Kwanini Wachaga wanapenda kuuliza hili swali?

Kwanini Wachaga wanapenda kuuliza hili swali?

Wachaga wanatuonaga sisi wasukuma mandezišŸ˜Ž

Cc Mallerina
How,mbona Wasukuma wengi wameona na Wachaga.
Hivi kuna mtu unaweza kumuona ndezi na muda huo ukatamani awe mwezi wa maisha.
Allegations zako hazina tija na umejawa na mizizi ya chuki.
Kumbuka mchanganyiko wa jamii huleta maendeleo(cultural diversity).
Wewe una mambo yako binafsi na Mchaga mligomba na mkatukanana huko na unakuja hapa kujumuisha jamii yote.
 
Hata makambako, Njombe mjini Kama Sio Mbena au Mkinga hutoboi!
Mara nyingi maeneo ambayo wenyeji wanaishi na hakuna mchanganyiko mkubwa ni kawaida kufanya biashara wao kwa wao.

Pia hii sio kwa jamii za Wachaga au Wabena hata Usukumani ipo na inachukua muda mpaka wakuzoee na kufanya biashara na wewe.

Ni vema ukafahamu sio rahisi leo hii uende Usambaani ukafungue duka na upate wateja,mteja anatabia ya kutaka kukufahamu na kujenga bond na wewe na hili huchukua muda,Ukitaka ufike leo na leo upate wateja lazima utasema watu hawa wana ukabila na hawafai kuishi na watu wa kabila tofauti.
 
Mara nyingi maeneo ambayo wenyeji wanaishi na hakuna mchanganyiko mkubwa ni kawaida kufanya biashara wao kwa wao.

Pia hii sio kwa jamii za Wachaga au Wabena hata Usukumani ipo na inachukua muda mpaka wakuzoee na kufanya biashara na wewe.

Ni vema ukafahamu sio rahisi leo hii uende Usambaani ukafungue duka na upate wateja,mteja anatabia ya kutaka kufahamu na kujenga bond na wewe na hili huchukua muda,Ukitaka kufika leo na leo upate wateja lazima utasema watu hawa wana ukabila na hawafai kuishi na watu wa kabila tofauti.
Sawa mkuu,ngoja tuone!
 
Hii mindset itakutesa sana..hapa duniani kila MTU ni unique ana attitude, behavior, character Na IQ tofauti...utachelewa sana...mjaji MTU kutokana Na tabia Yake mwenyewe...ndio maana sio wachagga wote wanafanya biashara..kuna wengine tumeawajiri kwenye biashara zetu Na wangine ni walala hoi wengi huko Kilimanjaro
Na wengine ni mafundi ujenzi wako kwenye masaiti sio wote wanamiliki biashara.
 
🤣🤣unabahati mada za kisukuma zimepungua naona moto upo kwa wachaga😁
Sijui kwa nini tunachukiana sana,ila ndo ubinadamu maana asili yetu tunafikiria mabaya muda mwingi.
Hakuna aliyechagua kuzaliwa mwauame,mwanake,Kabila au rangi.
Na mtu akifikia hatua ya kutojali haya mambo ya ubaguzi anakuwa amefikia kilele cha utu wa hali ya juu.
Segregation is the source of destruction and hostility in the whole World.
 
Wamarangu sio wavivu mkuu ila wanatumia akili kwenye kufanikiwa sio nguvu bila akili. Ndio maana wengi wamesoma sana. Ingekuwa ni wavivu Marangu isingekuwa namba moja kwa maendeleo uchagani.

Hata Wakirua Vunjo huo ushamba ni zamani sio leo. Wana positive nyingi sana. Kwa hiyo badala ya kuongelea negative tuu ungeongea negative na positive. Au mpaka tuongelee na negative za Wakibosho na Wamachame ambapo ndipo ulipo wewe.
Mkuu mbona umecatch? Mie nimetolea mfano tu mbona nimesema Wanawake wa Kimarangu ni wazuri hilo hujaona ni negative?
 
at last katokea mtu humu kusema kile ambacho nimekuwa nasema mara nyingi, nacho ni kuwa watanzania hususan tanzania bara wana ukabilia. Hii tabia sio kwa wachaga tu, ni tatizo ambalo limeenea kote. toka enzi za Nyerere, kwa mfano, ilikuwa mtu akipewa wadhifa tu basi watu wanataka kujua katokea pande gani ya tanzania, watu wanataka kujua kama ni mtu wa butiama au wa karibu etc. Na hadi hii leo ndio hivyo hivyo. Tabia ambayo kuna watanzania wamekwenda nayo hadi katika nchi za nje wanakoishi hivi sasa.
Binafsi nikiuliza halafu ukasema ni Mzanzibar basi naona niko na Shetani kabisa
 
Na wengine ni mafundi ujenzi wako kwenye masaiti sio wote wanamiliki biashara.
Hata ufundi ujenzi unaweza kuwa biashara pia. Mdogo wangu ni fundi wa umeme majumbani na hajasomea popote ila anaweza kuwa na site kama 6 kwa pamoja anaweka vijana wanafanya kazi yeye anakagua tu. Biashara siyo lazima umiliki duka
 
Huwa tunauliza hilo swali kwa sababu za kiuchumi na kisaikolojia.
Ukisema ni Mkinga au Mbena tunajua unaweza kuwa mtu wa system maana ni wanoko sana na wamejazana huko. Ukisema ni Mkinga tunakaa na wewe kwa akili tukijua muda wowote unaweza kuwa mpinzani wa kiuchumi. Kuna makabila ukitutajia tunajua huyu atakuwa mvivu au ana matumizi mabaya ya pesa, kwa mfano Msambaa au Mngoni. Kuna makabila ukitutajia tunajua huyu ili tumkamate tumuweke mahali kuna wanawake wazuri atatufanyia kazi bure. Kuna makabila ukiyataja tunajua hapa hamna tunachopata ila tunasaidia tu mtu. Makabila mengine ukitutajia tunajua huyu atakuwa anapiga kazi sana kama Wasukuma, Wanyamwezi au Wanyakyusa.
Hilo swali ni "very technical" na ni muhimu sana kwetu.
Ukweli ni kuwa mwezi wa 12 huwa tukikutana tunajadili makabila yote kutokana na sehemu tunazoishi hivyo tunawajua wote vizuri sana.
Hata huku Uchagani huwa tunaulizana kama ni wa wapi ili tujue... Mrombo au Mkibosho-mzuri sana kwenye Biashara.
Muuru- Mcha Mungu ila anaamini kwenye uganga sana.
Mmachame- mzuri kwenye kilimo na ugugaji wa kisasa. Mkirua-Mshamba, Mmarangu- wavivu wanategemea uzuri wa dada zao kufanikiwa.
Bottom Line : hilo swali hatuwezi kuacha kuuliza. Ni swali muhimu sana.
Chasaka mkubwa wee
 
Back
Top Bottom