Kwanini Rais akitaka kufanya jambo anazunguka sana kupata uhalali?

Ondoeni hii dhana kwamba kila anayemkosoa Mama, anataka awe kama Hayati.
Mkuu ndio kwanza mama kashika madaraka hata siku 100 bado!

Subiri tu utajionea show! Hawa wanaofikiri wanamkomoa marehemu watakuja kula haya matapishi yao.

Nakushauri kuwa mtazamaji tu kwa sasa!
 
Mkuu ndio kwanza mama kashika madaraka hata siku 100 bado!

Subiri tu utajionea show! Hawa wanaofikiri wanamkomoa marehemu watakuja kula haya matapishi yao.

Nakushauri kuwa mtazamaji tu kwa sasa!
Nashangaa hawa watanzania wenzangu kila tukimkosoa Mh Rais Samia. Wanarukia eti Mwendazake kashakufa. Sasa hii inahusiana vipi?!

Wanakosea sana kuona kila mtu alinufaika eti na Hayati JPM...
 
Lazima aulize washauri ...unafikiri kuwa Rais ndio kujua kila kitu??

Unataka watu warudi zama zile zile mtu mmoja ana-act kujua kila kitu..

Mhandisi yeye, tabibu yeye,mchumi yeye , kila kitu anataka maamuzi yatoke kwake mwisho wa siku ndio tulishuhudia uharibifu karibu kila sehemu sababu ya kutoshirikisha wataalam husika
 
Kwa upande wangu nafikiri hiyo ndio njia sahihi ya utawala bora. Kuwashirikisha wengine. We humsikii akiongea lazima aweke maneno "tutafanya, tutashughulikia, tutajadiliana" n.k
Unashirikisha ukiwa huna jibu. Sio unaandaa majibu halafu unaenda kuzuga kwa kuuliza uliza maswali..
 
Mama ni weak mno and soft, in short huwa hajiamini, ni MTU wa michakato km awamu ya 4. Expect nothing new within this 4 years. Dalili za mvua ni mawingu mkuu. First impression matters a lot, mama ashasomwa tayari na subordinates, wanajua hajui vitu vingi, na siyo mfuatiliaji, expect atakuwa anaingizwa choo cha kiume na matango pori ya kufa mtu.
Ajiamini afanye kazi. Urais ni mambo makubwa..
 
Mama ni weak mno and soft, in short huwa hajiamini, ni MTU wa michakato km awamu ya 4. Expect nothing new within this 4 years. Dalili za mvua ni mawingu mkuu. First impression matters a lot, mama ashasomwa tayari na subordinates, wanajua hajui vitu vingi, na siyo mfuatiliaji, expect atakuwa anaingizwa choo cha kiume na matango pori ya kufa mtu.
Mama ana Mapungufu yake kama Binadamu. Lakini ana Mazuri Mengi sana Muhimu. Moja ya sifa kubwa aliyojaaliwa na Mwenyezi Mungu ni aina ya Kiongozi ambaye Uwepo wake tu unafanya Watu WAWE NA AMANI.

Katika familia ni muhinu sana watoto wakikuona wanakuwa na Amani. Ni muhimu sana Mzazi anayehubiri HAKI na KUISIMAMIA kwa kauli na vitendo. Ni muhimu sana Mzazi asiye na upendeleo wala chuki.

Samia ni Kiongozi ambaye hata kama kuna ulazima wa kuwatoa wamachinga sehemu au kuvunja nyumba kupisha Barbara atawaondoa lakini ataonyesha Utu na kuthamini/huruma. Sio Kiongozi wa " Tokaaaa" au " kwani niliwaleta Mimi hapa.

Wananchi wengi hawataki Kiongozi aina ya OLE
 
Tz. Akiendesha hvi nchi tunatengeneza taifa la kisenge sana
Nchi za kiafrika zinahitaji vichwa vigumu km . Magufuli
 
no 2.

Raisi anajuwa anachokifanya. Na anajua wazi kuwa ugonjwa wa Corona kwa Tz si tishio sana. Anachofanya ni kuwazuga wazungu ili kma kuna chochote kitu wasitunyime. Lazma twende sambamba na dunia inavyotaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo la kwenda sambamba na dunia hapana! Kuleta chanjo kidogo ni muhimu kwa ajili ya wale ambao kutokana na shughuli zao wanalazimika kusafiri nje ya nchi. Lakini kusema ni kwa ajili ya kupambana na corona hiyo siyo kabisa!! Hakuna corona ya kupambana nayo! Hata waliokuwa wanaitafuta hata kwa tochi wameshanyosha mikono, haipo, Mungu alishatuponya. Ila ukiitaka binafsi unaweza kuipata maana hiyo ni roho na ina macho na masikio ya kuwaona na kuwasikia wanaoitaka!! Kwa Tanzania kupata corona ni hiari!! Ukitaka kupata corona ni rahisi sana, wewe kataa tu kuwa Mungu hajakuponya na corona, baada ya hapo ni suala la muda tu na corona itatia timu kwako na kwa familia yako! Hiyo ndiyo siri kwa nini mataifa ambayo yalimweka Mungu pembeni kwenye kupambana na corona hadi leo bado yanateseka!! Wana chanjo na wanavaa barakoa lakini bado corona inawatesa!!
 
Ohoo! Si wamesema TAKUKURU wamempa dhamana.

Binafsi taarifa nilizonazo ataitwa tena mara kadhaa, halafu ishu itaisha.
Ametoka kwa sababu za kiafya. Aliumwa! Sijui ndo mambo ya arosto hayo! mimi sijui lakini huku mitaani ndo wanadai hivyo!
 
