Kwanini Tanganyika Law Society isifutwe?

Kwanini Tanganyika Law Society isifutwe?

Oops kumbe ni za Goma, my bad. This is the goodness of arguing with an ass-hole thinking that you're arguing with someone sensible.
Yeah after the authenticity check I've proved that those pics are from Goma, it's the Goma massacre done by lady President of Goma.
Toa hint ili kuonyesha hizi maiti ni za oct29 tz. Kwanza tz tuna sheria ya kutopiga maiti na kusambaza, wewe ulizipata wapi?

Kaka sisi wote sio wajinga kama wale.
 
Sasa ndo mnaua watu hadi kwenye makazi na shughuli zao binafsi?
Haya mshawaua kwa mamia na maelfu, miili iko wapi?

Msiwachukulie poa hawa WaTanganyika... Soon mtaanza kuwindwa!
Kama kijana wako kachoma kituo cha polisi, kuua polisi na kuiba silaha kisha akakimbilia nyumbani kwako kwanini wasimfute nyumbani kwako hukohuko alikojificha?

Jambo la msingi mfundishe mwanao Junior hatari ya kuchoma mali ya uma, polisi, TRA au ATM.
 
Unataka kufuta chama kikongwe kuliko Serikali yako?
TLS ilianzishwa 1954-58 huko, Tanganyika hata haijapata uhuru.

Wanasheria sio wajinga na huwezi kuwaendesha kama vyama vingine kutokana na historia yake pamoja na taaluma yenyewe ya sheria.

Ushauri: unayo haki kikatiba kwenda mahakamani kama unaona kuna hoja ya kisheria. Ila utahitaji Wakili ambaye unataka chama chake kifutwe, 😂
 
Ni wapi mahakama zinaaminika? Hata Marekani wanalia na mahakama, Kenya wanalia na mahakama, SA, hivyohivyo. Usituaminishe ujinga wako. Kesi ikishakuwa mahakamani subiri hukumu na ukate rufaa kama hukuridhika na maamuzi. Rule of law inatutaka tufanye hivyo, kwani mwabukusi hajui hilo?
Kwahiyo watu wataendelea kusubiri hadi mahakama iamue kufanya maamuzi kwa maagizo ya hao majizi wa ccm? Marekani uaniongelea? Kenya hapo mahakama Zina weledi hakuna mfano ,utafananisha na haya majengo ya mahakama yanayosimamiwa na makada wa ccm?
 
Kwa hisani ya mavi ya kijani ya mama
Kaka nchi inasongambele kwa kasi ya mwanga. Wahisani wana hiari ya kutupa au kutunyima. Bahati mbaya hata wakoloni sasa hivi wana hali mbaya sana kiuchumi.

Prof. Mkumbo ni mtu muhimu sana kwenye taifa.

View: https://www.youtube.com/live/nH2_Oh62BAk?si=RqT-BYafsnWw0WbU
Unataka kufuta chama kikongwe kuliko Serikali yako?
TLS ilianzishwa 1954-58 huko, Tanganyika hata haijapata uhuru.

Wanasheria sio wajinga na huwezi kuwaendesha kama vyama vingine kutokana na historia yake pamoja na taaluma yenyewe ya sheria.

Ushauri: unayo haki kikatiba kwenda mahakamani kama unaona kuna hoja ya kisheria. Ila utahitaji Wakili ambaye unataka chama chake kifutwe, 😂
Nashukuru kujua ilianzishwa lini. Taasisi ambayo hailindi maslahi ya watanzania dhidi ya wahuni sio muhimu na haifai kuwepo
 
Unataka kufuta chama kikongwe kuliko Serikali yako?
TLS ilianzishwa 1954-58 huko, Tanganyika hata haijapata uhuru.

Wanasheria sio wajinga na huwezi kuwaendesha kama vyama vingine kutokana na historia yake pamoja na taaluma yenyewe ya sheria.

