Kwanini wagonjwa wanaogopa Mloganzila?

Kwanini wagonjwa wanaogopa Mloganzila?

Mlonganzila ni hospital yenye wataalam wa afya waliobobea hivyo wangonjwa kupelekea wangonjwa wanaopelekwa pale ni wale wa very critical cases (survival rate ni not more than 30%). Utaona hapo rates ya vifo ni kubwa kutokana na aina ya Wangonjwa wanaopokelewa pale.
So Mlonganzila haina tatizo.
 
maswali ya mleta mada yakijibiwa ipasavyo kwa data sahihi sio za kupika tutakuja na conclusion halisi itakayobadili zana potofu iliyojengeka miongoni mwa watz wengi.
 
maswali ya mleta mada yakijibiwa ipasavyo kwa data sahihi sio za kupika tutakuja na conclusion halisi itakayobadili zana potofu iliyojengeka miongoni mwa watz wengi.
Yeye kaja na hizo data?
 
Akili za kijinga tu za watanzania walio wengi.pale mloganzila wana madaktari wengi tu tena wenye uzoefu na mabingwa kutoka muhimbili . Vifaa vya kutosha vipo .labda niwaulize tu ni hospitali gani wagonjwa hawafi?
Mkuu nadhani hujaelewa lengo la mleta mada au umesoma juu juu;

i) kaongelea issue za kufuata unatoka hospital ya Taifa unapelekwa ya mafunzo,

ii) Rate ya watu kufariki kulinganisha na wanaopona unapokuwa umepelekwa pale.

Hayo ni machache tu na pia kuna wadau wamegusia kuondokewa na ndugu zao. Pengine ungeusoma uzi vizuri ungekuja na mawazo tofauti na haya.
 
Binafsi jamaa zangu wawili na majirani watatu walipelekwa mloga kwa nyakati tofauti na wote tulizika
Na kwa maongezi ya waliowengi nathani ipo shida pale kweli kabisa
 
Sasa watu kama wewe ndiyo mnafanya wananchi wazidi kuiogopa hiyo hospital. Mnatoa majibu yenye kujaa kiburi badala ya maelezo ya ushawishi. Hapa hakuna mtu anayesema kuwa kuna hospital ambayo watu hawafi. Mbona Muhimbili wagonjwa wanafariki na ukienda kila siku unakuta kuna pilikapilika za umati wa watu kwa ajili ya mazishi? Huwezi kujiuliza ni kwa nini watu wameogopa hiyo hospital na siyo Muhimbili ambayo pengine kuna vifo vingi zaidi? Tatizo kubwa ni kuwa Tanzania kila kitu kimetekwa na kufanywa kama tawi la CCM. Wasiwasi wa aina hii ungeweza kumalizwa kwa kuwa na vyombo vya habari vyenye weledi wa kufanya uchunguzi au vyama vya madaktari.
Hata mloganzila ni muhimbili ambayo wafanyakazi na Uongozi ni ule ule tofauti ni locations tu tena nadiriki kusema muhimbili ya mloganzila wana vifaa vya kisasa zaidi kuzidi muhimbili ya upanga.
 
Nenda pale emergency department utaelewa kwa nini wagonjwa wengi wanafia Mloganzila, uliza wengi wakifika pale hali zao za afya zikoje.

Imagine una mgonjwa Bosch, ametibiwa for a month, wakiona huyu anakufa wanampa rufaa kwenda MNH, wakipiga simu emergency ya MNH wanaambiwa huyo mpelekeni tawi la Mloganzila(kuna emergency correspondent anaelekeza either aletwe Upanga au Mloga), akipokelewa hakai hata siku mbili anakufa. Lawama mnapeleka kwa Mloganzila.
Hila kweli.
 
Hasa sisi wanaume ndio kabisaa,unaweza ukaenda kwa kikohozi tu mara pa unarudi umeongezwa makalio haya utamlaumu nani?
 
Hizo bed sores alizipata akiwa MLG? Na kwa taarifa yako hayo mabed sore yanasababisha infection ya hatari sanaaa, haisikii antibiotics wala nini, ukiyapata yakinoga lazima uondoke tu just a matter of time hata uende USA
Ndio alizipatia MLG, na shida yangu sio kupata hizo souls, shida yangu ni mgonjwa kukaa muda mrefu bila kupewa huduma mpaka mimi nilipofika mchana kwa ajili ya kumpa chakula ndio nikagundua tatizo, inamaana nisingetokea?
 
Mnalinganisha death rate ya Mloganzila na hospitali za kutibu ukurutu na kikohozi mnakuja kulalamika hapa.

Mnajua status za wagonjwa wanaoenda kutibiwa Mloganzila. Ile ni heavy duty, hao wagonjwa wangefia hizo kliniki zilizochangamka ila wakawahishwa Mloganzila angalau kujaribu kuokoa maisha yao kwa vifaa vya kisasa zaidi.

