Kwanini wagonjwa wanaogopa Mloganzila?

Kwanini wagonjwa wanaogopa Mloganzila?

Tujadili kupata uelewa mpana.

Kumezuka mtazamo hasi unaoshika kasi ya kusambaa kwenye jamii pana kama moto wa nyika ambapo ndugu za wagonjwa na wagonjwa wenyewe wamejenga dhana hasi juu ya huduma za tiba, uuguzi na uchunguzi zinazotolewa na Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila.

Unaweza kusikia haya kwenye jamii yakihojiwa:-

Amepewa rufaa!!??

Ndiyo.

Kwenda wapi!!?

Eti Mloganzila!!

Uuuwiii... Mungu wetu tusaidie...

Huyo harudi... tujihesabie huyo si wetu tena... jamani lakini kwanini hivi?

Wamewapa sababu gani ya kumpeleka Mloganzila!!?? Kwani mmeshindwa bei MNH?

Hapana, eti wanasema wagonjwa wamejaa MNH hakuna nafasi.

Maskiniii... kwani hatuwezi kuungana tukachangishana tumtoe huko tumpeleke hospitali binafsi bora mara 100?

Sijui mwenzenu mie nimechanganyikiwa mazima sijui cha kufanya, nawaza mengi bila majibu.

NB.
Hiyo hapo juu ni taswira halisi inayojengeka kwenye jamii kuhusu Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila.

Maswali:-
1. Rufaa inatokaje hospitali kuu ya taifa kwenda hospitali ndogo ya mafunzo? Rufaa za kimatibabu zinapanda juu hazishuki chini kwa mujibu wa itifaki ya tiba.

2. Hospitali ya Mafunzo inakosaje (inasajiliwaje) bila kuwa na madaktari bingwa wanaopaswa kuwepo hospitalini full time?

3. Ni uwiano gani wa wagonjwa mahututi wanapona na wasiopona?

4. No. 3 hapo juu ni asilimia ngapi?

5. Wakati MUCHS inafundisha wanafunzi wa udaktari na uuguzi MNH (kabla ya Mloganzila) No. 3 na 4 takwimu zilikuwaje?

6. Wakati MUCHS iko MNH je, dhana hasi ya wagonjwa na ndugu zao kuogopa kufa kwa kigezo cha matibabu-mafunzo ilishamiri?

7. Unadhani nini kifanyike kuondoa dhana hasi hii na kurejesha matumaini yaliyotoweka ya wagonjwa na ndugu zao kwa Mloganzila kama siyo jamii nzima?

8. Kwanini viongozi na matajiri hawapewi rufaa kwenda Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila ilhali madaktari bingwa na wauguzi bingwa wanapangiwa kufanya tiba-mafunzo pale?

9. Ina maana Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila ni ya makabwela ambao ndiyo roho zao zinatumika kufundishia?

10. Inakuwaje mfano wagonjwa wa saratani wanalazwa Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila wakati vifaatiba vya teknolojia ya hali ya juu viko Hospitali-bobezi ya Saratani Ocean Road ambayo ni Hospitali bingwa pekee ya Saratani EAC, Shoroba za Kusini mwa Afrika na Afrika ya Kati.

NB.
Jamii itapomaliza mjadala na kujipatia plan B yafuatayo yatajiri:-

1. Hospitali binafsi zitatajirika.

2. Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila itakosa wagonjwa wa kufundishia na itakuwa inawatafuta hospitali binafsi kwa gharama kubwa.

3. Viwango vya mafunzo Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila vitashuka ubora.

Tujadili.
Uko sahihi. Hii hospital inaogopewa na watu wengi. Tatizo kubwa la Tanzania ni kuwa serikali imeua media na vyama vya kitaalam vyote na kuvifanya kama matawi ya CCM. Hili linafanya kukosekane vyombo huru vya kufuatia na kutoa majibu ya kitaama kuhusu hizi tuhuma. Muhimbili wananchi wanaiamini sana lakini sijui kwa nini hii inaogopwa.
 
Akili za kijinga tu za watanzania walio wengi.pale mloganzila wana madaktari wengi tu tena wenye uzoefu na mabingwa kutoka muhimbili . Vifaa vya kutosha vipo .labda niwaulize tu ni hospitali gani wagonjwa hawafi?
Sasa watu kama wewe ndiyo mnafanya wananchi wazidi kuiogopa hiyo hospital. Mnatoa majibu yenye kujaa kiburi badala ya maelezo ya ushawishi. Hapa hakuna mtu anayesema kuwa kuna hospital ambayo watu hawafi. Mbona Muhimbili wagonjwa wanafariki na ukienda kila siku unakuta kuna pilikapilika za umati wa watu kwa ajili ya mazishi? Huwezi kujiuliza ni kwa nini watu wameogopa hiyo hospital na siyo Muhimbili ambayo pengine kuna vifo vingi zaidi? Tatizo kubwa ni kuwa Tanzania kila kitu kimetekwa na kufanywa kama tawi la CCM. Wasiwasi wa aina hii ungeweza kumalizwa kwa kuwa na vyombo vya habari vyenye weledi wa kufanya uchunguzi au vyama vya madaktari.
 
Tujadili kupata uelewa mpana.

Kumezuka mtazamo hasi unaoshika kasi ya kusambaa kwenye jamii pana kama moto wa nyika ambapo ndugu za wagonjwa na wagonjwa wenyewe wamejenga dhana hasi juu ya huduma za tiba, uuguzi na uchunguzi zinazotolewa na Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila.

Unaweza kusikia haya kwenye jamii yakihojiwa:-

Amepewa rufaa!!??

Ndiyo.