Ushauri: unayo haki kikatiba kwenda mahakamani kama unaona kuna hoja ya kisheria. Ila utahitaji Wakili ambaye unataka chama chake kifutwe, 😂
Kinapoteza dira na uelekeo. Hata mbwa wako nyumbani unaempenda sana kama atakuwa kichaa na kuanza kuuma wanafamilia badala ya kuwalinda utamuua
 
Ni kweli nadhani. Mtu kama Mh. Mwabukusi ni mwanasheria mkubwa na kiongozi mkubwa wa wanasheria wenzake wa taaluma yake, lakini anasema Tundu Lissu hana hatia nje ya mahakama huku akijua kuwa kesi yake iko mahakamani na hukumu haijatolewa. Ni layman wa sheria tu kama mimi au mwanasiasa ambae anaweza kusema hivyo. Hii ni kuonyesha kuwa ama elimu yetu imeshuka sana au kweli tunatumia chini ya asilimia 1 ya akili zetu. Hii haina tofauti na kuvuta mlango ulioandikwa SUKUMA, umepunzisha akili na kutumia mazoea.

Kama mtu anatumia akili yake sawasawa angehoji watoto na mke wa Lissu wako wapi kabla hajaandamana kumtoa Lissu gerezani. Angehoji mbona watoto wa wanasiasa wakuu hawakufa kwenye vurugu za Oct29. Wangehoji mbona wachungaji, mapadre, maaskofu na masheikh na watoto wao hawakufa kwenye vurugu za Oct29?

Hawahoji kama mbayuwayu kwakuwa hawatumii akili zao kabla ya kutekelezwa wanachoambiwa.
0_0Z7rzeZzrNHEtuoJ.png
 
Kinapoteza dira na uelekeo. Hata mbwa wako nyumbani unaempenda sana kama atakuwa kichaa na kuanza kuuma wanafamilia badala ya kuwalinda utamuua.
Nampeleka hospital akapatiwe matibabu na atapona mbwa kua kichaa suluhisho sio kifo tuwapende wanyama jama ila sio panya waharibifu nazungumzia mbwa km mbwa hata awe kichaa usimuue mpatie matibabu mkuu, accept my condolences
 
Ni kweli, kuna watanzania wanahoji ni kwanini sisi hatupigani na hatuandamani kila siku kama nchi jirani. Kama huu sio ujinga ni nini? Yaani unakwenda kukodi watu wanaojua kuchoma nchi yako bila woga.

Mtu anahoji ni kwanini serikali hii hata njiti za meno tunaagiza kutoka China. Yaani anataka serikali itengeneze njiti za meno badala ya yeye atengeneze na kuuza apate faida.
 
Nampeleka hospital akapatiwe matibabu na atapona mbwa kua kichaa suluhisho sio kifo tuwapende wanyama jama ila sio panya waharibifu nazungumzia mbwa km mbwa hata awe kichaa usimuue mpatie matibabu mkuu, accept my condolences
Huwezi kumtibu mbwa akishapata kichaa (rabies) atakufa muda mfupi tu ujao, ila unaweza kumkinga asipate kichaa.
 
Vijana wamekufa kwa kushawishiwa kikondoo kondoo nikama wametupiwa PEPO la kifo na viongozi wao wa Dini ukiacha w Siasa 👈

Kabla ya Mo29 👈

Rudi nyuma mwezi mzima na zaidi

Vijana walikuwa wanapiga kelele kama walevi kama wamebebeshwa kitu kichwani kizito

kelele zao zilikuwa RAIS Samia must Go
SAMIA Must Go 😥😥‼️

Sasa Sababu za kelele zile zilitokana nanini????

Mana hakukuwa na kifo cha kijana yoyote ‼️‼️‼️

wkt ule RAIS Samia Suluhu Hassan aliwakosea nini hawa Vijana kiasi kupiga ukelele ule RAIS Samia Must Go

Ndiomana wengine tunasema waliuwawa kikondoo kondoo wamedanganywa na kumchukia RAIS wao pasi na Sababu yoyote

Leo sasa wanasema RAIS Samia Suluhu Hassan muuaji ‼️

Sasa Kabla Mo29 mlimchukia kwasababu zipi?????