Ukitaka kulinganisha vifo vya hospitali pia linganisha na chanzo cha kifo. Sasa mtu figo zimefeli completely unataka asife hiyo miujiza anatoa daktari wa hospitali gani nchi hii. Mloganzila inapokea wagonjwa walioshindikana lazima vifo vyao viwe vingi, ukiwatoa ukawapeleka hospitali nyingine watakufa mapema na kwa wingi zaidi kuliko pale.
Nisipokupa like sitakua nimekutendea haki,kuna sister wangu alizima kabisa kutoka Mwananyamala hospital akapewa referral to Mloga tukajua hapa habari imeisha,ebana eeeh jamaa walipambana hapa navyokwambia anadunda anakula ugali wa mama Samia
 
Mpaka unafika MNH maana yake upo serious ill then na wao wanakupa referral hauoni kama unakaribia kufa hata wakiandika uende India?
 
Tujadili kupata uelewa mpana.

Kumezuka mtazamo hasi unaoshika kasi ya kusambaa kwenye jamii pana kama moto wa nyika ambapo ndugu za wagonjwa na wagonjwa wenyewe wamejenga dhana hasi juu ya huduma za tiba, uuguzi na uchunguzi zinazotolewa na Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila.

Unaweza kusikia haya kwenye jamii yakihojiwa:-

Amepewa rufaa!!??

Ndiyo.

Kwenda wapi!!?

Eti Mloganzila!!

Uuuwiii... Mungu wetu tusaidie...

Huyo harudi... tujihesabie huyo si wetu tena... jamani lakini kwanini hivi?

Wamewapa sababu gani ya kumpeleka Mloganzila!!?? Kwani mmeshindwa bei MNH?

Hapana, eti wanasema wagonjwa wamejaa MNH hakuna nafasi.

Maskiniii... kwani hatuwezi kuungana tukachangishana tumtoe huko tumpeleke hospitali binafsi bora mara 100?

Sijui mwenzenu mie nimechanganyikiwa mazima sijui cha kufanya, nawaza mengi bila majibu.

NB.
Hiyo hapo juu ni taswira halisi inayojengeka kwenye jamii kuhusu Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila.

Maswali:-
1. Rufaa inatokaje hospitali kuu ya taifa kwenda hospitali ndogo ya mafunzo? Rufaa za kimatibabu zinapanda juu hazishuki chini kwa mujibu wa itifaki ya tiba.

2. Hospitali ya Mafunzo inakosaje (inasajiliwaje) bila kuwa na madaktari bingwa wanaopaswa kuwepo hospitalini full time?

3. Ni uwiano gani wa wagonjwa mahututi wanapona na wasiopona?

4. No. 3 hapo juu ni asilimia ngapi?

5. Wakati MUCHS inafundisha wanafunzi wa udaktari na uuguzi MNH (kabla ya Mloganzila) No. 3 na 4 takwimu zilikuwaje?

6. Wakati MUCHS iko MNH je, dhana hasi ya wagonjwa na ndugu zao kuogopa kufa kwa kigezo cha matibabu-mafunzo ilishamiri?

7. Unadhani nini kifanyike kuondoa dhana hasi hii na kurejesha matumaini yaliyotoweka ya wagonjwa na ndugu zao kwa Mloganzila kama siyo jamii nzima?

8. Kwanini viongozi na matajiri hawapewi rufaa kwenda Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila ilhali madaktari bingwa na wauguzi bingwa wanapangiwa kufanya tiba-mafunzo pale?

9. Ina maana Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila ni ya makabwela ambao ndiyo roho zao zinatumika kufundishia?

10. Inakuwaje mfano wagonjwa wa saratani wanalazwa Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila wakati vifaatiba vya teknolojia ya hali ya juu viko Hospitali-bobezi ya Saratani Ocean Road ambayo ni Hospitali bingwa pekee ya Saratani EAC, Shoroba za Kusini mwa Afrika na Afrika ya Kati.

NB.
Jamii itapomaliza mjadala na kujipatia plan B yafuatayo yatajiri:-

1. Hospitali binafsi zitatajirika.

2. Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila itakosa wagonjwa wa kufundishia na itakuwa inawatafuta hospitali binafsi kwa gharama kubwa.

3. Viwango vya mafunzo Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila vitashuka ubora.

Tujadili.
Mlonganzila na Benjamini mkapa ya dodoma, ni hospitali zenye uzembe na vifaa havitoshi. pia malipo ya madaktari nadhani ni madogo ndio maana wengi wana stress na hawahudumii wagonjwa kwa kiwango kinachostahili. malipo madogo + upungufu wa vifaa vya kutendea kazi = huduma mbovu.

hatuwezi kusema hospitali hizo zina wanafunzi wanaojifunzia kwa wagonjwa kwasababu palipo na daktari mwanafunzi lazima yupo specialist anayesimamia. serikali iboreshe maslahi ya madaktari ili watu wafanye kazi kufa na kupona badala ya kufanya kazi wakiwa exposed kwenye risk za kufa tu.
 
Back
Top Bottom