nje ya bibilia Hakuna Jibu la kweli mkuu.
Yote haya yalianza miaka zaidi ya 6000 hapo mashariki ya kati maeneo ya Iraq. Karibu na mto tigris ilipokaa bustani nzuri
ya Eden. Kwingine kote utadanganywa. Na summary yake ipo kitabu cha mwanzo 1,2,3.
Ukielewa vizuri ndio utauliza maswali mapya.
1:Kwa nini Kiyama?
2:Kwa nini kondoo/ndama alichinjwa mtu akimkosea Mungu?
3:Kwa nini Yesu Afe?
4:Ni nini Dawa ya kifo?
5:Kuna kufa mara ngapi? Kwa nini hupaswi kuogopa kifo hiki tunachokiona sasa (Temporal death)?
kwanini unasema kitabu cha mwanzo hakidanganyi wakati kitabu cha mwanzo kina makosa yafuatayo:
1. Mwanzo 2:2,3
Inasema Mungu alipumzika siku ya saba baada ya kumaliza uumbaji. inakuaje asiyechoka, mwenyeuweza wote akahitaji kupumzika au usingizi?
2. Mwanzo 2:17
Mungu alimuambia Adam asile tunda la mti wa kujua mema na mabaya. Mwanzo 3:5 inasema utapata kujua mema na mabaya endapo utakula tunda kutoka mti huo. Kwa maana hiyo wakati eva anakula tunda hakuwa na ufahamu wa mema na mabaya. Kwahiyo wakati anakula alikua nafanya kama vitendo vingine anavyofanya, manake hauwa na uwezo wa kuelewa maana hauwahi kula tunda hilo kabla.
3. Mwanzo 3:14
Inasema kwamba nyoka hula vumbi. hili halipo sawa kisayansi, hata watu ambao ni layman wanajua kwamba nyoka wanakula vitu ambavyo ni orgainic kama vile Wanyama wengine, mayai na vinginevyo lakini sio vumbi.
4.Mwanzo 3:14
Inasema nyoka kutembea kwa kutambaa kwa tumbo ni adhabu yake. Yaani kana kwamba hapo awali nyoka alikua anatembea kwa miguu alafu akanyang'anywa miguu ili atembee kwa shida. ila mimi nnavyomuona nyoka sioni kama anatembea kwa shida na kwanaza nashindwa kuelewa mtu mzima anawezaje kuamini kitu kama hichi.
5.Mwanzo 3:16
Inaonyesha kwamba kuzaa kwa uchungu ni adhabu. Adhabu kwa binadamu?? Lakini inajulikana kwamba Wanyama wengi tu wanapata maumivu wakati wa kuzaa. Fisi anazaa kwa shida sana na anapata maumivu makali sana wakati wa kuzaa (asilimia 18 ya kuzaa kwa fisi husababisha kufa kwa mama fisi) je hao Wanyama wengine walifanya amakosa gani mapaka wapate adhabu hiyo?
6.Kuna hadithi nyingi sana kwenye biblia ambazo hazina mantiki na hazipaswi kutiliwa maanani na mtu mzima. hadithi kama kuna lugha mbali mbali kwa kua hapo zamani binadamu walitaka kujenga mnara mrefu kumfikia mungu. hadithi kama mwanamke akizaa mtoto anakua najisi na akizaa mtoto wa kike anakua najisi Zaidi na hatakiwi kuhudhuria ibada kwa siku 66 ( walawi 12:5).
Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vya kale na katika kitabu hicho kuna vingi ambavyo haviendani na hali ya maendeleo ya binadamu kwa sasa. Yaani kwa kifupi kuna vitu vingi vimepitwa na wakati na havina uhalisia.