Mlikuwa na PEPO chafu la kifo tu👈

na Wapinzani wamefanikiwa project yao kutumia Vifo vyao 🫎🫎🫎🫎kujiimalisha kisiasa 👈

Najiuliza Kabla ya vile Vifo uyu Heche uko Ulaya angepokelewa nanani au uko Marekani ¿¿¿¿

baadhi ya Viongozi wa Dini wameshiriki kwenye mradi wa kuwaangamiza Watoto wetu wenyewe😥😥😥

faida gani tumepata leo kuwapoteza watoto wale👈

Ndiomana kwasasa Viongozi wa Dini kwa kujutia matokeo yale sijasikia kiongozi yoyote kuunga mkono fujo za 7+7. 👈

Wengine wamejitokeza kabisa kudai wanapinga izo fujo lau 7+7✅️

sijui walikuwa wapi kiakili Kabla ya Mo29

Mwisho walewale waliokosea kushawishi Mo29 ndio leo wanajaribu kumtupia ZIGO kibubusa
RAIS Samia

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN hasingeweza kuzuiya watu wenye Chuki za kupandikizwa kiasi kile 👈

Chuki ukizipa nafasi zinageuka na kuwa PEPO chafu la kifo👈

unawaza kuuwa tu chochote kuchoma chochote ata ndugu yako unaweza kumuuwa
wkt w ilo PEPO 👈

Vijana wenye chuki wameanza kuichoma nchi ‼️

wkt RAIS yoyote Duniani huapa kulinda Sheria za nchi sio kuapa kulinda wachoma nchi 👈

sio kwa RAIS Samia Suluhu Hassan

hata angekuwa RAIS wa nchi ni father Kitime bado yangetokea mauaji yale👈

mana makundi ya vijana wanaichoma nchi 👈

ktk wkt huu jeshi
lingefanyaje apo!!!!

Tena siku ipo kisheria ni siku ya Uchaguzi rasmi wa kitaifa,😥
 
Kama ambavyo hatutarajii watoto wa viongozi kupata vyeo na upendeleo ndivyo ambavyo Si lazima watoto wa viongozi wa harakati za mabadiliko wawepo mstari wa mbele wa vita.

Wakati wakoloni wazungu wanashughulishwa na wadai uhuru hakuna Mtanganyika timamu alisema kina Nyerere na viongozi wa TANU watangulize watoto wao kulete hamasa!
Jifunze kutofautisha.

Kuhusu picha... WaTanganyika wanao ukweli wote... Wao ndo waliwatafuta ndugu zao... Wao ndo walipiga hizo picha!
View attachment 3618776
Wenye nia njema walidiriki kutumia teknolojia kuhakiki... Lakini kama kawaida yenu mlipuuzia na kutoa hoja za kijinga kuwapinga!

Anyways, kwa hatua Tanganyika ilikofikia... Ni suala la muda tu. Risasi hazitotosha kudhibiti madai ya mabadiliko.
Hizi ni mbinu chafu za kutafuta idadi ya watu waliokufa inayohitajika kukidhi vigezo vya kupata msaada wa ICC na taasisi nyingine za ulaya na marekani. Yaani watu wanafanya kila mbinu ili watu wauane wengiiiiii kufikia idadi ya kimbari, maana ili ICC ichukue hatua lazima kuwe na idadi fulani ya watu waliouliwa. Ujinga huu unafahamika tayari, tafuteni mbinu nyingine.

Ukigombana na mwanamke wewe mwanaume utaonekana punguani, na ni vigumu sana kushinda.
 
Vijana wamekufa kwa kushawishiwa kikondoo kondoo nikama wametupiwa PEPO la kifo na viongozi wao wa Dini ukiacha w Siasa 👈

Kabla ya Mo29 👈

Rudi nyuma mwezi mzima na zaidi

Vijana walikuwa wanapiga kelele kama walevi kama wamebebeshwa kitu kichwani kizito

kelele zao zilikuwa RAIS Samia must Go
SAMIA Must Go 😥😥‼️

Sasa Sababu za kelele zile zilitokana nanini????

