1. Hio 6gb ram kuijaza ni rahisi sana mkuu sina simu ya 6gb ram hapa ningekuonesha kwa vitendo ila kama una acess nayo hapo apps hizi zinaweza.
-download app yoyote inayokuwezesha ku run multiple instance of app mfano kuwa na whatsapp mbili, insta mbili, facebook mbili etc. App hizo ni kama secure folder inayokuja na samsung yenyewe ama parallel space. Technically unakuwa na kama simu mbili. Mimi simu yangu ina 3GB ram kuna kipindi nilikuwa nafanya kazi kampuni fulani hivyo simu yangu nikaigawanya mara 3, ndani ya simu moja nina maeneo matatu kama ifuatavyo.
-sehemu ya kwanza personal kuna whatsapp yangu ya kila siku na app zangu kama mtu mwengine.
-sehemu ya pili ya biashara, whatsapp ya kazini, insta ya kazini etc
-sehemu ya tatu ya michezo vitu vyangu kama magames na test zangu mwenyewe.
Hayo ni matumizi ya kawaida tu ila simu yangu ilikuwa slow sana, ni kama simu 3 ndani ya simu moja, 6gb ram ingesaidia japo nayo haitoshi pengine 8gb ram kuendelea ingenifaa zaidi.
Kwa wale wanaotumia virtual box kwenye pc wanaelewa kiasi gani inademand ram, same here.
Pia kama unataka ku extract url kwenye streaming service inakula sana resource, inategemea na ugumu utaokutana nao. Utahitaji kuanza kustream, uwe na url snooper, uwe na text editor, sometime hex editor, kuwe na media player, sometime ssl decrypter inahitaji kurun kama vpn etc vyote hivi virun at same time, natumia s5 kufanya hii kazi na inakuwa slow na moto sana kwa hii kazi.
Simu karibia zote zinazorun android 6 kupanda zina option ya unlimited user account, theoretically unaweza tumia hata ram gb 120 na zaidi.
2. Issue ya kucopy naona bado upo enzi za s2 kipindi kile cha icons na round corner, tupo 2018 sasa hivi hebu nitajie miaka 3 iliopita samsung kacopy nini na nini toka Apple? Maana simu kama iphone x almost kila unachogusa Apple kamcopy samsung na Oems wengine wa Android.
Unakumbuka maneno ya steve job? Alisema hakuna mtu atakaenunua simu kubwa, na sasa Apple wanaramba matapishi
Steve Jobs Turned Out To Be Completely Wrong About The Key Reason People Like The iPhone
Mambo mengi kati ya 10 niliokutajia juu Apple walikuwa wakiyapinga ila sasa wao ndio vimbele mbele wa kucopy, kifupi hawana innovation wanafata tu trend za watu, dual sim, vioo vikubwa, edge to edge display, fast charge, water proof, high resolution, oled na trend kibao.
3. Kuhusu game, lete video inayoonyesha setting zilizotumika simu zote mbili, by default samsung ina 2k screen hivyo kwenye native resolution itakuwa slow kuliko simu ya 1080p ama 720p hivyo nataka video inayoonyesha setting sawa maybe zote kwenye 720p halafu ueke hapa.
4. Kuhusu efficiency.
Sasa mkuu nimekuekea video tena toka kwa fans mkubwa wa Apple anakiri mwenyewe samsung ipo faster kuliko iphone, at same time iphone ina processor yenye nguvu kushinda samsung. Hebu jiulize
processor yenye nguvu inarun vitu slow na processor isio na nguvu ina run vitu fast je ipi ni efficient?
Jibu ni rahisi tu ila unapenda tu uzunguke uzunguke, fans wenzako wa Apple wanakubali we endelea kutafuta visingizio.
5. Kuhusu Nokia mkuu its far from dead company, Ni network manufacture mkubwa duniani, ngoja nikupe point kadhaa kukufumbua macho.
1. Kampuni ya Apple inamtegemea Nokia kununua vifaa vyake vyote vya network
2. Karibia mitandao yote duniani yenye kasi zaidi inanunua network equipments toka Nokia, mfano vodacom Tanzania ina achieve 50mbps kwenye 3rd world country kama Tanzania kitu ambacho ni above average ya 40mbps ya dunia.
3. Robot manage robot, Nokia ana kiwanda pekee duniani ambacho kinafanya kazi na marobot tu, kuna hadi marobot mafundi yanayotengeneza marobot wenzao wakiharibika, kifupi kiwanda kinafanya kazi chenyewe tu.
4. Nokia ni pioneer wa 5g na ameshatangaza atacharge dola 3 kwa kila kifaa kitacho run 5g, hivyo around shilingi 7000 kwa kila simu, ununue iphone ununue tecno ununue kishkwambi kama kina 5g utawalipa tu.
5. Nokia karibuni ameinunua Alcatel lucent kwa dola bilioni 16 ni moja kati ya manunuzi makubwa duniani upande wa tech. Zaidi ya trilioni 30 za kitanzania.
Sidhani kama hizo activity ni za dead company mkuu. Hapo sijataja licence hata moja, huuzi simu ulaya au marekani bila Nokia kugonga hodi kila kampuni ya simu unayoitaja Wanamlipa nokia.
Na jamaa wana maabara kubwa za kitafiti kuna innovation kubwa sana wanafanya miaka ya karibuni toka maabara kama bell labs.
Unafahamu Nokia anatengeneza hadi nyambizi za chini ya maji?