Kwenda wapi!!?

Eti Mloganzila!!

Uuuwiii... Mungu wetu tusaidie...

Huyo harudi... tujihesabie huyo si wetu tena... jamani lakini kwanini hivi?

Wamewapa sababu gani ya kumpeleka Mloganzila!!?? Kwani mmeshindwa bei MNH?

Hapana, eti wanasema wagonjwa wamejaa MNH hakuna nafasi.

Maskiniii... kwani hatuwezi kuungana tukachangishana tumtoe huko tumpeleke hospitali binafsi bora mara 100?

Sijui mwenzenu mie nimechanganyikiwa mazima sijui cha kufanya, nawaza mengi bila majibu.

NB.
Hiyo hapo juu ni taswira halisi inayojengeka kwenye jamii kuhusu Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila.

Maswali:-
1. Rufaa inatokaje hospitali kuu ya taifa kwenda hospitali ndogo ya mafunzo? Rufaa za kimatibabu zinapanda juu hazishuki chini kwa mujibu wa itifaki ya tiba.

2. Hospitali ya Mafunzo inakosaje (inasajiliwaje) bila kuwa na madaktari bingwa wanaopaswa kuwepo hospitalini full time?

3. Ni uwiano gani wa wagonjwa mahututi wanapona na wasiopona?

4. No. 3 hapo juu ni asilimia ngapi?

5. Wakati MUCHS inafundisha wanafunzi wa udaktari na uuguzi MNH (kabla ya Mloganzila) No. 3 na 4 takwimu zilikuwaje?

6. Wakati MUCHS iko MNH je, dhana hasi ya wagonjwa na ndugu zao kuogopa kufa kwa kigezo cha matibabu-mafunzo ilishamiri?

7. Unadhani nini kifanyike kuondoa dhana hasi hii na kurejesha matumaini yaliyotoweka ya wagonjwa na ndugu zao kwa Mloganzila kama siyo jamii nzima?

8. Kwanini viongozi na matajiri hawapewi rufaa kwenda Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila ilhali madaktari bingwa na wauguzi bingwa wanapangiwa kufanya tiba-mafunzo pale?

9. Ina maana Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila ni ya makabwela ambao ndiyo roho zao zinatumika kufundishia?

10. Inakuwaje mfano wagonjwa wa saratani wanalazwa Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila wakati vifaatiba vya teknolojia ya hali ya juu viko Hospitali-bobezi ya Saratani Ocean Road ambayo ni Hospitali bingwa pekee ya Saratani EAC, Shoroba za Kusini mwa Afrika na Afrika ya Kati.

NB.
Jamii itapomaliza mjadala na kujipatia plan B yafuatayo yatajiri:-

1. Hospitali binafsi zitatajirika.

2. Hospitali ya Mafunzo ya Muhimbili-Mloganzila itakosa wagonjwa wa kufundishia na itakuwa inawatafuta hospitali binafsi kwa gharama kubwa.

3. Viwango vya mafunzo Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila vitashuka ubora.

Tujadili.
ni muhimbili tu katika ujumla wake.
Mpeleke hapo muhimbili mgonjwa akiwa walau ana nguvu kidogo, lakani akiwa katika hali mbaya hawezi rudi mara100 umpeleke private hospital.....
 
Hio ni sababu pia ya masifa ya bwana yule, alienda MLOGANZILA akaona vitanda vipo tupu halafu Upanga kuna wagonjwa shazi, akasema wagonjwa wa upanga wapelekwe MLG,
Upanga wakawa wanachagua soon to be dead patients wanawapeleka mloganzila, (yan wale hata aje nan hawatoboi) kwa hio kilichofuata ni ndugu kwenda kuchukua miili mloganzila na hapo ndo jina na kashfa hii ikaibuka, ila mwendazake alizingua sana
Kwa hiyo sasa hivi hawafi?
 
Rafiki yangu Raymond Alifia pale,..alipelekwa akiwa na Hali nzuri TU...ila baada ya kukaa hapo Kwa muda flan Hali yake ilibadilika ghafla...akapoteza maisha
 
Mwezi uliopita tumezika mdogo wangu mmoja!

Aligongwa na pikipiki akaangukia kichwa tukampeleka temeke wqkampiga ct scan wakasema huyu kuna damu imevujia kwenye ubongo na imevilia ndani!

Wakasema tunampa rufaa ya mloganzila, I ila baadae wakatupa rufaa ya MOI pale muhimbili, na alikaa siku tatu tu pale emergency ya MOI akafa.
 
Poleni sana mkuu,
Issue nyingine zipo nje ya uwezo wa binadamu
 
Rafiki yangu Raymond Alifia pale,..alipelekwa akiwa na Hali nzuri TU...ila baada ya kukaa hapo Kwa muda flan Hali yake ilibadilika ghafla...akapoteza maisha
Wew uliona yupo kwenye hali nzuri, ila ushajiuliza waliompa rufaa kwenda pale waliona nin?
 
Mimi nilimpoteza dada yangu pale, baada ya kumkuta akiwa amelala kwenye dimbwi la damu nyingi iliyovuja kwa muda mrefu kutokana na bed souls, baaya ya kuwataarifu manesi ndio wakaanza kumpa huduma lkn siku ya tatu alifariki, hata damu tuliyoambiwa tumchangie mgonjwa hakuongezwa.Nina wasiwasi na huduma za pale.
Hizo bed sores alizipata akiwa MLG? Na kwa taarifa yako hayo mabed sore yanasababisha infection ya hatari sanaaa, haisikii antibiotics wala nini, ukiyapata yakinoga lazima uondoke tu just a matter of time hata uende USA
 
Back
Top Bottom