Zingatia Haya Ili Kuipita Changamoto/ Shida Unayopitia.

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Kwanza ujipe muda ili kuitatua changamoto yako.

Changamoto na shida zinaweza kutokana na;
Makosa yako mwenyewe kwa kurudia kosa,
Makosa ya wengine mpaka yamekuathiri,
Makosa katika kufanya kitu kipya,
Kukosa rasilimali za kutimiza malengo yako, au
Kuwa katika sehemu mbaya, isiyokufaa, unayoonewa.
Na ubaya wa changamoto ni kuwa kadri unavyozidi kuipa nguvu na yenyewe inazidi kukua na kukuathiri. Hata akili zetu zenyewe ni rahisi kuweka nguvu kwenye changamoto zaidi kuliko kutatua changamoto.

Inawezakana umeshawahi shuhudia watu walioathiriwa na changamoto walizopitia. Ukajisemea hutaki yakupate. Lakini unaona hujui pa kuanzia ili usiishie kuangamizwa na changamoto.

Fanya haya kwa kurudia rudia ili kuyashinda unayopitia mana inachukua muda.
.
Kubali kwamba changamoto imetokea.
Changamoto hutokea kadri unavyozidi kujiendeleza. Ni jambo zuri.
Jiwekee akilini kuwa utakutana na changamoto na utayashinda.
Ukishaikubali changamoto, ujue umeitatua 50%.

Na pale changamoto inapotokea usianze kusema “natamani nirudishe muda nyuma …” au “kwanini mimi”. we kubaliana na hali kisha jifunze kusonga mbele. Japo itakua ngumu siku za mwanzoni ila unayaweza.

Usitumie sana kauli ya ‘nge’, mana utapata shida kukubaliana na changamoto.

Wanadamu tumeumbiwa changamoto, lakini shida huanza pale tunapojilinganisha na wengine. Kiasi cha kujiona maisha yako pekee ndo yenye changamoto. Achana na hilo na ujikumbushe sio wewe tu unayepitia changamoto.
Utambue kila mtu anapitia changamoto
.
Usisahau kujiliwaza.
Ukipata changamoto unaweza jipoza kwenye kitu ukipendacho.
Lakini usikitumie ukipendacho kukwepa changamoto.
Ila ukiona hautaweza kujitawala, heri uache kabisa.
.
Kuwa na malengo.
Malengo ni kama taa kwenye maisha.
Malengo ndio yanachagua mwelekeo wa maisha.
Malengo yanakusaidia kukukumbusha nini unataka ili usizame na ukamezwa na changamoto mpaka ukashindwa kabisa. Mfano, una mpango wa kuongeza kipato, alafu ghafla ndugu anaumwa. Au una mpango wa kupata mwanamke ambaye utajenga naye maisha lakini unakutana na madanga. Kamwe usilie juu ya hilo jambo we endelea kuweka kichwa chako katika lengo lako.
Huku ukiendelea kutatua changamoto lakini una imani utafikia malengo.

Hata kama unaona hakuna mwanga wa kufikia malengo.
Kaa na imani, endelea kuamini utafanikiwa kwenye malengo.
Na hiyo ndo maana ya imani.
.
Chagua watu vizuri.
Watu wa kuwashirikisha unayopitia.
Kuna watu wanasubiri upate shida wakucheke, wakuseme na wakushushe. Jiepushe nao. Utaishia kuona changamoto yako ni kubwa kuliko uhalisia. Hata kwenye mitandao pia uchague watu vizuri.
Ukishapata watu unaowaamini, usisite kuwashirikisha kiundani yanayokusibu.
.
Kuwa mtu wa shukurani.
Kwa mimi nimekulia kanisani, nimeshuhudia watu wanaotoa shukrani ya pekee wengi wao hubarikiwa zaidi.
Kwanini?
Sababu ni rahisi kuendelea kumridhisha mtu anayekushukuru.
Pia atakuvutia zaidi, kuliko mtu unayemsaidia kitu alafu hata shukrani hana. Si ndio?
Na kwa kuwa tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, naye Mungu yupo hivyo, kadri unavyomshuru ndivyo anazidi kukubariki.
Au chukulia mtu anayelia lia kuomba kitu. Mara nyingi kesho ukimwona utabadili njia, utamkataa au utajifanya una haraka na kupanda boda. Hivyo hivyo, wengi wanaomlilia lilia Mungu ovyo hawapati kile wanachokililia.

Pia usilalamike sana.
Unapolalamika maanake huna shukrani, na unaposhukuru maanake huna malalamiko.
Ila pale panapohitaji malalamiko yatoe, lakini isiwe ndo tabia.

Badala ya kulalamika mwanamke fulani amekuacha na ulikua unampenda, we shukuru kwa kuwa mlipata muda mzuri pamoja au kwa kuwa amekufundisha kitu na maisha yasonge.
.
Jaribu kuandika shida zako/ changamoto yako.
Nilikua naambiwa kuhusu hili tangu zamani ila nikawa mbishi.
Lakini siku moja nikaamua kuandika kinachonisumbua akili kama kilivyo. Kwanza nilipata unafuu. Na nikagundua kumbe ni vitu tu kawaida kulinganisha na jinsi nilivokua navichukulia vikiwa kichwani.

Unaona kitu kwa upande wa pili. Unakiona kwa undani zaidi.

Hii ndo mbinu inatumiwa na wauzaji wazuri, au madokta, wanaandika vile unajisikia ili kupata uhalisia wa vitu kuliko kikiwa kichwani kwako.

Kadri unavyozidi kuona changamoto yako ni jambo la kawaida ndivyo unazidi kupata nguvu ya kuitatua. Ili usijikute unazama kwenye anasa kukwepa changamoto.
Hivyo, ni muhimu usikubali changamoto unayopitia ikufanye uone dunia ndo imeaisha.

Nikutakie mapumziko mema na maandalizi mazuri ya wiki ijayo.
 
Back
Top Bottom