Hivi mkuu, NAOT huwa wanakagua Data na Kufanya Data verification za afya
Kuna aina hizi za ukaguzi ambazo zinaweza kujibu hoja yako.
-Ukaguzi wa Mifumo ya TEHAMA
-Ukaguzi wa Kiuchunguzi
-Ukaguzi wa Ufanisi
Tupo kwenye digitalization, hata awamu hii ya Kichere inajipambanua ni awamu ya Digitalization, kazi zake imejielekeza kidigital ili iweze kuzifanya vizuri zaidi.
Siku hizi TEHAMA inatumika sana katika kurun mambo mengi ikiwemo utoaji wa huduma za Afya. Katika huo ukaguzi wa Mifumo ya TEHAMA lazima wachunguze na kukagua jinsi data zinavyokuwa developed, kutunzwa na kutumika katika utendaji kazi wa hiyo mifumo.
-Ukaguzi wa Kiuchunguzi ni ukaguzi unaolenga kuzuia na kugundua makosa, kama vile udanganyifu, ubadhirifu na rushwa kwa kutumia wa ujuzi wa ukaguzi kwa hali ambazo zina mwelekeo wa kisheria.
-Ukaguzi wa Ufanisi huu unaangazia matumizi sahihi ya fedha kama yametumika kulingana na thamani yake na kufuata sheria.
Kwa hiyo katika ukaguzi wowote ule, matumizi ya data hayaepukiki, lazima data zitumike kwani wakati wa kukagua au kuchagua eneo la kukagua lazima data zikuongoze katika uchaguzi wa eneo la kukagua.