Naunga mkono hoja, japo nyuma ya hii ni kutafuta ushawishi kwa jamii na kuungwa mkono. Vilevile kuungwa mkono na mabeberu ambao wanatusaidia kwenye bajeti ya kundesha nchi.

Lakini kama mtu asiye mnafiki, na mweledi mwenye kujiamini haina haja ya kutengeneza sinema za uongo za kusadikika . Kama nyeupe nyeupe nyeusinyeusi.

Tumuunge mkono mama kipindi chake kikimalizika tutasonga mbele. Baadhi ya watendaji sasa hivi wamekuwa wavivu wakati enzi za JPM ndani ya siku 2 unapewa majibu sasa hivi hata wiki 2 hupari majibu ni danadana tuu. Wanenda na upepo wa mama wa upole .
 
Issue ya Sabaya inazima issue ya makinikia pia. Ila mie nawapenda sana wanasiasa. Wanatoa nafasi kwa wajanja kula nchi. Sasa kama wewe umezubaa utaishia kushangilia uhuru wa kubwabwaja ila mfukoni huna kitu.
Kama hizi ndiyo njia za huyu mama kutawala, basi atakuwa mbovu sana.

Maanake yote haya hayawezi kufichika.

Mwishowe watu watayaweka pamoja na kuona picha kamili ya udanganyifu wake.

Sasa mkuu wangu 'gongolamboto', itawezekana vipi nchi nzima sote tuwe "wajanja"?

Huku kula kwa "wajanja" hakutatuletea matatizo kweli, wajinga wakizinduka?
 
Habari wana JF,

Tangu Mh. Rais ameshika madaraka, ameonekana akitaka kufanya jambo anatafuta "zuga" flani ili aeleweke.

Swali ninalojiuliza kwa nini asiwe anachukua msimamo na kulifanya jambo moja kwa moja?

Mfano:
1. Inafahamika kabisa swala la kuondolewa kwa "machinga" alishalipitisha siku nyingi tu. Na hii itakuwa operation katika majiji yote makubwa. Sasa Mh Rais akaona afunge ziara aende kariakoo, kisutu, n.k akidai eti ameenda kujionea. Hivi pale kariakoo alijionea nini kipya?

Pia ktk mpango huu, wameona ni lazima Halmashauri/jiji wachukue uendeshaji wa masoko yaliyo kwa viongozi au vyama vya masoko (mf. kariakoo shimoni). Sasa hili nalo badala ya kutamka tu, Yeye akasema ameenda, amesikia malalamiko, na akasimamisha uongozi ili soko liendeshwe na jiji. while inafahamika kabisa ni maamuzi walishayapanga.

Swali: Kwani Machinga Complex haipo chini ya Halmashauri?

2. Mfano namba mbili, ni ishu ya kupambana na corona. Inafahamika kabisa Mama alishakubaliana na swala la chanjo. Sasa namna alivyozunguka na kuunda tume utafikiri kweli, TUNAPAMBANA NA CORONA.

Swali la kumuuliza Mama, mbona hafafanyii kazi mapendekezo mengine, ila anafanyia kazi pendekezo moja tu la chanjo? vipi kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, vipi physical distance, vipi uvaaji barakoa? Mbona si lazima? au uongozi ni kuvaa wewe tu? Kwa nini usingetamka kwamba tunafanya taratibu namna ya kupata chanjo, ukazunguka kuunda tume!!

3. Ishu ya Manji
Inafahamika kabisa ashapata 'clearance' huko juu. Pale TKKR mmempeleka ili asafishwe na kufanya "zuga" flani.
Sasa kwa nini msimuache tu.

Najua ipo "zuga" unayowaandalia CHADEMA. Hahaha...

Binafsi hii style ya 'zunguka-zunguka' ili uamue jambo sioni haja yake. Simamia tu kile unachokiamini moja kwa moja.

Asante.
Mama siyo mtu wa kukurupuka anafikiri kabla ya kuamua
 
Makuzi na mazingira ambayo mtu amekulia, kwa kiasi kikubwa, humfanya awe alivyo. Mathalani ukiwa mfugaji wa punda, tangu utoto wako umeona ambavyo punda haendi bila mijeledi, likitokea kosa ukaja kuwa kiongozi, kama huna IQ ya hali ya juu, utawapelekesha watu kama punda. Kila siku utamtafuta wa kumtandika bakora kama ambavyo ulikuwa ukiwafanyia punda.

Kuzuia hilo, ndiyo maana tunakuwa na katiba na sheria. Lakini ikitokea anayeongoza akawa hataki kufuata hata katiba na sheria, lazima mtaswagwa kama punda. Punda huchapwa kila siku, na wala haitegemei kama amekosea au hapana, hutegemea mfugaji wake ameamua kumtandika au kumwacha. Punda haulizi wala kushauri, yeye ni wa kupokea tu bakora na kuelekezwa kwa kwenda.

Wale ambao walizoea kuona mahusiano kati ya punda na mfugaji, ni lazima washangae sana, wakiona Rais anawataka ushauri anaowaongoza.
Na kweli jamii anayotoka Mwendazake ina shuruti mbaya sana watoto hupigwa hadi kuzirai kisa kamwaga maji.
 
Huo ni mtazamo wako. Ukweli ni kuwa Mheshimiwa SSH hakurupuki kama mnavyotaka nyie; anajiridhisha kwanza kabla ya kufanya maamuzi.
Unaonaga teuzi za express? Na wengine huwa hawajui? Don't lie to us mkuu, huwa hapay attention to details.
 
vidole vyangu koma usiandike ninachokiwaza oho... kuna maisha zaidi ya siasa hivyo tulia!
 
Back
Top Bottom