Mana hakukuwa na kifo cha kijana yoyote ‼️‼️‼️

wkt ule RAIS Samia Suluhu Hassan aliwakosea nini hawa Vijana kiasi kupiga ukelele ule RAIS Samia Must Go

Ndiomana wengine tunasema waliuwawa kikondoo kondoo wamedanganywa na kumchukia RAIS wao pasi na Sababu yoyote

Leo sasa wanasema RAIS Samia Suluhu Hassan muuaji ‼️

Sasa Kabla Mo29 mlimchukia kwasababu zipi?????

Mlikuwa na PEPO chafu la kifo tu👈

na Wapinzani wamefanikiwa project yao kutumia Vifo vyao 🫎🫎🫎🫎kujiimalisha kisiasa 👈

Najiuliza Kabla ya vile Vifo uyu Heche uko Ulaya angepokelewa nanani au uko Marekani ¿¿¿¿

baadhi ya Viongozi wa Dini wameshiriki kwenye mradi wa kuwaangamiza Watoto wetu wenyewe😥😥😥

faida gani tumepata leo kuwapoteza watoto wale👈

Ndiomana kwasasa Viongozi wa Dini kwa kujutia matokeo yale sijasikia kiongozi yoyote kuunga mkono fujo za 7+7. 👈

Wengine wamejitokeza kabisa kudai wanapinga izo fujo lau 7+7✅️

sijui walikuwa wapi kiakili Kabla ya Mo29

Mwisho walewale waliokosea kushawishi Mo29 ndio leo wanajaribu kumtupia ZIGO kibubusa
RAIS Samia

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN hasingeweza kuzuiya watu wenye Chuki za kupandikizwa kiasi kile 👈

Chuki ukizipa nafasi zinageuka na kuwa PEPO chafu la kifo👈

unawaza kuuwa tu chochote kuchoma chochote ata ndugu yako unaweza kumuuwa
wkt w ilo PEPO 👈

Vijana wenye chuki wameanza kuichoma nchi ‼️

wkt RAIS yoyote Duniani huapa kulinda Sheria za nchi sio kuapa kulinda wachoma nchi 👈

sio kwa RAIS Samia Suluhu Hassan

hata angekuwa RAIS wa nchi ni father Kitime bado yangetokea mauaji yale👈

mana makundi ya vijana wanaichoma nchi 👈

ktk wkt huu jeshi
lingefanyaje apo!!!!

Tena siku ipo kisheria ni siku ya Uchaguzi rasmi wa kitaifa,😥
Hata baharini, anaetoboa mtumbwi wanaosafiria wanamtosa majini azame aliwe na papa. Vijana wetu walikumbana na pepo baya sana la kujitoa mhanga walilotupiwa na watu waliowaamini sana.
 
Wewe una mwili ambao hujaupata? Za kuambiwa changanya na zako , usiaminishwe ujinga.
Zaidi ya ndugu zangu watatu na marafiki kadhaa hawajulikanani walipo kuanzia Oct 2025. So tunapoandika hapa usifikiri wengine ni maboya kama wewe!
 
Malizeni kwanza dhuluma ndani familia na ukoo zenu ya kunyima watoto wa kike haki yao ya kurithi mali za wazazi wao kabla ya kurukia haki nyingine. Charity begins at home.

Familia inamkeketa biti yao bila idhini yake, halafu familia hiyohiyo anatoka mwanafamilia kuadamana kudai haki Ikulu.

Mwanaume baada ya kumaliza kumcharaza mkewe eti kwanini alichelewa kutoka sokoni anavaa gwada na kusema piiiiipoooooz, haki kwa wote.

Hapa nataka kusema kuwa vurugu tunazoziona sio za kudai demorasia wala haki maana jamii zetu zina uwezo mkubwa sana wa kuvumilia dhuluma na uonevu. Yaani watoto wa baba mmoja na mama mmoja wananyimana urithi na maisha yanaendelea, mtoto anapewa mimba na kumalizana kifamilia hukohuko nyumbani. Ukosefu wa demokrasia haujafikia levels za kuchoma kituo cha polisi, mwendokasi au ofisi za TRA.

Watanzania amkeni!!!
Umesoma na kuelewa kilichoandikwa?
 
