Dah,nilikuwa wapi muda wote huu kuja kutoa majibu sahihi?
Iko hivi, binadamu anapokufa hawezi kufufuliwa kama gari kifufuliwavyo kwasababu, mwili wa binadamu na viumbe hai wengine wana mpangilio ufuatao katika miili yao,
Seli› Tishu› Ogani› Sistimu(mfumo)› kiumbe hai
Na hiyo oganaizesheni hapo juu zinategemeana kila moja,yaani moja ikishindwa kufanya kazi inaathiri ufanyaji kazi wa kingine,
Mfano: Moyo ukifeli kusukuma damu, kuna seli zitakosa chakula,oksijeni n.k hivyo kufanya hizo semi kufa, na ikumbukwe pia kuna seli za aina mbalimbali, seli za ubongo, seli za Neva, seli za kwenye mapafu,figo,INI,utumbo, tumbo n.k hivyo kushindwa kwa Moyo kusukuma damu kutasababisha seli hizo zote kukosa chakula na oksijeni hivyo kupelekea hizo seli kufa.
Kwa maana hiyo mtu akifa kwa tatizo la moyo kushindwa kufanya kazi maana yake sehemu nyingine za mwili zimefeli pia, hivyo hata ukibadilisha moyo bado haitaweza kumfufua kwasababu kuna seli zingine za mwili zitakua hazifanyi kazi.
Hii inatofautiana na gari, gari inaweza ikafa injini lakini sehemu zingine ziko njema hivyo ukiweka injini nyingine gari inarudi kuwa nzima.
Bila shaka utakua umeelewa kwanini hatuwezi fufuliwa kama gari baada ya kufa