Kwanini aweke 6GB of rams ikiwa 3 GB inatosha? Kwanini aweke 8 cores ikiwa 6 zinatosha? Unaweza ukaweka more features wenye kitu then ikawa useless, umeweka ilimradi uvutie wateja tu. My point iko pale pale, Ios au Apple are more efficient then androids. Sitoshangaa next iphone ikitoka ikawa ina specs izo izo zaid ya kusikia A12 processor lakini ram ikabaki 3gb au 4gb.
Nilishakueleza hapo juu kwamba havitoshi kuna matumizi kibao ambayo yanahitaji zaidi processor yenye nguvu na ram kubwa, pia kuna vitu kama multitasking vinahitaji as much ram as possible same kwenye emulation.
Kaangalie video za fortinite kote kwenye android na ios game linalag kama halina akili nzuri sababu simu hazina uwezo, then leo hii unasema hizo specs hazihitajiki?
Sababu tu hakuna breakthrough ya technology bado ila nguvu inahitajika zaidi.
Legacy ya Steve Jobs ni kuunda features ambazo ni usable, sio kwamba aweke features ilimradi tu awe na features nyingi bro. Samsung wakati wa S4 aliimock Apple kwa kutumia gesture controls, sijawahi kumuona mtu akipokea simu kwa kuwave, au anasoma message kwa kuweka kidole karibu na screen, hizi ndio useless features Samsung used to lure customers. So far Apple is not on that path...
Mbona na nyie pia mnatengeneza useless na gimmick feature? Ipo wapi 3d touch? Imekuja miaka kadhaa sasa hivi imekuwa discontinued kwenye iphone mpya, sasa hivi Apple ndio anamcopy samsung na kununua vifaa kwake, kuanzia misimu yenye kioo kikubwa, lcd hamuitaki tena mnataka oled kama samsung, mnatoa bezel, etc
Chief, swali la kujiuliza, was that power needed for that iphone and was it usable? kama it was usable tatizo liko wapi? hata Samsung kama 6GB of rams na octa core za 2.5 km ntakua sijakosea zinatumika, mbona fresh tu. iwe reasonable. Sio unafungua app ya benchmark halafu unasema kuwa ndio inatumika. We need day to day use, sio kwa average person, tuzungumzie kwa heavy user. Hata photoshop doesnt need 6GB of ram kwenye PC where unapata full functions, Ume mention game ya fortnite, tena ukasema unahitaji 3GB of rams tu, samsung imeweka 6GB. Hio fortnite kumbe unaweza ukacheza kwenye iphone x bila kuhitaji more rams?
Ukiambiwa game linataka 3gb ram haimaanishi simu iwe na 3gb ram bali linamaanisha uwe na free ram 3gb, simu inaweza ikawa na ram 4gb ila free ram ikawa 2gb tu hivyo isirun hilo game.
Na photoshop inategemea unafanya nini inaweza ikahitaji hata 32GB ram ama zaidi si kila kazi ya photoshop inafanana.
Kifupi specs zinahitajika zaidi kuna apps kibao hazifanyi kazi hadi simu zitakavyokuwa na nguvu zaidi.
Bro hapa tuchukue gari mbili zenye 4 cylinders zote tuzifanyie comparison. Ukichukua V8 ukacompare na V6 itakuwa sio fair.
Unataka kucompare 8 core na 6 core? 3GB of rams kwa 6GB of rams? Niletee video hapa ya android phone yenye same specs, 3GB of rams na 6 cores akisha tuone perfomance yake.
Au tusubiri Apple na yeye atoe 8 core na 6GB of rams akisha tuone....
Kwanza mkuu usi mistake number of cores na nguvu ya processor, japo Ya Apple ina core 6 ila ina nguvu zaidi ya samsung core 8 atleast kwa benchmark ya geekbench,
Soc zinazotumika kwenye android zinaitumia mfumo wa big little, kunakuwa na core 8, core 4 kubwa zenye nguvu na core 4 ndogo zinazotunza chaji.
So simu ya samsung inaporun kitu heavy ni core 4 ndio zinapiga ile kazi.
at same time A11 ina core 6 ambazo zote kwa pamoja zinapiga mzigo. Hivyo Apple anakuwa kwenye advantage simu zikirun kitu heavy.
Ila mwisho wa siku hata iphone iwe na power vipi ios italimit hio power sababu inalimit mambo mengi ikiwemo multitasking.