As far as specification Apple wapo pande mbili kuna vitu wapo vizuri zaidi ya competition na kuna vitu wapo ovyo. Mfano.
1. Soc yao kwa sasa ndio best sokoni hakuna simu yenye processor yenye nguvu kushinda iphone japo kwenye gpu bado qualcomm yupo juu na mambo mengine kama modem na wifi anapitwa na simu za android.
2. Usiangalie tu ukubwa wa ram nipo radhi nitumie simu ya 2gb ram yenye dual chanell na ddr4 memory zenye speed kuliko simu ya 4gb ama 8gb ram ambayo ni single chanell na ram za ddr2 ama ddr3 zenye speed ndogo. Zipo simu zenye ram nzuri zaidi ila iphone zake pia sio mbaya zinapita hizi ram kimeo za kichina. Ukumbuke simu gpu yake inatumia ram ya simu hivyo jinsi ram ya simu ilivyo fasta na ndio apps na games zitarun smoothly.
3. Pia megapixel kwenye camera humaanisha ukubwa wa picha na sio quality. Dslr camera kali unaweza kuta ni 8mp tu. Kifupi kuchukua content za 4k inahitajika mp 8 tu. Ambayo kwa sasa ndio vifaa vya kisasa kama tv na pc vinaitumia. Quality ya picha sana inasababishwa na sensor iliotumika pia kuna vitu kama software, ois, aperture, lens etc vinachangia.
Kuhusu mambo mengine nakubaliana na wewe Apple innovation yao ni ndogo sana na ukikuta kitu chao kizuri basi utakuta kina mkono wa kampuni nyengine mfano display za samsung, memory za smasung etc. Kifupi ana asemble vitu best toka makampuni mengine na sio mvumbuzi kama baadhi ya kampuni nyengine.
Kuhusu software na Ecosystem zao zimetengenezwa kwa watu ambao hawataki mambo mengi kwenye simu, upige simu utumie whatsapp na insta etc.
Ila ukitaka mambo makubwa zaidi vitu kama VR, casting, file management, etc ios si yako.