Uhai wa watu kwanza!
Uko sahihi kaka uhai wa watu kwanza mengine yafuate. Ndiyo maana mabaharia wanamtosa majini aliwe na papa mwenzao anaetoboa mtumbwi wao. HAKUkua NA njia nyingine ya kuwasaidia vijana wale wasife zaidi ya kukataa kuichoma nchi yao. Wapumbavu waliwadanganya vijana wale kuwa jeshi litakuwa nyuma yao wasiogope huku wakijua kuwa walikuwa wakiwadanganya. Vijana walimwamini askofu wao, mwenyekiti wao na viongozi wao kuwa hawadanganyi. Hii ni kama ile Kinjekitile Gwale alivyowadanganya askari wake kuwa risasi za wajerumani zitageuka maji kwenye vita ya majimaji, lakini wakauliwa wengi sana.
 
Zaidi ya ndugu zangu watatu na marafiki kadhaa hawajulikanani walipo kuanzia Oct 2025. So tunapoandika hapa usifikiri wengine ni maboya kama wewe!
Nakuuliza tena, wewe uliponaje usiuliwe? acha ngonjera zako.
 
Unadhani kwanini nchi za jirani walipoingia opposition parties madarakani hawana hamu tena na vyama vya vilivyotangulia kutawala, chama chochote makini(hapa nalenga TZ) vinajua fika kuwa CCM inachukiwa kwa sababu(japo nao wanajua ila wanakomaza shingo tu wakiamini kuwadhibiti wanachi kwa mabavu bila ridhaa yao ni jambo lisilosumbua) na hivyo vyama kamwe haviwezi kutawala kwa upumbavu wa kidikteta ili kuepuka kuchukiwa na raia. Si kila chama kitataka kiwe kinaongoza kwa kutumia vyombo vya dola to intimidate citizens.
Huo ni ushahidi kuwa hata atuongoze nani hali yetu itabaki ileile Afrika yote ya weusi. Utamtoa mpigaji huyu unamwingiza mpigaji zaidi mwingine. Hivi kwa akili yako kutoka moyoni Lissu akiwa rais kuna kitu gani ataboresha kwetu? George Weah alionekana mshua, anajuana na wazungu na ameishi ulaya kama ilivyo kwa Lissu, Liberia wakampa urais na kumwanguza Bibi Sariff. Walichemka wenyewe wakampiga chini fasta; no change.
 
Ni jambo la hatari kwa taasisi ya umma kama vile Yanga, Simba, Tanganyika Law Society (TLS) au TFF kuchukua mwelekeo kamili wa kisiasa. Madhara yake ni makubwa sana. Na Unaweza kutambua uelekeo wa taasisi kwa kuangalia na kuwasikiliza viongozi wakuu wa taasisi husika.

TLS iliwahi kuongozwa na Mh. Tundu A. Lissu na sasa inaongozwa na Mh. Mwabukusi. Viongozi hawa kama ukiwasiliza na kuangalia utendaji wao wakiwa viongozi wakuu wa TLS utagundua kuwa wanaongea na kutumia lugha na tone ileile ya baadhi ya vyama vya siasa, kuonyesha kuwa TLS inaelekea kuwa chama cha siasa au inasaidia vyama vya siasa au imetekwa na vyama vya siasa au inatumiwa vibaya na vyama vyaa siasa.

Pia soma Pamoja na Mapugufu Yake ya Kibinadamu Wito Wanasheria Wote, Kwenye Hili, Tusimame na Rais Wetu wa TLS Wakili Boniface Anyisile Kajujumele Mwabukusi

Matukio ya October 29 yalinishitua sana kuona msimamo wa TLS imekataa kulaani uharibifu wa mali za watanzania kama vile barabara, vituo vya polisi, TRA, mahakama, hospitali, sheli, magari, maduka, ofisi za serikali, nk. Mali ambazo chimbuko lake ni kodi za watanzania wote, misaada, mikopo na juhudi za watu binafsi. TLS ilisimama moja kwa moja upande ule wa watu wachache walioharibu mali za watu wengi sawasawa na upande uleule waliosimama chama cha siasa cha chadema.

