HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Wakuu na mm namshukuru Mungu nimelamba asali PDF ya Jana.
Status ni selected for oral both app na website kwa taasis zote 3 nilizofanya usahili
Interview nilifanya 10 mwaka Jana mbili nilitoboa oral ya mwezi wa 9 na 12. Mwaka huu pia February nilitoboa oral zile za LGA & MDA.
Hivyo sijajua if ni database au ni interview ipi imenipa kazi.

Nadhani mnakumbuka nilivyokua huku nikilalamika na kukata tamaa. Yani toka Jana na stress sijui nafanyeje
Kwani mwezi uliopita nilipata kazi kwenye NGO nikasaini contract ya 3 years.
Hapa nawaza niache NGO au nibaki
Sababu ukilinganisha huku NGO kutamu Yani salary per month ni Dola 1100 bado Kuna allowance kibao

Yani wakuu nimevurugwa. Sikutegemea kama placement itanipa stress hv
Haya maisha ni mtihani sana sana, unaomba upate placement ikija inakuja na majaribu mengine basi shida tupu.
 
Wakuu habari,kuna ushuhuda hapa...hatimaye kwenye PDF la jana,na mimi nimefanikiwa kulamba asali katika moja ya mashirika ya usafirishaji nchini,yaan nmelala jobless nkaamkia asalini.
Nmemaliza chuo mwaka Jana, post yetu ya ajira imetoka mwez wa 3 mwaka huu,nmfanya written kwa mara ya kwanza ,oral kwa mara ya kwanza na nmpata placement hapo hapo!Hakika Mungu ni mwema,nmejiunga na uzi huu km miez 8 hv iliyopita na sasa nmefanikiwa kulamba asali.
Ndugu zangu,tuendelee kusali na kumuomba Mungu ,hakika atatenda kwa kadri ya mapenzi yake na muda wake. Tuko pamoja wakuu hadi kieleweke,hakuna kukata tamaa, hakuna kurud nyuma
Daah we jamaa una bahati sanaaa...
 
Nimekua kimya kwa muda humu kwa kua nilikua nmeshakata tamaa,nilichoka.

But Mungu ni mwema ktk pdf za wiki iliyopita nami nimo. Nikasema nkitulia ntakuja kuleta mrejesho humu.

Mungu ni mwema sana,nashukuru nyote tuliokua pamoja kipindi chote cha heka heka.

Guys Mungu anaskia vilio vyetu,tusikate tamaa.
Hongera sana, Mungu ni mwema
 
Nimekua kimya kwa muda humu kwa kua nilikua nmeshakata tamaa,nilichoka.

But Mungu ni mwema ktk pdf za wiki iliyopita nami nimo. Nikasema nkitulia ntakuja kuleta mrejesho humu.

Mungu ni mwema sana,nashukuru nyote tuliokua pamoja kipindi chote cha heka heka.

Guys Mungu anaskia vilio vyetu,tusikate tamaa.
Hongera sana Yesamrich! Ulipotea sana jukwaani humu watu wakajua ushalamba Ajira..
 
Uhakika upo ni ipo chini ya UN lakin contract ikiisha miaka 3 kurenew sio rahis Sana maana katoka mtu Mimi ndio nikaingia
Maisha ni hesabu na kuishi tunaishi leo, Wengi wanaopenda Serikali ni waoga wa Changamoto lakini pia wengi wao hawaingii kwa malengo ya kuwajibika, inshort serikalini maisha ni marahisi, uwe mzembe, mvivu, utumie muda wa muajiri kwa issue zako nyengine ndiyo mambo ambayo wengi wanapenda tofauti na Sekta binafsi na Asasi za kiraia, Sekta binafsi na asasi za kiraia zimeajiri watu wengi kuliko serikali, Serikali ya sasa Msukumo wake ni kusaidia sekta binafsi ikiamini sekta binafsi ikiimarika itaisaidia serikali kwa mambo mengi kama kukuza uchumi na kuzalisha Ajira. Sekta binafsi unalipwa kulingana na unachozalisha au thamani unayoleta kwenye taasisi husika, juhudi, maarifa, ubunifu na uchapakazi wako ndio karata yako pekee ya kukufanya u survive kwenye sekta binafsi wakati serikalini ni utiifu kwa mamlaka na ujanja ujanja ndo utakufanya u survive, Mshahara unaoupata sasa hivi utakupa NSSF ambayo mtu wa serikalini ili akufikie itamhitaji miaka 6 hadi 10, Sekta binafsi unaweza kupata kazi ambayo kodi ya mapato unayokatwa kuna mtu yeye ndo analipwa mshahara. Hiyo 700k ya Halmashauri kuna watu ni Kodi wanayokatwa, kuna watu hiyo ni pesa ya mafuta au communication tu lakini serikalini inakuhitaji miaka 5 hadi 10 kuja kufikia channels zenye pesa nzuri. Maisha ni Hesabu, wapo watu maisha yao yote ya utafutaji ni Sekta binafsi, wapo waliojiajiri, wapo waliamua kuwa watumishi wa Umma. Ila ningekuwa mimi nimevaa viatu vyako katu nisingerudi kwenye 700k nikaacha 2m+ who knows unaishi leo, Job Security una assurance gani ya kuishi hadi miaka 60? Una makubaliano na Mungu kuwa hicho kibarua cha serikalini hakitaota nyasi? Hautasimamishwa? Rais Akibadikilika Je? Huwa ni kujipa uzembe usio na tija kwa kigezo cha Job Security unaishi leo hujui kama kesho utaamka. Fikiri kwa busara na hekima
 
Back
Top Bottom