Kwanini Wachaga wanapenda kuuliza hili swali?

Kwanini Wachaga wanapenda kuuliza hili swali?

Huwa tunauliza hilo swali kwa sababu za kiuchumi na kisaikolojia.
Ukisema ni Mkinga au Mbena tunajua unaweza kuwa mtu wa system maana ni wanoko sana na wamejazana huko. Ukisema ni Mkinga tunakaa na wewe kwa akili tukijua muda wowote unaweza kuwa mpinzani wa kiuchumi. Kuna makabila ukitutajia tunajua huyu atakuwa mvivu au ana matumizi mabaya ya pesa, kwa mfano Msambaa au Mngoni. Kuna makabila ukitutajia tunajua huyu ili tumkamate tumuweke mahali kuna wanawake wazuri atatufanyia kazi bure. Kuna makabila ukiyataja tunajua hapa hamna tunachopata ila tunasaidia tu mtu. Makabila mengine ukitutajia tunajua huyu atakuwa anapiga kazi sana kama Wasukuma, Wanyamwezi au Wanyakyusa.
Hilo swali ni "very technical" na ni muhimu sana kwetu.
Ukweli ni kuwa mwezi wa 12 huwa tukikutana tunajadili makabila yote kutokana na sehemu tunazoishi hivyo tunawajua wote vizuri sana.
Hata huku Uchagani huwa tunaulizana kama ni wa wapi ili tujue... Mrombo au Mkibosho-mzuri sana kwenye Biashara.
Muuru- Mcha Mungu ila anaamini kwenye uganga sana.
Mmachame- mzuri kwenye kilimo na ugugaji wa kisasa. Mkirua-Mshamba, Mmarangu- wavivu wanategemea uzuri wa dada zao kufanikiwa.
Bottom Line : hilo swali hatuwezi kuacha kuuliza. Ni swali muhimu sana.

Ni muhimu sana hata mimi lazima swali la kujua historia lazima niulize. Kwa hiyo anataka aoe mtoto wa mtu ila asiulizwe asili yake.
 
U
Hii mindset itakutesa sana..hapa duniani kila MTU ni unique ana attitude, behavior, character Na IQ tofauti...utachelewa sana...mjaji MTU kutokana Na tabia Yake mwenyewe.
Uongo, uongo uongo, hata ukienda China hawaulizi unatoka Afrika, wanauliza unatoka Afrika Nchi gani?

Kuna kitu wanataka kujua🤣
 
Sababu ya Wachagga kuuliza kutaka kujua kabila la mtu si ili ambague lengo ni ili aweze kujua namna ya kuishi nae. Na hii pia sio kwa Wachagga tuu hata makabila mengine pia huuliza.
 
Hapo VIP!
Hili swali huwa sipendi ambao wachagga wengi wanapenda kuiliza.Eti Wewe ni kabila gani?
Hawa jamaa wanamambo ya Kipuuzi sana..nadhani kwasababu wanaukabila sana ndio maana wanapenda sana hili swali.
at last katokea mtu humu kusema kile ambacho nimekuwa nasema mara nyingi, nacho ni kuwa watanzania hususan tanzania bara wana ukabilia. Hii tabia sio kwa wachaga tu, ni tatizo ambalo limeenea kote. toka enzi za Nyerere, kwa mfano, ilikuwa mtu akipewa wadhifa tu basi watu wanataka kujua katokea pande gani ya tanzania, watu wanataka kujua kama ni mtu wa butiama au wa karibu etc. Na hadi hii leo ndio hivyo hivyo. Tabia ambayo kuna watanzania wamekwenda nayo hadi katika nchi za nje wanakoishi hivi sasa.
 
Swalli la kawaida sana wewe tu unalichukulia vibaya mbona unaweza kuhitajika kujaza Fomu na unakutana na hilo swali?
Nadhani mtoa post ni Gen-Z maana si kwa hasira hizo.
Swali ni zuri tu maana hata polisi huwa tunaulizwa na pia inakusaidia sana kupata utambulisho na kuboresha mahusiano.
Tatizo mtoa mada ana chuki na Wachaga na ndiyo kilichomfanya aje hapa akiwa na hasira kali.
 
Uko sahihi hata kwenye mahusiano kitu cha kwanza ni kufahamiana.
 
Watajitetea ila lengo lao ni ushamba wa ukabila
Hapana inategemea na wewe una taarifa gani.
Kama umekulia kwenye hayo mazingira ya kuwasema vibaya Wachaga lazima uchukie hilo swali.
Kwani wewe ulimjuaje aliyekuuliza ni Mchaga kama hufatilii makabila ya watu?
Nadhani lazima uwe tayari kuulizwa maswali na watu hasa kwenye mazingira ya kazi na biashara.
 
Uko sahihi hata kwenye mahusiano kitu cha kwanza ni kufahamiana.
Tatizo tunahangaika na watoto humu,Identify haijawahi kuwa tusi hata siku moja.
Jamaa zetu hawa akitokq nje ya nchi hatataka pia kuulizwa umetokea nchi gani na si ajabu ataukataa pia Uafrica wake na kujiita Black America,lengo ni kuokoteza ufahari usio na tija.
Ukienda UDSM hapo vijana wengi wanakana walikotokea na makabila yao na kudai wametokea Magomeni au Tegeta kumbe wamekea Kibondo,Mpanda au Sengerema. Slave mind haijawahi kumwacha mtu salama.
 
Wengi wao huwa wanadai wamezaliwa Muhimbili, Ocean Road n.k.
 
Back
Top Bottom