Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,058
- 1,711
Saudi Arabia yatangaza kufungua Duka la Kuuza Pombe Mjini Riyadh baada ya Marufuku ya zaidi ya Miaka 70
Wateja watakuwa ni Wafanyakazi wa Kidiplomasia wasio Waislamu , ambao kwa Miaka mingi wamekuwa wakiagiza pombe kwa njia rasmi ifahamikayo kama "Diplomatic Pouches."
Marufuku ya Pombe Nchini humo ilikuwa Sheria tangu Mwaka 1952, baada ya Mtoto wa Mfalme Abdulaziz, Mishari bin Abdulaziz Al Saud kulewa na kumuua kwa risasi Mwanadiplomasia wa Uingereza Cyril Ousman, Novemba 1951
Wateja watapewa Kiwango cha juu cha 240 "alama" za pombe kwa Mwezi, ambapo hawataruhusiwa kununua zaidi ya kiwango hicho. Lita moja ya Pombe Kali itakuwa na thamani ya alama 6, Lita moja ya Mvinyo itakuwa na alama 3, na Lita moja ya Bia itakuwa na alama 1.
Hatua hizi ni sehemu ya mipango inayojulikana kama "Vision 2030" ya kulegeza Sheria za Saudi Arabia chini ya Mwana-Mfalme na Mtawala wa nchi hiyo Mohammed bin Salman
Kulingana na Sheria ya sasa ya Saudi Arabia, adhabu kwa kunywa au kukutwa na pombe inaweza kujumuisha faini, kifungo, kupigwa hadharani, na kufukuzwa nchini kwa wale wasio Raia