Habari wana JF,
Tangu Mh. Rais ameshika madaraka, ameonekana akitaka kufanya jambo anatafuta "zuga" flani ili aeleweke.
Swali ninalojiuliza kwa nini asiwe anachukua msimamo na kulifanya jambo moja kwa moja?
Mfano:
1. Inafahamika kabisa swala la kuondolewa kwa "machinga" alishalipitisha siku nyingi tu. Na hii itakuwa operation katika majiji yote makubwa. Sasa Mh Rais akaona afunge ziara aende kariakoo, kisutu, n.k akidai eti ameenda kujionea. Hivi pale kariakoo alijionea nini kipya?
Pia ktk mpango huu, wameona ni lazima Halmashauri/jiji wachukue uendeshaji wa masoko yaliyo kwa viongozi au vyama vya masoko (mf. kariakoo shimoni). Sasa hili nalo badala ya kutamka tu, Yeye akasema ameenda, amesikia malalamiko, na akasimamisha uongozi ili soko liendeshwe na jiji. while inafahamika kabisa ni maamuzi walishayapanga.
Swali: Kwani Machinga Complex haipo chini ya Halmashauri?
2. Mfano namba mbili, ni ishu ya kupambana na corona. Inafahamika kabisa Mama alishakubaliana na swala la chanjo. Sasa namna alivyozunguka na kuunda tume utafikiri kweli, TUNAPAMBANA NA CORONA.
Swali la kumuuliza Mama, mbona hafafanyii kazi mapendekezo mengine, ila anafanyia kazi pendekezo moja tu la chanjo? vipi kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, vipi physical distance, vipi uvaaji barakoa? Mbona si lazima? au uongozi ni kuvaa wewe tu? Kwa nini usingetamka kwamba tunafanya taratibu namna ya kupata chanjo, ukazunguka kuunda tume!!
3. Ishu ya Manji
Inafahamika kabisa ashapata 'clearance' huko juu. Pale TKKR mmempeleka ili asafishwe na kufanya "zuga" flani.
Sasa kwa nini msimuache tu.
Najua ipo "zuga" unayowaandalia CHADEMA. Hahaha...
Binafsi hii style ya 'zunguka-zunguka' ili uamue jambo sioni haja yake. Simamia tu kile unachokiamini moja kwa moja.
Asante.