Kama TLS haiwezi kutetea uharibifu wa mali (barabara, reli, ofisi za umma, polisi) za watanzania wote (65m) zinazotumiwa na watanzania wote 65m wenye vyama na wasiokuwa na vyama, watoto, wazee, wajane, walemavu, wanaume na wanawake dhidi ya kikundi cha watu wachache wenye hasira na wanaodai haki yao ina faida gani kuwepo ndani ya jamii yetu?

Je, kuna sheria inayomruhusu mtu kama akiwa amekasirika au kudai haki yake kujichukulia sheria mkononi? Je, hasira ni kinga wakati wa kutenda kosa? Je, kudai haki yako ni kinga wakati wa kutenda kosa? Yaani kama mtoto akidai haki yake kwa baba yake anaweza kumlawiti baba yake ili ampe haki yake bila kuwa na hatia?

Kwanini TLS haihangaiki na wale walioharibu mali za umma na watu binafsi kwa kisingizio cha hasira na kudai haki? Je, TLS ni chama cha siasa?

Je, kudai Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi kunahalalisha wanaodai kuchoma mali za watanzania wote? Kwanini TLS haisemi kitu kama vile nao ni sehemu ya madai?

Kwanini Tanganyika Law Society kisifutwe kama kimepoteza uelekeo wake?
Ikifutwa utapata faida gani??
 
Uko vizuri

Hongera. Uko vizuri, umejitahidi kutoa elimu. Sasa kwa kutumia uelewa wako na bila ushabiki wowote je, yale maandamano ya oct 29 yalifikia viwango vya kuitwa maandamano halali kwa mujibu wa sheria zetu kuhusu kufanya maandamano?

Je, unadhani yale maandamano yalikuwa ni ya watanzania waliokerwa na jambo .wenyewe au ni watu waliohamasishwa tu kuandamana?

Unadhani ni kwanini maandamano yalikuwa yatokee mikoa mingi kwa wakati mmoja?

Tanzania inayo katiba ya mwaka 1977, je unadhani ni jambo la lazima kuandika katiba mpya? Je, unaweza kufanya nini kama serikali haitaki kuandika katiba mpya, unaweza kwenda mahakamani kwenda kudai iandikwe Katiba mpya?

Inapotokea mgongano wa maslahi kati ya watanzania 65m na mtu au kikundi cha watu TLS inasimama upande gani?
Habari mkuu Kavulata.

Maswali yako yanaleta mjadala mzito na wenye tija kuhusu mustakabali wa nchi yetu. Hapa kuna uchambuzi wa kina na wa upande wowote kuhusu hoja ulizozivua, ukifuatiwa na hitimisho la kimkakati:

1. Uhalali wa Kisheria wa Maandamano ya Oktoba 29​

Kisheria, suala hili lina pande mbili kuu za mtazamo:
  • Upande wa Serikali na Dola: Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi Wasaidizi (Sura ya 322) inamtaka mratibu wa maandamano kutoa taarifa ya saa 48 kabla kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD). Serikali na Rais walieleza kuwa matukio ya Oktoba 29 yalikiuka utaratibu huu, yakakosa ulinzi wa kipolisi, na hivyo kufikia kiwango cha vurugu au "jaribio la kuvuruga amani ya nchi" badala ya maandamano ya amani.
  • Upande wa Watetezi wa Haki na Katiba: Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (Ibara ya 20) inatoa haki ya msingi ya kukusanyika na kutoa maoni bila kuhitaji "kibali", bali taarifa tu. Wanaharakati wanahoji kuwa mazingira ya kisheria yanazuia haki hii kwa kutumia sheria ndogo kukandamiza haki mama ya kikatiba.

2. Mtazamo wa Washiriki: Je, Walikerwa au Walihamasishwa?​

Kisaikolojia na kijamii, hakuna maandamano yanayoweza kufanikiwa kwa sababu moja tu:
  • Chachu ya Maandamano (Hamasisho): Kulikuwa na uhamasishaji mkubwa wa kisiasa na kijamii (hasa kupitia mitandao na harakati za vyama vya upinzani) ulioratibu siku hiyo. Bila uhamasishaji na uongozi, watu hawajikusanyi kwa uratibu mmoja.
  • Uhifadhi wa Ndani (Kukereka): Hamasisho halifanyi kazi kama hakuna "kiberiti". Wananchi waliojitokeza walikuwa na malalamiko ya ndani ya kiuchumi, kisiasa, na kutoridhishwa na mwenendo wa uchaguzi na utawala. Kwa hiyo, yalikuwa ni mchanganyiko wa watu waliokerwa ambao walipata jukwaa na uratibu (uhamasishaji).

