Nzokanhyilu
JF-Expert Member
- Feb 19, 2007
- 1,078
- 93
Sasa wananchi wa Saudia nao wakimtimua Rais wao atakimbilia wapi?
Denmark!
Sasa wananchi wa Saudia nao wakimtimua Rais wao atakimbilia wapi?
Denmark!
kwa nini?
Nimekuwa nikifatilia kwa miongo mingi sasa viongozi wengi madikiteta wakipinduliwa huwa wanatafuta hifadhi za kisiasa Saudi Arabia. Nitatoa mifano michache hapa
Hii ni mifano michache ! Kwanini wanakimbilia Saudi?
- Waziri mkuu wa zamani wa Pakistani Nawaz Sharif baada ya kuangushwa alikimbia Saudi Arabia
- Waziri mkuu wa Syria 1951 bw Ma'ruf al-Dawalibi Alikimbilia Saudia hadi alipokufa mwaka 2004
- Idd Amin dada raisi wa zamani wa Uganda aliyeangusha na majeshi ya Nyerere na yeye alikimbilia huko mwaka 1980 kuishi huko hadi kifo chake mwaka 2003
- Raisi wa zamani wa Tunisia Mh Zine el-Abidin Ben Ali naye baada ya kukimbia nchi Jan 16, 2011 amekimbilia Saudi Arabia
- Mzee mzima Pervez Musharraf baada ya kulazimishwa kujiuzulu naye alikimbia Saudi Arabia tangia 2008
Mfalme wa Saudia yeye huenda atakimbilia kati ya nchi hizi mbili Afghanistan ama Pakistan, si unajua hata yule kinara wa ugaidi raia wa Saudia naye yuko kati ya Afghanistan na Pakistan.
It is a simple question. Udini ndiyo unawapeleka huko. Hakuna cha zaidi.
Marekani
Tafuta kitabuConfessions of an Economic Hit Man by John Perkins utapata jibu la swali lako na pengine mengine yanayohusiana na hayo.
Sasa wananchi wa Saudia nao wakimtimua Rais wao atakimbilia wapi?
Nadhani hata Robert Mugabe atakimbilia huko yakimshinda Zimbabwe.
Sidhani kama ni dhambi kumpokea kiongozi yoyote anaeomba hifadhi ya kisiasa kama vile Nawaz Shariff alikuwa kiongozi wa kuchaguliwa kidemokrasia na wananchi wake lakini aliempindua Musharaf na yeye baada ya kufukuzwa lakushangaza amepokelewa na Uingereza na kupewa hifadhi!
Mbona huzishangai nchi za Magharibi zinapowapokea vigogo wengi waliotoroka kwao kama vile Oscar Kambona toka Tanzania,Haile Selase wa Ethiopia, Sultani Jamshid bin Abdullah Al Said wa Zanzibar aliekimbilia Uingereza, Dikteta Shah wa Iran aliekimbilia Uingereza, Dikteta Augustino Pinochet wa Chile alikimbilia Uingereza na hata hapa kwetu Tanzania tulishawapokea madikteta waliopinduliwa kwao mfano: ni Milton Obote wa Uganda!
Sasa unaishangaa Saudia ambayo imempokea Zain Abi Din Ali wa Tunisia baada ya Ufaransa kukataa kumpokea wakati alikuwa ni kimpenzi mkubwa wa Ufaransa!
Picha hizi ni baadhi ya viongozi waliokimbilia Uingereza tujikumbushe:
View attachment 20812 Oscar Kambona View attachment 20810 SULTAN WA MWISHO ZANZIBAR JAMSHID
View attachment 20808 DIKTETA AUGUSTINO PINOCHET WA CHILE
View attachment 20811 MILTON OBOTE WA UGANDA HUYU ALIPOKELEWA NA JULIUS K: NYERERE
View attachment 20809 HAILE SELASI MUNGU WA RASTAFARI WA ABBYSINIA
Wote hawa walikimbilia Uingereza mbona hushangai unaishangaa Saudia?
sasa hivi anaumwa mzee wa watu sijui ndo israeli anataka kumpitia!Nadhani hata Robert Mugabe atakimbilia huko yakimshinda Zimbabwe.
Kwa nini Jerusalem?Atakimbilia Jerusalem..... najua utashangaa lakini kama hujui kwanini uliza.
Majina Yao na nchi wanayokimbilia kuna uhusiano kidogo mkuu
Marekani