Vincenzo Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2020
13,806
29,387
Acheni siasa mnaharibu soka letu mechi ya bara mnapeleka visiwani ili mgundue nini? TFF mnaipeleka Fainali Zanzibar, sehemu ya nje ya utawala wa FA husika?

Lini mmewahi kuona FA ya Uingereza imepeleka fainali Ireland, au Scotland?

Lini mmewahi kuona FA ya Ujerumani imepeleka fainali zao Uturuki?

TFF MJITATHMINI.

---

1716416829761.png
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza mabadiliko ya mchezo uwanja wa mchezo wa Fainali ya Kombe la FA kuwa kwa sasa utachezwa Amaan Zanzibar na sio Babati Manyara kama ilivyotangazwa awali.

Maamuzi hayo yamekuja baada ya uwanja wa Babati kutokuwa sawa kwa baadhi ya miundombinu na usalama hivyo kupelekea mchezo huo kuhamishiwa Zanzibar.

Mchezo wa fainali ya FA utazikutanisha Yanga na Azam FC June 2, 2024 saa 2:15 usiku.
 
Acheni siasa mnaharibu soka letu mechi ya bara mnapeleka visiwani ili mgundue nini? TFF mnaipeleka Fainali Zanzibar, sehemu ya nje ya utawala wa FA husika?

Lini mmewahi kuona FA ya Uingereza imepeleka fainali Ireland, au Scotland?

Lini mmewahi kuona FA ya Ujerumani imepeleka fainali zao Uturuki?

TFF MJITATHMINI.
Kuboresha Muungano na kudhibitisha kuwa hakuna m'Tanzania bara atakayedaiwa PASSPORT.
 
Kanuni za tifuatifua zinakataa shindano lililokwenye mipaka ya bara kufanyika nje.......ila kwasababu ya kujipendekeza hiyo Kanuni haijazingatiwa,hao wazenji wenyewe wabara tunajipendekeza tu hawatutaki kabisa.
Mzanzibar mibaguzi sana
Naunga mkono hoja
 
Wadau hamjamboni nyote?

Taarifa njema huyo hapoo chini!

Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limetangaza kuwa limebadili matumizi ya uwanja utakaochezewa fainali ya (FA) kutoka Manyara hadi New Amani complex Zanzibar.

Sababu za kiusalama na utayari mdogo wa miundombinu Babati Manyara zimetajwa na (TFF) kuchangia kuihamisha fainali hiyo.

Fainali hiyo itazikutanisha klabu za Yanga SC na Azam FC 2 June 2024.
 

Attachments

  • 1716378605285.jpg
    1716378605285.jpg
    228.6 KB · Views: 4
Back
Top Bottom