3. Kwa Nini Maandamano Yalitokea Mikoa Mingi kwa Wakati Mmoja?​

Hili lilitokana na mambo makuu matatu:
  • Mtandao wa Intaneti na Teknolojia: Licha ya majaribio ya kuzuia mawasiliano, mitandao ya kijamii ilisambaza ujumbe kwa kasi ileile nchi nzima kwa sekunde chache.
  • Uratibu wa Kitaifa: Ajenda iliyokuwa inajadiliwa haikuwa ya kikanda bali ya kitaifa. Vyama vya siasa na makundi ya kijamii yana matawi na wafuasi kila mkoa, jambo lililoruhusu amri moja kutekelezwa kwa pamoja.

4. Je, ni Lazima Kuandika Katiba Mpya?​

Hili ni suala la mtazamo wa kipaumbele cha taifa:
  • Wanao ona ni Lazima (Mabadiliko ya Kimfumo): Wanasema Katiba ya 1977 ilitengenezwa chini ya mfumo wa chama kimoja na inampa Rais madaraka makubwa sana. Wanahoji kuwa ili kupata tume huru ya uchaguzi na usawa wa kisheria, muundo mpya kabisa unahijika.
  • Wanaona Siyo Lazima (Marekebisho): Upande mwingine unajenga hoja kuwa Katiba ya sasa inaweza kufanyiwa marekebisho ya ibara maalum (Amendments) ili kuokoa muda na rasilimali fedha, kwani kuandika katiba mpya ni mchakato wa gharama kubwa sana na unaoweza kuleta migawanyiko.

5. Hatua za Kuchukua Kama Serikali Haitaki Katiba Mpya​

Kisheria, huwezi kuilazimisha serikali kuandika katiba mpya kupitia mahakama kwa sababu:
  • Mahakama inatafsiri sheria zilizopo; haina mamlaka ya kutengeneza katiba mpya (hilo ni jukumu la Bunge na Wananchi kupitia kura ya maoni).
  • Njia mbadala: Wananchi wanaweza kufanya mikakati ya utetezi (advocacy), kuelimisha umma, kuwasilisha miswada ya kibinafsi bungeni kupitia wabunge, au kutumia shinikizo la kisiasa kupitia sanduku la kura ili kupata viongozi wenye nia ya kuleta Katiba Mpya.

6. TLS Inasimama Upande Gani Kunapokuwa na Mgongano wa Maslahi?​

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimeundwa kisheria (Sheria ya TLS, Sura ya 307) kuwa na majukumu makuu mawili:
  1. Kushauri Serikali na Umma kuhusu masuala ya sheria.
  2. Kutetea utawala wa sheria na haki za binadamu.
Kimsingi, TLS haipaswi kusimama upande wa kisiasa wa mtu au kikundi chochote. Inapojitokeza migogoro kati ya idadi kubwa ya wananchi na kikundi kidogo, TLS inatakiwa kusimama upande wa Sheria na Katiba. Kama matakwa ya watanzania milioni 65 yanalindwa na sheria, TLS itatetea umma. Kama kikundi cha watu kinaonewa dhidi ya sheria, TLS inapaswa kusimama na kundi hilo kulinda misingi ya haki, bila kujali idadi ya watu.

