Enkulu
Member
- Sep 29, 2022
- 17
- 57
"Tulikupenda/Tulimpenda lakini Mungu kakupenda/kampenda zaidi" hii kauli, au sentensi au msemo umekuwa ukisikika sana katika misiba ya Wakristo. Sina hakika kwa upande wa Waislam ila kama pia hutumika mimi sijui.
Imekuwa ni sentensi ya kawaida sana kutamkwa misibani. Lakini sentensi hii fupi imenifikirisha na imenifanya kuibua maswali mengi kichwani mwangu.
Msiba si jambo jema, hasa kwa wanadamu. Hakuna mtu anaependa kufa, japo tunataka kwenda mbinguni lakini kufa au kumuona yule ampendae akifa; Hapana kwakweli.
Msiba huleta huzuni, majonzi, vilio, migogoro, uadui, na mambo mengine mengi. Sasa iweje upendo wa Mungu udhiirike pale mtu akifa? Mpaka ifikie hatua tuseme "...Mungu alikupenda zaidi".
Yaani Mungu akikupenda ndo unakufa?
Swali hili lilinifanya nijiulize kwanini tunakufa? Kama kifo sio kitu kizuri kwanini basi tunakufa?
Katika biblia kifo kilitajwa kwa mara ya kwanza katika kitabu cha Mwanzo 2:17. Adam na Hawa wanapewa maagizo ya kutokula matunda ya mti wa katikati la sivyo watakufa.
Adam na Hawa wakafanya kinyume, na kile kilichonenwa kikawa, Abeli akawa binadamu wa kwanza Kufa. Kumbe kifo ni matokeo yaliyokuja baada kwenda kinyume na maagizo ya Mungu.
Je kifo ni adhabu?
Kwa namna moja au nyengine twaweza kusema kifo ni adhabu. Adhabu ambayo Adam na Hawa waliileta kwa wanadamu wote baada ya kwenda kinyume na matakwa ya Muumba. Sasa kama kifo ni adhabu, iweje upendo wa Mungu udhiirike kwa mtu anapokufa? Ukiadibiwa ndo unapendwa?
"Tulimpenda lakini Mungu kampenda ziadi"
Kifo si adhabu, kifo ni ishara ya kuwa Mungu anatupenda bado, kifo ni pendo la Mungu. Mwanzo 3:22 "Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;"
Kumbe katika bustani ya Eden palikuwako na mti wa uzima, mti ambao ukila matunda yake unaishi milele. Na endapo Adam na Hawa wangekula matunda ya mti huu wangeishi milele.
Je Mungu hakutaka Adam na Hawa waishi milele hata akawafukuza? Jibu ni "HAPANA" Mungu alitaka Adam na Hawa waishi milele ndio maana hapakuwepo na kifo kabla ya wao kwenda kinyume nae. Sasa kwanini hakutaka wale tunda la mti wa uzima?
Kitendo cha Adam na Hawa kula tunda la mti wa katikati kilitia doa roho zao, wakawa wadhambi tayari. Mungu alitaka binadamu hawa waishi milele, lakini waishi milele wakiwa si wadhambi. Waishi milele roho zao zikiwa swafi kama theluji.
Mungu hapatani dhambi, sasa ili binadamu akombolewe na aje kuishi maisha yale aliyotakiwa kuishi ni lazima afe
Kumbe kifo ni utakaso? Kifo ni ukombozi? Soma Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."
Tunaona Mungu anamtoa mwanae (Yesu Kristo) aje kufa msalabani, kwanini anafanya hivyo? Kwasababu Mungu aliupenda ulimwengu na yoyote atakae mwamini huyo mwanae atakuwa na uzima wa milele.
Uzima wa milele umeletwa na kifo cha Yesu Kristo, kifo chake ni juu ya upendo wa Mungu kwa wanadamu. Kama Mungu asingependa huu ulimwengu Yesu Kristo asingekufa.
Kumbe kifo ni upendo. Basi tuko sahihi tukisema "Tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi"
Upendo ni nini?
Biblia inasema Mungu ni pendo, 1 Yohana 4:8 "Yeye asiyependa hakumjua Mungu kwa maana Mungu ni pendo"
Upendo ni kitendo cha kuonyesha hisia pengine umeridhishwa na mtu huyo, au umemkubali, au umemuhurumia, au unataka kumkaribia uwe karibu naye n.k
Mungu ameridhika nasi, ametukubali kama wanae (soma "Wagalatia 3:26") ,ametuhurumia na anataka kumkaribia tuwe karibu nae. Ili haya yote haya yatimie ni lazima tufe.
Binadamu hawezi kumkaribia Mungu kama hatokufa. Zamani Adam aliweza kuonana na Mungu ana kwa ana, unajua kwanini? Kwasababu roho yake ilikuwa nyeupe pasipo na dhambi. Leo hii Mungu huwasiliana na binadamu kwa namna ya tofauti (maombi).
Basi mtu anapokufa tusihuzunike sana bali tuwe na matumaini, tuamini kwamba hilo limemtokea yeye nasi pia litatutokea na yote ni kwasababu Mungu alitupenda anatupenda na ataendelea kutupenda.
Mungu katumia kifo kumkomboa binadamu, binadamu aliowapenda. Basi tusikiogope kifo bali tujiandae ili tutakapo kufa tuwe na matumaini ya kufufuliwa na kuishi Mbinguni.
Yatupasa kujiandaa wakati wote, kila mtu kwa imani yake. Kifo huja wakati wowote, siku yoyote, hakuna anayejua atakufa lini.