Eti Mloganzila!!

Uuuwiii... Mungu wetu tusaidie...

Huyo harudi... tujihesabie huyo si wetu tena... jamani lakini kwanini hivi?

Wamewapa sababu gani ya kumpeleka Mloganzila!!?? Kwani mmeshindwa bei MNH?

Hapana, eti wanasema wagonjwa wamejaa MNH hakuna nafasi.

Maskiniii... kwani hatuwezi kuungana tukachangishana tumtoe huko tumpeleke hospitali binafsi bora mara 100?

Sijui mwenzenu mie nimechanganyikiwa mazima sijui cha kufanya, nawaza mengi bila majibu.

NB.
Hiyo hapo juu ni taswira halisi inayojengeka kwenye jamii kuhusu Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila.

Maswali:-
1. Rufaa inatokaje hospitali kuu ya taifa kwenda hospitali ndogo ya mafunzo? Rufaa za kimatibabu zinapanda juu hazishuki chini kwa mujibu wa itifaki ya tiba.

2. Hospitali ya Mafunzo inakosaje (inasajiliwaje) bila kuwa na madaktari bingwa wanaopaswa kuwepo hospitalini full time?

3. Ni uwiano gani wa wagonjwa mahututi wanapona na wasiopona?

4. No. 3 hapo juu ni asilimia ngapi?

5. Wakati MUCHS inafundisha wanafunzi wa udaktari na uuguzi MNH (kabla ya Mloganzila) No. 3 na 4 takwimu zilikuwaje?

6. Wakati MUCHS iko MNH je, dhana hasi ya wagonjwa na ndugu zao kuogopa kufa kwa kigezo cha matibabu-mafunzo ilishamiri?

7. Unadhani nini kifanyike kuondoa dhana hasi hii na kurejesha matumaini yaliyotoweka ya wagonjwa na ndugu zao kwa Mloganzila kama siyo jamii nzima?

8. Kwanini viongozi na matajiri hawapewi rufaa kwenda Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila ilhali madaktari bingwa na wauguzi bingwa wanapangiwa kufanya tiba-mafunzo pale?

9. Ina maana Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila ni ya makabwela ambao ndiyo roho zao zinatumika kufundishia?

10. Inakuwaje mfano wagonjwa wa saratani wanalazwa Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila wakati vifaatiba vya teknolojia ya hali ya juu viko Hospitali-bobezi ya Saratani Ocean Road ambayo ni Hospitali bingwa pekee ya Saratani EAC, Shoroba za Kusini mwa Afrika na Afrika ya Kati.

NB.
Jamii itapomaliza mjadala na kujipatia plan B yafuatayo yatajiri:-

1. Hospitali binafsi zitatajirika.

2. Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila itakosa wagonjwa wa kufundishia na itakuwa inawatafuta hospitali binafsi kwa gharama kubwa.

3. Viwango vya mafunzo Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila vitashuka ubora.

Tujadili.

Mkuu mbona una roho ya kimasikini sana kwahiyo ulitaka hospitali binafs zife njaa hujui zimeajiri watanzania wangapi?kwahili umekosea sana hiyo point ifute.
 
Sema wabongo tunajua kujazana hofu,
Mleta mada kaja na maswali na conclusion bila kuwa na uelewa hata wa Mloganzila na Muhimbili zilivyo
Hajui kuwa hata mloganzila na Muhimbili- Upanga ni hospital moja
Hajui kuwa Mloganzila ina death rate ndogo sana kuliko MNH-Upanga,

Hajui kuwa MNH-MLG ilishatolewa chini ya MUHAS toka 2017 huko kipindi cha mwendazake ikawa chini ya MNH hivyo sio hospital ya mafunzo tena,

Kwa kukusaidia, Ile ni hospital ya taifa pale wanaenda watu hoi bin taaban walioshindwa hospital nyingine zooooote nchini hapa,
.halafu nenda japo siku moja MLG kaongee na wagonjwa wa pale na ndugu wakupe maoni yao
Mmmh...

Mloganzila ndiyo hospitali kubwa nchini?

Mloganzila ndiyo inapokea wagonjwa walioshindikana kwingineko?

Mloganzila siyo hospitali ya mafunzo?

MNH nayo siyo ya mafunzo?

MUCHS wanafundishia wapi?
 
Back
Top Bottom