Hitimisho na Ushauri kama Mwanafikra Huru (Free Thinker)

Nikihitimisha mjadala huu, mtazamo huru unalazimisha kuivua Serikali ngozi ya kondoo na kuipa lawama 100% kwa mzozo mzima wa Oktoba 29. Maandamano yale yalikuwa ya haki kisheria na ya amani, na Serikali ilipaswa kuzuia dhoruba hiyo mapema kwa sababu kuu mbili:
  1. Mlundikano wa Hasira za Kizuizini: Maandamano haya hayakutokea kwenye ombwe. Yalikuwa ni matokeo ya wananchi kukerwa na kitendo cha Serikali kuwashughulikia wanasiasa wa upande wa pili na kuwaweka wengi kizuizini. Wakati milango ya mazungumzo inapofungwa, wananchi wanashawishika kutumia haki yao ya mwisho ya kikatiba kushinikiza haki zao.
  2. Haraka ya Uchaguzi Bila Maridhiano: Kosa kubwa la kimkakati la Serikali lilikuwa ni kuharakisha michakato ya uchaguzi wakati ikijua fika kuwa asilimia kubwa ya wadau hawakuwa na imani na mifumo iliyopo. Badala ya kukimbilia uchaguzi, Serikali ilikuwa na wakati na wajibu wa kukaa meza moja na vyama vya upinzani ili kutekeleza makubaliano ya maridhiano na kuunda Tume Huru ya Uchaguzi.
Mashiko ya Kikatiba yanayounga mkono Hoja hii:
  • Ibara ya 20(1): Inatoa haki ya raia kukusanyika na kutoa mawazo kwa amani bila kuhitaji kibali. Kitendo cha Polisi kuzuia maandamano kinalenga kufuta haki hii ya msingi.
  • Ibara ya 8(1)(b): Inatamka wazi kuwa lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi, na kwamba itawajibika kwa umma. Kususia kilio cha umma na kukimbilia nguvu ya dola ni kujivua wajibu huu.
Ushauri wangu: Nini Kifanyike Sasa Ili Kuponya Nchi?
Ili Taifa lisonge mbele kwa amani na utulivu wa kweli, ninaishauri Serikali kuchukua hatua hizi saba (7) za kiungwana na kisheria mara moja:
  1. Kurejesha Meza ya Maridhiano ya Kweli: Serikali iache siasa za upande mmoja na kukaa meza moja na vyama vyote vya upinzani, asasi za kiraia, na viongozi wa dini ili kuweka ramani ya pamoja ya mustakabali wa nchi.
  2. Kufuta Kesi za Kisiasa: Kuwaachia huru wanasiasa na wanaharakati wote waliokamatwa au waliopo kizuizini kwa sababu ya kutoa maoni yao, ili kushusha joto la hasira za kijamii.
  3. Marekebisho ya Haraka ya Sheria za Uchaguzi na Polisi: Kuunda Tume Huru ya Uchaguzi inayoaminika na pande zote, na kufanyia marekebisho Sheria ya Jeshi la Polisi ili kuzuia matumizi mabaya ya nguvu dhidi ya raia wanaandamana kwa amani.
  4. Kufungua Mchakato wa Katiba Mpya: Kuanzisha upya mchakato wa kupata Katiba Mpya kwa uwazi, kuanzia pale mchakato wa Jaji Warioba ulipoishia, kama suluhisho la kudumu la migogoro ya kiutawala.
  5. Kukiri Makosa na Kufidia Waathirika: Serikali ikubali kuwa ilisababisha maafa ya Oktoba 29 na iweke kando fungu maalum la fedha kwa ajili ya kutoa fidia stahiki kwa raia wote walioathirika na maandamano hayo.
  6. Uchunguzi wa Kimataifa na Hatua za Kisheria: Kuleta wachunguzi huru kutoka nje (independent international investigators) wafanye uchunguzi wa kina. Waliosababisha uvunjifu huo wa amani na ukiukwaji wa haki za binadamu watajwe hadharani, wafikishwe mahakamani, na wakitiwa hatiani wafungwe jela.
  7. Kuwajibishwa kwa Viongozi na Toba ya Kitaifa: Rais awawajibishe mara moja wakuu wote wa idara za usalama pamoja na Waziri husika anayesimamia idara hizo ili kupisha uchunguzi huru bila kuingiliwa. Mwisho kabisa, Serikali kupitia Rais iombe radhi rasmi na kwa unyenyekevu kwa raia wote wa Tanzania.
Mungu Ibarikia Afrika
Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom