Wachezaji waanza muchos he's na ligi ya saudi arabia wengi waanza kuomba kuondoka

uwe hodari

JF-Expert Member
Dec 16, 2022
3,994
8,370
Pamoja na mapesa yanayomwaga na ligi ya saudi arabia "saud professional leugue lkn bado ligi hiyo haijawa darling league km zilivyo ligi za uropa

Utakubaliana na mimi angalia ligi ya uscoch ambayo ina vigogo km celtic na rangers inahamasa mvuto na upinzani kuliko saudi arabia

Upinzani na ladha ya ligi haujajengwa kutokana na kulipwa mapesa mengi ball ni passion ya mashabiki

Mchezaji anayelipwa pesa nyingi ligi ya scotland haifikii dola elfu hamsini kwa wiki

ile henderson aliyetimkia saud arabia mchezaji wa Zamani wa liverpool anakunja dola laki saba kwa wiki

Sasa basi baada ya serikali ya saudi arabia kuamua kuvifadhili vilabu vinne vikuu mishahara ya wachezaji ilipanda hadi 600%

Wachezaji wengi walipagawa ila mambo hayaendi km ilivyotarajiwa ligi imeanza kupoteza mvuto hata kabla msimu wa kwanza wenye nguvu haujamalizika

Majina makubwa yalikimbilia arabia alisema mchezaji maarfu Neymar na wengine wengi

Lkn katikati ya msimu wachezaji waliotoka ulaya tayari wameanza kuomba kuondoka Saudi kurejea ulaya

Mchezaji neymar inasemwa alipanga na daktari wake kuwachezea mchezo waarabu
Alicheza mechi mbili akaumia na sasa anatibiwa ulaya saudi arabia ataenda 2024 mwishoni akiwa katika msimu wake wa mwisho

Chrstiano Ronaldo ambaye anawafusi wengi kwenye mitandao ya kijamii na mchezaji maarfu duniani anapocheza uwanja haujai kabisa

Mechi moja yenye nyota kutoka ulaya ilishuhudia mashabiki mia saba tu wakati uwanja unaweza kuchukua watu alfu 20+

Pmj na mapesa yote lkn bado mashabiki wamekuwa wanasuasua viwanjani
Ukitoa vilabu byebye makazi yake Riadh vilabu vingine ni km vinacheza bila mashabiki majukwaa wazi

Sasa wachezaji wengi wanaanza kufikiria kurudi ulaya kutokana na kushindwa kuendana na mazingira ya kule

Ikumbukwe saudi arabia ni mwenyeji wa kombe la dunia 2030 hivyo anaimarisha timu yake kupitia ligi ya ndani lkn pesa anazolipa hazina uhalisia lazima atakwama tu

Serkali ya kifalme inalenga kutumia mpira kusambaza maadili yake duniani ambako kumetengwa matilion ya pesa

Je adhima yake hiyo itatimia?

Je saudi arabia itaendelea kusubiri mchezaji awe maarfu ulaya ndio wapande dau

Au itarudi kwenye misingi ya mpira km biashara inayojilipa yenyewe kwa kuzalisha vipaji na kuendeleza vipaji

Sina tatizo na wachezaji walioisha uwanjani wanaokaribia kustafi km kina ronaldo
 
Hizo ni retirement leagues kwa wachezaji ambao tayari walishafanya mambo kwenye leagues bora ulaya.

Unafikiri ni nini kimemzua Mbappe kwenda huko kuchukua magunia ya hela?

Kwanza ana umri mdogo so ana miaka mingi ya kucheza kwenye top leagues na kushinda medal/makombe yenye heshima.

Pili hajawahi kushinda taji la UEFA so lazima moja ya ndoto zake ni kuchukua UEFA akiwa pale Liverpool au Madrid.

Tatu ni Ballon d'Or. Kwa mchezaji wa callibre ya Mbappe lazima awe na ndoto ya kushinda tuzo ya mchezaji bora dunuani.

So akienda huko kwenye league za wastaafu ndoto zake zote zitakuwa zimeyeyuka.
 
Waarabu huu sio mchezo wao kuulazimisha kule ni kupoteza muda ila wangebaki na project Yao ya kununua vilabu vya Ulaya
Ulaya ibaki kuwa Ulaya aisee kupiku ligi kama Epl bundesliga laliga Seria A Ligue 1 n.k ni kazi mno maana passion ya mashabiki iko juu na Kila mchezaji anapenda pamoja na kupata hela apate na zile kelele za anfield
 
Waarabu huu sio mchezo wao kuulazimisha kule ni kupoteza muda ila wangebaki na project Yao ya kununua vilabu vya Ulaya
Ulaya ibaki kuwa Ulaya aisee kupiku ligi kama Epl bundesliga laliga Seria A Ligue 1 n.k ni kazi mno maana passion ya mashabiki iko juu na Kila mchezaji anapenda pamoja na kupata hela apate na zile kelele za anfield

uamuzi wliofanya ndio wa sahihi zaidi. fikra zako ndio fikra zinarojesha nyuma nchi za kiafrika.
 
Back
Top Bottom